Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kila ninapotembelea hifadhi ya SERENGETI kupitia vijiji vya ISSENYE, MOTUKERI, NATTA, MAKUNDUSI, IKOMA, BURUNGA vikiwa katika lindi la umasikini na ufukara, machozi huwa yananilengalenga!
Mleta uzi asante kwa kuwa na upeo wa kutuwekea katika janvi leetu tujadili. Kama unavyojiuliza "Sijui kwa nini Tanzania ni Maskini". Nina imani kila Mtanzania mzalendo anajiuliza swali hili la muhimu.Mimi ni mdau wa utalii na niko humo kwenye utalii katika sekta binafsi.Tuna kila sababu ya kujivunia kutokana na mbuga zetu na jinsi TANAPA wanavyojitahidi kuzitunza ukilinganisha na majirani zetu.Watalii wanaoingia Serengeti wanaongezeka mwaka hadi mwaka.Ukitoa utalii wa picha (photographic safaris), kuna uwindaji katika maeneo tengefu kama Selous na kwingineko.Gharama za kuingia katika hifadhi kwa wageni ni kati ya $ 35 na $ 50 kwa kichwa kwa siku kutegemeana na hifadhi, kuna wanaokwenda safari za kupiga kambi (camping safaris) hizi zina gharama za nyongeza.
Mdau Nasikia hata mkomazi kwa Sasa inakuja juu maana iko pembezoni mwa barabara ya Same to Dar hivo ni rahisi kufikika ila ngoma inakuja kwenye makusanyo hayataeleweka wala kusaidia Wakaazi wa Same Waliotunza pori hilo toka Enzi na Enzi.
mchawi ni ccm mkiendelea kuikumbatia watakaoendelea kuneemeka ni akinana RIz moko. huyu mama anayetembea na ndege ya serikali kwa ajili ya NGO yake binafsi ya WAMA.
Mbona hujataja sifa moja muhimu sana
h. kuwa na watu wavivu wanaotegemea porojo za wanasiasa ziwaletee maendeleo.
Chifu jibu swali.
Naona wewe ndiwe unaleta porojo!
Jibu la swali lako liko kwenye hiyo sifa h.
Uvivu wa watu na porojo za wanasiasa?!? Kwa ndiyo sababu ya umasikini wetu?
Kama ndivyo, kwa nini CCM bado inaendelea kuongoza taifa la watu wavivu na wapenda porojo?
Kwa miaka takribani 52 sasa, chama kinaongoza taifa la watu wavivu? Huoni kuwa ni dalili za chama kushindwa katika sera na mikakati yake? Kwani ilipaswa iwe na mikakati ya kuwafanya watu wafanye kazi!!
Kwa maana hiyo, taifa la watu wavivu na wapenda porojo ndilo utoa viongozi wavivu na wapenda porojo. Hivyo taifa la rais mvivu na mpenda porojo, waziri mkuu na mawaziri pia!!
Hii inamaanisha pia serikali ya wavivu na wapenda porojo.
Sasa na wewe chifu unawatetea wavivu na wapenda porojo?
Jibu lako ni RUSHWA. Watanzania ni wapenda rushwa. Kila mmoja anataka kujichumia zake. Na hili tatizo liko kwa wote sio CCM bali kwa watanzania wote.
Kwani CCM imeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki?