Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Kwa nini isiachie ngazi kama imeshindwa kutoa uvivu na upenda porojo wa watanzania?

Ndiyo haijaingia kwa mtutu, lakini kama unaona hiyo ndiyo sababu ya umasikini, basi serikali yako ya CCM iachie ngazi, maana imeshindwa kazi.

Sawa, maoni yako yamesikika na yanaheshimiwa...
 
Salaam wana JF!

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.

Umasikini huo upo licha ya maliasili lukuki zilizotapakaa kwenye kila kona ya nchi:

a. Maziwa makubwa yenye samaki na viumbemaji vya kutosha - Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Ruvuma n.k.

b. Mito mikubwa yenye samaki wa kutosha - Kagera, Mara, Ruvuma, Iringa, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro, Rukwa n.k.

c. Misitu mikubwa yenye rasilimali mbao, wanyamapori, madawa ya asili, matunda, nyuki n.k. - Manyara, Tanga, Lindi, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Rukwa, Iringa n.k.

d. Wanyamapori wa kila aina - Mara, Arusha, Kigoma, Iringa, Tanga, Manyara, Pwani, Kilimanjaro, Rukwa, Zanzibar n.k.

e. Bahari ya Hindi yenye viumbebahari wa kila aina - Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi na Zanzibar.

f. Madini ya kila aina - Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera n.k.

g. Na sasa ina gesi - Mtwara

Pamoja na rasilimali watu, takribani milioni 45.

Sasa swali kwa wanachama, wapenzi, washabiki na wanazi wa CCM, kwa nini Tanzania bado ni masikini sana?

Ni swali jepesi sana, lakini lenye kuhitaji majibu ya uhakika na kina.

Cc: Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka thatha @ Atongwele

Kawaambie CHADEMA fedha ya ruzuku wanayopewa kila mwezi takribani mil.300 fedha ya Tanzania waikatae kwani ingefaa zaidi ielekezwe kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa wa fedha kama zahanati n.k.

Ningewaona chadema waungwana kweli, kama walivyo wadanganya watanzania kuwa hawataki magari ya hanasa huku wanayachukua kwa siri.

Ulaji hauna chama, hata chadema wakiingia madarakani swali lako HALITAPATA JIBU.
 
Last edited by a moderator:
Dawa ni moja tu. Nchi igawanywe kila ukandaulinde resilimali zake,serikali kuu ipelekewe asilimia kidogo ya kuendesha nchi. Na viongozi serikali kuu wasiwe na mamlaka ya kubadili mikakati ya kiuchumi ya jimbo. Rushwa itapungua kwa asilimia 80% kama si 100%
 
hamy d habari za masiku?
Kwanini tanzania bado maskini chini ya ccm?

Hii dhana ya umaskini wewe unaielezeaje?

Maana wakati mwingine mwananchi anaweza akawa anakosa mahali fulani, ili kuficha kosa lake lisionekane basi anainyooshea serikali kidole, na serikali kwa sababu ni mzazi inakubali tu lawama.

Hapa najaribu kukuonyesha kuwa, serikali imekuwa ikitoa fursa sawa kwa kila mwananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha, ili utakubaliana na mimi HASWA kwenye elimu. Hapa wengi wetu pametusaidia sana kufika hapa tulipo maana tulizingatia elimu ambayo kimsingi ilitolewa kiusawa kwa wote bila kujali jinsia, udini, ukabila na hata ukanda.

Wengi wanaolia njaa humu JF na hata hao wa huko vijiweni ni kutokana na kupuuzia kitu kinachoitwa elimu, ikiwa ni moja ya sababu ya kujiletea maendeleo yako binafsi na jamii yako kwa ujumla.

Lakini pia kuna swala la afya na ustawi wa jamii, serikali kupitia sera yake ya afya, tumeona imetoa ahueni kwa watanzania walio wengi kuweza kupata matibabu na dawa katika vituo mbalimbali, japokuwa bado hali haijaridhisha lakini kwa namna moja hama nyingine, kuwepo kwa huduma hii nyeti kwenye eneo lako, basi kunakupa fursa ya kupata huduma za kimatibabu kwa gharama nafuu ukifananisha na isingekuwepo kabisa.

Swala la ulinzi na usalama, unasema Tanzania ni maskini? BASI UMASKINI TUNAJITAKIA WENYEWE, taifa linalotambulika ulimwenguni kote kuwa kisiwa cha amani, kwa juhudi zinazofanywa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kuwa na mbinu madhubuti za ki-intelijensia, watu wanatoka sehemu moja kwenda nyingine bila kubugudhiwa, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?

