katika swala hili nadhani yalikuwa makosa makubwa kuanza na kitambulisho na mpigakura kabla ya kitambulisho cha uraia..Kitambulisho cha uraia ni muhimu sana ktk jamii yoyote ya Utaifa na watu wake wakati kitambulisho cha Kupiga kura ni kwa wale tu wanao qualify kupiga kura...Na hata passport ni muhimu tu kwa wale wanaotaka kusafiri lakini kitambulisho cha uraia nina maana kubwa zaidi ambayo inaweza kuweka mfumo mzuri wa kiuchumi..

Leo hii tunashndwa kutoa takwimu vizuri za makusanyo ya kodi kutokana na kutokuona umuhimu wa kila mtu alipe kodi na ndio maana chini ya asilimia 10 ndio wanalipa kodi nchini. Tumeshindwa hata kuweka idiadi kamili ya Unemployed, hatufahamu ulazima wa kusajili mashirika au hata biashara tunazozifanya ili kujenga mazuri baina ya uraia wetu na serikali yenyewe..

Kinachonitatizo mimi haswa na nchi yangu ni kwamba hakuna kitu kinachopangwa bila kuwepo sababu ya UFISADI..Na ndio maana husema kila siku ya kwamba hatuwezi kuendelea kufikiria kulijaza pakacha ambalo lina tobo. Juhudi zote za kupata mikataba bora, kuongeza uzalishaji haziwezi kufanikiwa ikiwa tunashindwa kuziba ufa kwanza..Kwa hiyo kwa kila tunapoweka mikakati bora ya kuboresha uchumi ni sawa na kutumia nguvu nyingi bila maarifa kutambua kwamba pakacha lina tobo (mirija) ambazo zinatakiwa kuzibwa kwanza ili tupate kujaza ndoo..Kwa wale wanaohesabu makuzi ya uchumi wetu kina IMF wao wanatazama ni ndoo ngapi tunazipeleka kwa mwaka ili hali hawajali kama zimejaa au laa..
 
Mkuu Mkandara, nadhani Mtazamaji ana hoja kwa hili. Hoja yake kama nilivyoiona mimi ni kuwa Mradi wa vitambulisho hautaleta ile tija iliyokusudiwa kama ulivyosema ukusanyaji wa kodi, takwimu n.k. Amesema kuna tatizo la miradi kutokuwa shirikishi, kwamba inafuata masilahi na sio utaratibu. Hii ni matokeo ya ufisadi.

Kwa mfano, haina maana kuwa na kitambulisho cha taifa wakati hujaweka mfumo wa hati za kuzaliwa(birth certificate) vema.
Kwasasa hati hiyo inapatikana hata kama mtu hastahili. Matokeo yake baada ya mradi wa vitambulisho atakurupuka mtu mwingine na mradi wa hati za kuzaliwa, halafu mwingine kwa wale wallioomba urai. Itagundulika kuwa kunahitajika social insurance number na hapo kutakuwa na mradi mwingine. Kumbe yote yangeweza kuandaliwa kwa hatua na kufanyika pamoja kwa gharama ndogo kwa resource zile zile.

Nakubaliana nawe hata hivyo kuwa vitambulisho ni muhimu sana, na kukosekana kwa takwimu za vitu kama employment, nani anachangia nini katika ujenzi wa taifa ni zao la kutokuwa na vitambulisho. Lakini pia ni lazima tuwe na mfumo unaotegemeana kuziba mianya ya rushwa,ufujaji na urahisi wa kufuatilia.

Cheti cha kuzaliwa, social number, kitambulisho cha taifa, halafu Passport, leseni ya udereva, TIN za TRA n.k vyote vikakungwa kwenye kundi la mwanzo.

Vitu hivi ni muhimu sana katika kujua mambo mengi na kuyafanyia maamuzi. Mathalani takwimu za ajira Tanzania ni uongo mtupu. Hakuna anayejua nani kaajiriwa nani kapoteza kazi, ajira ngapi zimepotea ngapi zimetengenezwa, wakulima wanachangia nini au wanahitaji nini kama mifano tu.

