It may not be entirely but it factors/ factored majorly.
Zakumi,
Katika swala la viatu vya bora utakuwa huwatendei haki. Wakati wanazalisha viatu (Nyerere)hapakuwa na ushindani hata kidogo, na hata baada ya kuingia Ubepari tayari kiwanda hicho kilikuwa ktk list ya kuuzwa. Kwa nini tulifanya maamuzi hayo?
Kibaya zaidi ni kwamba viwanda vyote vilihukumiwa vyenyewe kwa uzembe wa binadamu kushindwa kutangaza, kutafuta masoko ndani na nje badala yake tukauza viwanda hivyo na kupoteza almost asilimia 60 ya wafanyakazi wa mashirika ya Umma. Na viwanda hivyo wala visiendelezwe wale walionunua wakauza machines na kadhalika kumbe lengo lao lilikuwa kushika viwanja for future development.
Ndio hapo nauliza tulikuwa tunatak au kufikiria nini kuua ajira zile leo tunafikiria tena ku Create ajira bila kutazama makosa ya awali. Why? Why even private investors hawataki kuwekeza ktk viwanda? Je, ni ukosekanaji wa miundombinu kama umeme na maji au tatizo lipo kwa wananchi wenyewe ktk uzalishaji au soko la ndani tunataka vitu vya nje zaidi.
Zakumi, kwahiyo kama serikali ilitoa nafasi kwa viwanda visimame vyenyewe,juhudi zilizoshindikana na aliyeshindwa ambaye unasema ni binadamu asiyeweza kufundishwa kuruka ndo yupi?Nimefanya industrial training Bora mwanzoni mwa 90 tena pale PUGU ROAD. Serikali ilitoa nafasi kwa viwanda visimame vyenyewe. Lakini juhudi zilishindika.
Huwezi kumfundisha mamba kurudka kama ndege.
Zakumi, kwahiyo kama serikali ilitoa nafasi kwa viwanda visimame vyenyewe,juhudi zilizoshindikana na aliyeshindwa ambaye unasema ni binadamu asiyeweza kufundishwa kuruka ndo yupi?
Mkuiu kiwanda cha Bora hakikuwa kiwanda cha Bata ila bata walikuwa na distribution centre yao Tanzania. Na nasema hivi kwa sababu Bora ilikuwa na mitambo ya kutoka Italia wakati Bata ilitumia mitambo ya Uingereza hata ukienda Kenya na kuuliza. Mitambo ya Bora haikufa kwa sababu ulozisema, bali tuliviua sisi wenyewe kwa kuviuza baada ya Ubinafsishaji. Na hata mashindano ya kweli ktk biashara hizi, imekuja miaka 10 baada ya Mwinyi ndipo tumeona vitu vikiingia madukani kwa wingi lakini hapo nyuma ilikuwa mitumba tu toka friji hadi chupi. Nyumba Kariakoo zilikuwa zikiuzwa less than Usd 20,000 only kama unakumbuka vizuri.Bata bado hipo hata Kenya. Baada ya vita vya pili vya dunia na Czechslovakia kuwa chini ya wakomunisti, Bata alihamua kununua mitambo ya zamani ya kutengeneza vitabu na kuja huku kweli kuanzisha biashara.
Serikali ya Tanzania ilipohamua kufuata ujamaa ilitaifisha viwanda vya Bata na kuwa Bora. Lakini kutokana na poor investment ambayo serikali iliweka katika kiwanda cha bora, mitambo ilishindwa kufanya kazi vizuri.
Niliwahi kufanya industrial training kwenye kiwanda cha bora pale Pugu Road, na mambo hayakuwa mazuri.
Hivyo biashara ya viatu ilikufa sio kwa sababu watanzania walikuwa hawataki viatu, bali kulikuwa hakuna business model yenye kuweza kufanya kazi.
