Kwanini wanawake mnakimbilia kupanga mkipata kazi?

Kwanini wanawake mnakimbilia kupanga mkipata kazi?

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,430
Reaction score
3,547
Habari ya maandilizi ya sikukuu,

Kuna hii tabia ya mabinti tena wadogo kwenye early 20s wakipata tu vikazi hata iwe saluni au mgahawani wanakimbilia kupanga ili wajitegemee.

Kusema kweli hii imekuwa kero kwa sie hasa wa maofisini, hawa mabinti wanaojitegemea ni kama wanageuka omba omba, hapa nazungumzia hawa wanaofanya usafi walioajiriwa kwenye kampuni za usafi, kuna wanaouza matunda na juisi maofisini wengine wanatembeza korosho na soksi, siongelei wote ila wengi wao ni kama wanajiuza au kuishia kuomba omba maofisini kwa sisi wafanyakazi wa kiume.

Ukimuomba namba leo kesho hana kodi na sio kwamba wanatania ni kweli unaona kabisa meseji za mwenye nyumba na missed calls kibao. Hasa unajiuliza why ulikimbilia kupanga kazi yenyewe ya laki 2.

Kwanini usibakie na wazazi au ndugu kama ulivyoishi kabla ya kuajiriwa? Wengi Wanaangukia kujiuza au kuwa omba omba maofisini.

Kwanini mnakimbilia kujitegemea?
 
Unaidharau laki mbili?
Hajadharau ila Kwa mtoto Wa kike kupanga kabla ya ndoa haileti picha Nzuri labda kipato kitosheleze au ufanye Kazi mbali na nyumbani. Kitamaduni zetu Binti anatakiwa atoke nyumbani ahamie Kwa mumewe tu. Mshahara laki 2 hautoshi Kwa Binti, ale, alipe bills, nauli n.k ndo maaana vingi vinakua vimalaya Malaya. Binti anaejielewa hawezi kimbilia kupanga mapema hvyoo wakati ana wazazi.
 
Mdogo wangu alikua anafanya Kazi makumbusho then anatoka toangoma tulimkataza kupanga ,ameondoka last month kwenda Kwa mumewe!!!

Hata Mimi nilipotoka mkoani nilivohamja kikazi Dar nilikatazwa kupanga nilipewa nyumba nzima niishi na familia yangu na wapangaji...

Sio kua tuna uwezo hapana ni kawada TU mama nyumba zenyewe ziko uswahilini hukooooo
 
Hajadharau ila Kwa mtoto Wa kike kupanga kabla ya ndoa haileti picha Nzuri labda kipato kitosheleze au ufanye Kazi mbali na nyumbani
Kitamaduni zetu Binti anatakiwa atoke nyumbani ahamie Kwa mumewe TU
Mshahara laki 2 hautoshi Kwa Binti ,ale,alipe bills ,nauli n.k ndo maaana vingi vinakua vimalaya Malaya
Binti anaejielewa hawezi kimbilia kupanga mapema hvyoo wakati ana wazazi
Anhaaa kwa hio kama anakaa mbali na wazazi wake ni ruksa kupanga?
 
Anhaaa kwa hio kama anakaa mbali na wazazi wake ni ruksa kupanga?
Unamjua Mkuu watu wana genaralized mambo hawajui Hali halisi za Watz hasa wakiwa mijini Kama Daslama mtu Ndugu anao yes lakini wapo hoi hata Sehemu ya kulala Hakuna achilia Mbali chakula

Demu/ Mwanamke kuamua kupanga ni startup nzuri ya kujitafta swala kuangukia Katika umalaya ni pale tu kukosa MAARIFA sahihi ya kujiendesha . Na tabia binafsi za mtu.
 
Hajadharau ila Kwa mtoto Wa kike kupanga kabla ya ndoa haileti picha Nzuri labda kipato kitosheleze au ufanye Kazi mbali na nyumbani
Kitamaduni zetu Binti anatakiwa atoke nyumbani ahamie Kwa mumewe TU
Mshahara laki 2 hautoshi Kwa Binti ,ale,alipe bills ,nauli n.k ndo maaana vingi vinakua vimalaya Malaya
Binti anaejielewa hawezi kimbilia kupanga mapema hvyoo wakati ana wazazi
Mbona vyuoni mnawaacha? Wanapanga Hostel za nje ya chuo. Mara wanapanga rooms?

Kama hujamrise well mtoto wako atakuwa malaya hapo hapo unapokaa nae. Akiliwa huko kazini utajua?
 
Sio wanawake tu, hata vijana wa kiume wakipata ajira hukimbilia zao kujitegemea.

Unataka uendelee kudharaulika nyumba za watu na tayari una access ya kipato?! Simama mwenyewe na mtu timamu anatakiwa awe na maamuzi hayo!
Wazo la kujitegemea ni zuri ila bado kipato inakuwa changamoto hivyo wengi wanaangukia kuwa kama wanajiuza , ni vizuri kushare room kama kuna ulazima wa kupanga ikiwa nyumbani ni mbali na kazini.
 
Anhaaa kwa hio kama anakaa mbali na wazazi wake ni ruksa kupanga?
Eehh km Kazi mkoani hukoo kupanga hakuepukiki dear,ila wote Dar mnakaa manzese Kazi anafanya tabata akae tu kwao
Na hata Kwa Ndugu sishauri Mtu akae km mfano umefika mkoani Bora km uko mbali na wazazi upange ila mkoa huo huo na sidhani Mtu anaeza hama mkoa Kwa Kazi ya laki 2 hizi private maana gharama za maisha ziko juu
May be kama wanampa malazi na Baadhi ya incentives
 
Unaidharau laki mbili?
Halafu hyo Laki mbili aliyoitaja Huwa hata haifaiki kwa Mishahara Yao.. kama kufagia maofisini ni 150,000/= kushuka chini.. So bado inakuwa ni pesa ndogo sana.. kama mdada mwenzie tu anayefanya kazi rasmi mshahara Laki 5 bado haimtoshi, huyo wa Laki na nusu lazima Alie njaa hadharani
 
😂 lakini kumbukeni hao wa laki na nusu hawana PAYE, NSSF, Bima nk
 
Back
Top Bottom