Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Kwanini mzungu ambaye ni dikteta, mnyonyaji, kupe, mla rushwa anaweza kuja Afrika na kujenga nchi wakati mwaAfrica mwenye kukaribia utakatifu jasho linamtoka?

Wazungu hao hao walienda Austalia na New Zealand na wakapajenga kweli kweli.

Wana nini hawa wazungu?
 
Jmushi1 and Nguruvi2,

Siku zisije mkawa very dissapointed. Dr Slaa anaweza kuchaguliwa kuwa rais na akamaliza muda wake nchi ikiwa bado masikini.Wanafalsafa wa uchumi wamesha-prove kuwa uongozi ni kitu muhimu but it isn't the only prerequisite for development. Africa ina-nchi zaidi 40, na huwezi kusema kuwa katika nchi zote hizi hajawahi kutokea kiongozi mzuri.

Nyerere mliyemtumia kwenye mifano, tulikaa naye na aliongoza kwa miaka 23 na watu tulimchoka.
Kwanini mzungu ambaye ni dikteta, mnyonyaji, kupe, mla rushwa anaweza kuja Afrika na kujenga nchi wakati mwaAfrica mwenye kukaribia utakatifu jasho linamtoka?
Mkuu Zakumi, nadhani umemuelewa Jmushi1 tofauti. Nadhani alikuwa anajenga hoja kuwa kuna kufanana kimtizamo, hakuwa na maana kuwa yeye Dr Slaa ni dawa ya umasikini.

Tukiangalia nadharia tulizojiwekea kuhusu maendeleo( watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora) utaona hivyo viwili vya mwisho vinamatatizo sana. Watu tunao na kwa Tanzania ya leo rasilimali watu ni bora kuliko Nyerere alipochukua nchini hasa kielimu, ardhi tunayo tena nzuri na ya kutosha.

Tutoe mifano ili twende pamoja. Nchi kama India inapiga hatua kubwa kwasababu kila wanapojitathmini hawakawii kufanya mabadiliko ya uongozi. Chama cha Congress (sawa) na CCM, kwasasa kipo benchi na wananchi wanaridhika na PJP. Wanakubali hata kwa machungu kuwa Mammohan Singh pamoja na u-singh wake ana uwezo wa kuioandoa nchi kutoka ilipo kwenda hatua moja. Hii haina maana India hakuna umasikini, upo tena uliokithiri lakini kasi yao ya maendelo inatisha

China ambayo haikuwa katika nchi tajiri sasa ni tishio. Angalia uongozi wao na maamuzi yao.Serikali ilipoamua kuwatuma wachina kwenda kuiba teknolojia magharibi ni mbinu ya hali ya juu.Angalia vision yao ya miaka 25 ijayo na inavyofuatiliwa 'chronoligically'. Nchi inapoamua kuwa mkuu wa mamlaka iliyotia hasara ya maziwa na kuathiri soko anyongwe ni tofauti na sisi tunaowastaafisha wezi kwa furaha na nderemo tukilea wizi na ubadhirifu kwa kutegemea misaada

Kwa miaka 2 nchi yetu imeshindwa kuzalisha chochote kwasabau ya umeme. Pesa za umeme wa dhararu zingetosha kabisa kuondoa tatizo hilo kwa miaka kadhaa katika mipango timilifu. Lakini pia, wale waliotia taifa hasara ya matrilioni bado wapo na wanazunguka wakihubiri utakatifu kwa kutumia pesa zile zile walizoiba. Mwenye dhamana ya kulikokoa taifa anasema waacheni wapunzike, ni sehemu ya genge la uhalifu.

Taarifa ya CAG inaonyesha kuwa pesa tunazopoteza kwa wizi na ufujaji zingeweza kuziba pengo la nakisi ya bajeti kwa kiasi kikubwa. Hakuna kiongozi anayeliona hili, wao wanona marupu rupu na posho za kufanya kazi. Kiongozi wa namna hii ana vision gani ya kumsaidia Mwandiga wa kule Mtimbira na nyumbani Muheza.

Unapomsikia kiongozi kama spika anadai posho zilingane na za Wakenya, hivi unadhani mtu wa namna hii amewahi kufikiri kwanini wananchi wa Nyakatende Musoma ni masikini sana? Huyu ni Spika sasa mipango ya kujikwamua atasimamia nani?

Waziri mkuu aliwahi kusema, posho ni kwa ajili ya kuwapa wananchi na hivyo wabunge wanastahili. Hivi huyu mtu anayeamini kuwa kazi ya mbunge ni kugawa pesa, yeye na mbunge wake wanaweza kukaa chini na kufikiri jinsi gani ya kutumia rasilimali kumkomboa masikini wa Isevya Tabora? Kwa mtazamo gani !

Hivi kiongozi aliyekaa madarakani miaka 20 na bado hajui kwanini Tanzania ni masikini, na anadhani ni muhimu kwenda kujifunza mabembea yanavyoweza kuvutia utalii ana mtazamo gani kuhusu utalii uliopo usiohitaji bembea na unajojiuza wenyewe!

Hoja ni kuwa watu na ardhi vipo. Siasa safi na uongozi bora hatuna. Inaweza kuwa siasa safi ipo lakini uongozi wa kusimamia siasa hiyo hakuna. Fikiria, azimio la Moshi na Iringa yalikuwa na matatizo gani hadi tufikrie azimio lingine la kilimo kwanza. Hivi kwanini ushindwe kusimamia sera za kuimarisha UFI kwa namna yoyote na ufikirie kununua jembe kutoka Bangladesh!

