Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,054
- 1,415
ujamaa na kujitegemea ni siasa mbaya sana . Siasa hii ndiyo iliyotuleta hapa katika umasikini uliopo. Siasa hiii ilipiga marufuku kuwepo kwa matajili na hata wale wenye kumiliki maduka . Haya niliyaona pale vywawa mbozi kwa wahindi kunyang'anywa maduka yao yote na kufungua duka moja tuu la walaji.
Siasa hii ya ujamaa na kujitegemea haikujenga shule wala vyuo vya ualaimu ili kutoshereza mahitaji ya watanznaia. Iliweka ualimu wa UPE na kila kukicha darsa la saba waliofeli walishindiliwa mashambani kufanya kilimo badala ya kusomesha vijana wengi kujenga nchi.
Siasa hii iliweka vikwazo kwa vijana kwenda jiunga na chuo kikuu na wakaweka azimio la musoma ili kila kijana kae nyumbani akifanya kazi kwa miaka miwili na baadae apply chuo kikuu.
Siasa hii chini ya azimio la arusha ilifuta hati miliki kwa wanamuziki na hivyo hata kukaktaa kujenga kiwanda cha santuli ili watu wenye fani ya muziki watajilike nayo. matokeao yake mziki ulikuwa haulipi kama ilivyi siku hizi. hakuna hata mwanamuziki mmoja wa kitanznaia aliyefikia pato la kununua gari. awe balisidya, mbaraka, malijani au ahmedi kipande wote waliishia kufa masikini wa kutupwa.
Halafu siasa hii ya ujamaa na kujitegemea haikupenda ma investors wala nchi tajiri. ma investors iliwaita wanyinyaji na investment iliita milija ya kunyonya.
halafu kitu kingine kibaya zaidi ni pale raisi mtawala wa nchi hii alipojiwekewa kinga kikatiba kuwa aharuhusiwi kishitakiwa hata akifanya kosa gani. Pili raisi kujiwekewa madaraka makubwa kupita mahakama kuuu na bunge.
Nchi yeyote inayolea wananchi katika mazingira kama hayo na raisi kijipendelea kikatiba namna hiyo inaishia kuwa masikini wa kutupwa ingawa ina rasilimali kali kupita ubelgiji. hii ndiyo sababu nchi yetu ni maisikini mpaka leo na kesho asubuhi. mimi naamini kuwa mungu yupo na aliukomalie ukomunisti ufe kwa sababu moja tuu, nayo kuiokoa nchi yetu ilikuwa inakwenda mbele bila dira. hata hayati horace kolimba aliisha wahi kusema.
Ndugu yangu ukibahataka kutoka nje ya nchi, halafu uone mataifa hapa duniani yanavyojitahidi kufanyia kazi kitu kiitwacho unemployment kwa kuweka urafiki na mataifa kama UK, USA na Israel. Halafu uone kwa jinsi nchi yetu ilivyo jifanya haijui kufanyia kazi kitu kiitwacho unemployment na kuzidi kuichukia USA, UK na Israel kwa mtazamo wa kisiasa tuu. utabakia unalia kila siku!! ndio maana umasikini wetu hauwezi kuisha kirahisi!
ULIFIKIRI AU!!!!!!!!!!!!!
China, Urusi na hata Venezuela ni nchi za Kibepari?
Kwa ufinyu wako wa mawazo na uelewa unataka kutufundisha kuwa UNEMPLOYMENT inaondolewa kwa kuwa rafiki na USA, UK na Israeli? Hao ndio HR sio!
Kama kila mtu atakuwa na mawazo ya kikoloni kama yako utashangaa nini tukiwa maskini.
Labda nikuulize Tanzania ni muungano wa nchi gani .............. maana naona hamna tofauti ktk akili zenu!
