Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
prof shivji alishawahi kuandika njia za kuendeleza uchumi wa nchi na kuepuka umaskini, alisema lazima kuwa makini na sekta ya kilimo lakini kilimo bila viwanda bado ni kazi bure kwani mkulima alimapo na baadae kupangiwa bei ya mazao ni bure. bali akilima vya kutosha na kuwa na soko la kutosha ndani ya nchi na nje ya nchi lakini pia serikali lazima iingilie kati inapokuja swala la biashara kati ya taifa letu na jingine na serikali ihakikishe faida inapatikana kwa taifa kwa kumuwezesha mkulima kuuza mazao yake nje.
lakini kukiwa na malighafi za kutosha na uzalishaji viwandani utaongezeka ajira zitapatikana kwa urahisi zaidi pato litaongezeka kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

hivyo basi kwa ufupi kilimo cha ukweli = food&materials -processing industries-manufacturing industries=employment&increase of govt income. goods produced create market inside and outside= trade

kama kuna kilimo cha kueleweka chenye lengo la maendeleo basi barabara umeme maji mawasiliano vitaboreshwa. viwanda navyo vijengwe karibu na mashamba hayo. watu wendao kufanya kazi huko watataka huduma hivyo masoko,hospitali,na huduma zote za kijamii zitasogea. kwa jinsi hii miji itapanuka na taifa litafaidika.hivyo kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kilimo na viwanda na maendeleo

hali ilivyo sasa nchini kwetu
kilimo hakijazingatiwa kiwe kilimo cha maendeleo wananchi bado wanalima kwa ajili ya chakula na kidogo kwa ajili ya biashara. serikali haijaamua kuzalisha katika sekta ya kilimo . hakuna viwanda vya kutosha hivyo wakulima bado wanateseka kupangiwa bei na watu wa nje. kwa sababu hakuna kilimo cha maendeleo bado vijijini hakuna miundo mbinu ya kutosha na kila mtu kukimbilia mjini. bado sisi tunasema kilimo ndio uti wa mgongo, kilimo kwanza?????????? wapi hatuko serious kabisa na maendeleo wa na hicho kilimo chenyewe
 
Jmushi1,
Statements zote ni sahihi, Tanzania na Afrika kwa ujumla ni tajiri kwa maana ya resources kama ardhi, madini, mafuta nk. Lakini watu wake ni maskini kwasababu tumeshindwa kutumia akili zetu kutengeneza added values kutoka kwenye hizo resources zetu.

Umaskini uko kwenye vichwa vyetu, akili zetu, fikra zetu nk. Hata tukipata uongozi bora sana bado itachukua miaka mingi kwa Watanzania kuwa matajiri. Ni rahisi kubadili uongozi lakini ni ngumu sana kubadili culture ya uvivu
na kutokuwajibika ambayo imejengeka Tanzania na Afrika. Sisemi Waafrika ni wavivu, maana wakija huku nje wanajituma kweli kweli.

Culture yetu ndio ya kimaskini, culture ya kukimbilia majibu rahisi na common sense. Culture ambayo haitufanyi tukae chini na kuwaza nje ya our comfort zone. Kuibadili hii itatuchukua muda mrefu sana na juhudi kubwa mno kuanzia level ya individuals mpaka kwenye viongozi wa nchi.

Ndio viongozi wa Afrika wameiba mabilioni ya resources zetu lakini mimi siamini kama ndio chanzo cha umaskini wetu. Matatizo yetu yanaenda ndani zaidi. Mwalimu Nyerere alijaribu kushughulikia kiini cha matatizo ya Watanzania lakini bahati mbaya akachagua siasa mbaya na chama kushika hatamu mpaka ikafikia mahali ambapo hakuwa challenged na hivyo kudumaa kama viongozi wetu wengine
Mkuu Jmushi1, narudi kule nilikoanzia ya kuwa uongozi ndiyo chanzo cha umasikini na wala sio culture. Kama kuna watu rahisi sana kuwabadilisha kwa culture ni Watanzania.
Tunayo mifano kama ya Nyerere, yeye alikuwa mkali kiasi kwamba pesa ikidhamiriwa kujenga shule au kituo cha Afya itafanyika hivyo. Haina maana ulaji haukuwepo, la hasha! tofauti ni kuwa mlaji alijua kuwa hatima yake ipo matatani.

