Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Sababu kuu hii hapa👇
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?Ugali haujawahi kuwa miongoni mwa changamoto yangu.Ninapigania HAKI na UTU kwa binadamu wote.
Kuhusu serikali kufanya kazi ndicho tunachopigania.Tunataka Katiba mpya ili nchi isonge mbele kwa sababu katiba tuliyonayo imeshindwa kujisimamia na siyo shirikishi.
Nimejaribu kukujulisha kuwa majukumu ya kutafuta Katiba mpya ni yetu wananchi,sifahamu kwa nini unahusisha hoja hii na upatikanaji wa ugali?Una njaa kiasi gani?Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?
Katiba Mpya ipo, ni suala la kumalizia mchakato tu. Au unataka nyingine wakati ipo Katiba Inayopendekezwa?Nimejaribu kukujulisha kuwa majukumu ya kutafuta Katiba mpya ni yetu wananchi,sifahamu kwa nini unahusisha hoja hii na upatikanaji wa ugali?Una njaa kiasi gani?
Tunahitaji Katiba itakayoifanya jamii kushiriki kufanya maamuzi na kujichagulia aina ya mfumo bora wa uongozi.Hadi leo hakuna anayepinga ubovu wa katiba ya sasa,wala kuwa katiba mpya inahitajika au haihitajiki?
Sehemu inayosababisha ubishi ni pale kunapokuwa na juhudi kubwa ya kuwanyima na kuchelewesha wananchi kuandika Katiba mpya.
Tujiulize juhudi hizo zinamnufaishaje mwananchi aliyegharamikia mchakato uliofanywa wa kuandika katiba kupitia Tume ya Warioba?
Na kwa kuongezea, Kuna gurupu kubwa la wazazi wanaodanganya watoto wao washinde wanalalamikia serikali kwa kushindwa majukumu yao, Kila mtoto akihudumia na wazazi wake kama jukumu lao na wale yatima wakalelewa na jamii yote hao watoto wakiwa taifa la kesho watahudumia vizazi vyao pia mwisho serikali inapata majuku ya maendeleo ya kisasa kwa watu wa kisasa maana wasipoleta kelele zake zitakuwa kubwa maana watu watakuwa wanaishi kisasa ila Sasa kelele nyingi ni za kijingajinga mfano mtu analalamika serikali kupeleka umeme, maji, barabara vijijini au hata viwanja vya ndege Ili watu wengi waendelee kuishi kama watu wa kale na ndo huu umasikini kwa kiwango kikubwa unaonekana. Swali la uchokozi hivi Kuna mzazi yupo proud kumpa mtoto wake Mali kama maandiko ya Dini yanavyosema? Mali na urithi mtu hupata kwa babaye Sasa tungejenga jamii ya hivi umasikini ungekuwa historia.Waafrika kwa ujumla wetu tunahangaishwa na:-
1 - Ushirikina
2 - Wizi
3 - Uongo
4 - Uvivu
5 - Kutojiamini
6 - Uthubutu
Hao ni watoto wa serikali wa kuhudumia jamii hakuna shida zikiwepo maana lazima dunia itengeneze mifumo ya watu wake kupata kazi za kufanya kama agizo la Mungu tufanye kazi Ili tule, shida inakuja kwenye matokeo ya huduma kama haziwafii watu kwa uzuri na gharama nafuu hapo kelele zipigwe.Shida ipo hapo na utitiri wa taasisi, angalia kuna TANROAD lakini hapo hapo kuna TARURA, kuna RUWASA lakini hapo hapo kuna mamlaka za maji yaani ni mambo ya hovyo sn
Hujawahi kujiuliza kwanini wazaramo ni malofa sana wakati ndio waliokuwa wanamiliki Kariakoo yote?
KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?
Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.
Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).
Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).
Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.
Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.
Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.
Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.
Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku.
Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..
Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.
Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).
KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, WAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.
===================
Return Of Undertaker anasema,
KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI
1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.
2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.
3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.
7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).
9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k
10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).
12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.
13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.
14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.
15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.
16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).
18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.
19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.
20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.
21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.
24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.
24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).
25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.
26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.
Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?
===================================
Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini
Huwa nashangaa na hii issue ya katiba hii iliyopo tu hatuijui wala hatuitekelezi badala ya kujikita kwanini hii iliyopo haitekelezi wala wengi wetu hatuijui ukiuliza moja utasikia tume huru basi watu wanatafuta madaraka. Tufanye kazi kuna nchi hazina hata katiba huko Qatar sijui UAE na watu wanasonga mbele tu.Katiba inaleta ugali? Kwani umezuiliwa kutafuta na kufanya kazi?
CCMKuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?
Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.
Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.
Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.
Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Katiba pendekezwa ni Katiba ya CCM japokuwa hata hivyo tofauti yake na Katiba ya 1977 ni cover tu.Mapendekezo yaliyomo yalipitishwa kwa mbwembwe na ushabiki wa kichama,Ref.sebene la Sanga baada ya kura za maruhani!Katiba Mpya ipo, ni suala la kumalizia mchakato tu. Au unataka nyingine wakati ipo Katiba Inayopendekezwa?
Kwani ukiunganisha TANROAD na TARURA wakawa ofisi moja hawezi kufanya kazi?Hao ni watoto wa serikali wa kuhudumia jamii hakuna shida zikiwepo maana lazima dunia itengeneze mifumo ya watu wake kupata kazi za kufanya kama agizo la Mungu tufanye kazi Ili tule, shida inakuja kwenye matokeo ya huduma kama haziwafii watu kwa uzuri na gharama nafuu hapo kelele zipigwe.
Utajiri huu wanafaidi viongozi wa serikali ya CCM, Familia zao na Magenge yao (Lumumba buku saba saba na MACHAWA).
KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?
Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.
Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).
Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).
Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.
Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.
Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.
Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.
Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku.
Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..
Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.
Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).
KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, WAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.
===================
Return Of Undertaker anasema,
KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI
1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.
2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.
3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.
7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).
9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k
10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).
12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.
13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.
14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.
15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.
16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).
18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.
19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.
20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.
21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.
24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.
24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).
25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.
26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.
Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?
===================================
Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini
CCM...Chama Cha Mafisadiniliulizwa swali na kijana wangu wa darasa la 5 "Baba kwa nini nchi yetu ni masikini ilihali tuna Watu, Madini, Mbuga za Wanyama, Bahari, Mito na Maziwa?"