Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Zakumi, kazi zikiwepo, uchumi utakuwa mzuri tu!Huwa nashangaa sana watanzania eti viongozi wanawaita wavivu nk, Mkapa kweli hana huruma.Ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, hawajui majukumu yao hawa viongozi wetu.
Turudi tu kwenye pointi ya mjadala huu na hususan hoja yako hapo juu, mtu kama Bill Gates alifanya alivyofanya kwasababu ulizozitaja, isipokuwa kwa kuongezea, bado tunarudi pale pale, uchumi mzuri unaletwa na kazi, wananchi wapate kazi zenye kuwaingizia vipato, thats the bottomline.Gates asingethubutu kudrop out kama kusingekuwa na potential to succeed!Ni uchumi wenye nafasi kwa kila mtu, yani opportunities na growth potential.
Kwa wamarekani, sijui kuhusu states nyingi, lakini wafanya kazi wengi wa banks ni high school leavers and many of them have worked their ways up, nazungumzia banks kwasababu ni mojawapo ya makampuni yenye hiring rate ambayo siyo mbaya, at least based on my experience.
Kwenye maeneo yenye viwanda, watu wenye familia za kati (middle class), na wenye kuishi vyema tu ni ma high school leavers tu na wamefanya kazi viwandani masiha yao yote na kuweza kuishi vizuri kabisa na kusomesha watoto nk, mambo kwasasa ni tofauti kutokana na hali ya uchumi kubadilika, uchumi kuelekea zaidi kwenye financial sector kuliko uzalishaji, lakini ukweli ni kwamba sisi hatujawahi kuexperince anything, ni kama vipofu kabisa ambao hatujawahi kuona(yani kiuchumi)
Hiyo ni topic nyingine, sitaki kwenda deep, mfano huo hapo juu unatosha kabisa kukuonyesha kwamba kama kuna kazi basi uchumi utakuwa bila wasiwasi, tutakuwa na watalii wetu hata kama wazungu wasipokuja hatutakufa njaa.
Lakini sasa kwetu high school wont get you anywhere hata kama mtu angetaka kufanya kazi yenye kipato baada ya kumaliza high school.
Ni viongozi wa marekani walitumia akili, na wakajua kabisa kuwa kijana wa high school ana uwezo wa kiasi gani kuweza kuajiriwa kwenye sekta za uzalishaji, finance nk. Na wakahakikisha kuwa elimu wanayoipata inaweza kuwawezesha kuweza kukabiliana na majukumu hayo ya kazi.Na hivyo ikawa rahisi kuweka kigezo cha kuajiriwa kuwa ni at least "high school graduate" Uchumi wenye ku provide opportunities ndo unaoweza kuwa sustainable.
Kwa marekani watu huwa wanaenda shule uchumi ukiyumba na ukianza kuwa safi wanakuwa wako more uquiped, yani mambo yao yako kiakili zaidi kwa maana ya strategics.
Tutakuwa na bidhaa zetu hatutategemea kutukanwa na wakenya kila kukicha.
Rasilimali, hata watu tunavyo, viongozi wenye akili hatuna!
Jobs don't fall down from outer space. We are responsible for creating them.