Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Zakumi, kazi zikiwepo, uchumi utakuwa mzuri tu!Huwa nashangaa sana watanzania eti viongozi wanawaita wavivu nk, Mkapa kweli hana huruma.Ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, hawajui majukumu yao hawa viongozi wetu.

Turudi tu kwenye pointi ya mjadala huu na hususan hoja yako hapo juu, mtu kama Bill Gates alifanya alivyofanya kwasababu ulizozitaja, isipokuwa kwa kuongezea, bado tunarudi pale pale, uchumi mzuri unaletwa na kazi, wananchi wapate kazi zenye kuwaingizia vipato, thats the bottomline.Gates asingethubutu kudrop out kama kusingekuwa na potential to succeed!Ni uchumi wenye nafasi kwa kila mtu, yani opportunities na growth potential.

Kwa wamarekani, sijui kuhusu states nyingi, lakini wafanya kazi wengi wa banks ni high school leavers and many of them have worked their ways up, nazungumzia banks kwasababu ni mojawapo ya makampuni yenye hiring rate ambayo siyo mbaya, at least based on my experience.

Kwenye maeneo yenye viwanda, watu wenye familia za kati (middle class), na wenye kuishi vyema tu ni ma high school leavers tu na wamefanya kazi viwandani masiha yao yote na kuweza kuishi vizuri kabisa na kusomesha watoto nk, mambo kwasasa ni tofauti kutokana na hali ya uchumi kubadilika, uchumi kuelekea zaidi kwenye financial sector kuliko uzalishaji, lakini ukweli ni kwamba sisi hatujawahi kuexperince anything, ni kama vipofu kabisa ambao hatujawahi kuona(yani kiuchumi)

Hiyo ni topic nyingine, sitaki kwenda deep, mfano huo hapo juu unatosha kabisa kukuonyesha kwamba kama kuna kazi basi uchumi utakuwa bila wasiwasi, tutakuwa na watalii wetu hata kama wazungu wasipokuja hatutakufa njaa.

Lakini sasa kwetu high school wont get you anywhere hata kama mtu angetaka kufanya kazi yenye kipato baada ya kumaliza high school.

Ni viongozi wa marekani walitumia akili, na wakajua kabisa kuwa kijana wa high school ana uwezo wa kiasi gani kuweza kuajiriwa kwenye sekta za uzalishaji, finance nk. Na wakahakikisha kuwa elimu wanayoipata inaweza kuwawezesha kuweza kukabiliana na majukumu hayo ya kazi.Na hivyo ikawa rahisi kuweka kigezo cha kuajiriwa kuwa ni at least "high school graduate" Uchumi wenye ku provide opportunities ndo unaoweza kuwa sustainable.

Kwa marekani watu huwa wanaenda shule uchumi ukiyumba na ukianza kuwa safi wanakuwa wako more uquiped, yani mambo yao yako kiakili zaidi kwa maana ya strategics.

Tutakuwa na bidhaa zetu hatutategemea kutukanwa na wakenya kila kukicha.

Rasilimali, hata watu tunavyo, viongozi wenye akili hatuna!

Jobs don't fall down from outer space. We are responsible for creating them.
 
Mkandara, adui yetu mkubwa ni yule anayenufaika na matatizo yetu, na wengi wao ndo wako kwenye powerfull positions, ni mtandao mkubwa unaoshirikisha pande zote, it is an industry on its own.

Swali ni vipi tutaweza kujinasua?

Kwa mfano huo mradi wa neti ni msaada wenye strings, ni lazima kuwe na makampuni ya marekani yenye kunufaika nk, na pia ni lazima kuwe na viongozi wenye kula ten pasenti ndani ya bongo nk.

Mbona marekani kulikuwa na malaria iliwasumbua sana na wameitokomeza, hata tukisadiwa tunasaidiwa based on our abilities to think.

Pia mataifa makubwa hususan marekani, wanalinda interests za makumpuni yao makubwa, hata hayo ya madawa, unakumbuka kuna kiwanda cha madawa kilipigwa mabomu na Clinton kule Sudan enzi zile Bin Laden akiwa kule?

Uvumbuzi wa dawa mpya lazima uwe chini yao na patent rights and so forth.

Nadhani utakuwa unajibu moja ya posti ya Mkandara. Alisema kuwa tungekuwa na uchumi unaomwangalia mtanzania kama ndie mlaji wa bidhaa, baadhi ya matatizo yangeweza kutoweka.

