Kwanini wanawake wa Sasa wanapenda utawala 50/50 wakati huo wanataka kuhudumiwa?

Hakuna anaepinga usawa wa kijinsia kwa namna ilivyoongelewa na huyo uliomnukuu. Kama umemsoma mtoa mada between the lines. utagundua topic iliyopo mezani ni utilization of gender equality.

Haki zote kama elimu na ajira mshapewa lakini privilege ya provision mliyokua mnaipata wakati wa patriarch ndio hamtaki kuiachia. Hicho ndicho anahoji mtoa mada

Ukipewa elimu maana yake unajengewa uwezo wa kuyatafsiri mazingira na kuja na majibu ya changamoto zinazokuzunguka wewe binafsi pamoja na jamii kwa ujumla.

Ukipewa ajira maana yake automatically unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi. Utawajibika kujihudumia mahitaji yako mwenyewe na kuchangia chochote ambacho unatumia.

Sasa mwanamke apewe elimu halafu jukumu la kutafuta majibu ya changamoto zake lilibebwe na mwanaume. Mwanamke apewe ajira halafu mahitaji yake kifedha haudumiwe na mwanaume. Hapo ndipo usawa wa kijinsia unakua questioned. Kuna mantiki gani mwanamke kupewa hizo fursa? Hauoni kama hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali?

Wanawake hamtaki gender equality, isipokua mnataka selective equality. Mnataka kuchagua ni wapi na kwa namna gani muwe sawa na mwanaume,na hii ni ili muweze kubadilika kimsimamo kwa kuangalia masilahi yapo upi

Pale ambapo patriarch inawanufaisha mnaikana feminism, na pale ambapo feminism inawanufaisha mnaikana patriarch. Hamuwezi kuchagua kimoja for once and for all kwa sababu mnataka benefits za kila upande lakini sacrifices zake hamzitaki.

Fanyeni review ya usawa wa kijinsia mnaopigania ili ieleweke mnataka nini haswa. Mnataka kuwa complementor au competitor wa mwanaume?
 
THANK YOU,
Hii comment inatakiwa uongozi wa JF ufanye namna iwe kila mtu akifungua tu jamii forum anaisoma kwanza kisha anaendelea na mada zingine🥳🥳🥳🎊
Cookie
Moderator
 
Yaani mwanamke anataka mpaka pesa ya pedi lakini muda huo huo anataka urudi mapema nyumbani
Twende tukaoe Taliban Mzee wangu kule wameruhusu kuwachapa mpaka fimbo wakileta hizo 50 50 ni kipigo ila tu wasivunjwe kwa hio unagonga nakoz safi ila usimvunje sheria imeishia hapo

Ila Kiongozi wa Taliban amepinda
 
Mkuu hapa umeongea kwa hisia zaidi bila kuzingatia saikolojia ya mwanaume na mwanamke. In most cases katika mahusiano mwanaume anakuaga na kipato kikubwa zaidi ya mwanamke, hii ninkwa sababu ya hypergamy nature ya mwanamke.

Kwa mwanamke mahusiano sio feelings exchange tu, ni elevation pia. Main mission ya mwanamke ni ku-settle na mwanaume atakaempandisha hadhi au kumtatulia matitizo yake, ni ukosefu wa machaguo bora au demand ya mwanamke husika sokoni kuwa ndogo ndio kunamlazimu ku-settle for less. Ndio hao wauza wafanya kazi ngumu uliowaongelea.

Hypergamy and selfish nature ya mwanamke hiyo ipo wazi labda kama umeamua kuwa mbishi tu. Na hiyo ndio inayokuja kuleta mkanganyiko kwenye suala la usawa wa kijinsia. Tumeona wakina dada wanaojimudu kifedha mfano niffer nao wanasema hawawezi kuwa na mahusiano na mwanaume ambaye amuhudumii mahitaji yake.

Sawa tutampa mwanamke haki sawa na mwanaume ikiwemo suala la kuwa na kipato. Likija suala la kulipa bill will she defeat her selfish nature?
 
...."My persuasion can build a nation,
Endless power, with our love, we can devour,
They'll do anything for us,
Who run the world again?.....Women"
👑🎊🥳🤣
 
Hauwezi kuongelea haki sawa bila kujumuisha wajibu sawa,kwa maana hiyo masuala ya kulipa bill ni lazima yajumuishwe maana hiyo ndio end point of gender equality.

Kama tumeamua kuwapa fursa sawa mwanaume na mwanamke basi na majukumu ya kulipa bill yabebwe sawa. Mbona hiyo ni mantiki ya kawaida tu.
 
Anachomaanisha mtoa mada ni kwamba. Mtu ukishakua tegemezi hauwezi ukawa na nguvu ya kumpangia cha kufanya yule ambae unamtegemea.
Ninachofahamu mapenzi yakishafikia kupangiana tayari hao wapenzi au wanandoa wanakuwa wameshachokana na wanakuwa wanaishi pamoja ilimradi liende tu kwa sababu mbalimbali za kuogopa au kushindwa kuvunja hayo mahusiano. Watu wanaopendana na waliopevuka hawapangiani bali wanakubaliana na kuelewana.
 
Nakubali nakubali
 
Lakini kumbuka hayo majukumu ya nyumbani wanawake wanayapiga vita na kuyaita utumwa.

Ulichoongelea hapa umefanya rejea ya ndoa ya mwanaume na mama wa nyumbani. Vipi kuhusu ndoa ya mwanaume na career woman?
 
Anataka hela ya Pedi, kwani Mimi baba ake???? Haya ndiyo madhara ya kuweka Kibanda kwa mtoto wa kike, wewe unatakiwa kupiga na kusepa
 
Hypergamy iko hata kwa Simba na wanyama karibia wote.

Hata nje ya mahusiano na ndoa wanaume bado wana kipato kikubwa zaidi kuliko wanawake.

Huyo Niffer kusema anataka mwanaume mwenye pesa sielewi tatizo liko wapi, Kuna wanaume wanaosema wanataka wanawake bikira, wenye "mizigo", warembo, Darasa la saba, wasio single mothers n.k
 
Sawa tutampa mwanamke haki sawa na mwanaume ikiwemo suala la kuwa na kipato. Likija suala la kulipa bill will she defeat her selfish nature?
Sijui kwa nini huwa mnaongelea usawa wa kipato kati ya mwanamke na mwanaume wakati huo usawa hata kati ya wanaume wenyewe haupo!
 
Ana Run dunia ndio maana unamuhudumia hadi pedi, mbona mwanaume mwenzio huwezi kumnunulia condom?
Sasa hiyo K inayonunuliwa pedi ndio inagundua teknolojia, inajenga miundo mbinu, inagundua dawa za magonjwa n.k. Kuwa na akili hata kidogo tu. Halafu kuna siku nilikuambia ondoa hiyo title ya Dr. kwenye username yako maana unawadhalilisha wenye taaluma yao
 
Kwako nini maana ya haki sawa kati ya mwanamke na mwanaume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…