Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
alafu kuna viongozi wanakalia bungeni kutangaza viwanja vya kimataifa sijui MWANZA sijui songwe huku wakiacha RELI ya ati na TAzARA zinakufa.

Hivi jamani kuna uchambuzi umeshhafanyika hii miradi ya vinwaja vya ndege kama cha songwe itasaidia nini wananchi?

Preliminary analysys yangu naona Viongozi sometime wanajisahau kabisa na kuwek PRIORITY kwa mambo ambayo yanakidhi haja za wachache.

Effort kubwa ya kuwaondoela wananchi umasikini kwenye MIUNDOMBINU inatakiwa ilekezwe kwenye sekta ya RELI na si anga . Baada ya kupoteza pesa kuanzisha na Internationa Airport mpya nadhani busara zaidi tuwe na International railway station Mwanza, Dar Mbeya Kigoma etc

Hakuna uchumi duniani ambao unaweza kupata mafanikio bila miundo mbinu ya reli, bandari na umeme. Sisi katika haya yote ni hopeless. As you rightly put it, kwanini effort zisiende kwenye reli ya Tazara kutokea DSM - IRINGA - MBEYA - ZAMBIA, na badala yake wana concentrate kwenye uwanja wa ndege? What's the cheapest way for Mbeya na Rukwa kwa mfano to industrialise au trade na nchi za SADC, ndege au treni? Kweli viongozi wetu hawana priority, na mbaya zaidi ni kwamba ni watoto wetu ndio watakaokuja kulipa madeni haya, sio hawa viongozi, wao watafaidika na hizo ten pct, through such dubious projects. Uwanja wa ndege Songwe ungekuja baada ya uwepo wa reli ya kuaminika, not vice versa;
 
Tanzania ni masikini kwa sababu watu wake wanaridhika kirahisi, ama hawajui zaidi.
 
Wakuu kabla ya ku comment ni vizuri sana kama tutakuwa tuna data. Bila kuwa na informatin za uhakika, mambo mengi yatakuwa yanajadiliwa kwa kutumia hisia na ushabiki.

Kwa mfano, miradi mingi ambayo serikali ya Jk imeanzisha na kuingia mikataba nayo, ina unafuu kuliko marais waliopita. (tukimuondoa nyerere).
JK hajaua shirika la reli. Shirika la reli lilishauzwa kwa RITES tangu May 2005. Na ni serikali ya JK ndiyo iliyositisha huo ubinafsishaji.
Halafu, neo-colonialism inaweza kuepukwa iwapo wananchi watakubali na wataweza kuendesha biashara na makampuni ya umma kwa utaalam na kwa kujitolea.
Ila ukiangalia kwa undani zaidi, watanzania hatujabarikiwa kuwa na akili za kuvumbua (innovation). Hili ndiyo tatizo kuu, mengine yapo kwenye nchi nyingi tu ambazo pia zimeendelea kama vile S.Korea, Singapore... etc kuna ufisadi, ila mafisadi wao wanawekeza kwenye nchi yao, kwa hiyo impact yake economically ni negligibly low..
 
Hakuna uchumi duniani ambao unaweza kupata mafanikio bila miundo mbinu ya reli, bandari na umeme. Sisi katika haya yote ni hopeless. As you rightly put it, kwanini effort zisiende kwenye reli ya Tazara kutokea DSM - IRINGA - MBEYA - ZAMBIA, na badala yake wana concentrate kwenye uwanja wa ndege? What's the cheapest way for Mbeya na Rukwa kwa mfano to industrialise au trade na nchi za SADC, ndege au treni? Kweli viongozi wetu hawana priority, na mbaya zaidi ni kwamba ni watoto wetu ndio watakaokuja kulipa madeni haya, sio hawa viongozi, wao watafaidika na hizo ten pct, through such dubious projects. Uwanja wa ndege Songwe ungekuja baada ya uwepo wa reli ya kuaminika, not vice versa;
nchi zote za viwanda miundo mbinu kama reli ni sehemu muhimu sana ya uchumi. Kuanzia Marekani, China, Uingereza na hata South Africa. PM Margareth alipotaka kuibinafsisha reli kabisa Waingereza walimwambiaalia akae pembeni. Ujenzi wa reli nchini china na India ni wa kutisha. Ni usafiri rahisi na wa uhakika katika kusafirisha watu na bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tazara ilipokuwa inafanya kazi si wakazi wa kisaki, mlimba, makambako, mbeya n.k waliofaidi tu bali hata watumiaji wa bidhaa wa Dar na kwingineko walinufaika. Ni reli hiyo iliyosababisha mikoa ya nyanda za kusini ikaitwa the big four.

Kama tusingekuwa na reli usafiri wakati wa vita ya kagera ungekuwa mgumu sana. Kwa wale wenye kumbu kumbu ilikuwa ni rahisi kupata supply kutoka Dar kuliko kuzitoa Mwanza hadi Kagera. Huu ni mfano tu wa umuhimu wa miundo mbinu.

Uwanja wa KIA ulijengwa kwasababu ya biashara za mazao mikoa ya kaskazini pamoja na soko la utalii. Bado umuhimu huo unaonekana labda kwa aliyegoma tu kuelewa.

Uwanja wa Songwe Kiwira labda kama una makusudi mengine, endapo ni hili la kubeba maua na si uchukuzi wa mahindi ninashaka na timu inayofikri hivyo na iliyo plan kama kweli haihitaji matibabu.

Mchambuzi, KIA ipo na maua ya kanda ya kaskazini ni mengi na bora. Sijui ni tani ngapi zinapitia hapo. Ninafahamu ndege zinachukua maua kutoka Nairobi! Labda unisaidie maua yanaingiza kiasi gani ukilinganisha na mahindi na mchele au bidhaa nyingine kutoka kanda ya kusini. Ipo siku tutasikia Kisiju mkamba wanataka uwanja wa kimataifa kwasababu wanatoa mihogo mizuri sana!!!

