katika swala hili nadhani yalikuwa makosa makubwa kuanza na kitambulisho na mpigakura kabla ya kitambulisho cha uraia..Kitambulisho cha uraia ni muhimu sana ktk jamii yoyote ya Utaifa na watu wake wakati kitambulisho cha Kupiga kura ni kwa wale tu wanao qualify kupiga kura...Na hata passport ni muhimu tu kwa wale wanaotaka kusafiri lakini kitambulisho cha uraia nina maana kubwa zaidi ambayo inaweza kuweka mfumo mzuri wa kiuchumi..Tuangalie vipi MIRADI yenye nia nzuri imamuongezea Mtanzania UMASIKINI
Mfano katika miradi mikubwa ambalo taifa linayo ni huu wa kitambulisho cha TAIFA. Je tunaweza kueleza huu mradi
Nauliza maswali haya sababu Nkisikia faida viongzi wanazosema juu ya faida za kitambulisho cha taifa unaon wengi wako misinformed. Sasa ukichanganya na gharama zake alafu ukaona kuwa tayari ni kama duplicate ya kitambulisho cha mpiga kura. ndio nashindwa kuelewa
- utamfaidisha vipi mwananchi ?
- Utasaidia kuandoa kero gani upande wa wananchi au serikali?
- kitambulisho cha Taifa na Passport na Kitambulisho cha mpigakura vina tofauti gani? I mean kwa Seriali isngefanya maboresho ya Kitambulisha cha mpiga kura kiwe kitambulish cha taifa
- Ni nchi gani uniani ya mfano ina kitambulisho cha Taifa na kinatumikaje ?
I mean nini kilizua kuboresha kitambulshi cha mpigga kura kuwe itambulisho cha taifa.
Tuna serikali moja lakini kila idara inaweza kutengeza system ya kitu kile kile amacho kipo idara nyingie tayari. So kesho Tarffic police wakitak kuwa na system ya number plate za magari yote Tanzania wanaanza mchakato mpya kabisa kama vile TRA hawana system hiyo.
Ili kupunguza umasiikini kuna miradi kwenye idara nyingine ni Redundant au duplicate . Idara za serikali zinatakiwa ushare taarifa.
Na kwa kigezo hicho kitambulisho cha mpig kura ndio kilitakiwa kuboreshwa kiwe kitambulisho cha taifa.
I mean kama kuna mjuvi anayeelewa How kitambulisho cha taifa kinaweza kumsaidi mtanzania katka kufight UMASIKINI au kurahisisha jambo fulani anijuze. Isije ikawa ni miradi ya kuiga na sisi tuonekane tumo kwenye karne ya TEKNOHAMA bila faida yeyote
Leo hii tunashndwa kutoa takwimu vizuri za makusanyo ya kodi kutokana na kutokuona umuhimu wa kila mtu alipe kodi na ndio maana chini ya asilimia 10 ndio wanalipa kodi nchini. Tumeshindwa hata kuweka idiadi kamili ya Unemployed, hatufahamu ulazima wa kusajili mashirika au hata biashara tunazozifanya ili kujenga mazuri baina ya uraia wetu na serikali yenyewe..
Kinachonitatizo mimi haswa na nchi yangu ni kwamba hakuna kitu kinachopangwa bila kuwepo sababu ya UFISADI..Na ndio maana husema kila siku ya kwamba hatuwezi kuendelea kufikiria kulijaza pakacha ambalo lina tobo. Juhudi zote za kupata mikataba bora, kuongeza uzalishaji haziwezi kufanikiwa ikiwa tunashindwa kuziba ufa kwanza..Kwa hiyo kwa kila tunapoweka mikakati bora ya kuboresha uchumi ni sawa na kutumia nguvu nyingi bila maarifa kutambua kwamba pakacha lina tobo (mirija) ambazo zinatakiwa kuzibwa kwanza ili tupate kujaza ndoo..Kwa wale wanaohesabu makuzi ya uchumi wetu kina IMF wao wanatazama ni ndoo ngapi tunazipeleka kwa mwaka ili hali hawajali kama zimejaa au laa..