Acha chuki!
Ngoja nikulime swali!
Unakubaliana na Kikwete,Slaa, ama Mengi!?
 

Mushi:

Naona Rev. Kishoka amejibu mambo mengi ya kukata kiu. Lakini kwa sababu posti ilikuwa-directed kwangu ni lazima nijibu.

Mpaka sasa ujatoa data na ulizotoa ni definitions. Kuna tofauti kubwa sana kati ya data na definitions.

Kwa mfano ni kisema: GDP (Gross Domestic Product) ni thamani ya pesa ya vitu na huduma zilizozalishwa katika nchi fulani kwa muda fulani nitakuwa nimetoa definition tu na sio data.

Lakini nikisema kuwa ukuaji wa GDP ya Tanzania mwaka 2007 ilikuwa ni asilimia 7 hapo nitakuwa nimetoa data.

Definitions ni universal na zinaweza kutumika katika nchi yoyote na jamii yoyote.

Kwa mfano: definition yako ya poverty au welfare of a given society, unaweza kuitumia Marekani, UK, Uganda au Tanzania na validility ya defition hiyo bado ikaendelea kuwepo.

Kwa upande wa data, vielelezo vinavyokuja ni specific kwa sehemu fulani na wakati fulani.

Hivyo huwezi kujibu swali na Tanzania ni Tajiri au Masikini kwa kutumia definitions. Kwa sababu definitions hizo zitakuwa valid ukizitumia Canada, USA au China.

Swali la Tanzania ni Tajiri au Masikini unalijibu kwa data. Na data zote zinaonyesha kuwa TANZANIA ni masikini.
 
Haya basi unataka kusema kuwa hatujifunzi?

Wewe umezaliwa unajua kila kitu?

Na mimi nikuulize wewe ni mchungaji wa kanisa gani na una waumini wangapi?

Na uchungaji wako umeusomea wapi?

Pencil Mentality!

Kwa kuwa unaelekea kukataa kuwa mwanafunzi makini na unataka kuwa mjuvi, nitakuacha uendelee na hoja zako.

Unakumbilia kusema "hatujifunzi" badala ya "sijifunzi" ukitaka kutamkia umma kuwa majibu yangu ni kwa umma, majibu ni kwako wewe na si mwingine.

Jaribu kuwa objective na si ku-formulate opinions that are blinding and detremental to your character and personality.
 
Acha chuki!
Ngoja nikulime swali!
Unakubaliana na Kikwete,Slaa, ama Mengi!?

Sina chuki nawe, nakuombea heri na baraka nyingi katika safari yako. Kinachosikitisha ni wewe kufanana na CCM kukataa kukaa chini na kutafakari mambo na kusikia maoni ya watu.

Of the three names you named up here, which one is absolute clean that could be used as term of reference in being accurate, honest and sincere?
 

Kweli ustake ncheke!

Halafu we ndio ulikuwa ukisema eti "longo longo" Sasa hivho hapo juu ni nini?

Anyways nimehighlight and onceagain nitajaribu....


NAOMBA UZINGATIE RED HIGHLIGHTS KUTOKA KWENYE QUOTATIONS HAPO JUU!

Kila namba hapo chini inawakilisha namba iliyoko hapo juu...

1)Unajua kuna watanzania wangapi wenye malnutrition na wenye kufa kwa njaa ewe Bin Maryam?

2)Wenye realitive porverty ni wachache mno pengine less than 10% qualitative dimension haiko applicable hapa accross the board!

3)Na ndio maana kuna wazee wa vijisenti!(msisitizo kwenye red highlight)

4)Na hapo bado pia unataka darasa?

5)Bado hujaona connection hapo?

6)Huamini kuna mafisadi?

7)Meaning ya welfare hapa sasa tutaitafsiri accordingly kama namba 8 itakavyoeleza..

8)THEREFORE ITS THE WELFARE OF THE STATE THAT WE WILL PICK!
NOW BIN MARYAM YOU ARE THE ONE TO TELL ME WHATS THE WELFARE OF OUR STATE!
 

There are 10 types of people in the world. Those who know binary and those who don't. It happens that I don't.
 

Turudi kwenye mjadala Mchungaji!

Sasa kama mambo ni hivi..Hao kondoo unaowachunga kuna usalama kweli?
 
Mushi,

Nimetafakari hii hoja yako na kutaka kujua ni madhumuni gani uliyonayo au ulikuwa unatarajia majibu ya namna gani, lakini nitajaribu tena kujibu kwa kufuatia swali lako , Je Tanzania ni Tajiri au Masikini.

