Sababu kuu hii hapa👇
Your browser is not able to display this video.
 
Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?
 
Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?
Nimejaribu kukujulisha kuwa majukumu ya kutafuta Katiba mpya ni yetu wananchi,sifahamu kwa nini unahusisha hoja hii na upatikanaji wa ugali?Una njaa kiasi gani?

Tunahitaji Katiba itakayoifanya jamii kushiriki kufanya maamuzi na kujichagulia aina ya mfumo bora wa uongozi.Hadi leo hakuna anayepinga ubovu wa katiba ya sasa,wala kuwa katiba mpya inahitajika au haihitajiki?

Sehemu inayosababisha ubishi ni pale kunapokuwa na juhudi kubwa ya kuwanyima na kuchelewesha wananchi kuandika Katiba mpya.
Tujiulize juhudi hizo zinamnufaishaje mwananchi aliyegharamikia mchakato uliofanywa wa kuandika katiba kupitia Tume ya Warioba?
 
Katiba Mpya ipo, ni suala la kumalizia mchakato tu. Au unataka nyingine wakati ipo Katiba Inayopendekezwa?
 
Raslimali za nchi tupa kule muhimu ni kuwa ombaomba upate easy money unawapa akina malope Wana Kodi soft ware kwa mhindi anawapa Chao maisha yanaendelea kana Jana tu.
 
Waafrika kwa ujumla wetu tunahangaishwa na:-
1 - Ushirikina
2 - Wizi
3 - Uongo
4 - Uvivu
5 - Kutojiamini
6 - Uthubutu
Na kwa kuongezea, Kuna gurupu kubwa la wazazi wanaodanganya watoto wao washinde wanalalamikia serikali kwa kushindwa majukumu yao, Kila mtoto akihudumia na wazazi wake kama jukumu lao na wale yatima wakalelewa na jamii yote hao watoto wakiwa taifa la kesho watahudumia vizazi vyao pia mwisho serikali inapata majuku ya maendeleo ya kisasa kwa watu wa kisasa maana wasipoleta kelele zake zitakuwa kubwa maana watu watakuwa wanaishi kisasa ila Sasa kelele nyingi ni za kijingajinga mfano mtu analalamika serikali kupeleka umeme, maji, barabara vijijini au hata viwanja vya ndege Ili watu wengi waendelee kuishi kama watu wa kale na ndo huu umasikini kwa kiwango kikubwa unaonekana. Swali la uchokozi hivi Kuna mzazi yupo proud kumpa mtoto wake Mali kama maandiko ya Dini yanavyosema? Mali na urithi mtu hupata kwa babaye Sasa tungejenga jamii ya hivi umasikini ungekuwa historia.
 
Shida ipo hapo na utitiri wa taasisi, angalia kuna TANROAD lakini hapo hapo kuna TARURA, kuna RUWASA lakini hapo hapo kuna mamlaka za maji yaani ni mambo ya hovyo sn
Hao ni watoto wa serikali wa kuhudumia jamii hakuna shida zikiwepo maana lazima dunia itengeneze mifumo ya watu wake kupata kazi za kufanya kama agizo la Mungu tufanye kazi Ili tule, shida inakuja kwenye matokeo ya huduma kama haziwafii watu kwa uzuri na gharama nafuu hapo kelele zipigwe.
 
Hujawahi kujiuliza kwanini wazaramo ni malofa sana wakati ndio waliokuwa wanamiliki Kariakoo yote?
 
Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?
Huwa nashangaa na hii issue ya katiba hii iliyopo tu hatuijui wala hatuitekelezi badala ya kujikita kwanini hii iliyopo haitekelezi wala wengi wetu hatuijui ukiuliza moja utasikia tume huru basi watu wanatafuta madaraka. Tufanye kazi kuna nchi hazina hata katiba huko Qatar sijui UAE na watu wanasonga mbele tu.
 
CCM
 
Katiba Mpya ipo, ni suala la kumalizia mchakato tu. Au unataka nyingine wakati ipo Katiba Inayopendekezwa?
Katiba pendekezwa ni Katiba ya CCM japokuwa hata hivyo tofauti yake na Katiba ya 1977 ni cover tu.Mapendekezo yaliyomo yalipitishwa kwa mbwembwe na ushabiki wa kichama,Ref.sebene la Sanga baada ya kura za maruhani!
 
Kwani ukiunganisha TANROAD na TARURA wakawa ofisi moja hawezi kufanya kazi?
 
PUTIN: AFRIKA HAITOKAA IWE HURU

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.

Mzungu au mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?

Quote
 
Labda kwa sababu ina watu wachache wenye uwezo mkubwa wa akili kuleta maendeleo ila wengi wao hawajihusishi na siasa.
 
Utajiri huu wanafaidi viongozi wa serikali ya CCM, Familia zao na Magenge yao (Lumumba buku saba saba na MACHAWA).

KATIBA MPYA ni muhimu sana ili kuweka haya mambo sawa.
 
Kwanza kabisa ningependa ku share na wanajamii forum wenzangu juu ya swali nililoshindwa kulijibu kutoka kwa kijana wangu, baada ya kijifikiria sana nikaona nina deni la kujibu swali lake.

Last week tukiwa tunaangalia hafla ya upokeaji wa ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania B767-300F) niliulizwa swali na kijana wangu wa darasa la 5 "Baba kwa nini nchi yetu ni masikini ilihali tuna Watu, Madini, Mbuga za Wanyama, Bahari, Mito na Maziwa?"

Ningependa kupata jibu na kumpatia maana aliishia kufokewa na mama yake kwa kuwa kabla ya hapo kulishakuwa na mfululizo wa maswali. Naomba msaada wa majibu ya wewe kama mzazi ungejibu vipi swali hili kwa kijana mdogo kama huyo.​
 
niliulizwa swali na kijana wangu wa darasa la 5 "Baba kwa nini nchi yetu ni masikini ilihali tuna Watu, Madini, Mbuga za Wanyama, Bahari, Mito na Maziwa?"​
CCM...Chama Cha Mafisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…