Hakuna anayejua nani anatibiwa, nani anapaswa kupata msaada wa serikali, nani anachangia kodi au kukwepa.
Mfano tu, unaweza toka Burundi ukaenda Bugando ukatibiwa kama Mtanzania mwingine.
Unaweza kuomba ardhi ukiwa raia wa Kenya ukapata kama Mtanzania mwingine, si passport zinanunuliwa!! nani ataweza ku trace original yako!

Umuhimu wa vitambulisho unakuwa diluted na ukweli kuwa haukulenga kutoa matokeo ya kulisadia taifa, ni zao la ufisadi litakalozaa ufisadi kwasababu hakuna mipango thabiti ya kitaalamu bali utaalam thabiti wa 10%.
 
Kweli kabisa mkuu wangu na ndivyo tunavyotaka kufahamu tuanzie wapi. Sasa kama tutaanza leo na vyeti vya kuzaliwa kuna watu zaidi ya milioni 40 waliokwisha zaliwa hawa utawahesabu vipi?.. Ingekuwa rahisi sana bila Ufisadi lakini maadam kila kitu nchini kinafungamana na Ufisadi bega kwa bega nashindwa hata kuchangia swala la vitambulisho maana najua fika haina tija sawa kabisa na mradi wowote wa uwekezaji nchini.

Hata huo mpango wa Mchuchuma mimi sina imani nao kabisa na nauloona ni hatari zaidi ya kuwa na tija kwa sababu najua watu wamevuta kitu, hapafu ni hatari ktk mazingira yetu ikiwa safety measures hazitafuatiliwa kwa ukaribu sana jambo ambalo hatuna utamaduni huo. Na nina hakika hao Wachina watauza nguvu za umeme kwa Tanesco kwa bei ghali ambayo bado itamgharimu mwananchi ili mradi tu kuhakikisha Wachina na serikali wanarudisha fedha za mkopo waliofadhili ujenzi wa mradi huo..

Na ndio maana najaribu sana kutafuta jibu la matatizo yetu hapa tulipokwama. Vitambulisho muhimu sana lakini kuna utaratibu ambao umerukwa sawa na tunavyojaribu kuboresha uzalishaji na uchumi wetu wakati tumeruka misingi bora ya kuwezesha zoezi hilo kufanikiwa.
 
Hakuna project ambayo ni sustainable kwasababu zote zipo under the umbrella of ufisadi.
Mchuchuma kuna mikono ya watu kwa kupitia mchina, subiri tu utaona umeme ni ghali kuliko wa mafuta na maji.Umesahau ahadi tamu za Kiwira, si baadaye tumegundua u-baba, ukwe, u-shemeji n.k.

Nadhani tunaweza kujikwamua kutoka katika tope kwa baadhi ya mambo:
1. Nidhamu- Nchi yoyote yenye mafanikio kuna nidhamu inayoanza kwa viongozi hadi kwa mzururaji. Nchi za wenzetu ni formula na sheria tu. Kiongozi akishajua kuwa anaongozwa na sheria na wananchi wakishajua sheria zinazomuongoza hapo hakuna ubabishaji.

Zomboko akijua kuwa ameajiriwa na Ngeleja na kesho kibarua kinaweza ota nyasi, Ngeleja naye akajua yanaweza kumtokea kwa Pinda, na Pinda naye akijua amekalia kuti kavu la Rais, na rais akajua kuwa wenye nchi wanaweza kumtaka aitishe uchaguzi kabla ya jumapili hapo hakuna kuoneana haya wala kulindana.

Sasa hivi aah! Kiongozi amuogope nani! hawa unaosikia wamesimamaishwa kazi ni boya tu watapewa ubalozi miezi 3 ijayo. Nani atahoji. Huko kwenye bodi za mashirika imekuwa sehemu za kuzawadiani pensheni.
Kuna loophole kubwa inayowapa viongozi kiburi na hiyo ndiyo ya kuanza kuziba

2. Haka ka kitu kanitwa katiba kakiwa kazuri kanaweza kutusadia maana kanaweza kutupa nguvu ya kuwaadabisha wanaotukwamisha. Ndiyo maana nasema lazima katokane na sisi na si wao. Ukiona wanavyohaha sasa ni kwasababu ya hofu.
Tukiwaachia wakatengeneza kama walivyofanya huko nyuma, watatumia katiba hiyo kutuzamisha kabisa.