Umetupa Kikwete, Slaa na Mengi kama term of reference, mimi nitatumia statistics ambazo ni true facts na indicators, kisha ufanye uamuzi kibinafsi kama Tanzania ni Tajiri au Masikini.

Naomba tuwe scientific katika kutafuta majibu haya ili tuweze kuwa na njia bora ya kutafuta ama utatuzi au suluhisho la kusema Tanzania ni Tajiri au Masikini.

Zitto ametoa definition kuwa Tanzania ni tajiri kwa kuwa na vianzio vya rasilimali, ardhi na mali ghafi. Lakini pamoja na utajiri huo kama madini, vivutio vya utalii, maji, ardhi, gesi, mafuta na watu, Watanzania kama raia na binadamu ni masikini.

Hivyo ambiguity ya hoja yako itajibiwa kama nfano huo wa nnchi yenye mali na watu masikini.

Naomba tufanye juhudi tuangalie "data na facts" ambazo zitatupa takwimu/statistics za kutoa vipimo bora ili tupime "utajiri" na "umasikini" huu.

Nitaanza kwa kuleta nukuu kutoka CIA fact book, baadaye nitatafuta ripoti ya kwanza ya BOT ya mwaka huu, kisha kuangalia ripoti za IMF, World Bank na kisha UN/UNDP.

Nafikiria na natumaini tukienda kwa njia hiyo, basi tutakuwa na uwezo kujenga hoja yenye maana ili kuthibitisha ama Tanzania ni Tajiri au Masikini, ama tunaweza pindua tunge na kusema Tanzania ni nchi Tajiri au Masikini.

Kwenye fact book ya CIA, tutapata takwimu nzuri ambazo tunaweza kujipima na nchi nyingine duniani na hata kujua ni kwa kiasi gani tupo mbali kufikia zile takwimu za majumuisho ya dunia nzima.

Nanukuu

 
Nukuu inayofuata..


 
Tunaingia mambo ya uchumi na hiki ni kichwa cha habari na tathmini nzima kuhusu Tanzania. Ningependa ninukuu kila kitu, lakini nitaishia hapa kwenye hii general overview, kisha nitatoa kiambatanisho ili kila mtu aende na kuchangua takwimu na hasa za uchumi.

https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html


 
Nimekaa kama kawaida yangu baada ya kufanya kazi nzito ya kulijenga taifa langu nilipendalo kwa dhati naanza ku peruzi mtandao kwa kuangalia websites mbali mbali ili kujipa updates ya mambo ya dunia jinsi yanavyokwenda.

Katika pitia pitia ninaguswa na kutaka kujua jinsi nchi yangu inavyotambulika kimataifa ili niweze kujisikia zaidi kama mtanzania na nizidi kuongeza bidii zaidi ili nchi yangu iweze zidi pata sifa kimataifa, kwa bahati mbaya sana bila kutegemea wazo la kwanza linanijia niingalie nchi yangu katika nyanja ya uchumi inatambulika vipi na inaheshimika vipi duniani...moja kwa moja na kwenda kwenye google naanza kusearch kwenye ''The World's Poorest Countries'' nime search hapo kwa makusudi nikitaka kujiridhisha kwanza kwa kudhania kwamba huko hatuwezi kuweko hata siku moja..labda kunawafaa nchi nyingine zizongwazo na vita kila kukicha......Cha kushangaza nafungua kwenye website moja nakuta list ya nchi kumi..najitahidi kurudi chini na kuta nchi yangu niipendeyo kwa dhati tena ninayo jivunia nayo kila siku niikiimba iko kwenye nafasi ya nane..my God!!!!!!

Mwili unasisimka,natamani kulia,,siwezi...moyo unaniuma najiona mdogo..tena mdogo wa kudharaulika mbele ya watu ...Tanzania tuko kwenye kundi moja na nchi kama Somalia amba kila kukicha ni vita? Chad? hata Sudan nchi iliyojaa vita inatushinda kwa GDP????haipo katika orodha iyo...Uganda Kenya wote wanatushangaa tumefata nini uko..nani katupeleka???? naenda kutafuta source nyingine nikidhani labda hiyo source ya awali hawakutafuta data vizuri..lakini waapi..nakuta ni yale yale..kama 5 sources zinataja Tanzania ni among the Top Ten of the Poorest Countries in this world..( wamebase kwenye GDP-Gross Domestic Product na Percapital Income)

Sasa najiuliza..nani katupeka huku?????? Je ni :

1.Nyerere na sera zake za Ujamaa ndio zilikua sumu???