Mkuiu kiwanda cha Bora hakikuwa kiwanda cha Bata ila bata walikuwa na distribution centre yao Tanzania. Na nasema hivi kwa sababu Bora ilikuwa na mitambo ya kutoka Italia wakati Bata ilitumia mitambo ya Uingereza hata ukienda Kenya na kuuliza. Mitambo ya Bora haikufa kwa sababu ulozisema, bali tuliviua sisi wenyewe kwa kuviuza baada ya Ubinafsishaji. Na hata mashindano ya kweli ktk biashara hizi, imekuja miaka 10 baada ya Mwinyi ndipo tumeona vitu vikiingia madukani kwa wingi lakini hapo nyuma ilikuwa mitumba tu toka friji hadi chupi. Nyumba Kariakoo zilikuwa zikiuzwa less than Usd 20,000 only kama unakumbuka vizuri.
Sasa ikiwa tumeshindwa wakati wa Ubepari kuendesha kitu kile kile tulichoshindwa kuzalisha zaidi wakati wa Ujamaa tutaweza vipi kufungua viwanda vipya. Na bado hujanijibu swali langu. Kwa nini hadi leo hakuna mtu alofungua kiwanda cha viatu wakati kuna soko kubwa sana la viatu toka China, mitumba na vyote ni ghali kupita kiasi. Bongo bei ya viatu ni kubwa kuliko hata Ulaya inakuwaje wawekezaji wafanyabiashara wameshindwa kufungua kiwanda cha viatu hata iwe kandambili hadi Wachina wenyewe wamekuja na kufungua viwanda vidogo vya Yeboyebo maeneo ya Kariakoo na wanatengeneza fedha kichizi? huoni kwamba sisi wenyewe ndio tuna matatizo!
Nimekupata, je market ya bidhaa ilikuwa ni wapi?East African Market?Jmushi1,
Viwanda vilipewa nafasi ya kujiendeleza vyenyewe. Na serikali ilitaka wafanyakazi wawe na share. Tatizo linakuja ni kuwa
viwanda vilikuwa na watendaji ambao hawakuwahi kufanya katika mazingira ya mashindano. Walikuwa hawajui marketing and advertising. Je ulitegemea nini kutoka kwao?
Duh mkuu wangu katika utafiti wangu nimekuta kumbe Bora bado ipo. BofyaNimefanya industrial training Bora mwanzoni mwa 90 tena pale PUGU ROAD. Serikali ilitoa nafasi kwa viwanda visimame vyenyewe. Lakini juhudi zilishindika.
Huwezi kumfundisha mamba kurudka kama ndege.
Duh mkuu wangu katika utafiti wangu nimekuta kumbe Bora bado ipo. Bofya
Sasa tujiulize ni watanzania wangapi wanajua hilo? mbona mjini tunayaona maduka ya bata lakini hatuyaoni ya Bora! halafu unajua miaka ya mwanzo 70s tulikuwa na kampuni nyingine ya kutengeneza viatu ikiitwa Avi walikuwa na duka pale Samora katibu na duka la Bora.. hiki nacho kilikufa vipi?
Kuhusu Sigara sio kweli kwamba sigara za Kenya zilikuwa deal hata kidogo wewe sii mvutaji basi. Ukisema kabla ya kutafishwa viwanda vile toka BAT labda lakini baada ya kuvitaifisha hakuna sigara iliyokuwa ikitoka Kenya tena basi sisi ndio tulikuwa tukipeleka sigara kwa magendo Kenya na Uganda kwa sababu ya bei yetu ilikuwa cheap zaidi. Kuna vijana kibao nawajua walitajirika kutokana na kusambaza sigara magendo.
Nimekupata, je market ya bidhaa ilikuwa ni wapi?East African Market?
Ama tulitegemea soko la ndani?
Binafsi nakumbuka nikiwa very young na mzee wangu alikuwa na kiwanda kidogo cha viatu, mikanda na mikoba ya ngozi, it did well, lakini kama ulivyosema, hatukutayarishwa na ushindani kutoka nchi jirani ya Kenya, bidhaa za Kenya zilizokuwa zikiingizwa kwa magendo zilikuwa cheaper zaidi, hiyo pia ilikuwa sababu mojawapo ya kudorora kwa uchumi wetu.
Kama ilivyotokea kwa Bora na viwanda vingine ie Tanneries, Kilimanjaro Machine Tools nk, tulikuwa na kiwanda cha sigara lakini sigara kutoka Kenya ndo zilikuwa dili, nakumbuka enzi hizo farasi walikuwa wakitumika kuwakimbiza wauza fegi wa reja reja ambao walikuwa wakiitwa walanguzi!