Yupo Sokoine na tunakumbuka mambo aliyoyafanya.
Augustino Mrema hakutumia hata senti tano kuwaambia watu wa soko la kariakoo kusafisha na kujiwekea utaratibu.
Keenja yeye alikaa kidete na jiji hadi tukaona japo vibara bara vya watembea kwa miguu vinasakafiwa, jiji linakuwa safi.
Paseko Kone yeye alisimama na kuwaambia wana singida itajengwa hospitali ya kisasa na imejengwa kwa kiwango alichoweza yeye.

Nimetoa mifano hiyo kuonyesha kuwa hakuna culture ya kudumu ili kuna culture inayolelewa.
Mifano ipo mingi sana na orodha ni ndefu ya viongozi hadi ngazi za wailaya waliojaribu japo tukaona.

Huwezi kuondoa umasikini kama hakuna nidhamu. Leo CAG anasema mabilioni yanayoweza kuedesha wizara yametafunwa na hakuna kiongozi yoyote anayohoji hatua gani zimechukuliwa ili kuziba mianya na wahalifu kuadhibiwa.
CAG amebaki kukabidhi ripoti katika televisheni na magazeti.

Hakuna kiongozi anayejiuliza je tunatumia tunachozalisha au tulicho nacho? Kwasababu hawaulizi na wameamini kuwa kuna wafadhili watatoa 40% ya bajeti, mipango iliyokichwani ni fenicha na VX achilia mbali kulamba pesa kwa njia haramu. Nusu karne hatujaweza ku-balance bajeti lakini unasikia ya akina Makinda na kujiuzulu kwa wabunge

Hakuna kiongozi anayetoka asubuhi akiwaza atawasadiaje watanzania wajikombea. Kama yupo nitashangaa kwasababu haiwezekani mahindi yaoze Sumbawanga halafu katibu mkuu au waziri anatia sahihi mkataba wa kuletewa mchele na mahindi kutoka korea. Hawana hata aibu sasa wazo la kuondoa umasikini watalipata wapi.

Culture ya uvivu na kutowajibikaji inajengwa na viongozi. Kwanini mfagizi wa ofisi awe muungwana sana na aache kuuza maandazi kama mbunge anayepokea milioni 12 kwa mwezi bado anaona maisha magumu.
Kwanini nimshataki afisa aliyeiba laki 3 kwa kufoji halafu Jairo astaafishwe na marupu rupu juu.

Nimalizie kusema, hoja yangu ni kuwa hata kama una vitu na rasilimali zote kama hakuna wa kuongoza namna ya kuzitafuta, kuzikusanya, kuzipangia na kuzigawa ili ziwe na tija hakuna chochote kitakachofanyika.
Mkuu Mkandara kasema sisi ni kama wamasai wenye ng'ombe 3,000 lakini hana mahali pa kulala.

Angalia sehemu zote duniani zilizopiga hatua, chagizo kubwa ni uongozi.
Naamini kabisa umasikini wetu unachangiwa na uongozi kama chanzo mengine ni sehemu tu ya tatizo.
 
Nimeuliza hilo swali kwa sababu ni lazima tutofautishe nchi masikini ambazo hazijawahi kuwa na maendeleo, na nchi masikini ambazo tayari zilichawahi kuwa ya namna fulani ya maendeleo lakini kutokana na sababu zinazoeleweka na zisoeleweka zinarudi nyuma na kuwa masikini.

