Nimekupata, je market ya bidhaa ilikuwa ni wapi?East African Market?
Ama tulitegemea soko la ndani?
Binafsi nakumbuka nikiwa very young na mzee wangu alikuwa na kiwanda kidogo cha viatu, mikanda na mikoba ya ngozi, it did well, lakini kama ulivyosema, hatukutayarishwa na ushindani kutoka nchi jirani ya Kenya, bidhaa za Kenya zilizokuwa zikiingizwa kwa magendo zilikuwa cheaper zaidi, hiyo pia ilikuwa sababu mojawapo ya kudorora kwa uchumi wetu.
Kama ilivyotokea kwa Bora na viwanda vingine ie Tanneries, Kilimanjaro Machine Tools nk, tulikuwa na kiwanda cha sigara lakini sigara kutoka Kenya ndo zilikuwa dili, nakumbuka enzi hizo farasi walikuwa wakitumika kuwakimbiza wauza fegi wa reja reja ambao walikuwa wakiitwa walanguzi!
Ilikuwa mbaya mkuu, watu wamesahau, pia maeneo mbali mali ya nchini yalikuwa na issues za tofauti, just depending on what main economic activities was there.
I will never forget this stuff kwasababu i was very young na imestick kwenye mind since then.
Ni kweli kuwa viwanda vilipewa nafasi ya kujiendesha vyenyewe, lakini je ni kweli serikali iliviandalia mazingira stahiki na policies ambazo zingeweza kuvifanya viwanda hivyo vithrive kwenye East African Market? Thats where the leaders failed us!
Kwa upande mwingine, ukweli ni kwamba hata hivyo viwanda vya wakenya tulivyokuwa tukishindana nao, wamiliki halisi ndo hao wazungu ambao tuliwafukuza Tanzania!