Ufumbuzi mkubwa wa matatizo ya mbu Marekani haupo kwenye matumizi ya vyandarua. Hupo kwenye sanitation systems. Tanzania inaweza kuwa sanitation systems kwa kutumia nguvu za ndani.

Vilevile kuhusina na madawa, nchi zilizoendelea zimefanya juhudi kubwa. Kwa mfano kampuni ikigundua dawa, itakuwa na patent ya dawa hiyo kwa miaka 10. Baada ya kipindi hicho, makampuni mengine yanaweza kutengeneza madawa hayo bila kibali. Cuba, India, na nchi zingine zinatumia kipengele kama hiki kuwa watengenezaji wa madawa.

Hivyo watanzania wanaposhindwa hata kwenye kutumia ujuzi wa copy and paste ni lazima tujiulize hatima yetu kama taifa.
 
Zakumi,
Mkuu wangu kama ulikuwa kichwani mwangu kuhusu IDENTITY - na ndio maana huzungumzia sana Lugha kwa sababu hii ndio chimbuko la ID wa Utaifa wa wananchi wake. Tumepoteza lugha zetu za asili sasa kuna hatari kubwa ya kupoteza hata Kiswahili na kama unavyona sasa hivi ati wasaniii wanakaa kuvumbua vazi la Taifa.. Huu umekuwa mtihani mkubwa kwa sababu tayari tumekwisha poteza Identity yetu. Sasa vazi la nini? na haiwezi kuingia akilini kwa Mtanzania yeyote.

JMushi1,
Sawa tunajua kwamba Globolazation imetokana na wao wenzetu kuweza kukidhi mahitaji yao sasa hivi wanataka Utajiri zaidi na huwezi kutajirika zaidi na zaidi kwa soko lile lile hivyo wamevumbua mbinu za kuzaa demand nje ya mipaka yao japokuwa priorities zao mwanzo zilikuwa kukidhi mahitaji yao. Ni tamaa ya UTAJIRI wa kukiuka ndio maana haramu hizi zimeingia lakini sisi ambao ni fukara hatuwezi kuiga hawa jamaa wakati hata mahitaji yetu tu yanatushinda. Elimu mnayoipata mashuleni ndio inatakiwa kutumika... wanapotulazimisha tutumie mbolea na mbegu zao za GMO tuwakatalie na kusema thank U kama alivyosema Mwandosya akiwa waziri wa Kilimo - Tanzania ardhi yetu haijafikia kuhitaji mbolea za maabara tutafanya kama Wakara wanaotumia mbole ya mavi ya ng'ombe. Lakini leo tunalima maua na mafuta ya alizeti (cholesterol kibao)wakati wananchi wanakufa njaa hakuna mahindi wala ngano.

Lakini kwa sababu tunatafuta Urahisi wa maisha kukwepa kazi ya kufanya utafiti yakinifu, kuvumbua njia ya kukidhi mahitaji na kutoa huduma hizo ndio maana leo ktk tatizo la maji tu tunachimba visima mji mzima Dar hadi vijijini ni visima na mashine za kuvuta maji ya ardhini ambayo Mungu kayahifadhi kwa ajili ya mimea na miti. Nchi inageuka kuwa jangwa taratibu kwa sababu ya kutafuta nafuu, sidhani kama mzungu au Mchina anatulazimisha kununua generators na matangi ya Plastic kutoka China..lakini hatujali wala kufikiria madhara ya visima mji mzima ili hali hata mchicha tunaopanda tunatumia madawa makali ya kukua na kuuwa wadudu kwa sababu mimea tunayopanda haina maji ya kutosha hivyo tunavumbua mbegu za maabara - Ni Toxic.

Kwa nini hatuwezi vuta maji safi kutoka Maziwa yetu au hata kuvuta ya bahari na kuyaboresha ili yaweze kunyweka - hakuna sababu. Binafsi namlaumu mzungu kwa sababu tofauti kabisa wala sii ya kututawala au kutuwekea mfumo huu. Bali alitudumaza kama mwanamke wa Uswahilini anayeshinda jikoni na hata kusifiwa kwamba mwanamke ni jiko..na yeye anaamini kabisa hawezi kufanya biashara, kazi maofisini, viwandani na kadhalika kwa sababu tu kuna mfumo dume. Pambana nao huo mfumo dume na ndicho sisi waafrika tunatakiwa kupambana na Ukoloni mamboleo sio kulalama wakati nchi zetu ni huru.