Ilikuwa mbaya mkuu, watu wamesahau, pia maeneo mbali mali ya nchini yalikuwa na issues za tofauti, just depending on what main economic activities was there.
I will never forget this stuff kwasababu i was very young na imestick kwenye mind since then.
Ni kweli kuwa viwanda vilipewa nafasi ya kujiendesha vyenyewe, lakini je ni kweli serikali iliviandalia mazingira stahiki na policies ambazo zingeweza kuvifanya viwanda hivyo vithrive kwenye East African Market? Thats where the leaders failed us!
Kwa upande mwingine, ukweli ni kwamba hata hivyo viwanda vya wakenya tulivyokuwa tukishindana nao, wamiliki halisi ndo hao wazungu ambao tuliwafukuza Tanzania!
Hapana hujanijibu lolote, mjadala huu ni mpana sana na kusema kutakuwa na majibu yote hapa si kweli, unless tuna zero down on specifics.Jmushi,
I guess I have already answered you. In Tanzania, income inequality didn't cause the misfortunes of your people. So it isn't an issue to be discussed here.
Secondly, distribution of wealth through various government programs works well when the country is so rich or has reached financial sovereignty. However, for poor country like Tanzania the distribution of wealth you have mentioned above does more harm than good. This is because it will increase the size of the government and unsustainable national debts.
For example, in 70s and 80s, Tanzanian government spent a huge amount of money to expand its social programs. However by mid 80s, the cost of servicing national debts yearly was more than ¼ of GNP, twice the combined budgets of education and health.
Ndo hapo tunapotofautiana...Mkandara,
Mtaendelea mpaka lini kulaumu serikali na ubepari wakati watu hamna management skills. Enzi zenu watu walikuwa wanamaliza shule na kupewa umeneja. Mtu hajawahi kutengeneza shilingi hata 1000 kwa kutumia akili yake mwenyewe anapewa kuendesha enterprize ya dollar 1,000,000. Hii ilikuwa worse than affirmative Action.
Duh! yaani unaniona mimi mtetezi wa Nyerere na Ujamaa kwa kuzungumzia Bora shoes?..Hapana mkuu wangu usiwe nawe ktk kundi la wale wanaotafuta mchawi tu maana unapozungumzia rationalize binafsi yangu nawaona nyie ndio hampendi ku face ukweli na reality bali mnaishi kwa vitabu zaidi vya IMF kama sababu ya kuanguka kwetu kiuchumi.Mkandara,
Kwikwikwi, tatizo lako una Uzalendo sana na nchi mpaka wakati mwingine unashindwa ku-rationalize. Bora walikuwa na mitambo mpaka ya kutoka Czechslovakia. Na mingi ilikuwa michakavu. Nikiwa training mitambo ilikuwa inafanya kazi na kufa. Na vilevile kulikuwa na mitambo ya kutengeneza tire and tube za baiskeli. Nayo ilikuwa michakavu japokuwa soko lilikuwa zuri tu.
Kiwanda kilichokuwa na mitambo ya kutoka Italy kilikuwa cha fahari Morogoro. Na huu ulikuwa ni mkopo wa Benk ya dunia. 4% ya viatu ilitakiwa kuuzwa Tanzania na iliyobakia soko lilikuwa liwe Ulaya. Mpaka serikali ilipohamua kukiuza, uzalishaji ulikuwa chini ya 1% na hakuna hata kiatu kimoja kilichokuwa exported to Europe.
Mtaendelea mpaka lini kulaumu serikali na ubepari wakati watu hamna management skills. Enzi zenu watu walikuwa wanamaliza shule na kupewa umeneja. Mtu hajawahi kutengeneza shilingi hata 1000 kwa kutumia akili yake mwenyewe anapewa kuendesha enterprize ya dollar 1,000,000. Hii ilikuwa worse than affirmative Action.
Ndo hapo tunapotofautiana...
Si kila mtu mwenye kuulaumu ubepari basi anauchukia ubepari.
Ndo maana kama unakumbuka, nilisema kuwa you're "pro status quo" Ndo maana yangu halisi, hata kama matatizo ni zaidi ya serikali, lakini serikali ndo the main.