Nimalizie kusema kuwa sisi kama nchi tuna kila kitu, tatizo letu tupo kama 'kiosiki' ambako kila bidhaa ipo lakini itachukua nusu saa kwa muuzaji kujua mafuta ya taa yapo wapi. Ili tubadilike ni lazima tuwe na uongozi utakaotusaidia kubadili kiosiki ili kiwe supermarket iliyopangika na kila kitu kinaonekana.
Anayeweza kubadili ni uongozi na hapa ndipo tatizo lilipo.
 
Jmushi1 and Nguruvi2,

Siku zisije mkawa very dissapointed. Dr Slaa anaweza kuchaguliwa kuwa rais na akamaliza muda wake nchi ikiwa bado masikini.

Wanafalsafa wa uchumi wamesha-prove kuwa uongozi ni kitu muhimu but it isn't the only prerequisite for development. Africa ina-nchi zaidi 40, na huwezi kusema kuwa katika nchi zote hizi hajawahi kutokea kiongozi mzuri.

Possibility of failure isikufanye uwe binadamu usiyetaka kutake risks, it all comes with the territory.
Kama maendeleo ya nchi flani ya kiuchumi yanaweza kuwa attributed to certain leaders ama uongozi, why cant we do the same with poverty?Ndiyo maana ya accountability.
It is a fact kwamba tunahitaji mawazo mbadala, ni risk kubadili uongozi, lakini maendeleo hayaji bila kutake risks.
 
Ngu3,

Kwanza nadharia ya kusema kuwa ukitaka maendeleo unahitaji vitu vinne sio ya kwetu. Watanzania hawakujiwekea. Hiyo ni nadharia ya Nyerere na sio ya nchi. Kaunda alikuwa na nadharia zake lakini waZambia hawasemi kuwa walijiwekea. Lenin alikuwa na nadharia zake, lakini sio za warusi.

Hivyo watanzania kung'ang'ania kuwa ukitaka kuwa na maendeleo unahitaji vitu vinne ni kujipunguzia uwezo wa kuangalia matatizo yao kiundani zaidi. Hii ni kwa sababu tupo tunaoamini ukitaka maendelelo kuna vitu vingi zaidi ya hivyo vinne. Na kuna watu kama Nyani Ngabu wanaoamini kuwa maendeleo ya nchi yanatokana na watu walivyo. Ni watu wanaochagua viongozi, ni watu wanapanga siasa na ni watu wanaotumia ardhi.

Mtu anayekwambia kuwa China haikuwa tajiri mwambie akasome tena historia. Haikuwa tajiri kwa mtazamo wa kimagharibi lakini walikuwa na ingridients za maendeleo.

Kwa mfano kabla mzungu hajaanza kutumia bunduki, mchina tayari alikuwa na mizinga, pump za kuvuta maji, matumizi ya noti, utengenezaji wa makaratasi, meli za kivita ambazo zilikuja Afrika mashariki kabla ya Vasco Da Gama. Kilichosumbua wachina ni distribution of wealth. Tatizo hilo vilevile lilikuwepo India.

Matatizo ya Tanzania yanatokana na kile ulichoandika katika paragraph yako ya mwisho. Watanzania wanaamini wana kila kitu. Wanaamini kuwa wana rasimali zote za kuleta maendeleo. Na matokeo yake they take their natural resources for granted.

Mpaka miaka ya 70, 3/4 ya ardhi ilikuwa haijatumika. Hivyo viongozi wakawa wanaambia watu, kama huna kazi rudi kijijini kalime.

Matatizo ya umeme yanatokana na hali ya hewa na ongezeko la watu. Kulikuwa hakuna sera yoyote mpaka matatizo yalipotokea. Na kulikuwa hakuna sera kwa sababu nchi ina vyanzo vya maji. Nchi kama Kenya have to think harder na matokeo yake wana sera zinazoeleweka kwenye nishati.
 
Possibility of failure isikufanye uwe binadamu usiyetaka kutake risks, it all comes with the territory.
Kama maendeleo ya nchi flani ya kiuchumi yanaweza kuwa attributed to certain leaders ama uongozi, why cant we do the same with poverty?Ndiyo maana ya accountability.
It is a fact kwamba tunahitaji mawazo mbadala, ni risk kubadili uongozi, lakini maendeleo hayaji bila kutake risks.

JM,

Tanzania ina matatizo mengi na uongozi ni moja wapo. Na nitafurahi kama uongozi utabadilika kesho. Na kuhusiana na ku-take risks, people don't take risks for sake of it. You have to take risks and fall down somehow safely.

Unataka watanzania wa-take risks kwenye nchi inayowatukuza waalifu. Chenge anaiba pesa, akirudi kwao watu wanafanya maandamano ya kumpokea. Lowassa anajiuzulu uwaziri mkuu, kwao wanasikitika na mkewe kutunga kitabu cha dini.
 
Zakumi;3426884]Ngu3,
Kwanza nadharia ya kusema kuwa ukitaka maendeleo unahitaji vitu vinne sio ya kwetu. Watanzania hawakujiwekea. Hiyo ni nadharia ya Nyerere na sio ya nchi. Kaunda alikuwa na nadharia zake lakini waZambia hawasemi kuwa walijiwekea. Lenin alikuwa na nadharia zake, lakini sio za warusi.