Pengine ndiyo maana tumeamua kungo'a KM 1,844 za reli ili tujenge uwanja wa ndege kuuza shanga na maua! Akili zetu zinatutuma kuwa kuuza maua ambayo hatujaweza kuyakuza katika viwango kutatukomboa. Yale ya Arusha na Moshi hatujaweza kuyadhibiti ili tunufaike tunafikiri Songwe itakuwa tofauti.

Kama Mjerumani aliona umuhimu wa reli 1905, na sisi tunaona umuhimu kujenga kiwanja cha kuchukua maua na shanga mwaka 2012 bado tunasafari ndefu.
 
Wakati Kikwete anachukuwa nchi life span ya Mtanzania ilikuwa miaka 50 leo miaka 55. Hiyo inakuonesha kuwa afya imeboreshwa.

Ukirudia posts zangu nasema maendeleo bado, miaka 120 toka aondoke Nyerere, yeye ndio alitumaliza kabisa. Mwinyi alianza Alif kwa kijiti. Kwa hiyo hesabu toka siku aliyoanza Mwinyi Alif kwa kijiti baada ya miaka 120 ndio tutahitimu. Kabla ya hapo, hakuna muujiza, labda hayo mafuta na gas yatoke kwa wingi halafu tuwalete wazungu washike sehemu muhimu. ndio hapo tutakata nusu ya hiyo 120.

Inaonesha kuwa kuna tatizo hapa. Sujio maana ya life span ni nini na inahusiana vipi na afya, unless uwe malaria Sugu, mtu ambaye ani islamist anayekuja jamvini kuleta pumba na sio kujadili issues zinazoisumbua Tanzania. Lakini kuna tatizo katika kuiona Tanzania ya sasa ikoje. Leo hii hapa Tanzania ni mpumbavu asiye na akili tu, ndiye anayeweza kusema life expectancy ya mtanzania imeongezeka (labda wewe ndio unaiita life span). Ni kitu gani kinachohusiana na afya ya mtanzania amekifanya JK na kuongeza life expectancy ya mtanzania kwa mwaka tangu aingie madarakani?

Hakuna anayepinga kuwa Umaskini upo tanzania, lakini kinachosemwa hapa serikali yetu inachangia kutudunisha, JK na serikali yake ametoa mchango mkubwa zaidi, na pia mentality za baadhi ya watu (wasio na elimu na wajinga) za kuridhika na vitu vidogo vodogo, kama kula chips mayai, bia, kuwa na vimada wengi, kuona ghorofa limejengwa katikati ya mji na kudhani kuwa ndio maendeleo ya nchi.

Siku JK alipoingia madarakani alikiri wazi kuwa amechukua "nchi yenye uchumi imara". Kwa kuwa alipokea nchi kutoka wa watu serious, sio wababaishaji. Look at the economy today, JK mwenyewe anasema serikali haina pesa.

Si kweli kuwa Mwinyi alipoikea nchi mbaya kivile. Kulikuwa na challenges for sure, lakini alipokea nchi very stable na ni yeyey alianza kuingiza elements za uswahili serikali. Lakini hakuna la maana sana katika kuwajadili waliopita. Let us go forward, tuwe na mawazo ya kujenge.
 
Life expectancy haipimwi katika kipindi kifupi na kuna vigezo sasa sijui mwenzetu anavitumia vipi. Wenzetu wako 88 to 98 sisi tunajivunia 55 kama basi ipo!!! .
By the way ni namba tu, je zina reflect real life ya vitoto vinavyokufa 0-5 kutokana na umasikini.

2005 inflation ilikuwa single digit, 2012 inflation 20%.
Anyway turudi kwenye mada
 
.......Mchambuzi, KIA ipo na maua ya kanda ya kaskazini ni mengi na bora. Sijui ni tani ngapi zinapitia hapo. Ninafahamu ndege zinachukua maua kutoka Nairobi! Labda unisaidie maua yanaingiza kiasi gani ukilinganisha na mahindi na mchele au bidhaa nyingine kutoka kanda ya kusini. Ipo siku tutasikia Kisiju mkamba wanataka uwanja wa kimataifa kwasababu wanatoa mihogo mizuri sana!!!

Hili swali lako ndio linaonyesha bado hatujitambua na kujua ni VIPAUMBELE GANI VITATUTOA hapa tulipo twende pale.
Sasa itakuwa kichekekesho kama tunajenga uwanja wa ndege kwa ajili ya soko la maua lakini hakuna anayejiuliza
  • kwa nini Mahindi na mchele unaharibikia chunya au Rukwa wakati watu wanakufa njaa maeneo mengine .
  • Kwa nini bei ya mchele wa chunya iwe iwe mara tatu ukifia kigoma
  • Kwa nini iwe kazi kusafirisha mafuta ya mawese kutoka kigoma kwenda kwenye viwanda vya kusindikaia mafuta ya kula vya mwanza?
Na kama ni sababu za maua basi kwa akili za namna hii tungekuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Musoma siku si nyingi sana toka nyerere sababu ya mbuga ya serengeti amabayo ni ya kipekee duniani. Haya mambo ya maua kama sababu uwanja wa ndege ni sabbau za KISIASA.

Kwenye uhaba wa resouces na finance ikiwa moja ya resource kuu tunahitaji watu wafanye maamuzi na vipaumbele sahihi. Kwangu Songwe international Airport wakati tazara Iko hoi ni Political Project. Hauna mchango wa kuondoa umasikini kwa mwanachi

Badala ya SONGWE IA tulitakiwa tusikie mradi wa kupunguza muda wa safari kati ya Dar na Mbeya kwa treni ya Tazara. Lakini nadhani kwa sasa muda wa safari kwa tazara umekuwa double
 
nchi zote za viwanda miundo mbinu kama reli ni sehemu muhimu sana ya uchumi. Kuanzia Marekani, China, Uingereza na hata South Africa. PM Margareth alipotaka kuibinafsisha reli kabisa Waingereza walimwambiaalia akae pembeni. Ujenzi wa reli nchini china na India ni wa kutisha. Ni usafiri rahisi na wa uhakika katika kusafirisha watu na bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tazara ilipokuwa inafanya kazi si wakazi wa kisaki, mlimba, makambako, mbeya n.k waliofaidi tu bali hata watumiaji wa bidhaa wa Dar na kwingineko walinufaika. Ni reli hiyo iliyosababisha mikoa ya nyanda za kusini ikaitwa the big four.

