Hakika Wanaume wengi hawa wathamini inavyopasika Wanawake zao.
Kumbuka kutokana na kuzaa na kazi kazi Wanawake wanachakaa haraka kuzidi wanaume.
Nina marafiki zangu wengi tu wamewaacha wake zao baada ya kuchakaa na kuona Wanawake wengine vijana na warembo.
Hili linapelekea Wanawake wengi Kutafuta nguvu za Imani ili kuwarudisha waume zao katika upendo wa awali.
Hapo Wanawake hasa wale wa kiasili huwa wanaaamua kutumia maombi au waganga wa kienyeji.
Ndio maana unaona kwenye Makanisa Kuna waumini wengi wanawake. Na wengine huamua kwenda kwa waganga wa kienyeji.
Wanaume tuwathamini wake zetu tulio anza nao maisha.
Huwa wanaumia sana tunapo waonesha Upendo hafufu baada ya kuishi nao muda mrefu.