Hivyo watanzania kung'ang'ania kuwa ukitaka kuwa na maendeleo unahitaji vitu vinne ni kujipunguzia uwezo wa kuangalia matatizo yao kiundani zaidi. Hii ni kwa sababu tupo tunaoamini ukitaka maendelelo kuna vitu vingi zaidi ya hivyo vinne. Na kuna watu kama Nyani Ngabu wanaoamini kuwa maendeleo ya nchi yanatokana na watu walivyo. Ni watu wanaochagua viongozi, ni watu wanapanga siasa na ni watu wanaotumia ardhi
Ni kweli ilikuwa nadharia ya Nyerere ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama tawala na serikali tawala. Kwa muda wote hakutokea mtu wa kuipinga na ilibaki kuwa nadharia ya nchi hata kama hutaki ukweli ndio huo.
Inaweza kuwa sio sahihi, na kwa mujibu wako tunahitaji vitu vingi zaidi ya hivyo, kwa bahati mbaya hujataja hata kimoja.
Kama unadhani Ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora havina ukweli na havifai, basi chambua kimoja baada ya kingine ili utuelimishe. Endapo hatuweza ni wazi kuwa mambo hayo ni muhimu. Tunakupa ukumbi ufafanue

Nchi kama Marekani, Canada n.k zina ardhi ya kutosha na sasa vinavutia wahamiaji kama manpower ambayo nadharia ya Nyerere inasema ni watu. Sera zao za uchumi ni nzuri kulinganisha na zetu na wana uongozi bora, mambo yanayohitimisha nadharia ya Nyerere kama unavyoiita.

China na India sio tu zinakubalika katika kasi ya maendeleo bali pia idadi ya watu ambayo kiuchumi ina mantiki sana kwa uchche tu wa kusema
Mtu anayekwambia kuwa China haikuwa tajiri mwambie akasome tena historia. Haikuwa tajiri kwa mtazamo wa kimagharibi lakini walikuwa na ingridients za maendeleo
Hakuna mahali niliposema China haikuwa tajiri kwa mantiki yako. Nilichosema ni kuwa katika nchi zenye uchumi China ilikuwa haitajwi. Kama ulikuwa na ufahamu katika miaka ya 60 na 70 China ilitambulika kama nchi zinzoendelea haikuwa katika kundi la industrialized countries. Kama unafuatilia utakumbuka kitu kilichokuwa kinaitwa super power, G7, G9 na sasa G20.
Katika dunia ya leo china ni ya pili kwa uchumi na inatakiwa kuwa na maamuzi katika masuala muhimu ya kimataifa.
Hali haikuwa hivyo miaka ya nyuma.

Kuhusu 'ingredients za maendeleo' hata sisi tunazo, kinachotushinda ni jinsi gani tunazitumia ili ziinue hali za wananchi. Ndipo tatizo la uongozi linapokuja. Fuatilia historia uone Spain na Portugal ziliyokuwa zinaongoza katika dunia, na jiulize kwanini leo zinahitaji bail out. Kwahiyo kuwa na meli zilizokuja Afrika mashariki kama zile za waajemi na waarabu haitoshi kuifanya nchi fulani ionekane kuwa na maendeleo.

Matatizo ya umeme yanatokana na hali ya hewa na ongezeko la watu. Kulikuwa hakuna sera yoyote mpaka matatizo yalipotokea. Na kulikuwa hakuna sera kwa sababu nchi ina vyanzo vya maji. Nchi kama Kenya have to think harder na matokeo yake wana sera zinazoeleweka kwenye nishati.[/QUOTE]Katika miaka 26 iliyopita ni sera gani ya nishati imetekelezwa kwa awamu tatu za uongozi. Hivi huoni hapo unakubaliana nasi kuwa uongozi ni tatizo!

Hali ya hewa ni visingizio kwasababu mwanadamu siku zote lazima awe tayari kukabiliana na mazingira.
Hatuna matatizo makubwa ya hali ya hewa kama unavyodhani. Marekani leo hii kuna misiba huko Indiana na hiyo ni kila mwaka lakini bado wanakabiliana na hali hiyo na kusonga mbele.
Japana wamepigwa na tsunami lakini leo wapo imara kana kwamba hakikutokea kitu.
Nchi kama Norwa, Denmark, Canada, Sweden hali zao za hewa ni za misimu tena michache sana. Yaani hali ya hewa ni extreme iwe majira ya joto au baridi. Bado wanakabiliana na hali hiyo na kutuuzia kama si kutusaidia chakula n.k.

Ongezeko la watu sio kitu kinakuja kama mvua. Kuna sensa zinafanyika na tafiti zinazoonyesha ni jinsi gani ongezeko la wanananchi linatokea. Tatizo hakuna uongozi unaotafsiri data hizo na kuziweka katika uhalisi kwa siku za baadaye.
Hapa pia unakubaliana na nadharia ya Nyerere kuwa upungufu wa nishati ni matokeo ya kuwa na uongozi usio na mtazamo wa leo au kesho.

Labda unijibu tu kuwa, hivi kiongozi anayeamini mbunge anapaswa kugawa pesa anaweza kufikiria nini katika kuoanisha ongezeko la watu na nishati. Hapa huoni tatizola uongozi kweli!
 
Ngur3,

Sijasema kuwa uongozi sio kitu muhimu. Nilichosema kuwa uongozi ni sehemu moja tu ya ufumbuzi wa matatizo. Nasema hivyo kwa sababu nataka watanzania wawe wana-manage expectations zao pale wanapochagua viongozi wapya.

Kuhusiana na China, Marekani, Canada na nchi nyingine, ni kweli kuwa uongozi wao umesaidia. Lakini uongozi wao haukushuka kutoka mbiguni kama chakula cha wana waIsrael.