2.Au ni Viongozi wa baada yake ambao walishindwa kusimamia sera zake vizuri na wakaingiwa na roho ya tamaa ya kujilimbikiza mali na rushwa?????

3. Au ni sisi wananchi wenyewe tumeshindwa kufanya kazi kwa bidii tukaliongezea taifa letu pato badala yake tumekua watu wakuridhika,wavivu,mdomo mwingi kuliko vitendo,tusiopenda kusoma..ushirikina unaendekezwa kuliko maendeleo..starehe nyingi kuliko kazi..pamoja na vitu vingine vingi???

Na nini kifanyike basi walau tujitioe katika hiyo list ya aibu??sababu Kwa ukweli Tanzania hatu stahili kuwepo uko..kwa kutazama mali zote tulizo jaaliwa na mwenyezi mungu..

Nafungua mjadala wadau naombeni michango yenu....


NB Nimeongelea swala la uchumi tu..ukienda kuangalia kwenye sekta nyingine kama afya..napo tuko chini mno, kwa uchafu ndio tuko kwenye kundi la wale wanaoongoza...kila sifa mbaya sie..whyyy???????????????

Wakunyuti Inc@
 
Poor Country, Rich Country
by Ari Armstrong

Following are a few contrasts between poor, developing, and rich countries. These are generalizations, so of course they admit exceptions. Still, I thought they were pithy. I'll consider this a work in progress, so if I think of additional points, or of somebody else sends along good suggestions, I'll add them. -- Ari Armstrong, January 19, 2005

In a poor country, many people lack jobs, or they are too weak to work hard because they lack adequate nutrition and medical care. In a developing country, people work as hard as they can and scrape to get by. In a rich country, people come home from well-paying, generally pleasant jobs and then pay to physically exert themselves at gyms.

In a poor country, people get sick from drinking the water. In a developing country, people can afford to put the toxin chlorine in their water to kill the germs. In a rich country, people can afford to take the chlorine out of the water before they drink it.

In a poor country, people try to eat as much fat as they can. In a developing country, people are able to eat as much fat as they want. In a rich country, people pay extra to eat less fat, fake fat, and special kinds of fat.

In a poor country, the poorest people in society often die from disease, starvation, or crime. In a developing country, the poorest people in society can, with good education, rise to the middle class and afford the basics of life. In a rich country, the poorest people in society often own an automobile, live in a comfortable house or apartment, and watch cable television on color sets.

In a poor country, children feel lucky if they can work. In a developing country, children are happy if they can attend school rather than work. In a rich country, children often complain about school because they can't even imagine an impoverished life.

In a poor country, people sometimes let animals scavenge for food. In a developing country, people meet the basic needs of their pets. In a rich country, people take their pets to schools and psychotherapists, put them on diets, and buy them Christmas presents.

In a poor country, socialists make people poorer and don't bother to try to justify their policies. In a developing country, socialists claim their policies will make people richer, even as free markets are accomplishing that goal. In a rich country, the socialists admit their policies will make people poorer, and proclaim that to be a virtue, even as they enjoy the wealth generated by economic liberty.

In a poor country, people are often restrained because of their genetics or place of birth. In a developing country, many people are able to profoundly improve their lives. In a rich country, people generally are able to determine the course of their own lives and pursue values mostly free from political impositions.

The Colorado Freedom Report--www.FreeColorado.com
 
Mawazo yote ni mazuri wakuu..Na mimi nilikuwa nimebanwa kwenye threads nyingine ila bado nategemea kundelea na pale nilipoishia!
 
Ndugu zangu ni wazi nilipoanzisha thread hii niliona kuwa tutafikia mahali ambapo mijadala kuhusu rasimali zetu itapamba moto...

Hii pia ni kutokana na hizi kashfa za UFISADI zilizoigubika jamii yetu hii.
Nilipoianzisha thread hii...

Nilijuwa kuwa mjadala unaweza kuelekea kule ambako wengi wetu hatukutegemea.

Kwamba wengi wetu sisi wananchi tulikuwa tumeridhika kabisa kuwa sisi ni masikini na hivyo hatuna la kufanya zaidi ya kusubiri Muungwana asafiri huku na kule kutuombea sisi wakosefu misaada ili walau tupate cha kuweka kinywani licha ya kwamba tunagundua kuwa kuna wengine ambao wanakufa kabla ya kuipata bahati hiyo ya mlo ili waendelee kuishi na kusubiri tena hadi hapo safari nyingine itakapopangwa na Muungwana ambaye kila kukicha mnaelewa Salva anawakilisha.