Kama tusingekuwa na reli usafiri wakati wa vita ya kagera ungekuwa mgumu sana. Kwa wale wenye kumbu kumbu ilikuwa ni rahisi kupata supply kutoka Dar kuliko kuzitoa Mwanza hadi Kagera. Huu ni mfano tu wa umuhimu wa miundo mbinu.

Uwanja wa KIA ulijengwa kwasababu ya biashara za mazao mikoa ya kaskazini pamoja na soko la utalii. Bado umuhimu huo unaonekana labda kwa aliyegoma tu kuelewa.

Uwanja wa Songwe Kiwira labda kama una makusudi mengine, endapo ni hili la kubeba maua na si uchukuzi wa mahindi ninashaka na timu inayofikri hivyo na iliyo plan kama kweli haihitaji matibabu.

Mchambuzi, KIA ipo na maua ya kanda ya kaskazini ni mengi na bora. Sijui ni tani ngapi zinapitia hapo. Ninafahamu ndege zinachukua maua kutoka Nairobi! Labda unisaidie maua yanaingiza kiasi gani ukilinganisha na mahindi na mchele au bidhaa nyingine kutoka kanda ya kusini. Ipo siku tutasikia Kisiju mkamba wanataka uwanja wa kimataifa kwasababu wanatoa mihogo mizuri sana!!!

Pengine ndiyo maana tumeamua kungo'a KM 1,844 za reli ili tujenge uwanja wa ndege kuuza shanga na maua! Akili zetu zinatutuma kuwa kuuza maua ambayo hatujaweza kuyakuza katika viwango kutatukomboa. Yale ya Arusha na Moshi hatujaweza kuyadhibiti ili tunufaike tunafikiri Songwe itakuwa tofauti.

Kama Mjerumani aliona umuhimu wa reli 1905, na sisi tunaona umuhimu kujenga kiwanja cha kuchukua maua na shanga mwaka 2012 bado tunasafari ndefu.

Ni matumaini yangu kwamba Faiza ameyasoma maelezo yako. Hajui kwamba hata mafanikio ya uwanja wa ndege wowote katika nchi iliyoendelea unategemea sana uwepo wa reli kuelekea uwanjani hapo. Katika nchi kavu na anga (ukiachia kwenye maji - meli), Reli ni the cheapest means kusafirisha bidhaa na abiria in huge volume per kilometre, ikifuatiwa na barabara. Pia dada yetu Faiza hafikirii faida ya reli in terms of linkages in the local economy na spill over benefits ambazo zinakuja na uwepo wa reli mule pote inapopita, tofauti na uwanja wa ndege. Labda kama wataweka kiingilio kwa wananchi mbeya kupanda kule juu kutazama ndege na kupungia wasafirishaji maua. Vinginevyo tusije kushangaa baadae kusikia kuna twiga na nyati wametoroshwa kutokea katavi.
 
Wakuu kabla ya ku comment ni vizuri sana kama tutakuwa tuna data. Bila kuwa na informatin za uhakika, mambo mengi yatakuwa yanajadiliwa kwa kutumia hisia na ushabiki.

Kwa mfano, miradi mingi ambayo serikali ya Jk imeanzisha na kuingia mikataba nayo, ina unafuu kuliko marais waliopita. (tukimuondoa nyerere).
JK hajaua shirika la reli. Shirika la reli lilishauzwa kwa RITES tangu May 2005. Na ni serikali ya JK ndiyo iliyositisha huo ubinafsishaji.
Halafu, neo-colonialism inaweza kuepukwa iwapo wananchi watakubali na wataweza kuendesha biashara na makampuni ya umma kwa utaalam na kwa kujitolea.
Ila ukiangalia kwa undani zaidi, watanzania hatujabarikiwa kuwa na akili za kuvumbua (innovation). Hili ndiyo tatizo kuu, mengine yapo kwenye nchi nyingi tu ambazo pia zimeendelea kama vile S.Korea, Singapore... etc kuna ufisadi, ila mafisadi wao wanawekeza kwenye nchi yao, kwa hiyo impact yake economically ni negligibly low..
Dah naona wana janvi tumekomalia kubishana juu ya Utawala wa Nyerere dhidi ya JK... Hivi hii nayo inaweza kuwa sababu ya Umaskini wetu maana tunabishana vitu vilivyokwisha pita na sii ya leo..

Soby kwa kukusahihisha tu ni kwamba RITES walisaini mkataba chini ya JK na nakumbuka vizuri sana wakati huo ndio kwanza Pinda anaingia madarakani. Na nakumbuka hata hotuba yake alosisitiza (kwa ukali) kwamba RITES ndio wamekwisha pitishwa na ndio watakao endesha TRC baada ya kushinda mchujo.. kama sikosei ilikuwa mwaka 2007. Mipango ya kuwachukua RITES ilifanyika Lowassa akiwa madarakani kwa hiyo usitake kurudisha calender nyuma ili mradi kumsafisha JK wakati yawezekana kabisa haikuwa wito wake. Hasara ndio hii tunayo leo sasa tunashindwa nini kuikarabati reli ya kati? Tumeshindwa nini kuboresha bandari za Tanga na Mtwara toka mabadiliko miaka 27 iliyopita..