China inapata viongozi wake kwa njia ya ukidikteta fulani. Kwanini basi viongozi wa China wawe wanawajibika kwa nchi na wananchi wao kuliko viongozi wa Tanzania wanaopatikana kwa kupigiwa kura za wananchi kila baada ya miaka mitano? Hii peke yake inaonyesha kuwa we aren't fit for Western Democracy.

Nimeangalia hotuba ya spika Makinda. Kawadanganya wananchi lakini alipotoa nafasi ya maswali wakawa wanamuuliza maswali ya huduma za bure. Kwani hakutokea mtu jasiri na kumpa vipande vya mawazo?
 
Fukara kinyume chake ni tajiri? Toa maana ya fukara unavyoelewa wewe.
Aaaah mkuu wangu hata hili neno tuanze kubishana.. Fukara ni maskini wa mali, mtu asiyekuwa na uwezo, rasirimali wala means of subsistence... Chakula, nguo, malazi yote Mungu ndio anajua japokuwa ni mzima wa afya na viungo > huyu ndiye fukara...
 
Kwa nini Afrika kusini mwa jangwa la sahara ni maskini? Na kwa nini Afrika Kusini (nchi) ni tajiri kushinda nchi zingine za Afrika?

Bila wazungu kulowea kule unadhani Afrika Kusini ingekuwa hapo ilipo sasa?
Kwa sababu sisi ktk mila na desturi zetu Utajiri haukuwa na tafsiri kama ya wazungu kama alivyosema Zakumi, tuliishia zaidi ktk kukidhi mahitaji yetu.. Na ndiuo maana utakuta hakuna Historia ya mtu mweusi kwenda nchi za nje kutafuta utajiri au mali maana tulijitosheleza kwa kile tulichokuwa nacho.

Hawa wenzetu kutokana na hali ya mazingira na historia ya nchi zao walihitaji vitu vingi ambavyo havikupatikana kwao (necessities)hivyo kulazimika kutoka nje maana vile walivyokuwa navyo havikuweza kukidhi mahitaji yao. Ukitazama nchi zote walizoenda wazungu na kuziendeleza ilitokana na soko la mahitaji yao makwao iwe dhahabu, baruti, chuma mazao ya cash crops au food.

Kama kesho dhahabu ikishuka bei hadi Tsh 100 kwa Ounce utaona hakuna mtu tena Bulyanhulu ama Buzwagi kwa sababu sisi wenyewe hatuthamini vitu hivi sawa na wao. Wao walianza kuthaminisha vitu kwa fedha sisi ndio kwanza tulitumia barter system na hata fedha zetu hatuna thamani nazo isipokuwa kwa kuthaminishwa na wao. Tunatofautiana sana upeo wa fikra maana wao wanafikiria kuishi hata mwezini sisi hatuoni umuhimu huo kwa fikra za kwamba kila kitu tukitakacho kipo within our reach, Mungu kisha tuandalia makazi yetu kuwa haya.

Sasa na ili waweze kuvipata vitu hivyo iliwabidi wajenge Empire zao kwa kuanza na kupora nchi zetu..Ni kama alivyosema tena Zakumi, wakati EL anapora mafedha kibao na kujenga majumba . viwanda na kadhalika Mmasai haelewi kitu lakini ukiwapima kwa jicho la maendeleo tunayopewa picha na wazungu tutasema El baabu kubwa bila kujali kauppataje utajiri huo.
 
Jmushi1 and Nguruvi2,

Siku zisije mkawa very dissapointed. Dr Slaa anaweza kuchaguliwa kuwa rais na akamaliza muda wake nchi ikiwa bado masikini.

Wanafalsafa wa uchumi wamesha-prove kuwa uongozi ni kitu muhimu but it isn't the only prerequisite for development. Africa ina-nchi zaidi 40, na huwezi kusema kuwa katika nchi zote hizi hajawahi kutokea kiongozi mzuri.

Nyerere mliyemtumia kwenye mifano, tulikaa naye na aliongoza kwa miaka 23 na watu tulimchoka.

Kwanini mzungu ambaye ni dikteta, mnyonyaji, kupe, mla rushwa anaweza kuja Afrika na kujenga nchi wakati mwaAfrica mwenye kukaribia utakatifu jasho linamtoka?
Labda nikujibu swali hili kwa jinsi navyolifikiria mimi na mtazamo wangu. Nchi za kiafrika hatuna maendeleo kwa sababu hatuna necessities zetu zaidi ya kukidhi necessities za wazungu. Tumepanda zao la Korosho, Pamba, Katani na kadhalika kwa sababu yao na sii yetu maana kama tungelima pamba ilit utengenezen nguo zetu tungefikiria kuwa na viwanda vya nguo. tungefikiria kuwa na wajuzi wa kuchora na kushona (designers) lakini leo imefikia hata kuvaa kwetu tunafanya kwa kuiga zaidi ya mahitaji yenyewe. Ndio maana nasi siku hizo tuna show za mavazi ya kikwetu lakini targeting masoko ya nje kuwaizia Ulaya.

Sii dhahabu, chuma, uranium, vinyago wala wanyama yoote haya tunayafanya kwa sababu ya mahitaji ya mzungu lakini huwezi kuona mzungu akivumbua kitu kwa ajili ya mahitaji ya Mwafrika au Mchina. Wewe Mdanganyika ambaye unakihitaji ndio utaagiza kitu hicho kutoka kwao lakini wao kamwe hawatengenezi kitu bila kutokana na kukihitaji. Chukulia mfano wa ugonjwa wa malaria tu, bila huruma za UN upande wa madawa basi hata dawa ya malaria au hata vyandarua tusingekuwa navyo kwa sababu sisi hatutazami mahitaji yetu na kuyatafutia ufumbuzi bali tunatafuta maendeleo kuwa kama Ulaya.

