Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Ifike mahali mnaopinga masuala ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke mjifunze kujenga hoja zenye mashiko.Anataka mshahara kama wa mmuwe ila wakati huo kwenye kulipa ada za watoto na kutimiza majukumu ya kifamilia anataka mme ayabebe peke yake hela yake ni yakufanyia mambo anayo yajua yeye.
Anataka afanye biashara kama mmewe ila mtaji wa kufanyia hiyo biashara anataka apewe na mumewe na si kuhaso kuutafuta.
Kiufupi mwanamke na mwanaume hawawezi kuwa sawa kila mtu kapewa majukumu yake kutokana na maumbile yake tuache tabia ya kujifanya tunajua kuliko mungu aliye tuumba.
Hivi kuna mwanamke mfano ni mwalimu atataka kulipwa mshahara sawa na mume wake ambaye ni Daktari Bingwa, Mwanasheria, Professor au Engineer?
Huwa mnapata wapi mawazo kwamba wanawake walioolewa na wenye vipato vyao binafsi huwa hawachangii na waume zao
kuendesha familia zao? Wanawake mnaowaona wanakimbizana na makapu ya mboga asubuhi, wanakesha kufanya biashara masokoni, mama ntilie, wanaochuuza bidhaa stendi, wenye sugu za kulima n.k mnafikiri hizo pesa kidogo wanazopata ni kwa ajili ya make up na kuhonga hawara zao??
Tatizo lenu mkijizungusha na kuzinguana na vi-slay queens vichache mjini mnafikiri huo ndio uhalisia wa maisha makubwa ya raia wengi katika hii dunia.