Mitandao ya miundombinu iliyotandazwa hapa nchini, inayowezesha kusafirisha bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?

Kwa uchache tu nimeelezea namna ambavyo serikali imejitahidi kuwezesha kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutimiza wajibu wake, LAKINI SWALI LA MSINGI LA WEWE RAIA KUJIULIZA, UMETIMIZA WAJIBU WAKO?
 
Kwanza kabisa, ni hao mnaohemea njaa ndiyo wanaiweka Tanzania katika kundi la nchi masikini sana.

Pili, serikali uwekwa madarakani na wananchi ili wakusanye kodi na kuzitumia kodi hizo kuleta maendeleo.

Sasa nikikosa maji, umeme, huduma bora ya afya, elimu bora, usafiri bora n.k., lawama zote nazipeleka kwa serikali. Kwani inakuwa imeshindwa kutumia kodi kuleta maendeleo.

Hapa najaribu kukuonyesha kuwa, serikali imekuwa ikitoa fursa sawa kwa kila mwananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha, ili utakubaliana na mimi HASWA kwenye elimu. Hapa wengi wetu pametusaidia sana kufika hapa tulipo maana tulizingatia elimu ambayo kimsingi ilitolewa kiusawa kwa wote bila kujali jinsia, udini, ukabila na hata ukanda.

Chifu wewe mtanzania kweli? Unaongelea fursa sawa za elimu? Fursa sawa zitakuja kwa mfumo wa shule za kata kweli? Umeona matokeo yake, 94% wamefeli!! Acha utani aisee.

Wengi wanaolia njaa humu JF na hata hao wa huko vijiweni ni kutokana na kupuuzia kitu kinachoitwa elimu, ikiwa ni moja ya sababu ya kujiletea maendeleo yako binafsi na jamii yako kwa ujumla.

Hii imekuwa ni nyimbo ya CCM baada ya kushindwa kutimiza 'maisha bora kwa kila mdanganyika'. Serikali lazima iweke misingi mizuri ya raia wake kujiletea maendeleo. Sasa, kwa kupeleka mbolea baada ya msimu wa kilimo, maendeleo yatapatikana kweli? Bila matumizi bora ya pesa za umma, madawa yanakosekana, barabara hazijengwi ipaswavyo, shule zinakosa walimu na maabara n.k., hapo maendeleo yatapatikana kweli?!

Lakini pia kuna swala la afya na ustawi wa jamii, serikali kupitia sera yake ya afya, tumeona imetoa ahueni kwa watanzania walio wengi kuweza kupata matibabu na dawa katika vituo mbalimbali, japokuwa bado hali haijaridhisha lakini kwa namna moja hama nyingine, kuwepo kwa huduma hii nyeti kwenye eneo lako, basi kunakupa fursa ya kupata huduma za kimatibabu kwa gharama nafuu ukifananisha na isingekuwepo kabisa.

Nakuuliza tena, wewe ni mtanzania kweli? Na upo Tanzania kwa sasa?
Huduma ya afya Tanzania ni mbovu kuliko maelezo!! Au hizo bajaji za wajawazito unaona ni kitu cha kujivunia?
Unaongelea upatikanaji wa dawa kwenye hospitali za serikali au kwenye maduka ya madawa binafsi? Maana kama hospitalini, dawa ni msamiati!

Hapa hupaswi kusema swala la huduma ya afya kutokuwepo. Ina maana unataka kusema serikali inatusaidia kwa kutoa huduma hiyo? Ah wapi! Huo siyo msaada, ni lazima serikali itoe huduma bora za afya kupitia kodi inazokusanya.

Swala la ulinzi na usalama, unasema Tanzania ni maskini?

Wewe mjomba haupo Tanzania. Ulinzi gani na usalama, kama nchi inashindwa kuwapata majambazi tu, mpaka iombe msaada?!? Viumbepori wanasafirishwa mchana kweupe!! Wahamiaji haramu wanaingia nchini, tena hadi makao makuu ya nchi bila kukamatwa?!?

Mitandao ya miundombinu iliyotandazwa hapa nchini, inayowezesha kusafirisha bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?