Na magonjwa yote ya Tropical ndio yanatuua zaidi lakini hakuna nchi hata moja ya kiafrika imeweza kugundua kinga au dawa za ponya kwa sababu elimu tunazopewa ni kuwahudumia wao zaidi ya kukabiri mahitaji yetu sisi wenyewe. hatuna maji tunapigwa siasa, hatuna Umeme - siasa, Shule - siasa, Afya - siasa, hata Kilimo - Siasa yaani sisi ni malimbukeni na ndio mnaana hatuna vision kwa sababu mahitaji yetu pia ni ya ku copy na kupaste..
 
JM,

Tanzania ina matatizo mengi na uongozi ni moja wapo. Na nitafurahi kama uongozi utabadilika kesho. Na kuhusiana na ku-take risks, people don't take risks for sake of it. You have to take risks and fall down somehow safely.

Unataka watanzania wa-take risks kwenye nchi inayowatukuza waalifu. Chenge anaiba pesa, akirudi kwao watu wanafanya maandamano ya kumpokea. Lowassa anajiuzulu uwaziri mkuu, kwao wanasikitika na mkewe kutunga kitabu cha dini.
Zakumi, sidhani kama unataka tuingie kwenye mjadala wa namna ya kutake risk ya kubadili uongozi, huo ni mjadala mwingine.

Ni kweli kuwa baadhi yetu tunakubaliana kuwa uongozi ndiyo the main obstacle, lakini haina maana kuwa tunajadili namna ya kupata uongozi mpya kwenye mjadala huu.

So sitoweza kuzungumzia lolote kuhusiana na hoja yako ya "You have to take risks and fall down somehow safely", because i believe that the "hows" will divert this disscussion...Ila nataka kukumbushia tu kwamba hiyo safety inawezekana with a solid new people's constitution.

Hilo litafix hoja yako ya "Kutake risk kwenye nchi yenye kuwatukuza wahalifu"

@Mkandara,hoja yako ina nguvu, however usisahau kuwa wananchi wakiwa na kazi na vipato, wataspend, na hivyo wafanyabiashara wataya target mahitaji yao na hivyo kukuza soko la ndani na uchumi kukuwa.Hilo litasaidia kutokuwategemea wazungu peke yake.Hiyo ni hatua ya kwanza, lazima tuwe na uwezo wa kutegema soko la ndani kwa bidhaa zetu.

So tunarudi kwenye kushindwa kwa uongozi ku create jobs nk, its a total failure, but i still belive that we can!
 
Sikuwa na maana uliyofikiria. Ukweli ni kuwa kati nchi zilizoendelea people are risk takers katika fani zote. Kitendo cha Bill Gates kuacha shule na kuanza biashara ni risk taking adventure.

Mchukue mtanzania aliyetoka nje ya DSM na kwenda kusoma UDSM. Mpe nafasi nzuri na mwambie aachie masomo kama Bill Gates. Je atakubali?

Mmarekani anaweza kuachia shule kwa sababu akianguka,ataanguka salama. Anaweza kurudi tena shule. Mmarekani akiandamana kuipinga serikali ana uhakika atarudi nyumbani mzima.

Kwa Tanzania usalama haupo. Hivyo watu sio risk takers. Lakini wanaanza kubadilika taratibu.
 
Labda nikujibu swali hili kwa jinsi navyolifikiria mimi na mtazamo wangu. Nchi za kiafrika hatuna maendeleo kwa sababu hatuna necessities zetu zaidi ya kukidhi necessities za wazungu. Tumepanda zao la Korosho, Pamba, Katani na kadhalika kwa sababu yao na sii yetu maana kama tungelima pamba ilit utengenezen nguo zetu tungefikiria kuwa na viwanda vya nguo. tungefikiria kuwa na wajuzi wa kuchora na kushona (designers) lakini leo imefikia hata kuvaa kwetu tunafanya kwa kuiga zaidi ya mahitaji yenyewe. Ndio maana nasi siku hizo tuna show za mavazi ya kikwetu lakini targeting masoko ya nje kuwaizia Ulaya.

Sii dhahabu, chuma, uranium, vinyago wala wanyama yoote haya tunayafanya kwa sababu ya mahitaji ya mzungu lakini huwezi kuona mzungu akivumbua kitu kwa ajili ya mahitaji ya Mwafrika au Mchina. Wewe Mdanganyika ambaye unakihitaji ndio utaagiza kitu hicho kutoka kwao lakini wao kamwe hawatengenezi kitu bila kutokana na kukihitaji. Chukulia mfano wa ugonjwa wa malaria tu, bila huruma za UN upande wa madawa basi hata dawa ya malaria au hata vyandarua tusingekuwa navyo kwa sababu sisi hatutazami mahitaji yetu na kuyatafutia ufumbuzi bali tunatafuta maendeleo kuwa kama Ulaya.

Na magonjwa yote ya Tropical ndio yanatuua zaidi lakini hakuna nchi hata moja ya kiafrika imeweza kugundua kinga au dawa za ponya kwa sababu elimu tunazopewa ni kuwahudumia wao zaidi ya kukabiri mahitaji yetu sisi wenyewe. hatuna maji tunapigwa siasa, hatuna Umeme - siasa, Shule - siasa, Afya - siasa, hata Kilimo - Siasa yaani sisi ni malimbukeni na ndio mnaana hatuna vision kwa sababu mahitaji yetu pia ni ya ku copy na kupaste..
Mkuu Mkandara, kuna wakati tunawalaumu wazungu kwa makosa yetu. Wao walitumia elimu yao kuvumbua viwanda na hakika sisi tumeiga teknolojia yao ya vitu kama viwanda vya nguo si kwa faida yao bali kwa faida yetu ili tusivae vibwende kama akina Rumanyika, Kimweri n.k.