Hivi kweli wenzangu hamuoni makosa anayoyafanya JK kujenga castle juu ya mchanga na mnayaita maendeleo wakati infrastructure mbovu kabisa.. hata iwe hayo maghorofa yanajengwa wakati hatuna ziada ya nguvu ya maji, umeme, barabara na hata sewerage system ni ile toka Mjarumani!..Hivi kweli tupo radhi kuyaona makosa ya Nyerere ili kujenga hoja kama ndio sababu ya kukwama na hatuwezi kutoka pamoja na elimu mlizokuwa nazo..

Nakumbuka sana wakati wa Nyerere vijana wengi walikuwa na ubunifu tena sio wasomi bali vijana wa mtaani tu. Mkokoteni ni ubunifu mmoja wapo tena basi nakumbuka vizuri kuna vijana walikuwa wakitengeneza hata radio za mbao, na hata hivyo viatu vya matairi ilikuwa ubunifu ambao wazungu huuthamini zaidi ya kila kitu. Sasa ikiwa mtu amegundua sole ya kiatu toka tairi la gari ni bora zaidi tumeshindwa nini sisi kuendeleza ubunifu ule kwa kuongezea tu ngozi au plastic juu. Hiyo mikokoteni kuiwekea motor badala ya kurudi ktk baiskeli, basi hata kitu katikati yake.

Hivi kweli tumefumbia macho kuona kwamba kila kitu Dar na Tanzania nzima ni kutoka nje tena China toka furniture za chipboard badala ya mwininga kuboreshwa vile vile. Hivi kunamtu amewahi kuona mbao ya Mnazi inavyopendeza?..Kwa nini toka tumeingia Ubepari tumekuwa wavivu hata wa kufikiri na ubunifu.

Leo hii wanawake wako radhi kununua bodyspray feki ya Victoria Secret kutoka China kwa Tsh 30,000 wakati marashi ya Udi na maua yanaweza kabisa kubuniwa na kuwa perfume nzuri isipokuwa tunalima maua kwa fikra zetu ni kuyauza Ulaya bila kujua kwamba ni maua hayo hayo tunayosafirisha kwa bei ya mali ghafi ndio yanayotengeneza manukato (perfume) tunazonunua as finished product kwa Tsh 150,000. Ni wapi wakuu zangu tumekosea?.. Mimi bado siridhiki kabisa na hizi hadithi za kurudi nyuma kusodoana. Hivi tunapofanya utetezi wa JK vs Nyerere au kumpinga inatusaidia kipi ktk kujikwamu hapa tulipo, Au ndio tusubiri tena mwaka 2015 tuingize ubishi wetu ktk sanduku la kura!
 
Life expectancy haipimwi katika kipindi kifupi na kuna vigezo sasa sijui mwenzetu anavitumia vipi. Wenzetu wako 88 to 98 sisi tunajivunia 55 kama basi ipo!!! .
By the way ni namba tu, je zina reflect real life ya vitoto vinavyokufa 0-5 kutokana na umasikini.

2005 inflation ilikuwa single digit, 2012 inflation 20%.
Anyway turudi kwenye mada

0-5 hawafi kwa umaskini, wanakufa kwa Malaria na Ukimwi.

Inflation isikustuwe sana, hata mataifa makubwa duniani yana matatizo ya kiuchumi, tena sisi tunafanya vizuri kuliko wengine, tuna GDP ya 6.3 kwa mwaka uliopita.

Kumbuka misingi ya kibiashara inayowekwa sasa hivi ilikuwa iwekwe miaka 50 nyuma. Unategemea nini?miaka 24 ya utawala wa mwanzo ulikuwa wa majaribio. Huo ndio ulikuwa utawala mbovu kuliko yote. Ulishindwa kuweka misingi ya kibiashara. Ulishindwa kuchimba madini, ulishindwa ku attract investment, ulishindwa ku attract watalii, ulikuwa bize kujenga kanisa katoliki.

Uanze kuweka msingi leo, usimamishe nyumba Taifa lenye uchumi bora leo? unahitaji muda, upate utaaalam. Huwezi wewe mwenyewe kuunda hata sindano ya charahani, ngoja kwanza siku utakapojuwa, kwa sasa jifundishe.

Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu.
 
nchi zote za viwanda miundo mbinu kama reli ni sehemu muhimu sana ya uchumi. Kuanzia Marekani, China, Uingereza na hata South Africa. PM Margareth alipotaka kuibinafsisha reli kabisa Waingereza walimwambiaalia akae pembeni. Ujenzi wa reli nchini china na India ni wa kutisha. Ni usafiri rahisi na wa uhakika katika kusafirisha watu na bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tazara ilipokuwa inafanya kazi si wakazi wa kisaki, mlimba, makambako, mbeya n.k waliofaidi tu bali hata watumiaji wa bidhaa wa Dar na kwingineko walinufaika. Ni reli hiyo iliyosababisha mikoa ya nyanda za kusini ikaitwa the big four.

Kama tusingekuwa na reli usafiri wakati wa vita ya kagera ungekuwa mgumu sana. Kwa wale wenye kumbu kumbu ilikuwa ni rahisi kupata supply kutoka Dar kuliko kuzitoa Mwanza hadi Kagera. Huu ni mfano tu wa umuhimu wa miundo mbinu.

Uwanja wa KIA ulijengwa kwasababu ya biashara za mazao mikoa ya kaskazini pamoja na soko la utalii. Bado umuhimu huo unaonekana labda kwa aliyegoma tu kuelewa.

Uwanja wa Songwe Kiwira labda kama una makusudi mengine, endapo ni hili la kubeba maua na si uchukuzi wa mahindi ninashaka na timu inayofikri hivyo na iliyo plan kama kweli haihitaji matibabu.

Mchambuzi, KIA ipo na maua ya kanda ya kaskazini ni mengi na bora. Sijui ni tani ngapi zinapitia hapo. Ninafahamu ndege zinachukua maua kutoka Nairobi! Labda unisaidie maua yanaingiza kiasi gani ukilinganisha na mahindi na mchele au bidhaa nyingine kutoka kanda ya kusini. Ipo siku tutasikia Kisiju mkamba wanataka uwanja wa kimataifa kwasababu wanatoa mihogo mizuri sana!!!