Barabara hizi za Makomeo!?! Hizo ni wajibu wa serikali, hamna haja ya kujisifia. Si ndiyo maana mkapata 'ridhaa' ya kuongoza nchi; ili mtumie kodi zetu kuleta maendeleo. Hapa unachojisifia ni sawa na mzazi kujisifia juu ya yeye kumpeleka mtoto wake shule!!

Pili, barabara zenyewe ni za chini ya viwango mno! Barabara gani ukipita na gari unakuwa kama unapita kwenye barabara zenye makorongo?!?

Kwa uchache tu nimeelezea namna ambavyo serikali imejitahidi kuwezesha kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutimiza wajibu wake, LAKINI SWALI LA MSINGI LA WEWE RAIA KUJIULIZA, UMETIMIZA WAJIBU WAKO?

Serikali haipaswi kujitahidi! Inapaswa ifanye yale wananchi waliowaweka madarakani, wanayataka. Hili la kujitahidi, ni dalili za kushindwa. Suluhisho lake ni kukaa pembeni.

Mimi natimiza wajibu wangu kwa taifa. Lakini nasikitika kodi zangu hazionekani ni vipi zinasaidia maendeleo mazima ya taifa! Pili, nasikitika kile ninacholipwa na serikali hakiendani na shughuli ninazofanya! Mshahara kiduchu, huku kodi zangu zikienda mifukoni mwa wateule wachache!!
 
Dawa ni moja tu. Nchi igawanywe kila ukandaulinde resilimali zake,serikali kuu ipelekewe asilimia kidogo ya kuendesha nchi. Na viongozi serikali kuu wasiwe na mamlaka ya kubadili mikakati ya kiuchumi ya jimbo. Rushwa itapungua kwa asilimia 80% kama si 100%
Ukanda ni nini na kitambulisho chake ni kipi katika dhana nzima ya nchi. Zipi ni raslimali za nchi na zipi niza ukanda?.
 
Hii dhana ya umaskini wewe unaielezeaje?

Maana wakati mwingine mwananchi anaweza akawa anakosa mahali fulani, ili kuficha kosa lake lisionekane basi anainyooshea serikali kidole, na serikali kwa sababu ni mzazi inakubali tu lawama.

Hapa najaribu kukuonyesha kuwa, serikali imekuwa ikitoa fursa sawa kwa kila mwananchi kuondokana na hali ngumu ya maisha, ili utakubaliana na mimi HASWA kwenye elimu. Hapa wengi wetu pametusaidia sana kufika hapa tulipo maana tulizingatia elimu ambayo kimsingi ilitolewa kiusawa kwa wote bila kujali jinsia, udini, ukabila na hata ukanda.

Wengi wanaolia njaa humu JF na hata hao wa huko vijiweni ni kutokana na kupuuzia kitu kinachoitwa elimu, ikiwa ni moja ya sababu ya kujiletea maendeleo yako binafsi na jamii yako kwa ujumla.

Lakini pia kuna swala la afya na ustawi wa jamii, serikali kupitia sera yake ya afya, tumeona imetoa ahueni kwa watanzania walio wengi kuweza kupata matibabu na dawa katika vituo mbalimbali, japokuwa bado hali haijaridhisha lakini kwa namna moja hama nyingine, kuwepo kwa huduma hii nyeti kwenye eneo lako, basi kunakupa fursa ya kupata huduma za kimatibabu kwa gharama nafuu ukifananisha na isingekuwepo kabisa.

Swala la ulinzi na usalama, unasema Tanzania ni maskini? BASI UMASKINI TUNAJITAKIA WENYEWE, taifa linalotambulika ulimwenguni kote kuwa kisiwa cha amani, kwa juhudi zinazofanywa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kuwa na mbinu madhubuti za ki-intelijensia, watu wanatoka sehemu moja kwenda nyingine bila kubugudhiwa, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?

Mitandao ya miundombinu iliyotandazwa hapa nchini, inayowezesha kusafirisha bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, UTASHINDWA KUPAMBANA NA UMASKINI?

