Job creation nayo ni challenge kubwa. Kwa vioongzi wetu njie pakee wanayotegemea ni Uwekezaji tena wa nje. Na serikali amabayo ndiyo muajiri mkubwa kuna shemu nyigine kuna watu wafanyakazi wengi zaidi ya mahitaji na mbaya zaidi smometime perfomence haiendani na idadi.
Ebu tuambiane katika local level
- How can job be created.
- Ni jukumu la nani kutengeza ajira. ( Kila mwanamanchi ,viongozi, serikali, wenye uwezo)
Labda mimi nichangie kidogo kulingana na jinsi navyofahamu na mtazamo wangu.
Kwanza kabisa ni lazima tu identify Mahitaji yetu kisha ili tuyakidhi mahitaji hayo tunahitaji misingi na nguzo zipi, kishwa tujenge policies zinazowezesha ujenzi wake ili tupate kuzalisha vitu vinavyokidhi mahitaji hayo. Huwezi kufikiria kuongeza ajira nchini ikiwa swala kubwa lkama umeme na maji ni shida. Huwezi kufikiria kuongeza ajira ilwa Elimu na Afya huvipi umuhimu zaidi ya kubakia kwenye makabrasha..
Kitu anachozungumziia Nyani Ngabu kuhusiana na DNA, hakipo isipokuwa sisi waafrika kwa ujumla wetu hatuna MAHITAJI ya maendeleo zaidi ya fikra au niseme ile mentality ya kuiga. Kama tungekuwa kweli tunathamini nguvu ya maji na umeme ktk kukuza uchumi wa nchi basi leo hii nchi nzima ingekuwa na umeme au maji kabla hata ya kufanya mengineyo. Lakini SHIDA na uhaba wa vitu imekuwa utamaduni wetu (umaskini) ambao hatuoni sababu ya kubwa ya maendeleo zaidi ya kujikimu na shida hizo siku hadi siku (day by day).
Hata Yule Simba wa Serengeti angekuwa akiishi Ulaya basi angejifunza kula na kuwinda wakati wa Spring hadi Fall (Autum) na kuweza kujichimbia wakati wa winter na mwili wake ku hibernate. Na kwa jinsi hiyo mnyama anayeishi Iceland au Yellow Knife ataonekana ana akili zaidi ya huyu wa Serengeti iwe ktk mawindo na hata ujenzi wa hifadhi (nyumba). Tofauti za mazingira ndizo sababu ya activeness ya viumbe wake, na imetokea kwamba sisi waafrika tunaoishi karibu na Tropical ndio tunaonekana tuko nyuma sana kuliko mataifa mengineyo maana sii joto sana wala baridi na hivyo tume jilimit ktk mahitaji..
Ni jukumu letu sote, toka serikali, viongozi na wananchi kwa nafasi zetu kutambua kwanza NECESSITIES na kisha kutumia fursa zilizopo kuunda policies zitakazo tuwezesha kukidhi mahitaji hayo. Innovation sio Ubunifu bali uwezo wa kuboresha huduma au services zilizopo ambazo zimeshindwa kukidhi mahitaji hayo iwe hata Umeme. Sasa tunapobishana juu ya umeme ilihali mazinira yetu yana Upepo mkubwa sehemu za Singida, tuna jua kali masaa 12 kwa siku, tuna makaa ya mawe na kadhalika lakini inachukua miaka 50 tumeshindwa kabisa kuboresha nguvu hizi wakati mahitaji yake yamezidi mara 100. Inabidi sisi kujiuliza uwezo wetu ktk kufikiri na hasa umakini wetu wa kukidhi mahitaji haya.
Mbali kabisa na utumwa wa fikra nadhani pia IMANI zetu za dini zimevuka kiwango cha kuamini tunafanya kufuru au bado kabisa tamaduni na mila za zetu zinachukua nafasi kubwa ktk maamuzi yetu. Kwa sababu haiwezekani watu wanakufa kwa malaria kila mwaka sii chini ya millioni lakini hadi leo hatuna kinga wala kuandaa mazingira ambayo yatazuia mbu hawa kuzaana ila jibu kubwa ni KAZI YA MUNGU, bwana ametupa bwana ametwaa!. Kwa hiyo tunaendeleza utamaduni wa kushughulikia kitu kinapokuwa epidemic kwa kusema ni kazi ya Mungu...Utamaduni wa maintanance hatuna unakuta mtu bomba la maji linavuja mtu anafunga na mpira hadi siku litakapo haribika kabisa beyond repair..
Kwa hiyo Job creation inatakiwa sisi tuthamini vitu vyetu, tujithamini sisi wenyewe kwa kuyapenda maendeleo na sio kujaribu kuiga tuonekane tunapendeza kama wazungu au Ulaya.. Let's start with ourselves, tubadilike na kuwekea mkazo mkubwa ktk ELIMU, AFYA, MAJI na UMEME vitu vingine vitajipanga tu kutokana na mahitaji yatakayo jitokeza.