Kuhusiana na umasikini wa Tanzania kuna mambo mengi. Moja ya matatizo hayo ni watanzania kuambiwa kuwa wao ni masikini kwa kutumia mtazamo wa jamii zingine. Hivyo umasikini ni relative term. Ukienda Bagamoyo, unaweza kumkuta mtu na minazi yake 1000 ambayo inatosheleza mahitaji yake. Katika jamii yake yeye ni tajiri, lakini kwa sababu utajiri wake hau-meet your definition utamwita masikini.

Vilevile maisha ya mmasai mwenye ng'ombe 500, yataitwa ya kimasikini kwa sababu tu mfumo wake wa maisha ni tofauti na wa kwako.

Hoja yangu sio kutetea watanzania. Lakini Tanzania ikitaka kuondoa umasikini na kuboresha maisha ya watu ni lazima iwe na definitions za umasikini.
Lakini mkuu wangu huopni hii ya Mmasai mwenye ng'ombe 500 inafanana na Tanzania yenye rasilimali kama dhabau, gas na ardhi yenye rutuba?..Kuna watu wana mishahara mikubwa sana lakini familia yake inaishi ktk hali mbaya sana.. Je hawa utawaita vipi?..Utajiri siku zote unasomeka pale unapofanya kazi kwenye mabadilishano kama vile huwezi kudai huna njaa kwa sababu kipo nyama ndani ya friji na gunia la mchele. Umaskini wetu ni sawa na njaa na hatujui/hatutaki/tunapuuza/ulimbukeni na kadhalika ktk kupika chakula kuondoa njaa hiyo..Hakuna definition zaidi ya hiyo.

Nyani Ngabu,
Mkuu tupe wewe sababu zake na sio ile ya Miafrika ndivyo Tulivyo! nadhani kubadilishana mawazo kunaweza kuchangia sana tukubali makosa au mapungufu yetu.
 
Nyani Ngabu, Mkuu tupe wewe sababu zake na sio ile ya Miafrika ndivyo Tulivyo! nadhani kubadilishana mawazo kunaweza kuchangia sana tukubali makosa au mapungufu yetu.
succinct!
 
Lakini mkuu wangu huopni hii ya Mmasai mwenye ng'ombe 500 inafanana na Tanzania yenye rasilimali kama dhabau, gas na ardhi yenye rutuba?..Kuna watu wana mishahara mikubwa sana lakini familia yake inaishi ktk hali mbaya sana.. Je hawa utawaita vipi?..Utajiri siku zote unasomeka pale unapofanya kazi kwenye mabadilishano kama vile huwezi kudai huna njaa kwa sababu kipo nyama ndani ya friji na gunia la mchele. Umaskini wetu ni sawa na njaa na hatujui/hatutaki/tunapuuza/ulimbukeni na kadhalika ktk kupika chakula kuondoa njaa hiyo..Hakuna definition zaidi ya hiyo.

Nyani Ngabu,
Mkuu tupe wewe sababu zake na sio ile ya Miafrika ndivyo Tulivyo! nadhani kubadilishana mawazo kunaweza kuchangia sana tukubali makosa au mapungufu yetu.

Mkandara,

Nipo hapo Marekani kwa sababu ya ubora wa maisha na sio utajiri. Na ubora huo ungepatikana Tanzania, labda hata wazo la kuja Marekani lisingekaa kichwani.

Utajiri na umasikini ni relative terms. Cha muhimu ni ubora wa maisha. Hivyo Mmasai mwenye ng'ombe 500 ambaye anajisikia kuwa tajiri katika jumuia yake, akishindwa kufikia ubora wa maisha fulani basi utajiri wake usiwe na maana.

Vilevile mfanyakazi wa benki mwenye kulipwa pesa nyingi ambaye anajenga jumba la kifahari sehemu yenye mbu wengi, usafiri mbovu, maji machafu, umeme wa taabu, naye kipato chake kinakuwa hakina maana.

