Labda nikujibu swali hili kwa jinsi navyolifikiria mimi na mtazamo wangu. Nchi za kiafrika hatuna maendeleo kwa sababu hatuna necessities zetu zaidi ya kukidhi necessities za wazungu. Tumepanda zao la Korosho, Pamba, Katani na kadhalika kwa sababu yao na sii yetu maana kama tungelima pamba ilit utengenezen nguo zetu tungefikiria kuwa na viwanda vya nguo. tungefikiria kuwa na wajuzi wa kuchora na kushona (designers) lakini leo imefikia hata kuvaa kwetu tunafanya kwa kuiga zaidi ya mahitaji yenyewe. Ndio maana nasi siku hizo tuna show za mavazi ya kikwetu lakini targeting masoko ya nje kuwaizia Ulaya.
Sii dhahabu, chuma, uranium, vinyago wala wanyama yoote haya tunayafanya kwa sababu ya mahitaji ya mzungu lakini huwezi kuona mzungu akivumbua kitu kwa ajili ya mahitaji ya Mwafrika au Mchina. Wewe Mdanganyika ambaye unakihitaji ndio utaagiza kitu hicho kutoka kwao lakini wao kamwe hawatengenezi kitu bila kutokana na kukihitaji. Chukulia mfano wa ugonjwa wa malaria tu, bila huruma za UN upande wa madawa basi hata dawa ya malaria au hata vyandarua tusingekuwa navyo kwa sababu sisi hatutazami mahitaji yetu na kuyatafutia ufumbuzi bali tunatafuta maendeleo kuwa kama Ulaya.
Na magonjwa yote ya Tropical ndio yanatuua zaidi lakini hakuna nchi hata moja ya kiafrika imeweza kugundua kinga au dawa za ponya kwa sababu elimu tunazopewa ni kuwahudumia wao zaidi ya kukabiri mahitaji yetu sisi wenyewe. hatuna maji tunapigwa siasa, hatuna Umeme - siasa, Shule - siasa, Afya - siasa, hata Kilimo - Siasa yaani sisi ni malimbukeni na ndio mnaana hatuna vision kwa sababu mahitaji yetu pia ni ya ku copy na kupaste..
Mkuu Mkandara, kuna wakati tunawalaumu wazungu kwa makosa yetu. Wao walitumia elimu yao kuvumbua viwanda na hakika sisi tumeiga teknolojia yao ya vitu kama viwanda vya nguo si kwa faida yao bali kwa faida yetu ili tusivae vibwende kama akina Rumanyika, Kimweri n.k.
Tulikuwa na viwanda vyetu tukitengeneza nguo za viwango vyetu. Kabla wazungu hawajasema tuvifunge ili wapate pamba, genge la wahuni wakajikusanya Zanzibar na kupitisha azimio la kuagiza mitumba, vibiriti, kuku waliokaa katika friji miezi 3, chupi za mitumba n.k Hawakufanya kwa shinikizo au manufaa ya taifa, walifanya hivyo ili waweze kugawana viwanda na kuuza chuma chakavu kama Mang'ula, Moproco, Mutex n.k. Hapa si tunawasingizia wazungu!
Tunawasingizia kwasababu ugunduzi wa dawa ya malaria yasiyokuwepo kwao ni jukumu letu na sio lao.
Wao wamewekeza katika maradhi kama ya moyo kiasi kwamba kifo cha heart attack kinachunguzwa sana maana ni tatizo wanaloweza kukabiliana nalo. Sisi hatuwekezi katika R&D tunawasubiri wao.
Fuatilia bajeti ya research institutes za Tanzania utashangaa, wakati huo huo tumewekeza katika kununua VX na kulipana posho.Unakumbuka Hitler alivyoweza kuwabana egineers kubuni vifaa vya kivita kwa amri!
Nakuhakikishia kiongozi kama spika Makinda anayewaza mishahara ya Kenya hana wazo la ukubwa wa tatizo la malaria.
Mkuu, kwa ufahamu wangu hatuhitaji dawa za malaria na pengine uvumbuzi wake usingetusumbua sana.
Wenzetu wa Mexico walikuwa na tatizo la malaria kama sisi, lakini sasa ni historia.
Wao wanajua usipokuwa na contact na mbu huambukizwi malaria, na wanfahamu kuwa elimu kwa umma ikiwa ni pamoja na utumiaji wa dawa na kuziba mazalio ndiyo dawa pekee. Katika viongozi wetu pengine ni watatu au wanne wanaojua habari ya mexico, sasa hapa tunawalaumu wazungu kwa lipi?
Tuliletewa msaada wa mradi wa malaria Dar es salaam. Wajapan walipokabidhi mradi viongozi wakagawana magari na vifaa mradi umekufa. Kwanini tuwalaumu Wajapan kwa hili na si kuona tatizo la uongozi wetu.
Ninakuhakikishia kuwa baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wabunge, ukiwakusanya diamond jubilee uwaulize kwanini mradi wa malaria, lower moshi irrigation vimekufa hakuna anayeweza kukupa maelezo ya kisayansi ya kujitosheleza.Kama unataka majibu mengi uliza;ni VX au Vogue ya aina gani na bei zake! Hapa wazungu tunawalaumu kwa nini!
@Mkandara,hoja yako ina nguvu, however usisahau kuwa wananchi wakiwa na kazi na vipato, wataspend, na hivyo wafanyabiashara wataya target mahitaji yao na hivyo kukuza soko la ndani na uchumi kukuwa.Hilo litasaidia kutokuwategemea wazungu peke yake.Hiyo ni hatua ya kwanza, lazima tuwe na uwezo wa kutegema soko la ndani kwa bidhaa zetu.So tunarudi kwenye kushindwa kwa uongozi ku create jobs nk, its a total failure, but i still belive that we can!
Niongezee tu mfano mmoja, utalii umefanywa kitu cha wageni. Kwani kuna ubaya gani ukiwa na soko la ndani na la nje? Soko la ndani litumike katika ku sustain miradi na la nje kwa development.
Utashangaa yametengwa mabilion kuweka matangazo ya utalii Heathrow na CNN! Hakuna hata jitihada za kutangaza utalii kwa watu wa ndani. Mimi nakumbuka miaka ya nyuma utalii ulitangazwa hadi mashuleni, na nimetembelea mbuga za Selous, Mikumi kama sehemu ya elimu lakini baadaye nimejikuta nakwenda Ngorongoro, Serengeti n.k kwasababu tayari nilishapata hamasa.
Najua ipo hoja kuwa tunaongelea umasikini na wangapi watamudu! Hoja hii ni rahisi sana jibu lake kwasababu katika mashirika yanayotengeneza faida za mabilioni ni viwanda vya bia. Wateja ni akina nani?
Hoja ni kuwa ni lazima ujue namna ya kuitumia jamii yako kwa manufaa ya jamii hiyo hiyo ili kukata 'vicious circle' ya umasikini. Kuna watu wanoweza kutusadia au ni hawa viongozi wa matangazo Heathrow kwasababu ya 10%?