Pengine ndiyo maana tumeamua kungo'a KM 1,844 za reli ili tujenge uwanja wa ndege kuuza shanga na maua! Akili zetu zinatutuma kuwa kuuza maua ambayo hatujaweza kuyakuza katika viwango kutatukomboa. Yale ya Arusha na Moshi hatujaweza kuyadhibiti ili tunufaike tunafikiri Songwe itakuwa tofauti.

Kama Mjerumani aliona umuhimu wa reli 1905, na sisi tunaona umuhimu kujenga kiwanja cha kuchukua maua na shanga mwaka 2012 bado tunasafari ndefu.

Kujenga reli ni long term projects na zinafanyiwa kazi na hilo linajulikana au hujui hilo?

Kujenga viwanja vya ndege ni short term projects zenye tija za haraka haraka.

Reli zitajengwa na kama wewe unaweza kujenga kwa sasa jenga tu, hakuna anaekuzuwia, tumeshaondoka kwenye kutegemea Serikali sasa hivi kuna uwekezaji binafsi unaotiliwa mkazo. Tumeshindwa kuendesha reli mbili na tumeacha huduma zake zimekufa kwa kuwa tu kila mtu anajuwa ni mali ya umma kwa hiyo aibe atakavyo. Huo wakati umekwisha, reli itajengwa kwa uwekezaji wa binafsi, labda serikali iwe na shares tu lakini si kama mpango wa Nyerere ulioshindwa.

Huko Kisiju, wewe unakisia tu lakini ukweli ni kwamba huko ni uwanda wa Gas na mafuta na kunahitaji uwanja wa ndege kwa haraka sana kuliko sehemu nyingine yoyote. Hivi tuavyoongea tunachelewa. Kalagabaho.

Hiyo mikoa haikuitwa big four kwa ajili ya reli, wacha kupotosha, huko ni rutuba na ardhi inayokubali kilimo ndiyo iliyofanya iitwe hivyo. Reli ilijengwa kwa sababu ya kusafirisha shaba na mizigo ya Zambia ambayo ilikuwa ikipita Zimbabwe na Msumbiji kwa wingi na huko kulikuwa kuna vita. Kwa sasa hiyo Reli inakuwa na umuhimu pale tu tutakapoweza kushinda kwa huduma na Zimbabwe, South Afrika, na Msumbiji. Tukishindwa kutoa huduma zinazokubalika wakati wa amani basi tutashinda, la sivyo tutabaki kulalama. Nnaona Omar Nundu yuko juu, kuboresha huduma zote hizo kuanzia bandari, reli, ndege, Tusitake kuleteana pumba za kutaja vijiji na stations ambazo ni "by the way", lakini si primary reason ya kujengwa reli hiyo.
 
FaizaFoxy;3288597]0-5 hawafi kwa umaskini, wanakufa kwa Malaria na Ukimwi.
Inflation isikustuwe sana, hata mataifa makubwa duniani yana matatizo ya kiuchumi, tena sisi tunafanya vizuri kuliko wengine, tuna GDP ya 6.3 kwa mwaka uliopita..Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu
Ndugu yangu, Umasikini ndio tatizo kubwa linaozaa Malaria, ukimwi, surua, kifaduro, malnutrition n.k. Sijui kama unapitia majarida kama ya WHO uone dunia inafanya nini a inasema ni ni kuhusu poverty.
Nina maana ukizungumzia ukimwi,malaria n.k vipo under the umbrella of poverty.

GDP 6.3!! bajeti 40% misaada. Unawezaje kusema GDP inakusaidia wakati hujaweza ku balance bajeti. GDP is just a number, jiulize kwanini watu wamekuwa wakali na wenye uchungu sana, halafu mwangalie mtu wa kawaida pale kariakoo ndio uone kama GDP inamsaidia.

Kuhusu madini, Mwalimu aliwahi kuulizwa akajibu hivi ' madini hayaozi yaacheni yakae hapo watanzania watakapokuwa tayari watayachimba'. Sijui dhahabu ile ya Buzwagi inasadiaje yule mpanga nyanya wa kariakoo!! Hivi huoni wizi wa mchana wewe unaaamini madini yanamsaidia Mtz
Kama unaamini tunaenda vizuri mungu akusaidie naakufungue macho Inshallah, hilo lipo juu ya uwezo wa wengi
FaizaFoxy;3288624]Kujenga reli ni long term projects na zinafanyiwa kazi na hilo linajulikana au hujui hilo?
Kujenga viwanja vya ndege ni short term projects zenye tija za haraka haraka. Tumeshindwa kuendesha reli mbili na tumeacha huduma zake zimekufa kwa kuwa tu kila mtu anajuwa ni mali ya umma kwa hiyo aibe atakavyo. Huo wakati umekwisha, reli itajengwa kwa uwekezaji wa binafsi,.
Hiyo mikoa haikuitwa big four kwa ajili ya reli, wacha kupotosha, huko ni rutuba na ardhi inayokubali kilimo ndiyo iliyofanya iitwe hivyo
Reli ipo katika mipango 50 ya JK? Yeye si amepita akiahidi kila kijiji. Hivi na reli ni sehemu ya mkakati wa Kikwete wa kugeuza Kigoma iwe Dubai!! Ehhe Mola

Hujajibu jibu swali la Mcahmbuzi. Mwaka 1985 tulikuwa na Km Kadhaa za reli, leo zimepungua Km 1844. Zimekwenda wapi? Halafu unang'oa mataruma kwa kushirikiana na Wahindi kwa njia za ufisadi wizi na uporoji anamwaninisha FF kuna mipango.
Hivi kipi rahisi kuweka mabehewa juu ya reli au kung'oa mataruma na kuwakabidhi Wahindi halafu uwe na mipango ya kujenga reli kama 'long term plan'

Badala ya kuwa na short term plan za kumsaidia mtanzania asife na njaa ili hali mahindi yanakwenda Kongo, unafikiria short term plan za kusafirisha maua na shanga! Ukiulizwa maua ni tani ngapi kwa mwaka hujui lakini upo kisutu sokoni unatafuta mchale na mahindi ya Mbeya.

