Kuhusu mwanamke kuchangia majukumu ya familia ni hiyari yake na utashi wake alio nao ila habanwi na sheria yeyote ana weza akaacha na asifanywe chochote lakini kwa mwanaume anabanwa na sheria.
Usawa hauwezi kuwepo kati mwanaume na mwanamke kwa sababu hata kimaumbile hamko sawa acheni ujuaji wa kijinga.
Kama mungu angetaka mwanaume awe sawa na mwanamke basi angemfanya abebe mimba,apate hedhi,anyonyeshe,awe mwili mlaini kama mwanamke.
Mfano kwenye kuendeleza kizazi ni lazima mwanamke na mwanaume washirikiane ndo waweze kuleta mtoto duniani lakini ukiangalia katika jukumu hilo kila mtu amepewa jukumu lake, mwanaume kazi yake ni kumwaga mbegu tena kwa kupata starehe ndani ya dakika 3 tu, lakini mwanamke amepewa jukumu la miezi 9 iliyo jaa mateso na bado amepewa jukumu la kumsukuma huyo mtoto kutoka tumboni zoezi ambalo ni chungu kuliko kitu chochote duniani lakini bado akapewa jukumu la kumnyonyosha huyo mtoto miaka 2.
Huo mfano niliyo toa ni dhihirisho tosha kuwa mwana mke na mwanaume hawawezi kuwa sawa kimajukumu kwa namna yeyote ile hata mngerazimishaje.