Kutembembea ni kujifunza ndo mnaita(exposure) ni kweli.
Ila kuna tofauti ya kujifunza alafu ukabaki mtupu na kujifunza ukaona fulsa zilipo.
Marekani ni dream land kwa masikini wakiafrica wanaishi kupigania green card ila kwa level za juu za kuelewa na kuchambua mambo bas nchi zilizoendelea zote hua ni shure alafu africa ni field ya shure yako.
NYERERE alienda nje kaelewa mchezo karudi africa kafanya jambo lake nalikatimia hakurudi katoboa pua wala kuvaa milegezo na kazikwa huko kwao kwa wazanaki.
MENGI kaenda nje kajifunza karudi home kafanya revolution kwenye media na kazikwa machame uko.
RUGE kazaliwa nje[emoji1] ingekua kina ww sijui kama wangekubal kubadiri utaifa wake[emoji1]#jokes, but alisoma akaona fulsa akarudi kaengeneza fulsa kwa mamia ya watu mpaka leo kwa exposure yake na kazikwa huko kwa wahaya kwa wazaz walikozaliwa.
Hawa ni mifano michache ya watu ambao tunaweza kuwapa jina la kisasa (WANYAMA) maana walikua na exposure yakutosha mali pia fedha lakini hawakua na ushamba wenu wakipa jina nchi yenu kua ni ARDHI YA LAAANA wa walio wengi wakishafika nje wanaanza kuvimbia watu na akili zao kulala kuamka wanawaza green card ili waendelee kupata easy money na kazi za welcome to America na ndo fikra zao hua zimeishia hapo.
Sio mbaya kwenda nje na hata ukiamua kuishi ni wewe ila unapoanza kuona wenzako walio baki kwenye nchi zao ni wapuuzi na wajinga unakumbilia sehemu ilotolewa jasho na watu zaidi ya miaka na miaka wakajitafuta wakajipata we ndo unaona raha kutembea juu ya ardhi yao na kutukania wenzako wanao ipambania ardhi yao nawao wafike walau robo ya izo nchi zilizondelea huo ndo ujinga wenyewe.
Kuishi Tanzania sio tatizo wala laana na kuishi nje sio akili wala mafanikio kila mtu yupo sawa kulingana na uwezo wake na namna yake yakuingiza kipato system ziko tofauti ila kilammoja anaweza kufanikiwa na kuenjoy maisha vile atakavyo akiwa mahala popote.
nikuulize we tokea umeishi huko US unaweza kufikia maisha anayoishi Diamond hapa bongo??? na uyu nimetolea mfano sababu bado ni kijana anaweza kupata visa ya kuishi nje akitaka na amejitafuta hapa hapa nchini kwake.
Wapo watu wengi tuu hapa bongo wanaingiza five 5m as profit perday kwenye duka tu la hardware bila kuangaika kabisa ukienda kariakoo wakinga wanaingiza zaidi ya izo ela kwenye kazi zao ila nyie mkifanya Uber uko mkapata 1M perday au kulea wazee mkalipwa 60k per hour ndo mnaanza kutukana watanzania wenzenu!!!! Ni ujinga na ushamba the bright one ataona matatizo hapa tz kama fulsa akiwa nje ila mshamba ndo anaweza kuona ni laana.
Tanzania yenye miaka 62 ya kujiongoza yenyewe Ingekuwa imepambaniwa na hao unao wasema, Leo hii mwaka 2023 kungekuwa hakuna haja ya watu kutamani kwenda Marekani na Ulaya.
Tanzania na yenyewe Ingekuwa na muelekeo wa kuwa kama ulaya na America. Lakini hata dalili HAIPO.
Hao ulio watolea mifano hawaku pambania maslahi ya Taifa, Bali Familia zao na kizazi chao. Labda wachache sana ndio walifanya hivyo kupambania Taifa.
Wapambanaji hao wangekuwepo tangu mwanzo, Tanzania ya leo isingekuwa na mifumo mibovu ya rushwa, wizi uhujumu uchumi, ubadhirifu wa mali za umma na kujilimbikizia mali.
Tanzania hakuna wapambanaji wa taifa bali kuna wachumia matumbo, mafisadi, machawa, wala rushwa na wajinga.
Wapambanaji hao wangekuwepo, Kizazi cha leo kisinge hangaika kwenda kutafuta Fursa nchi za ughaibuni, Kungekuwepo na mifumo mizuri ya upatikanaji wa fursa kwa kila raia kwa haki na usawa.
Badala yake upatikanaji wa fursa, unagubikwa na mifumo ile ile ya rushwa, wizi, kujuana na ufisadi.
Sasa, unataka watu waendelee kuvumilia huu ujinga?
Na watawala wa kiafrika ni vichwa ngumu, wasiotaka mabadiliko wala kukosolewa!
Acha watu waende ughaibuni angalau wakafaidi nguvu kazi za "Ancestors" wetu walio ijenga Amerika kipindi kile cha utumwa.
Hakuna Uzalendo kwenye umaskini na kwenye Taifa ambalo Wanasiasa na viongozi wa serikali wanapata Hela nyingi sana kushinda Viwanda, makampuni wafanyakazi, wafanyabishara na Raia walipa kodi.
Uafrika hasa utanzania ni laana.