Kwa uchache tu nimeelezea namna ambavyo serikali imejitahidi kuwezesha kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutimiza wajibu wake, LAKINI SWALI LA MSINGI LA WEWE RAIA KUJIULIZA, UMETIMIZA WAJIBU WAKO?
Jibuni hoja,achane uongo uongo,huo unafuu wa matibabu unaouongelea ktk afya upi?Umezunguka vijijini ukaona jinsi Zahanati zilivyo na uhaba wa dawa?Au unaongea tu kwasababu uko mjini?Unazungumzia Tz ni kitovu cha amani,amani gani?Viongozi wa dini wanauwawa,makanisa yanachomwa,vita za Koo Mara,waandishi wa habari na raia wa kawaida wanauwawa na Polisi,halafu unasema kitovu cha amani.Acheni kuwadaa watanzania.Na 2015 mtaona ni jinsi gani watanzania tulivyoamka,na mtaona ni jinsi gani hizo porojo zenu zisivyopewa nafasi.
 
Rushwa? Sasa serikali ya CCM inaendeleaje kuongoza taifa la wapenda rushwa? Kwa nini isiseme imeshindwa na iachie ngazi?
kama ni swala la kuachia ngazi kwa sababu ya rushwa basi itabidi mimi na wewe pia tuachie ngazi. Hata CCM wakiachia ngazi na wakaja wengine hiyo haitazuia watanzania kuomba na kutoa rushwa.
 
Fanya kaz uone ka tutaendele kuwa maskn na uwambie wenzio wasiandamane ila wa work hard ndo utayaona maendeleo
 
Mbona hujataja sifa moja muhimu sana
h. kuwa na watu wavivu wanaotegemea porojo za wanasiasa ziwaletee maendeleo.

.....

Baada ya sisiem kuuza viwanda vijana wamekosa ajira kwa hiyo watu wanashida Fb,jf na kwenye vijiwe vya kahawa kupiga zogo na ndio maana hata fast jet alijitoa fahamu kuwa hajui chanzo cha umasikini wetu.
 
Hivi mlevi anaewanunulia walevi wenzake pombe.anaweza akaacha pombe?ni sawa na kuiambia serikali ya ccm iache kuongoza wala rushwa wakati wenyewe ndio wala rushwa wakubwa wanaoongoza?
 
Mbona hujataja sifa moja muhimu sana
h. kuwa na watu wavivu wanaotegemea porojo za wanasiasa ziwaletee maendeleo.

.......

Ni kweli kabisa watu wavivu porojo wakisaidiwa mikopo na taasisi hawataki kurudusha wakipewa maeneo ya madini kama wachimbaji wadogo wakipata madini hayo hukwepa kulipa kodi na kuwauzia wafanya magendo.

Hawa ndio watanzania na milele na milele tutabaki vilevile kutafuta mchawi wa umasikini wetu
.
 
Salaam wana JF!

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.

Cc: Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka thatha Atongwele

......

JIBU: sio watanzania wote masikini sisi viongozi wa CCM sio masikini,hivyo tunashangaa kwa nini watanzania ni masikini.
 
kama ni swala la kuachia ngazi kwa sababu ya rushwa basi itabidi mimi na wewe pia tuachie ngazi. Hata CCM wakiachia ngazi na wakaja wengine hiyo haitazuia watanzania kuomba na kutoa rushwa.

Kwa hiyo suluhisho ni serikali kuendelea kuongoza kwa kuwa hakuna atakayeweza kuzuia watanzania kutoa na kuomba rushwa? Seriously? Mbona unakuwa mtabiri?

Hivi uwa unajiuliza kwanini kuomba na kutoa rushwa kumeshamiri? Huoni kwamba huduma mbovu za kijamii ndiyo pengine sababu? Mtu unaenda hospitali, hakuna madawa, manesi na madaktari hawana morali, unaona ukitoa visenti kadhaa utaweza kuboost morali ya hao jamaa ili upate huduma! Ingawa si sawa, lakini mfumo mbovu wa huduma za jamii ndiyo inapelekea iwe hivyo.

Hivi kiongozi wa serikali (waziri ama katibu mkuu) kuomba asilimia 10 ya mradi fulani wa mwekezaji ili mambo yaende sawa, nayo unasema haitaweza kuzuilika? Kama kungekuwa na uzingatiaji na utekelezaji wa sheria kali za kupambana na rushwa hizo, unafikiri yangeendelea kuwepo? Sasa, kama hadi rais anampigia debe mtuhumiwa wa kesi ya rushwa, hapo kweli kuna utashi wa kuzuia rushwa?

Bado hajatoa jibu; bado mnakuja na majibu mepesi katika swali jepesi!!
 
CCM someni na hii ili mjue tatizo liko wapi na kwa nini hatusongi mbele????…….

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.

Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?

Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA?

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa.
 