Tulikuwa na viwanda vyetu tukitengeneza nguo za viwango vyetu. Kabla wazungu hawajasema tuvifunge ili wapate pamba, genge la wahuni wakajikusanya Zanzibar na kupitisha azimio la kuagiza mitumba, vibiriti, kuku waliokaa katika friji miezi 3, chupi za mitumba n.k Hawakufanya kwa shinikizo au manufaa ya taifa, walifanya hivyo ili waweze kugawana viwanda na kuuza chuma chakavu kama Mang'ula, Moproco, Mutex n.k. Hapa si tunawasingizia wazungu!

Tunawasingizia kwasababu ugunduzi wa dawa ya malaria yasiyokuwepo kwao ni jukumu letu na sio lao.
Wao wamewekeza katika maradhi kama ya moyo kiasi kwamba kifo cha heart attack kinachunguzwa sana maana ni tatizo wanaloweza kukabiliana nalo. Sisi hatuwekezi katika R&D tunawasubiri wao.

Fuatilia bajeti ya research institutes za Tanzania utashangaa, wakati huo huo tumewekeza katika kununua VX na kulipana posho.Unakumbuka Hitler alivyoweza kuwabana egineers kubuni vifaa vya kivita kwa amri!
Nakuhakikishia kiongozi kama spika Makinda anayewaza mishahara ya Kenya hana wazo la ukubwa wa tatizo la malaria.

Mkuu, kwa ufahamu wangu hatuhitaji dawa za malaria na pengine uvumbuzi wake usingetusumbua sana.
Wenzetu wa Mexico walikuwa na tatizo la malaria kama sisi, lakini sasa ni historia.

Wao wanajua usipokuwa na contact na mbu huambukizwi malaria, na wanfahamu kuwa elimu kwa umma ikiwa ni pamoja na utumiaji wa dawa na kuziba mazalio ndiyo dawa pekee. Katika viongozi wetu pengine ni watatu au wanne wanaojua habari ya mexico, sasa hapa tunawalaumu wazungu kwa lipi?

Tuliletewa msaada wa mradi wa malaria Dar es salaam. Wajapan walipokabidhi mradi viongozi wakagawana magari na vifaa mradi umekufa. Kwanini tuwalaumu Wajapan kwa hili na si kuona tatizo la uongozi wetu.

Ninakuhakikishia kuwa baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wabunge, ukiwakusanya diamond jubilee uwaulize kwanini mradi wa malaria, lower moshi irrigation vimekufa hakuna anayeweza kukupa maelezo ya kisayansi ya kujitosheleza.Kama unataka majibu mengi uliza;ni VX au Vogue ya aina gani na bei zake! Hapa wazungu tunawalaumu kwa nini!
@Mkandara,hoja yako ina nguvu, however usisahau kuwa wananchi wakiwa na kazi na vipato, wataspend, na hivyo wafanyabiashara wataya target mahitaji yao na hivyo kukuza soko la ndani na uchumi kukuwa.Hilo litasaidia kutokuwategemea wazungu peke yake.Hiyo ni hatua ya kwanza, lazima tuwe na uwezo wa kutegema soko la ndani kwa bidhaa zetu.So tunarudi kwenye kushindwa kwa uongozi ku create jobs nk, its a total failure, but i still belive that we can!
Niongezee tu mfano mmoja, utalii umefanywa kitu cha wageni. Kwani kuna ubaya gani ukiwa na soko la ndani na la nje? Soko la ndani litumike katika ku sustain miradi na la nje kwa development.

Utashangaa yametengwa mabilion kuweka matangazo ya utalii Heathrow na CNN! Hakuna hata jitihada za kutangaza utalii kwa watu wa ndani. Mimi nakumbuka miaka ya nyuma utalii ulitangazwa hadi mashuleni, na nimetembelea mbuga za Selous, Mikumi kama sehemu ya elimu lakini baadaye nimejikuta nakwenda Ngorongoro, Serengeti n.k kwasababu tayari nilishapata hamasa.

Najua ipo hoja kuwa tunaongelea umasikini na wangapi watamudu! Hoja hii ni rahisi sana jibu lake kwasababu katika mashirika yanayotengeneza faida za mabilioni ni viwanda vya bia. Wateja ni akina nani?

Hoja ni kuwa ni lazima ujue namna ya kuitumia jamii yako kwa manufaa ya jamii hiyo hiyo ili kukata 'vicious circle' ya umasikini. Kuna watu wanoweza kutusadia au ni hawa viongozi wa matangazo Heathrow kwasababu ya 10%?
 
JM,

Sikuwa na maana uliyofikiria. Ukweli ni kuwa kati nchi zilizoendelea people are risk takers katika fani zote. Kitendo cha Bill Gates kuacha shule na kuanza biashara ni risk taking adventure.

Mchukue mtanzania aliyetoka nje ya DSM na kwenda kusoma UDSM. Mpe nafasi nzuri na mwambie aachie masomo kama Bill Gates. Je atakubali?

Mmarekani anaweza kuachia shule kwa sababu akianguka,ataanguka salama. Anaweza kurudi tena shule. Mmarekani akiandamana kuipinga serikali ana uhakika atarudi nyumbani mzima.