Jamani hata Mchina kasema maneno haya hivi kweli tumeyatazama undani wake.. "Give a man a fish and you feed him for a day. Teach a man to fish and you feed him for a lifetime".
- We do give our kids education for the wrong reason..supposed to teach them how to fish not how to survive.
 
Jobs don't fall down from outer space. We are responsible for creating them.
Zakumi bana, sasa si tunazungumzia failure to create ndo sababu kuu ya a failed economy?

Wewe unadhani kwanini wenzetu wanapiga kura based on economy and job creations?

Si ndicho tunachozungumzia?Haya ya space yametoka wapi?lol

Ama ulikuwa hujaipata point?
 
Duh, nyie vijana wa siku hizi mbona mnakuwa wagumu kutumia figure of speech. Maana yangu ilikuwa nafasi za kazi hazijitokezi zenyewe kwa miujiza ya Mungu kama chakula cha wana wa Israel walipokuwa jangwani.

Ukitaka ziwepo nafasi za kazi ni lazima watu wawe na juhudi za kuzianzisha.
 
Sasa hilo linatofauti gani na kusema "Uongozi umeshindwa"?
 
Nyani Ngabu,
Hakuna kitu DNA yetu tofauti huu ni uongo mtupu. Mimi sina elimu ya juu ya biologia lakini sidhani kama ukiweka ubongo wa mtu mweusi na mzungu ukampa mtaalama anaweza kusema huu ni wa mzungu na huu ni wa mtu mweusi..Sidhani ndani ya bongo zetu kuna tofauti hizo isipokuwa tofauti inakuja kwenye kuitumia akili hiyo ama kuiboresha akili hiyo ifanye kazi ipaswavyo.

Mimi nadhani sisi tuna tatizo la kutokuwa na necessities ktk maisha, sawa na Mmasai isipokuwa tofauti imekuja tu kwamba tumetoka ktk Ummasai na kufikiria Kuwa kama Ulaya. Hivyo jitihada zenu kubwa zipo ktk kuigeuza Afrika na watu wake wafanane na wazungu kama mtu anayetumia mchubuo. Tunatumia nguvu kubwa sana kuonyesha we are not inferior kwa kujifananisha na wazungu toka culture zetu iwe lugha, mavazi hadi chakula. Ukiamka asubuhi na kumkaribisha mgeni uji wa mtama basi hiyo story utaikuta hadi kwa Mange na Michuzi.
 
Sasa hilo linatofauti gani na kusema "Uongozi umeshindwa"?

Kama uongozi umeshindwa kwanini hufanyi juhudi za kuondoa? Hivi kufanya mambo mazuri hata majumbani kunahitaji uongozi wa nchi?
 
Ukitaka ziwepo nafasi za kazi ni lazima watu wawe na juhudi za kuzianzisha.
...Labda tujiulize, watu hawa ni wapi? Hawa vijana wasiojua kusoma na kuandika, hata jina lao, ilhali wamemaliza darasa la saba. Au tunaongelea wale walio kwenye maofisi wakipanga kununua vitu visivyodumu toka China [ili kamchezo hako kajirudie tena na tena], na kuacha vya vijana wao wenyewe wa kuwazaa, vikidoda pale Keko na kwingineko?

...Nadhani hapa ndio tutapata jawabu la juhudi zinazohitajika kuzianzisha hizo nafasi za kazi.

...Twende mbele zaidi na tujiulize, je, ni nafasi zipi za kazi zinahitajika kuanzishwa? kama umeme utaendelea kuwa si wa uhakika, na maji hakuna. Bila kusahau huduma mbaya kabisa ya usafiri wa umma.
 
DAR sii LAMU,
Vitu ulivyovitaja hapo chini Maji, Umeme na Usafiri ndivyo nguzo kuu ya uzalishaji bila vitu hivyo hatuna sababu ya hata kuendeleza mjadala wa uchumi, huwezi kukuna meli kuitumia jangwani..
 
Nyani Ngabu,
Hakuna kitu DNA yetu tofauti huu ni uongo mtupu. Mimi sina elimu ya juu ya biologia lakini sidhani kama ukiweka ubongo wa mtu mweusi na mzungu ukampa mtaalama anaweza kusema huu ni wa mzungu na huu ni wa mtu mweusi..Sidhani ndani ya bongo zetu kuna tofauti hizo isipokuwa tofauti inakuja kwenye kuitumia akili hiyo ama kuiboresha akili hiyo ifanye kazi ipaswavyo.