Ni kweli kabisa watu wavivu porojo wakisaidiwa mikopo na taasisi hawataki kurudusha wakipewa maeneo ya madini kama wachimbaji wadogo wakipata madini hayo hukwepa kulipa kodi na kuwauzia wafanya magendo.

Chifu, hizo si ndiyo stahili za wakubwa wa serikali ya CCM? Ujanja ujanja kwenye mali za umma! Hadi wanauza viumbepori hai mchana kweupe! Hadi wanauza ardhi kubwa kwa waarabu mchana kweupe! Kodi kwa makampuni makubwa hazilipwi; tena wanapewa misahama mikubwa ya kodi, huku wakipewa miaka ya kufanya majaribio, kama wakiona hakuna faida, wanaruhusiwa kuacha!

Hawa ndio watanzania na milele na milele tutabaki vilevile kutafuta mchawi wa umasikini wetu

Vyema. Kama ndiyo hivyo, kwanini tunaweka serikali madarakani? Kuna haja gani ya kuwa na serikali kwa mtazamo wako?
 
Jibu lako ni RUSHWA. Watanzania ni wapenda rushwa. Kila mmoja anataka kujichumia zake. Na hili tatizo liko kwa wote sio CCM bali kwa watanzania wote.

Mkuu kama watu ni wapenda rushwa anayetakiwa kuwathibiti si Serikali?

Katika mataifa kama Japan, Korea, rushwa ni ndogo sana sana kutokana na hatua kali zinazochuliwa na serikali yao dhidi ya wala rushwa.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Salaam wana JF!

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Tanzania ni moja kati ya mataifa masikini sana duniani.

Umasikini huo upo licha ya maliasili lukuki zilizotapakaa kwenye kila kona ya nchi:

a. Maziwa makubwa yenye samaki na viumbemaji vya kutosha - Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Ruvuma n.k.

b. Mito mikubwa yenye samaki wa kutosha - Kagera, Mara, Ruvuma, Iringa, Mtwara, Tanga, Kilimanjaro, Rukwa n.k.

c. Misitu mikubwa yenye rasilimali mbao, wanyamapori, madawa ya asili, matunda, nyuki n.k. - Manyara, Tanga, Lindi, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Rukwa, Iringa n.k.

d. Wanyamapori wa kila aina - Mara, Arusha, Kigoma, Iringa, Tanga, Manyara, Pwani, Kilimanjaro, Rukwa, Zanzibar n.k.

e. Bahari ya Hindi yenye viumbebahari wa kila aina - Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi na Zanzibar.

f. Madini ya kila aina - Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera n.k.

g. Na sasa ina gesi - Mtwara

Pamoja na rasilimali watu, takribani milioni 45.

Sasa swali kwa wanachama, wapenzi, washabiki na wanazi wa CCM, kwa nini Tanzania bado ni masikini sana?

Ni swali jepesi sana, lakini lenye kuhitaji majibu ya uhakika na kina.

Cc: Ritz chama zomba Jichola3 ZeMarcopolo Nduka thatha Atongwele

Jibu ni kwamba sisi ni maskini kwa sababu tunatunza mazingira hatutaki kuharibu Mazingira kwa shughuli nyingi za kiuchumi hivyo tunapaswa kupongezwa🙂

Kawaambie CHADEMA fedha ya ruzuku wanayopewa kila mwezi takribani mil.300 fedha ya Tanzania waikatae kwani ingefaa zaidi ielekezwe kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa wa fedha kama zahanati n.k.

Ningewaona chadema waungwana kweli, kama walivyo wadanganya watanzania kuwa hawataki magari ya hanasa huku wanayachukua kwa siri.

Ulaji hauna chama, hata chadema wakiingia madarakani swali lako HALITAPATA JIBU.

Waliopaswa kuliona hilo wakwanza kabisa ni wale wanaozitoa fedha hizo (serikali ya CCM).

lakini CCM kwa mfano baada ya kukaa madarakani kwa miaka zaidi ya 40 na ushee.......na kujijenga vilivvyo, na kujimilikisha mali nyingi ambazo hazikuwa zao, hao ndio wangekuwa wakwanza kukataa ruzuku au kuzielekeza ktk maeneo ya uhitaji kama ulivyopendekeza.

Badala yake hata ruzuku haiwatoshi wanaongezea nyingine kwa njia za ufisadi au hilo umesahau???????????
 
Back
Top Bottom