FaizaFoxy;3288597]0-5 hawafi kwa umaskini, wanakufa kwa Malaria na Ukimwi.
Inflation isikustuwe sana, hata mataifa makubwa duniani yana matatizo ya kiuchumi, tena sisi tunafanya vizuri kuliko wengine, tuna GDP ya 6.3 kwa mwaka uliopita..Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu
Ndugu yangu, Umasikini ndio tatizo kubwa linaozaa Malaria, ukimwi, surua, kifaduro, malnutrition n.k. Sijui kama unapitia majarida kama ya WHO uone dunia inafanya nini a inasema ni ni kuhusu poverty.
Nina maana ukizungumzia ukimwi,malaria n.k vipo under the umbrella of poverty.
GDP 6.3!! bajeti 40% misaada. Unawezaje kusema GDP inakusaidia wakati hujaweza ku balance bajeti. GDP is just a number, jiulize kwanini watu wamekuwa wakali na wenye uchungu sana, halafu mwangalie mtu wa kawaida pale kariakoo ndio uone kama GDP inamsaidia.
Kuhusu madini, Mwalimu aliwahi kuulizwa akajibu hivi ' madini hayaozi yaacheni yakae hapo watanzania watakapokuwa tayari watayachimba'. Sijui dhahabu ile ya Buzwagi inasadiaje yule mpanga nyanya wa kariakoo!! Hivi huoni wizi wa mchana wewe unaaamini madini yanamsaidia Mtz
Kama unaamini tunaenda vizuri mungu akusaidie naakufungue macho Inshallah, hilo lipo juu ya uwezo wa wengi
FaizaFoxy;3288624]Kujenga reli ni long term projects na zinafanyiwa kazi na hilo linajulikana au hujui hilo?
Kujenga viwanja vya ndege ni short term projects zenye tija za haraka haraka. Tumeshindwa kuendesha reli mbili na tumeacha huduma zake zimekufa kwa kuwa tu kila mtu anajuwa ni mali ya umma kwa hiyo aibe atakavyo. Huo wakati umekwisha, reli itajengwa kwa uwekezaji wa binafsi,.
Hiyo mikoa haikuitwa big four kwa ajili ya reli, wacha kupotosha, huko ni rutuba na ardhi inayokubali kilimo ndiyo iliyofanya iitwe hivyo
Reli ipo katika mipango 50 ya JK? Yeye si amepita akiahidi kila kijiji. Hivi na reli ni sehemu ya mkakati wa Kikwete wa kugeuza Kigoma iwe Dubai!! Ehhe Mola
Hujajibu jibu swali la Mcahmbuzi. Mwaka 1985 tulikuwa na Km Kadhaa za reli, leo zimepungua Km 1844. Zimekwenda wapi? Halafu unang'oa mataruma kwa kushirikiana na Wahindi kwa njia za ufisadi wizi na uporoji anamwaninisha FF kuna mipango.
Hivi kipi rahisi kuweka mabehewa juu ya reli au kung'oa mataruma na kuwakabidhi Wahindi halafu uwe na mipango ya kujenga reli kama 'long term plan'
Badala ya kuwa na short term plan za kumsaidia mtanzania asife na njaa ili hali mahindi yanakwenda Kongo, unafikiria short term plan za kusafirisha maua na shanga! Ukiulizwa maua ni tani ngapi kwa mwaka hujui lakini upo kisutu sokoni unatafuta mchale na mahindi ya Mbeya.
Kwako kusafirisha Rose ndiyo sehemu ya kukua GDP! sio kumsaidia Mtanzania wa kisiju. kariakoo, Maneromango, Msanga ngongele, Ikwiriri, Saadan, Bigwa mwarusembe, Nyamato, Kimazichana, Mkamba, Kivinje n.k.