Kitu ambacho sikutaka kusahahu ni kwamba wananchi sasa wanapotajiwa hayo mabilioni ya pesa viongozi wetu waliyoyachota na kuanza kusema eti ni vijisenti...Ni kauli zilizopelekea mshituko na mswali mengi kwa wananchi...Halah...Kumbe na sisi ni matajiri?

Swali nalowaachia ndugu zangu ni moja...
Ni viongozi wapi wazuri zaidi?

Wale wanaosema sisi ni masikini huku mabilioni yakifujwa ama wale wanaosema sisi ni matajiri na utajiri wetu sasa utatukomboa?
 
Tumeshagundua Tanzania ni TAJIRI NA KIKWETE ANATUDANGANYA KWASABABU NA YEYE NI MAFIA MFISADI!
 

Watanzania pia msisahau kumwuliza kiongozi yeyote kabla ya kumpigia kura swali hili....TANZANIA NI MASIKINI AMA TAJIRI?

Atakayejibu kwamba Tanzania ni masikini...MSIMPE KURA!

Atakaye sema TANZANIA NI TAJIRI...HUYO MUMPE KURA...LAKINI KWA SHARTI MOJA...AWAELEZE NI KIVIPI UTAJIRI HUO UTAWALETEA KAZI, BARABARA,HOSPITALI,SHULE,MAJI,CHAKULA NA UHURU WA KUJIAMULIA NJIA SAHIHI ZA KUJIPATIA MAENDELEO.

HUYO ATAKAYEWAELEZA HAYO...BASI HUYO NDIYE KIONGOZI WETU.
 
Hali ya umaskini nchini imeendelea kuwa mbaya. Mimi nilifikiri huu mwaka hali ya maisha ingekuwa ni rahisi sana. Mwelekeo wa huu mwaka unaonyesha dalili mbaya.Ukabaji umeongezeka kila mahali, vijana wa kike na wakiume wanajiuza kila kukicha. Mambo hayo yote yanatokea kwa sababu watu wengi bado wanafikiria mwaka mpya. Watu hawajajipanga kuhusiana na usalama wa watu na mali zao. Je nini kifanyike?
 

Ni kweli unachokisema. Nchi yetu ni tajiri sana karibu kwa kila kitu ila tuna viongozi ambao wanahujumu utajiri wetu kwa kushirikiana na watu wachache wenye hela.

Mfano, sekta ya madini tu ingeweza kutuinua kwa kiasi kikubwa sana lakini ni kama hayapo. Mbuga za wanyama na hifadhi za taifa nazo fedha zake hatujui zinaendaje na pia uangalizi wa mbuga na hifadhi hizo hauridhishi. Tuna Bahari ya Hindi, maziwa na mito mingi hapa nchini lakini wapi.

Kilimo ni uti wa mgongo na kila mwaka tunasikia bungeni "Wananchi waondokane na jembe la mkono" lakini nacho ni kichekesho tu. Kwani wasipotumia jembe la mkono, mfano, kule Ukerewe, ambako, si rahisi mtu kupata hata nusu ekari watatumia nini, trekta kwa nusu ekari?

Ukusanyaji wa kodi nao sidhani kama unafanywa kikamilifu. Kuna baadhi ya makampuni yanakwepa kodi lakini serikali ama inayalea au yanaizidi akili. Uchunguzi unatakiwa kupitia wafanyakazi au hata mamlaka husika. Baadhi ya watu hawawajibiki kiasi cha kutosha na ndiyo maana tunapata hiyo shida.

Tunatakiwa tubadilike - tuipende nchi yetu na kwa kufanya hivyo tutaweka usimamizi mzuri wa vyanzo vyetu vya mapato na kuvisimamia na hivyo kuanza kukuza uchumi wetu.

Kila kitu kinaonekana kuwa njia panda na hata kama Watz wakisema mambo yanayowakera wanaambiwa wanakalia kulalamika hawafanyi kazi kiasi cha kutosha. Watakuwaje na moyo wa kufanya kazi wakati wanaona wanaibiwa bila huruma? Si kwanza huo wizi ukomeshwe ili pamoja na kufanya hiyo kazi matunfda yake yaonekane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…