Kwako kusafirisha Rose ndiyo sehemu ya kukua GDP! sio kumsaidia Mtanzania wa kisiju. kariakoo, Maneromango, Msanga ngongele, Ikwiriri, Saadan, Bigwa mwarusembe, Nyamato, Kimazichana, Mkamba, Kivinje n.k.
 
Nnaona Omar Nundu yuko juu, kuboresha huduma zote hizo kuanzia bandari, reli, ndege...

Nadhani waziri husika angekuwa na jina la John Kidevu , usingempa pongezi hizi, and that has been the tenet behind all your arguments kuhusu mafanikio ya awamu ya pili na ya nne. Vinginevyo kuna awamu gani ambayo imeipiku awamu ya Mkapa in terms of economic performance? Na hata baadhi ya mafanikio ya awamu hii ni kutokana na sound economic policies zilizowekwa na Mkapa. Nenda katika balozi mbalimbali au international agencies usikie jinsi gani wanalalamika on how awamu ya nne inamomonyoa kila kitu kilichowekwa na awamu ya tatu. Nina hakika kabisa kwamba Rais wa awamu hii ya nne angekuwa na jina la 'Peter',mungu anajua nini watu wenye mtazamoa uliopitiliza hata ule 'mtazamo hasi', mngesema au mngefanya. Hoja zenu hazina miguu wala kichwa, hazina mantiki yoyote. Hata mnashindwa kujibu swali la msingi kabisa kwanini Ujamaa kwa miaka 18 na soko huria kwa miaka 27 haujabadili maisha ya mwanakijiji wa Tanzania.

Nadhani ili kuweka mambo sawa, tuache tu Rais ajaye awe Rashidi au Abdul, kwani kwa mtanzania mzalendo, hilo halijalishi, watanzania wengi wanataka Rais mchapa kazi, awe huseni, jumanne, Ashura, Anna, James, hiyo sio issue ya msingi.
 
Kuhusu madini, Mwalimu aliwahi kuulizwa akajibu hivi ' madini hayaozi yaacheni yakae hapo watanzania watakapokuwa tayari watayachimba'. Sijui dhahabu ile ya Buzwagi inasadiaje yule mpanga nyanya wa kariakoo!! Hivi huoni wizi wa mchana wewe unaaamini madini yanamsaidia Mtz

Na taarifa zilizopo ni kwamba Sweden walifanya utafiti mkubwa sana juu ya jinsi gani migodi ya dhahabu inamaliza watanzania wa maeneo yale kwa sumu n.k. Wa Sweden hawa waliwachukua wananchi wengi wa maeneo yale na kuwafanyia vipimo vya miili yao. Wamiliki wa migodi wakaipata ripoti hiyo kwa kuhonga mamilioni ya fedha kwa wahusika waliokabidhiwa na baadae kuipelekea kwenye ofisi kubwa sana nchi kwetu kuificha. Na imefichwa. Vinginevyo tusubiri ndugu zetu wa maeneo yale ya migodi waje kuwa na wajukuu wenye ulemavu wa akili, viungo, kama wale wa nagasaki na hiroshima kule Japan.
 
FF hoja zako sometime zinaji contradict sana

0-5 hawafi kwa umaskini, wanakufa kwa Malaria na Ukimwi.

Hawafi kwa umasikini wanakufa kwa malara na Ukimwi.!!!!!!!!! inashangaza Je kufa kwa malaria na ukimwi sio moja ya kiashiria cha umasikini. Bora uendelee kusisitza kuwa vifo vyote ni sababu ya msingi mbvu alioacha mzee Nyerere.

Faiza Foxy said:
Inflation isikustuwe sana, hata mataifa makubwa duniani yana matatizo ya kiuchumi, tena sisi tunafanya vizuri kuliko wengine, tuna GDP ya 6.3 kwa mwaka uliopita.
Mhh kumbe sasa tunaaza kujilinganisha na walio kimbia miaka ya zamani wakati sisi tunatembea. Sasa wao watembea kama sisi tujisifie.
Angalia Uchumi wa brazil ,China na India . Hivyo ndio vipimo vya nchi zinazochipuka. Usijilinganishe na USA , UK na france zinazochechemea kwa sasa.... zilishakimbia zamani

Kumbuka misingi ya kibiashara inayowekwa sasa hivi ilikuwa iwekwe miaka 50 nyuma. Unategemea nini?miaka 24 ya utawala wa mwanzo ulikuwa wa majaribio.
Sawa tu assume huyu mzee na majribio yake yalishindwa kabisa .. Lakini jiulize tena

  • alicha deni la shlingi ngapi?
  • Je aliacha BOT ikiwa na reserve ya dhahabu kiasi gani?.
  • Je tanzania ilifanikiwa kufuta Ujinga kwa kiasi gani.( Huo ndio msingi . Je unajua hivi sasa kuna watoto wanafika darasa la tatu hawajui kusoma na kuandika...... )
  • Je huyu mzee JKN aliacha wasomi wangapi na sera zake za elimu zimezalisha wangapi ambao ndio sasa wanamsaidia au kumvurugia huyo unayemsifia.....

Huo ndio ulikuwa utawala mbovu kuliko yote. Ulishindwa kuweka misingi ya kibiashara. Ulishindwa kuchimba madini, ulishindwa ku attract investment, ulishindwa ku attract watalii, ulikuwa bize kujenga kanisa katoliki
.
Yes lakini hata Kikwete analiwezesha Kanisa. Hajataisfisha hata kimoja . NI juzi kafungua mradi wa umeme wa Kanisa huko Iringa. Sikuona ukisifia kitendo hicho cha upuza makali ya umeme . Hiyo Imekaaje? Ukweli ni Kwamba ni Viongozi kama Mrisho. Kikwete na Hassan M ndio wanaliweszesha Kanisa na wala sio Kina Ben au Julius.