Kwa Tanzania usalama haupo. Hivyo watu sio risk takers. Lakini wanaanza kubadilika taratibu.
Zakumi, kazi zikiwepo, uchumi utakuwa mzuri tu!Huwa nashangaa sana watanzania eti viongozi wanawaita wavivu nk, Mkapa kweli hana huruma.Ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, hawajui majukumu yao hawa viongozi wetu.

Turudi tu kwenye pointi ya mjadala huu na hususan hoja yako hapo juu, mtu kama Bill Gates alifanya alivyofanya kwasababu ulizozitaja, isipokuwa kwa kuongezea, bado tunarudi pale pale, uchumi mzuri unaletwa na kazi, wananchi wapate kazi zenye kuwaingizia vipato, thats the bottomline.Gates asingethubutu kudrop out kama kusingekuwa na potential to succeed!Ni uchumi wenye nafasi kwa kila mtu, yani opportunities na growth potential.

Kwa wamarekani, sijui kuhusu states nyingi, lakini wafanya kazi wengi wa banks ni high school leavers and many of them have worked their ways up, nazungumzia banks kwasababu ni mojawapo ya makampuni yenye hiring rate ambayo siyo mbaya, at least based on my experience.

Kwenye maeneo yenye viwanda, watu wenye familia za kati (middle class), na wenye kuishi vyema tu ni ma high school leavers tu na wamefanya kazi viwandani masiha yao yote na kuweza kuishi vizuri kabisa na kusomesha watoto nk, mambo kwasasa ni tofauti kutokana na hali ya uchumi kubadilika, uchumi kuelekea zaidi kwenye financial sector kuliko uzalishaji, lakini ukweli ni kwamba sisi hatujawahi kuexperince anything, ni kama vipofu kabisa ambao hatujawahi kuona(yani kiuchumi)

Hiyo ni topic nyingine, sitaki kwenda deep, mfano huo hapo juu unatosha kabisa kukuonyesha kwamba kama kuna kazi basi uchumi utakuwa bila wasiwasi, tutakuwa na watalii wetu hata kama wazungu wasipokuja hatutakufa njaa.

Lakini sasa kwetu high school wont get you anywhere hata kama mtu angetaka kufanya kazi yenye kipato baada ya kumaliza high school.

Ni viongozi wa marekani walitumia akili, na wakajua kabisa kuwa kijana wa high school ana uwezo wa kiasi gani kuweza kuajiriwa kwenye sekta za uzalishaji, finance nk. Na wakahakikisha kuwa elimu wanayoipata inaweza kuwawezesha kuweza kukabiliana na majukumu hayo ya kazi.Na hivyo ikawa rahisi kuweka kigezo cha kuajiriwa kuwa ni at least "high school graduate" Uchumi wenye ku provide opportunities ndo unaoweza kuwa sustainable.

Kwa marekani watu huwa wanaenda shule uchumi ukiyumba na ukianza kuwa safi wanakuwa wako more uquiped, yani mambo yao yako kiakili zaidi kwa maana ya strategics.

Tutakuwa na bidhaa zetu hatutategemea kutukanwa na wakenya kila kukicha.

Rasilimali, hata watu tunavyo, viongozi wenye akili hatuna!
 
Nguruvi3,
Mkuu samahani, ebu nambie unakijua kiwanda gani cha nguo ambacho kimeanzishwa na mwafrika, au hata owner ni mwafrika? utatafuta sana na Afrika nzima unaweza kukuta viwili navyo sana pengine utaambiwa ni vya serikali. Hatuna uvumbuzi wala kutengeneza vitu kulingana na mahitaji yetu, utamaduni huopo kutokana na kwamba deep down ktk fikra zetu tunakwenda shule kupata elimu ili tupate AJIRA...

Kama alivyosema Jmushi1 hapo juu kunijibu hoja yangu akisema ya kwamba kama wananchi watakuwa na kazi na kipato wataspend maana wafanyabiashara wataya target mahitaji hayo. Sasa jiulize kwa nini hadi leo gonjwa kubwa kama Malaria ambalo linayaingizia mashirika ya nje nabillioni, zaidi ya Bajeti yetu ya serikali kwa mwaka mmoja sisi hatujapata mtu alovumbua wala kutengeza dawa ama kinga ya Malaria? maana demand ya dawa ya kinga au ponya ipo kubwa sana, lakini tulishindwa vipi kuvumbua dawa tujenge kiwanda cha dawa ambacho kingetoa ajira kwa wananchi. Sii hilo tu mahitaji yetu yapo sehemu zote toka Maji, umeme, baiskeli hadi sindano na kadhalika..Ila tunaagiza toka nje.

Na nimekwisha sema huko nyuma ya kwamba kuwa na elimu ya sayansi na Teknoligia sio kuiga, hii ni ELIMU, elimu ambayo watu wote duniani husoma ili kuwawezesha wao kukabiri mahitaji yao kitaalam zaidi lakini kwetu imetumika sivyo. Sisi Elimu tunaipata ili tuajiriwe, tunaenda shule ili kumwandaa mtoto apate kuajiriwa kazi nzuri zaidi hata kama ana Phd.. maleongo ni tutumike (nguvukazi) na hivyo kusubiri ajira ambazo serikali haiwezi kuzizaa kulingana na mfumo uliopo bali serikali inaandaa na kuunda sera bora (siasa safi) za kutuwezesha kufanya utafiti yakinifu, uvumbuzi, uwekezaji, uzalishaji na usambazaji ili vitu hivyo viweze kuwafikia wahitaji. Hatuna utamaduni wa toka Utafiti hadi uzalishaji ktk kukidhi mahitaji yetu bali tunachukua njia rahisi za kuigeuza Tanzania iwe kama Ulaya..