Hilo ndo tunalopingana na wale pro governments.
Everything, and i mean everything is about govt policies, hizo ndo foundations za any succesfull economy or even a failed one.All are to be atributed to governmental policies, and ofcourse its implementations, hapo ma pro status quo ndo mlipokuwa blind sided!
Hapana hujanijibu lolote, mjadala huu ni mpana sana na kusema kutakuwa na majibu yote hapa si kweli, unless tuna zero down on specifics.
Nimekwambia income inqualities first ipo kila pahala duniani, however utofauti wa nchi na nchi ni only some degrees.
Na kama nilivyokwambia, serikali ndo yenye majukumu ya kupunguza hayo makali ya inequalities, nimemention social programs za serikali za kibepari kwa wananchi wake etc.
Umegusia kuhusu soacial servives za 70's na 80's Tanzania bila kusema kuwa it was a policy failure rather than just "spending huge amount of money to expand social programs"
Hayo ya costs za ku service national budgets tumeshayazungumzia kwenye ule mjadala wa MMM wa "what can we do to save our economy"
Hakuna pahala nimezungumzia "distribution of wealth" Hizo ni kauli za mabepari wenye kupingana na policies flani flani ambazo wanadhani na kuamini kuwa ziko geared towards their demise!
Kuna policies ambazo ni sustainable lakini mabepari huwa wanazibrand kuwa ni policies aimed at "wealth redistributions."
Mfumo wa ubepari, uzuri wake ni kama serikali itaplay part yake inavyotakiwa, na uwepo wa demokrasia ambapo si mabepari tu ndo wenye influence kwenye sera za uchumi, na kama that will be the case, wenzetu wana make sure kuwa wanatake care of those who are impacted by the inequalities, ndo maana nikakupa mfano wa serikali ya marekani ambayo ni ya kibepari lakini hizo sera zake nyingine ni za kisoshalisti, hilo ni kuepuka dhahma toka kwa masikini.
Nilichosema mimi ndo hicho, sijasema welath has to be redistributed, hizi ni kauli za kisiasa tu.
Duh! yaani unaniona mimi mtetezi wa Nyerere na Ujamaa kwa kuzungumzia Bora shoes?..Hapana mkuu wangu usiwe nawe ktk kundi la wale wanaotafuta mchawi tu maana unapozungumzia rationalize binafsi yangu nawaona nyie ndio hampendi ku face ukweli na reality bali mnaishi kwa vitabu zaidi vya IMF kama sababu ya kuanguka kwetu kiuchumi.
Mimi nakijua viwanda cha Bora vizuri tu na ndio maana nasema walikuwa na mitambo ya kutoka Italy nakumbuka vizuri tu sijafika ktk hicho kiwanda cha Morogoro..Wewe umeenda pale miaka ya 90 mimi nimefika pale miaka ya 70s tena ujamaa umeiva haswa sasa tofauti ya miaka 20 inaweza kabisa kuwa na majibu tofauti. Jambo moja tu ulonipa hapa na sikulielewa ni Bora kutengeneza matairi na tubes kusema kweli hilo sikujua hadi leo unaponambia..
Na hata kama walikuwa na mitambo mingine ya Czechoslovakia lazima ukumbuke pia Chek hawakuwa nyuma sana ktk taaluma ya sayansi na teknolojia maana robo ya population yao walikuwa Wajarumani. Wakitengeneza magari, ndege za kivita na kadhalika bado hii sio sababu ya kufa kwa viwanda vile isipokuwa sisi wenyewe ndio tuloviua. Unachonishinda kuelewa nipale unapojaribu kusema sababu ilikuwa utafutaji wa masoko, mkuu wangu enzi zile za Nyerere nothing kilikuwa kinaingia nchini zaidi ya sisi kununua vilivyopo.
Ruksa ya Mwinyi ilikuwa kupurura!..watu waliparua viwanda sii mchezo, sisi tulikuwa mjini mkuu wangu nimeondoka Bongo 87!.. Vipuri vikiuzwa kama chuma chakavu watu wamejenga majumba kwa kuuza spareparts unasema nini mkuu wangu. Na upande wa soko watu walikuwa na hiyari ya kuvaa viatu vya matairi na kandambili kuliko viatu vya bora... kama alivyosema Nyani Ngabu - tulikuwa brainawashed na bado tupo kabatini, hatujasafisha vichwa vyetu hadi leo hii..
