joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 19,513
- 41,719
Hao wenyewe wazungu walio anzisha hiyo movement wenyewe hawaielewi ndio,ndio imewavuruga mpaka sasa ndoa zimedrop, Single mother wameongezeka stability kwenye familia hakuna, jamii yao imeendelea kwenye maswala ya Kisayansi ila kijamii inapotea.Pamoja na hili nafikiri kwamba ishu ya usawa wa kijinsia ilipofika Africa ilieleweka kinyumenyume au haikueleweka vizuri hasa ni jambo gani linalengwa labda kwa sababu ya uduni wetu wa Elimu na maarifa.
Watu wengi waliposikia usawa wa kijinsia walifikiri ndio hayo mambo ya kulipa bills/mahitaji ya familia sawa, kugawawanya kazi/ajira sawa nusu kwa nusu n.k Watawala nao waliharibu zaidi baada ya kutumia hiyo kama fursa ya kujaza na kupachika wanawake tu katika nafasi za utawala mfano viti maalumu kwa ajenda zao na maslahi yao binafsi.
Wengi hawakuelewa ajenda ya usawa hasa ilikuwa ni kuondoa ubaguzi, ukandamizaji na violence dhidi ya wanawake, kwamba watoto wa kike waruhusiwe kwenda shule na wawezeshwe kupata muda sawa wa kusoma na wale wa kiume ili hata upimaji katika mitihani uwe na uhalisia, kwamba wanawake wanapoenda kuomba ajira wasinyimwe kwa kigezo cha jinsia kama wanakidhi vigezo vingine
Hayo mambo sijui ya nani analisha familia zaidi na hata huo msemo wa 50/50 ni ujinga mtupu uliotokana na kushindwa kuelewa dhana nzima na lengo kuu.
Labda wewe Genius uwaeleweshe vijana dhana ya 50/50,ila mzungu mwenyewe imemvuruga na haielewi.