Idadi ya vyuo vikuu unavyosifia kama ni kujenga kanisa chini ya Nyerere basi mpaka leo vinge kuwepo zaidi ya 40 .

Tazama vizuri nani alitaifisha nani alirudisha kwa anisa . Julus kataifisha Hassana karudisha. Muache mzee apumzike usiharibu hii mada.

Na Itapendeza na kulitendea haki hili jukwa la Great thinker kwa kutoigeuza hii mada na kuleta mambo ya Kanisa Vs Msikiti . Hizo mada tumsubiri Mohamed Said . Hilo ni ombi

faiza Foxy said:
Uanze kuweka msingi leo, usimamishe nyumba Taifa lenye uchumi bora leo? unahitaji muda, upate utaaalam. Huwezi wewe mwenyewe kuunda hata sindano ya charahani, ngoja kwanza siku utakapojuwa, kwa sasa jifundishe.

Kumbe JK hawezi
  • kuweka msingi leo????!!!!!
  • kusimamisha nyumba leo?!!!!!!!
  • kupata mtaalama leo?!!!!!
Sasa Kama kwa Jakaya M . K na mkapa na mwinyi imekuwa ngumu sasa wa huyo aliyechukua nchi mikononi mwa wakoloni ulitaka afanye maajabu ya malaika...... Kama hawa wa sasa na wasomi waliopo na uzoefu wao wa kuwa mawaziri kwa miaka zaidi ya 15 bado wanaingia mkenge kwenye mikataba vipi Huyu Nyerere angeingia mikataba ya maisha na akiwa bado hajapata wataalam ungesemaje?

FF do u mean JK hafai kukosolewa sababu ndio kama kaipokea nchi kutoka kwa Mkoloni na waliomtangulia hakuna chochte chema walichoacha amabco yeye anakitumia

Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu
Tunakwenda vizuri lakin taratibu mno Usikatae kuna matatizo au wewe unaona sawa Kanisa kuzalisha umeme...... Unasifia kuwa idadi ya vyuo sasa ni vingi lakini vinamilikiwa na nani.......
 
Wanabodi,
Huyu MajiMshindo kazi yake ni kuvuruga mijadala ya watu. Ukisoma maandishi yake hutaelewa anasema nini au kama ana anufahamu na kile anachokijua. Angalieni mfano huu tu, halafu mfikiri kidogo
FaizaFoxy;3288947]Kwanza dhanna ya kuwa Tanzania ni maskini, ni dhanna potofu. Tanzania ni tajiri sana. Watanzania ndio maskini, tena wana umaskini wa bongo zao. Kwanza ipite miaka 120 ndipo kidogo watakuja watu waliokwisha pata bongo zenye maana, sio sasa.Unaambiwa chandaru hiki, tumia usipate malaria, wewe unaenda kuvylia dagaa. Sasa huo kama si umaskini wa akili ni nini? mwingine alioneshwa katengeneza wavu wa banda la kufugia kuku. Haya, jamani, sasa hapo utasema ni umaskini? ni umaskini wa fikra
halafu hii
Yule mzee asingebomowa kila kitu, saa hizi tuko kwenye neema
amesahau kuwa aliadika hivi
Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu
anaendelea
Ukimwi mnaambiwa wacheni ngono nje ya ndoa. Hamtaki, halafu msingizie umaskini
Yeye anaamini ukimwi hauna uhusiano na umasikini, na hapo hapo anaamini unasambazwa na mahusiano nje ya ndoa. Kwamba ukiwa huna ndoa upo salama. Bwana FF anaendelea
mimi nakuambia hata akili za usafi wa choo hatuna. Si unayaona majumba haya mazuri yanajengwa na maofisi mazuri? nenda chooni. Ndio utapojuwa kuwa sisi ndio watu ambao bado sana. Badala ya choo ndio kiwe kisafi wakati wote, hapa kwetu choo kwa kuwa mtu anaenda ku dump kule basi ndio kitu cha mwisho kwa usafi. Ikiwa huko bado, wewe unaongolea ku innovate?Tunachojuwa kuvumbuwa kila siku ni maneno na misemo mipya tu, ufataani tu ndio mabingwa Sisi bado sana kijana, miaka 120 kwa uchache
na hatimayae ana maliza kwa kuwaambia watu
Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu
!!!! ????

Turudi kwenye mada
 
Wanabodi,
Huyu MajiMshindo kazi yake ni kuvuruga mijadala ya watu. Ukisoma maandishi yake hutaelewa anasema nini au kama ana anufahamu na kile anachokijua. Angalieni mfano huu tu, halafu mfikiri kidogo halafu hiiamesahau kuwa aliadika hivi anaendeleaYeye anaamini ukimwi hauna uhusiano na umasikini, na hapo hapo anaamini unasambazwa na mahusiano nje ya ndoa. Kwamba ukiwa huna ndoa upo salama. Bwana FF anaendeleana hatimayae ana maliza kwa kuwaambia watu!!!! ????

Turudi kwenye mada

Hii thread washiriki wake wengine, ni moja za threads za JF zilizonivutia sana. Washiriki ni watu wa kujenga na watu wa maana wenye kuipenda Tanzania, ispokuwa kuna infestor mmoja anayeleta ujinga ujinga na asiye na hoja yoyote ya maana. I wish mod angem-ban
 
0-5 hawafi kwa umaskini, wanakufa kwa Malaria na Ukimwi.

Inflation isikustuwe sana, hata mataifa makubwa duniani yana matatizo ya kiuchumi, tena sisi tunafanya vizuri kuliko wengine, tuna GDP ya 6.3 kwa mwaka uliopita.

