Grill sio njia ya kumzuia kibaka endapo nyumba haina uzio.
Nilipanga geto mitaa ya Mecco South(Mwanza) nyumba ilikuwa haina uzio ila ina grills.
Siku nikawa nachati na kinokia changu double line huku nachaji. Kosa kubwa nlilofanya ni kuacha taa inawaka, maana usingizi ulinipitia, nilikuja kushtuka saa tisa usiku chaja inaning'inia simu haipo. chungulia uvunguni hola, cheki kitandani hola, Vibaka wakawa "wamelowa".
Asubuhi nikazunguka dirishani nikakuta wameniwekea line zangu.
Ikapita muda akaja ndugu wa mwenye nyumba akiwa na mkewe walikuwa wana safari, sababu walikuwa na mtoto mdogo anaumwa wakaacha taa inawaka, suruali ya jamaa ilivutwa na vibaka kwa waya toka alipotundika wakachukua hela ambazo walikuwa wazitumie wakati wa safari yao.