Tukija kwa nchi. Nchi zinaitwa tajiri kwa sababu serikali za nchi hizo zinaweza kutumia kipato kufanya maisha ya wananchi wake kuwa bora. Kwa mfano kujenga barabara nzuri, kusambaza maji n.k.

Tukirudi kwa nchi masikini. Serikali zake hazina kipato cha kuboresha maisha ya wananchi wake au kujenga miundo mbinu itakayofanya watu wanufaike.

Kitendawili kilichopo Tanzania kwa miaka mingi ni jinsi gani serikali itaongeza kipato chake hili kuboresha maisha ya wananchi. Kwa sasa hivi njia kubwa ya kukusanya mapato ya serikali ni kodi ya bidhaa, misaada kutoka nje, biashara ya utalii, uuzaji wa rasimali za nchi n.k

Mapato haya peke yake hayatoshi kufanya maisha ya mtanzania yawe sawa na wengi tunavyotaka. Pamoja na hayo waendeshaji wa serikali sio wabunifu kutumia kile kidogo kinachopatikana ili kilete tija kubwa kwenye kuboresha maisha ya mtanzania.

Kwa mfano serikali imejenga mashule ambazo elimu ya wahitimu wake haina mchango wowote kwa taifa kwa sababu ni elimu duni. Hivyo badala ya kufanya investment, serikali inapoteza muda na resources. Vilevile muundo wa serikali una watendaji wengi ambao hawana ufanisi wowote hule. Mishahara ya watumishi hao sio investment yenye manufaa kwa taifa.

Kwa maoni yangu binafsi, Tanzania inaweza kuendelea kwa kasi sana iwapo matumizi ya serikali na binafsi yatalenga kwenye kuleta tija na ufanisi. Na vilevile hili kuleta tija, umasikini lazima upatiwe definition kwa ngazi ya taifa hili ijulikane nani tayari amevuka ubora wa maisha na nani anatakiwa kusaidiwa.
 
Wadau
Kila kukicha asubuhi najiuliza swali "Kwa nini Tanzania ni Masikini kama tulivyo". Swali hili linanitatiza sana. Nasikia tuna migodi mikubwa tu ya Gold, Diamond, n.k. Tuna sehemu kubwa ya Ziwa kubwa kuliko yote Africa (Ziwa Victoria). Tuna ziwa lenye kina cha jini kuliko yote duniani (Ziwa Tanganyika). Tuna sehemu kubwa ya Bahari ya Hindi (Nchi nyingi zinalilia bahari). Tuna mbuga kubwa za wanyama na vivutio vingine vya utalii.
- Ni jinsi gani tunatumia hizi mali tulizonazo kujikomboa katika umasikini?
- Je tatizo ni viongozi tuliowahi kuwa nao na tulionao sasa hivi?
- Je tatizo ni sisi wananchi?
- Je tatizo ni rangi yetu?
- Je tatizo ni utamaduni wetu?
- Je tatizo ni mfumo mzima?
- Au je tatizo ni kuona kwetu na kufiria kwetu na kutojua maana ya maendeleo ni nini?

Sikubaliani na jibu la kuwa hatuna pesa. Nina imani kubwa nchi yetu kama serikali ina pesa za kutosha za kuleta tofauti kulinganisha na tulivyo. Nimetembelea nchi tofauti Africa, Ulaya na Marekani na nimeona tofauti kati ya nchi ILIYOENDELEA na nchi INAYOENDELEA. Nchi yetu kwa kweli bado hiko nyuma sana.
Kila nikipata kuendesha gari katika nchi za Ulaya i.e UK, huwa najiuliza swali, HAWA WATU WALIJENGA HIZI BARABARA LINI? Hizi ni barabara kuu (Motorways) na barabara ndogo (A & B) na hata barabara za vijijini. Watu Ulaya wanaosha magari yao mara moja kwa mwezi, si kwamba ni wachafu ila gari linakuwa bado safi kwani halijapita kwenye vumbi au matope. Sisi tulimkosea nini Mungu mpaka kila kukicha houseboy lazima aoshe gari kabla baba hajaondoka?