3. Wananchi wetu waambiwe ukweli na si kuambiwa tu waelezwe kuwa wakati wa kujikwamua umepita, tunatakiwa tufanye haraka sana. Hatuwezi kupoteza maisha wakati watu wanahudhuria dhifa za taifa, watu wapo Dodoma wanapiga soka.
Ifike siku kila kiongozi aone ofisi ni 'gereza'. Hapo walio waadilifu tu watakubali kuingia.

Sasa hivi kila mtu anataka kuwa Rais kwasababu Urais si dhima na majukumu ni Urahisi wa mambo!!
 
Tanzania sio maskini ila ina viongozi maskini wa fikra, wasioona mbali na wenye kujipenda wao na familia zao tu na wale marafiki zao
Mkuu umenikumbusha kitu kimoja... Kuna mshikaji aliwahi nambia Umaskini wa Mtanzania ni sawa na mmasai mwenye ng'ombe 3,000 lakini bado maskini, hivyo utajiri sii kuwa na umezikalia bali pale mali zinapokuwa sokoni. Tukirudi ktk mbinu za kiuchumi, jamani mbona mbinu nyingi sana zimefanywa toka mpango Structural Adjustment Program (SAP) - Kukata matumizi ktk social expenditure, food subsidies, retrenchments, devaluation na intro ya fees kwa Elimu na Afya chini ya Mwinyi, kisha wakati wa Mkapa tukaingizwa ktk Ubinafsishaji na mkakati wa Enhanced Structural Adjustment Facility (ESAF)..haya ndio hayo ya miaka mitano watu wanauziana kukwepa kodi..Na ndio kwanza tukajiingiza katika madeni makubwa na kumbuka mwaka 1997 alone tulikopa almost 1 bil Usd na muda wote wa Mkapa tulikuwa tukituma 40 ya matumizi ya serikali kulipa madeni na hakika sijui aloipoondoka alituachia madeni kiasi gani maana tunajua tu ule msamaha wa 133 mil.. watu wakatiua ndani wakati wa EPA..

Kote huko tukashindwa kupata sustained economic growth wala wala kupunguza umaskini bali madeni matupu... Mwisho wakasema oooh turudi kwenye shina - Umaskini, wakaja na Poverty Reduction Strategies (PRS) ndio tumeharibikiwa kabisaaaa tunaletewa sijui malaria haiwezekani na kina Bush kutuuzia vyandarua mradi wa mama Bush, yaani madeni juu ya madeni wakati tunao wasomi nchini wanajua fika kwamba nchi yoyote bila infrastructure haiwezi kwenda mbele..tuna reli ya toka mkoloni, bandari toka mkoloni, tuna viwanja vya ndege toka mkoloni na Nyerere lakini maajabu tunategemea tuwe na treni, meli zetu, ndege zetu nzuri ktk usafiri ili tupate kuendelea..

Jamani mimi nachoka kabisa, yaani sijui tunatakiwa kuanzia wapi maana tukisema soko huria na Ubepari, Watanzania wenye access tu ya biashara nje huweka fedha zao nje zaidi ya kurudisha nyumbani. yaani nyumbani ndiko kuna mtaji na faida zao huwekwa benki za nje na kinachorudi ni Vogue ya baba, mama, mtoto na kipapi.. Sasa tutaweza vipi kufikiria kuuza mazao nje ili hali wadanganyika wenyewe hatuaminiani?..Na kibaya zaidi unapoweka fedha zako benki itakuchukua saa 2 hadi 4 kuchukua fedha hizo wakati mwinge hata kufanya deposit tu na kiazi mpya lazima uwe na mtu ndani ambaye unamkatia kidogo kuharakisha mambo..Yaani hata sijui niseme nini wakuu zangu nachoka na nchi yangu japokuwa naipenda sana!
 
Mkuu thread hii si inafana na ile uliyoianzisha kule GT?

Nilianzisha thread similar na imeungwa na hii, nadhani zina maudhui sawa na ile kule ambayo ni sticky.
 

Well said Mkuu, tatizo letu kubwa ni Uongozi! Ninaposema uongozi ni zaidi ya mtu mmoja pale Magogoni, HAPANA! tuende ndani zaidi na kutazama mfumo mzima wa uongozi katika ngazi zote; na hapo utaona kwanini tumekwama kwenye shimo hili la umaskini.