Mimi nadhani sisi tuna tatizo la kutokuwa na necessities ktk maisha, sawa na Mmasai isipokuwa tofauti imekuja tu kwamba tumetoka ktk Ummasai na kufikiria Kuwa kama Ulaya. Hivyo jitihada zenu kubwa zipo ktk kuigeuza Afrika na watu wake wafanane na wazungu kama mtu anayetumia mchubuo. Tunatumia nguvu kubwa sana kuonyesha we are not inferior kwa kujifananisha na wazungu toka culture zetu iwe lugha, mavazi hadi chakula. Ukiamka asubuhi na kumkaribisha mgeni uji wa mtama basi hiyo story utaikuta hadi kwa Mange na Michuzi.

Kama kuna tofauti ya rangi ya ngozi, macho, nywele, maumbile na kadhalika kwa nini tofauti ya DNA isiweze kuwepo?
 
Kama kuna tofauti ya rangi ya ngozi, macho, nywele, maumbile na kadhalika kwa nini tofauti ya DNA isiweze kuwepo?

Hata kama tukiacha mambo ya baioloji, excellence ya kazi inarithishwa. Tunaopiga mabox huku tunaona. Unatoka university, unaanza kazi chini kabisa. Na matokeo ya kazi yako ndio yatakupandisha juu.
 
Hata kama tukiacha mambo ya baioloji, excellence ya kazi inarithishwa. Tunaopiga mabox huku tunaona. Unatoka university, unaanza kazi chini kabisa. Na matokeo ya kazi yako ndio yatakupandisha juu.

Na kwa ujumla, kila kazi halali inaheshimika.
 
Kama kuna tofauti ya rangi ya ngozi, macho, nywele, maumbile na kadhalika kwa nini tofauti ya DNA isiweze kuwepo?
Nitoke nje ya mada kidogo. Ni ukweli usiopingika kutoka kwa wataalamu wa vinasaba na maumbile kuwa DNA za mwanadamu hazina tofauti. Kuna kitu kinaitwa DNA codes ambacho kina idadi na ufanano wa kila kitu katika DNA za mwanadamu, vivyo hivyo kwa viumbe wengine katika jamii inayowiana.

Mfano, Waafrika ni weusi si kwasababu wana DNA tofauti. Kinachotokea ni kuwa wao wana kitu kinaitwa 'melanin' kinachotoa rangi ya ngozi. Melanin ipo kwa wanadamu wa race zote. Kinachotokea ni kuwa Waafrika melanin zao zinakuwa dominant kutoka na kuwa katika tropical ambako jua ni kali muda wote. Hii hutokea kama adaptation ya mwanadamu kukidhi na kukabiliana na mazingira fulani. Ndiyo maana maradhi kama ya Cancer ya ngozi ni kidogo sana ukilinganisha na watu weupe.

Watu weupe wana melanin lakini ni 'recessive' kwa maana ya kuwa hazijitokezi kutokana na mazingira yao. Haiwezekani mtu anayeishi Arctic au Iceland akawa na melanin kwa kiwango kinachotokeza sawa na Mnubi wa Arua kule Uganda.

Ni kwasababu ya kuwa na melanin ikitokea mwanadamu ana upungufu au matatizo yake basi mtu huyo anakuwa albino hata kama ni mzungu, mchina au mhindi. Hii ni ushaidi kuwa DNA ni sawa kwa wanadamu wote

Hakuna literature yoyote ya medicine inayoonyesha kuwa wanadam wana DNA tofauti, lakini zipo literature zinazoonyesha mapungufu fulani ambayo hutokana na mazingira na haya mara nyingi huwa ni sehemu ya maradhi hata kama hayatoi dalili za maradhi.

Kuna jamii katika visiwa ndani ya bahari ya hindi wana ugonjwa wa damu unaojulikana kama 'Thalassemia'. Hii haina maana jamii hiyo ina DNA tofauti bali ina DNA zinazo carry trait za Thalassemia. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa magonjwa ya kurithi.

Nguli wa mambo ya genetics miaka 4 iliyopita alitoa madai kuwa Ubongo wa mwafrika una kiwango cha chini. Alipoitwa kuhojiwa na panel ya watu wa genetics kuthibitisha madai yake kisayansi hakuweza kufanya na hivyo. Ameishia kunyanga'anya haki zake za kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuondolewa mkataba wake na kampuni kubwa ya utafiti.
 