Kumbuka misingi ya kibiashara inayowekwa sasa hivi ilikuwa iwekwe miaka 50 nyuma. Unategemea nini?miaka 24 ya utawala wa mwanzo ulikuwa wa majaribio. Huo ndio ulikuwa utawala mbovu kuliko yote. Ulishindwa kuweka misingi ya kibiashara. Ulishindwa kuchimba madini, ulishindwa ku attract investment, ulishindwa ku attract watalii, ulikuwa bize kujenga kanisa katoliki.

Uanze kuweka msingi leo, usimamishe nyumba Taifa lenye uchumi bora leo? unahitaji muda, upate utaaalam. Huwezi wewe mwenyewe kuunda hata sindano ya charahani, ngoja kwanza siku utakapojuwa, kwa sasa jifundishe.

Tunavyoenda sasa ni vizuri sana na kila dalili zinaonesha hivyo. Na Gas tuliyokuwa nayo, ambayo awamu ya kwanza ilishindwa ku explore, itatusaidia sana katika kukuza uchumi wetu.

Pumba kabisa, ni umri gani wanaokufa kwa umaskini? Hiyo gesi unayosema tunayo inatumiwa wapi? Imekuza vipi uchumi wenu?

Uchumi kukua kwa asilimia 6 na kuwepo kwa inflation ya asilimia 20 unaelewa maana yake? Mjinga tu anaweza kusema uchumi unakua katika hali hiyo.

yes we are better kuliko Somalia, we are better kuliko hata Burundi. labda kwa asilimia moja tu.
 
Na taarifa zilizopo ni kwamba Sweden walifanya utafiti mkubwa sana juu ya jinsi gani migodi ya dhahabu inamaliza watanzania wa maeneo yale kwa sumu n.k. Wa Sweden hawa waliwachukua wananchi wengi wa maeneo yale na kuwafanyia vipimo vya miili yao. Wamiliki wa migodi wakaipata ripoti hiyo kwa kuhonga mamilioni ya fedha kwa wahusika waliokabidhiwa na baadae kuipelekea kwenye ofisi kubwa sana nchi kwetu kuificha. Na imefichwa. Vinginevyo tusubiri ndugu zetu wa maeneo yale ya migodi waje kuwa na wajukuu wenye ulemavu wa akili, viungo, kama wale wa nagasaki na hiroshima kule Japan.
Hapo wapo waliochukua 10%! kama watatokea wagonjwa na walemavu hiyo 'to hell'.
Ile kauli ya kuwa Watanzania watakapokuwa tayari watayachimba ilikuwa na maana sana.
Unajua baadhi ya mambo yaliyochochea maasi ya 1964 ni pamoja na kile walichokiita Africanization. Yaani watu walikuwa na hamasa sana ya kujitawala na kuona mzungu ilikuwa kama tusi. Wakati huo Mwlimu hakuwa na injinia wala mhasibu. Kwa maneno mengine ingebidi wazungu ambao ndio kwanza tu wameachia nchi wachimbe madini. Hilo halikuwa tatizo sana, tatizo ni kuwa isingekuwa rahisi kwa mwalimu kueleweka kwa wananchi, lakini pia hakuwa na wasadizi wa kujua kama yangechimbwa kwa faida ya nchi.

Kinachoendelea sasa hivi ni uporaji halafu mashimo na madhara. Hakuna anayejali kila mtu yupo busy kufuatilia 10%, wakishakatiwa basi mengine mtajua wenyewe.

Ni kwanini hawajali? Jibu nikuwa hawana hofu, sisi wananchi tunadhani wametuajiri bila kujua tumewaajiri. Laiti kama ingetokea mmoja akaadabishwa vema tusingekuwa tunaona haya mauza uza. Hivi ni lini tutajitambua
 
Tuangalie vipi MIRADI yenye nia nzuri imamuongezea Mtanzania UMASIKINI

Mfano katika miradi mikubwa ambalo taifa linayo ni huu wa kitambulisho cha TAIFA. Je tunaweza kueleza huu mradi
  • utamfaidisha vipi mwananchi ?
  • Utasaidia kuandoa kero gani upande wa wananchi au serikali?
  • kitambulisho cha Taifa na Passport na Kitambulisho cha mpigakura vina tofauti gani? I mean kwa Seriali isngefanya maboresho ya Kitambulisha cha mpiga kura kiwe kitambulish cha taifa
  • Ni nchi gani uniani ya mfano ina kitambulisho cha Taifa na kinatumikaje ?
Nauliza maswali haya sababu Nkisikia faida viongzi wanazosema juu ya faida za kitambulisho cha taifa unaon wengi wako misinformed. Sasa ukichanganya na gharama zake alafu ukaona kuwa tayari ni kama duplicate ya kitambulisho cha mpiga kura. ndio nashindwa kuelewa

I mean nini kilizua kuboresha kitambulshi cha mpigga kura kuwe itambulisho cha taifa.

Tuna serikali moja lakini kila idara inaweza kutengeza system ya kitu kile kile amacho kipo idara nyingie tayari. So kesho Tarffic police wakitak kuwa na system ya number plate za magari yote Tanzania wanaanza mchakato mpya kabisa kama vile TRA hawana system hiyo.

Ili kupunguza umasiikini kuna miradi kwenye idara nyingine ni Redundant au duplicate . Idara za serikali zinatakiwa ushare taarifa.

Na kwa kigezo hicho kitambulisho cha mpig kura ndio kilitakiwa kuboreshwa kiwe kitambulisho cha taifa.

I mean kama kuna mjuvi anayeelewa How kitambulisho cha taifa kinaweza kumsaidi mtanzania katka kufight UMASIKINI au kurahisisha jambo fulani anijuze. Isije ikawa ni miradi ya kuiga na sisi tuonekane tumo kwenye karne ya TEKNOHAMA bila faida yeyote
 
Back
Top Bottom