Haya mengine yote ya Ufisadi na Ukoloni Mamboleo yanaweza kupata majibu iwapo kutakuwa na uongozi makini. Na hata sera tunazosomewa kila mara kwenye matamasha, zinaweza kutukwamua endapo zitasimamiwa inavyohitajika.
 
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo
 
Ni kweli tanzania ni tajiri, but our leaders are empty in the head. Brainless
 
Wewe mwenyewe kama mtanzania unafanyajuhudi gani na unafanya nini katika nafasi yake kulinda na kuhakikisha utajiri wetu unasaidia watanzania wote
 
Asavali walau leo umeweka thread isiyolandana na tabia zako. Bravo jane_000!
 
Wewe mwenyewe kama mtanzania unafanyajuhudi gani na unafanya nini katika nafasi yake kulinda na kuhakikisha utajiri wetu unasaidia watanzania wote
Nikipa tafasi naiba tu mali ya uma
 
Nikipa tafasi naiba tu mali ya uma

Na kwa ubinafsi huu uliojengeka miongoni mwetu ipo kazi kubwa kumkomboa MTZ ambaye kupat nafasi ya ofisi ni ndoto na maisha yake ameyaweka rehani kwa watu kama nyie lol!
 
Wewe mwenyewe kama mtanzania unafanyajuhudi gani na unafanya nini katika nafasi yake kulinda na kuhakikisha utajiri wetu unasaidia watanzania wote

hakuna juhudi unaweza kufanya chini ya mafirauni wa ccm ukaikomboa tanzania ya watu waliostaarabika. Resources zote ambazo zingeleta maisha bora kwa wananchi zimemilikishwa kwa wachache. Jambo la msingi ni kufanya mapinduzi ya kisiasa na kuizika serikali ya majambazi wa ccm. Watanzania ni wastaarabu sana, lakini ustaarabu wao umepitiliza mpaka wanaonekana watumwa ndani ya nchi yao
 
Ni kweli Maskini sana kiasi kwmba tunapitwa hata na nchi zisizo na rasilimali za kutsha kama Rwnda.....But siku zote miaka itapita kwa kulalamika UMASKINI wakati vijana tuna nafasi kubwa ya kubadilisha hali hii kwa kuweka viongozi imara kipindi cha UCHAGUZI.Vjana wengi hawaendi kupiga kura kwa mana moja CCM itaiba kura.

2010 wasipiga kura walikuwa zaidi ya milion 10,wengi wao kati ya hao hawkupiga kwa mafikirio KURA ZITAIBWA TU bt POPOTE KUNA KIWANGO UNACHOWEZA KUIBA BT si kwa kiwang hata cha kufikia KURA Mil 8....Vijana tuhamasishane kupoteza siku 1 kwenda kupiga kura kweny CHAGUZI MBALIMBALI kwa maendeleo YETU KULIKO KUKAA NA KULALAMIKA TU umaskini na wizi wa kura wakati HATUJITOKEZI.....
 
Kuna nchi kama singapore haina ardhi ya kulima wala madini lakini wanakuwa kwa kasi ajabu...

Juzi nimesikia tuna uranium tani za kutosha tu na makaa ya mawe kibao hatujachimba, lakini la ajabu sisi wananchi wa kawaida hata hatutaona faida ya hizi rasilimali.

Mi nadhani hizi rasilimali nyingine bora tuingia ubia na wakubwa itusaidie kupunguza madeni tu wanayotudai kuliko kusimamiwa na hii serikali iliyoshindwa kazi.
 
Tanzana ina utajiri mwingi lakini Viongozi wanaotuongoza wanatumia rasilimali za nchi vibaya, kwani fedha tunazozipata hatuwekezi kwenye Viwanda na tecknolojia nyingine ambazo zingewatoa Watanzania kwenye Umasikini badala yake fedha zinatumika kulipana posho na kutumika kununua magari ya kifahari na kugharamia Safari za Viongozi nchi za Nje.
Kwa mwendo huu, Watanzania tutabaki masikini daima.
 
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo
DADA, Jana Ulijiita mtu wa system!! Vipi tena unawakandia mabosi wako??
 
nchi yetu nitajiri tena sana lakini viongozi wetu wana maji kwenye vichwa na tamaa zimewazunguka na wanapenda kula na kuvimba matumbo

umebadilika?? juzi tu ulikua unamsifia JK hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…