Mfumo wa reli (London Underground) ulianza kujengwa mwaka 1886. Je sisi sasa hivi hatuna akili ya Mzungu wa miaka hiyo? Je hatuna pesa kama walizokuwa nazo waingereza mwaka 1886? Kwa nini hata leo hii tunashindwa kubuni mbinu za kuondokana na foleni hapa Dar. Nina uhakika tukiwa na mfumo wa usafiri kama waliokuwa nao wenzetu miaka 75 iliyopita tutakuwa tumepiga hatua kubwa.
Kwa nini tunashindwa? Naomba msahada wa majibu.
 
Ina maana inaliwa na viongozi? au wawekezaji tunaokaribisha?
 
Miafrika Ndivyo Tulivyo. - Nyani Ngabu
 
Mkuu matatizo nimeyahighlight hapo juu...Hivi inaingia akilini eti unamchagua mtu awe kiongozi kisa handsome? Sisi wananchi tuna matatizo sana. Pili ni mfumo mzima hasa rushwa ndogo na kubwa..siasa kila kona hata kwenye mambo muhimu yanayohitaji umakini wa hali ya juu..pia kuwekana kindugu kwenye nafasi nyeti za uongozi na kulipana fadhila!!!! Inabidi tubadilike sana..elimu ya uraia inahitajika hasa kwenye jambo la kupiga kura na kuchagua viongozi bora wenye vision ya miaka 50 ijayo.
 
Basi kama tatizo ni sisi Wananchi na Mfumo mzima kazi ipo. Inabidi kila mtu asali kwa imani yake tuweze kuwa na maono watu tuweze kujua maana ya maendeleo na tujue kuwa inabidi tuangalie Plan B kwa kuwa plan A imeshindwa
 
Nchi yetu ni maskini kwa sababu idadi kubwa ya raia wake kama wewe hawajui kwa nini nchi hii ni maskini hivyo kupelekea kutojua nini cha kufanya.
 
Vilema wa akili. Mtu ana dizaini barabara leo ambayo hata Mjerumani miaka 100 nyuma alidizaini pana ya kuweza kutumika miaka 200 mbele (Tanga). Tazama na ma injinia wa Kitanzania walio dizaoni sinza na buguruni. Tofautisha na miaka 70 nyuma Muingereza aliodizaini Kariakoo. Hapo ndio utajuwa sisi hatuna akili na ni wajinga sana tu.

Injinia anaruhusu majengo ya ghorofa 10 na kuendelea (Kariakoo na Uhindini Dar) wakati miundio mbinu ya huko ilikuwa imedizainiwa kwa nyumba zisizozidi gharofa 1 au 3. Halafu unafikiri tutakuwa na maendeleo?

Viwanja vya Jangwani vilizhwa wazi miaka na miaka bila kuruhusiwa mtu kujengwa, mainjinia wetu, mtu anajenga wanamtazama macho, anazaa wanamtazama macho, anajukuu wanamtazama macho, ikitokea dizasta wanampeleka mabwe pande. Na huko mabwe pande hakuna dizaini wala nini, kila mtu atajijengea anavyotaka, nyumba zitaelekea anapoona mjengaji, ubora utakuwa ndio wa kikwetu (bora liende) na hii ndio tupo kwenye age ya dot com.

Umaskini wetu ni akili hatuna, hatujui maana, wavivu, wajinga, wapumbavu. Kazi kutafuta visingizio.
 
Miafrika Ndivyo Tulivyo. - Nyani Ngabu

Nilishasema humu miafrika mungu angeliumba dunia ya waafrika upya. As long as bado kizazi hiki cha miafrika kinaendelea, miafrika will remain poor.
 
Back
Top Bottom