Juice ya Bakhresa haipendwi kuliko ile ya Urabuni japokuwa ni matunda yetu wenyewe. Nenda Mlimani mall mtu anatumia 100,000 kwa matunda yasiyojaa hata mifuko miwili lakini asinunue soko la Kawe matunda fresh kabisa na pengine angetumia 20,000.. Basi tu sisi tuna tatizo kubwa sana vichwani ila kukubali hapo ndipo maneno! Wadanganyika mna unconscious defense mechanism isiyokuwa na kifani yaani utafikiri tumejaaliwa kipaji hicho hata ktk vitu ambavyo viko wazi kabisa.
Kuhusu Sigara mkuu wangu ktk madhambi ambayo nimewahi kuyafanya ni pamoja na uuzaji wa sigara na matairi Kenya na Uganda, Ulanguzi huo nazungumzia baada ya vita ya Uganda in early 80s kabla sijagundua soko la Korosho, Prawns, Crabs na Lobsters huko Zimbabwe na South Africa nikabadilisha majeshi. Nasema vitu through experience na wala sifichi kuogopa sijui kesho yatanirudi maana nimefanya kweli na vijana wengi Dar walifuata nyayo enzi hizo nikipewa sifa za ubunifu wa ajira - haaa! haaa! haaa!
...Haikutoa nafasi. Iliambiwa ivibinafsishe au ivifilisi kama haviwezi kubinafsishwa, ili, tupewe misaada na mikopo ya fedha.Nimefanya industrial training Bora mwanzoni mwa 90 tena pale PUGU ROAD. Serikali ilitoa nafasi kwa viwanda visimame vyenyewe. Lakini juhudi zilishindika.
...Je, tulikuwa na sera yeyote ya viwanda kwa ajili ya export na huo mradi ulipitia mchanganuo uliouhakikishia kwamba utaanza vizuri? au tulifikiria kujenga kiwanda bila kujali matokeo, alimradi jamaa wa WB na IMF wamesema?Kiwanda kilichokuwa na mitambo ya kutoka Italy kilikuwa cha fahari Morogoro. Na huu ulikuwa ni mkopo wa Benk ya dunia. 4% ya viatu ilitakiwa kuuzwa Tanzania na iliyobakia soko lilikuwa liwe Ulaya. Mpaka serikali ilipohamua kukiuza, uzalishaji ulikuwa chini ya 1% na hakuna hata kiatu kimoja kilichokuwa exported to Europe.
...Ushasema walikuwa wanapewa. Nani alikuwa anawapa hao wasio na skills? Ukizingatia kwamba karibu viwanda vyote vya maana vilikuwa ni vya umma, nani ni wa kulaumiwa? Je, unafahamu mameneja wa viwanda hivi hawakuwa na uhuru wa maamuzi. Tusiende mbali. Unafikiri TANESCO wangeingia mikataba kadhaa yenye gharama kubwa za kuacha madeni ya kufa mtu, peke yao kama menagement?Mtaendelea mpaka lini kulaumu serikali na ubepari wakati watu hamna management skills. Enzi zenu watu walikuwa wanamaliza shule na kupewa umeneja.
...Sasa, hapo kosa la nani? anayemweka mtu wake au huyo mtu?Mtu hajawahi kutengeneza shilingi hata 1000 kwa kutumia akili yake mwenyewe anapewa kuendesha enterprize ya dollar 1,000,000. Hii ilikuwa worse than affirmative Action.
...Its more than that, my friend. Unaangalia malighafi unapata wapi. Je, chuma ilishaanza kuchimbwa na kuyeyushwa huko Liganga? Halafu, skills, established supporting infrastructure, getaway to markets, lengo la kuanzisha kiwanda, and the list goes on. Wakati mwingine location ni swali gumu sana katika kupanga mradi.Kwa maoni yangu binafsi. Kilimanjaro machine tools, Mang'ula machine tools, Nyumbu Auto project, UFI vilitakiwa kujengwa Mbeya. Huko kunapatikana chuma na Makaa ya mawe.