Kama uongozi umeshindwa kwanini hufanyi juhudi za kuondoa? Hivi kufanya mambo mazuri hata majumbani kunahitaji uongozi wa nchi?
Mkuu kama nilivyosema hapo awali, sidhani kama mjadala huu ni kuhusu namna ya kupata uongozi mpya.
 
Nitoke nje ya mada kidogo. Ni ukweli usiopingika kutoka kwa wataalamu wa vinasaba na maumbile kuwa DNA za mwanadamu hazina tofauti. Kuna kitu kinaitwa DNA codes ambacho kina idadi na ufanano wa kila kitu katika DNA za mwanadamu, vivyo hivyo kwa viumbe wengine katika jamii inayowiana.

Mfano, Waafrika ni weusi si kwasababu wana DNA tofauti. Kinachotokea ni kuwa wao wana kitu kinaitwa 'melanin' kinachotoa rangi ya ngozi. Melanin ipo kwa wanadamu wa race zote. Kinachotokea ni kuwa Waafrika melanin zao zinakuwa dominant kutoka na kuwa katika tropical ambako jua ni kali muda wote. Hii hutokea kama adaptation ya mwanadamu kukidhi na kukabiliana na mazingira fulani. Ndiyo maana maradhi kama ya Cancer ya ngozi ni kidogo sana ukilinganisha na watu weupe.

Watu weupe wana melanin lakini ni 'recessive' kwa maana ya kuwa hazijitokezi kutokana na mazingira yao. Haiwezekani mtu anayeishi Arctic au Iceland akawa na melanin kwa kiwango kinachotokeza sawa na Mnubi wa Arua kule Uganda.

Ni kwasababu ya kuwa na melanin ikitokea mwanadamu ana upungufu au matatizo yake basi mtu huyo anakuwa albino hata kama ni mzungu, mchina au mhindi. Hii ni ushaidi kuwa DNA ni sawa kwa wanadamu wote

Hakuna literature yoyote ya medicine inayoonyesha kuwa wanadam wana DNA tofauti, lakini zipo literature zinazoonyesha mapungufu fulani ambayo hutokana na mazingira na haya mara nyingi huwa ni sehemu ya maradhi hata kama hayatoi dalili za maradhi.

Kuna jamii katika visiwa ndani ya bahari ya hindi wana ugonjwa wa damu unaojulikana kama 'Thalassemia'. Hii haina maana jamii hiyo ina DNA tofauti bali ina DNA zinazo carry trait za Thalassemia. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa magonjwa ya kurithi.

Nguli wa mambo ya genetics miaka 4 iliyopita alitoa madai kuwa Ubongo wa mwafrika una kiwango cha chini. Alipoitwa kuhojiwa na panel ya watu wa genetics kuthibitisha madai yake kisayansi hakuweza kufanya na hivyo. Ameishia kunyanga'anya haki zake za kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuondolewa mkataba wake na kampuni kubwa ya utafiti.

Kwani DNA hai-determine melanin?

Na kuhusu huyo mwanasayansi aliyenyang'anywa haki zake kitaaluma, haya mambo ni controversial sana kiasi kwamba kupata watu wa kuhoji utofauti wa DNA bila severe consequences ni ngumu sana.

Kwa dunia ya sasa iliyo politically correct kwa kiasi kikubwa, yeyote yule atakayehoji utofauti baina ya races ataitwa mbaguzi na atakuwa ostracized.

Lakini mwisho wa siku ukweli wa mambo uko kwenye hali halisi. Ni ukweli usiopingika kuwa Wazungu wamechangia sana katika uvumbuzi wa vitu vingi sana na katika nyanja nyingi sana.

Hata hili li-www wamevumbua na kuliendeleza wao na leo mimi na wewe tunalitumia kujadili mada mbalimbali. Wazungu hao hao wameenda katika sehemu nyingi sana za dunia na wamezitawala kwa kila aina. Angalia Autralia...angalia New Zealand...angalia Brasil hususan sehemu zile za wazungu...angalia Afrika Kusini. Angalia hata Zimbabwe baada tu ya uhuru.

Kwa wakati huo huo angalia Afrika kusini mwa jangwa sa Sahara. Kuna kitu sisi weusi tunakikosa! Angalia Haiti...angalia Jamaica....

Surely kuna kitu mahali....
 
Back
Top Bottom