Hizi fikra za kwamba Sisi sio maskini ila nchi yetu ndio maskini... ni maneno ambayo sijui kama watu wameyafikiria vizuri. Nchi yetu sio maskini, ina kila kitu toka vito, madini, mito, maziwa, miti, Upepo, jua la masaa 12, mabonde, milima, majabari yote haya ni UTAJIRI wa nchi yetu lakini maadam sisi tumeshindwa kuvitazama vitu hivi ili kukidhi mahitaji yetu na ya nje ndio maana hadi leo hatuna maji, umeme. chakula na kadhalika. hakuna connnection between WATU na MAZINGIRA na ndio umaskini unapochukua nafasi yake. Sisi ni MAFUKARA ktk nchi TAJIRI, sisi tumeshindwa kutumia elimu zetu kuunganisha vitu hvyo kwa sababu hatuna vision, hatuna necessities kutokana na Utumwa, imani zetu za dini na itifaki kuwa na nguvu zaidi ya Sayansi na Teknologia..Ndio maana Malaria inatuua tunasema kazi ya Mungu, leo hii ajali barabarani mwaka jana tu wameathirika ni karibu 30,000. Wastani wa waathirika 20,000 kwa miaka 10 iliyopita, bado hatujaangalia ajali za meli, boti na mitumbwi.

Na binafsi yangu siwalaumu wazungu hata kidogo kwa sababu najua fika kwamba wao hufanya uvumbuzi, utengenezaji na kadhalika kwa manufaa yao sasa iwe hata walitukanyaga, kututawala na kadhalika bado jibu linakuja waliyafanya waliyo yafanya kwa sababu ya kukidhi mahitaji yao. Hata wao walitawaliwa, tazama Historia ya Uingereza na hata Italia utakuta walitawaliwa vile vile tena miaka mingi zaidi yetu na kuingizwa utumwani lakini wao waliweza vipi kugeuza experience ya utumwa kuwa fundisho la kutotawaliwa tena na kuwa faida yao ktk kujilinda na kutumia elimu kukidhi mahitaji yao.

Matatizo yetu ni mengi sana hasa ukizingatia mifano kama ulonipa ya viwanda..Na ndio hapo tunasema Uongozi bora ni ule wenye vision anafahamu vizuri WATANZANIA na MAZINGIRA yake ili kuweka katiba na sheria ambazo zinamfunga Mtanzania ktk uzalendo, zitatakazo mwongoza Mtanzania ktk kuipenda nchi yake na kutafuta elimu na maarifa ili kufanya yaliyo bora ktk kukidhi mahitaji yetu wenyewe. Ile Ruksa ya Mwinyi ndio ulikuwa mwanzo wa disconnection baina ya Uongozi, watu na mazingira na ndio maana vijana waliiba vipuri vya viwanda hadi magari ya serikali - UDA na viwanda vyote nchini havikufa bure tulipoteza mwongozo.

Nyerere aliweza sana lakini baada yake hakna kitu japokuwa watu wengi wanashindwa kumwelewa. Leo hii KILIMO KWANZA kimeshindwa kwa sababu VIONGOZI wetu wameshindwa kuwahusisha WATU na ARDHI (MAZINGIRA) ktk mchakato mzima wa mkakati huo kiasi kwamba leo hakuna mtu anayetaka kulima japokuwa leo hii chakula sio ktk mahitaji tena ila ni ADIMU yaani supply imeshindwa kabisa kukidhi demand hivyo tunarushwa bei hata mchicha leo unaliwa na wenye uwezo. Kila siku idadi kubwa ya watu wanaingia ktk kundi la ufukara kutokana na kutokuwa na uwezo wa ku afford hata maharage, mchicha au dagaa..
 
Kwenye posti moja niliulizwa kutoa vitu vingine muhimu vya msingi vya kuleta maendeleo. Zaidi ya watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora naweza kusema kwa nchi za kiAfrika zinahitaji kitambulisho cha jamii, identity.

Tuna mgawanyiko mkubwa sana ndani ya mataifa yetu. Mgawanyiko wa kidini, kikabila, kimajimbo n.k. Tanzania ni nchi ya amani. Lakini ni watanzania wachache ambao wamevuka kasoro za kijamii na kumwangalia mtanzania yoyote kama ndugu yake.
 
Mkandara, adui yetu mkubwa ni yule anayenufaika na matatizo yetu, na wengi wao ndo wako kwenye powerfull positions, ni mtandao mkubwa unaoshirikisha pande zote, it is an industry on its own.

Swali ni vipi tutaweza kujinasua?

Kwa mfano huo mradi wa neti ni msaada wenye strings, ni lazima kuwe na makampuni ya marekani yenye kunufaika nk, na pia ni lazima kuwe na viongozi wenye kula ten pasenti ndani ya bongo nk.

Mbona marekani kulikuwa na malaria iliwasumbua sana na wameitokomeza, hata tukisadiwa tunasaidiwa based on our abilities to think.

Pia mataifa makubwa hususan marekani, wanalinda interests za makumpuni yao makubwa, hata hayo ya madawa, unakumbuka kuna kiwanda cha madawa kilipigwa mabomu na Clinton kule Sudan enzi zile Bin Laden akiwa kule?

Uvumbuzi wa dawa mpya lazima uwe chini yao na patent rights and so forth.
 
Back
Top Bottom