Tatizo ni viongozi hawana nia thabiti ya kuleta maendeleo
 
Tanzania Sio maskini bali Kuna baadhi ya watanzania ni maskini Sio wote
Watanzania wote ni masikini hao unaowaona matajiri wengi ni janja janja na wizi. Ukifanya nao kazi utaelewa, hakuna mtu tajiri analipa wafanyakazi mishahara duni au kuwadhulumu.
 
Mazi
Sababu ni hizi:
1. Wa Tanzania hatuna Uzalendo na Nchi yetu.

2. Ubinafsi unatufanya tuendelee kuwa masikini. Ukiwa na Chance unashindwa nini kumsaidia jirani yako? Watu wanaogopa kuwasaidia sababu wanajua watawazidi au wanajua wakisaidiwa wakafanikiwa wataaza kuwakejeli na kuwatharau.

3. Bado hatuna malezi manzuri, Kijana muda wote anawaza Ngono na Pisi Kali huyo atapambana kweli?? Jibu hapana. Kadri unavolala na wanawake wengi do unapata nafasi kubwa ya kuwa masikini.

4. Uzembe do unaotufanya tuendelee kuwa masikini, imagine mtu asubuhi anaamkia kucheza Draft au Kamali unategemea huyo mtu ataweza kujikwamua na umasikini.

5. Hatuna uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii, watu ili wafanye kazi wanahitaji External Force.

6. Extended Family inachangia sana, Mwanaume unauwezo wa kulea watoto 5 wewe unazaa watoto 15, hapo utatoboa kweli?

7. Elimu zetu zinatuandaa kuwa waajiriwa wa serikalini sababu, Somo la biashara hawalipati wengi zaidi ya asilimia 90 ya wanachuo hawajasoma somo la biashara, hata kama wagesoma bado tu wasigeweza kufanya vizuri sabab mitaala yetu ni theory oriented.

8. Serikali bado haitusaidii sisi wana nchi wake, Jiulize tu HARRIER inauzwa Milioni 15 hadi 16 Japan hadi bandari ya DSM, bado hapo mtu unapaswa kulipa KODI KUBWA kuliko bei ya Gari, what do you expect hapoo??

9. Kukithiri kwa Rushwa hii inachangia kuendelea kuwa masikini.

10. Upendeleo au kutokuepo kwa usawa katika Suala nzima la Maendeleo ya kijamii na kitaifa.

11. Usimamizi mbaya wa Rasilimali Mama za Taifa (Madini, Banfari, Hifadhi, Mapato)

12. Ukosekanaji wa Viwanda vya kisasa, sababu tunachokizalisha hatuwezi kukichakata kwa ajiri ya kuwa Rawfull material na kuuza kweny masoko ya Dunia.

Sababu ni nyingiii sana.

Ushauri wangu.

Mtoto anapoaza shule ya msingi tu litolewe somo la:

1. Somo la uzalendo
2. Somo la biashara
3. Somo la malezi na utamaduni
 
Tatizo ni ccm.
 
Watu wananunua magari mpaka nambe E zinakaribia kujaa halafu unasema hii Inji ni maskini?....…..........alisikika mwehu mmoja akiuliza............na bado tutaendelea kuwa maskini na maskini kama tutaendelea kuongozwa na watu wale wale.
 
Usizifananishe nchi za S.Africa,China,S.Arabia na kitongoji kinachoitwa Tanzania
 
The green mambas(CCM)!!
 
Kikwete alipokuwa rais aliulizwa hilo swali na Bob Geldof, akajibu hajui.
 
Hifunze kuongea kwa Takwimu
 
Samia alisema tumetoka uchumi wa kati na sasa tuko uchumi wa chini yaani nchi zenye umaskini mkubwa.
Wewe unajazwa ujinga na unaendelea kukujaa. Mimi naamini kama nchi Tanzania sio masikini. Bali, Watanzania ndio masikini wa akili.
 
MTU mweusi ndivyo alivyo

Kama unadhani watu ni masikini kisa hawana pesa ,majumba au magari utakuwa unakosea.

Tafuta masikini yeyote umpe hela then utazame matumizi yake!

Duniani kote alipo MTU mweusi huwa hakuna maendeleo
🙄
 
Mkuu, what a good publication you have presented today about the opposition more especially CDM!

In your presentation you have convey your deepest fears concerning the strength and the position occupied by CDM ina particular in the mind and heart of the masses!

Your presentation is a good media publicity advert free of charge, Hongera sana, na uendelee na huo moyo Mkuu!
 
Kwa sababu ya CCM.
Hilo halina mjadala.
Ni kama Cuba bado wanaishi maisha ya miaka ya 1950's.
Inasikitisha sana.
Tatizo ni zaidi ya ccm. Ingekuwa tatizo ni ccm peke yake, basi chadema sasa hivi kingekuwa chama cha kupigiwa upatu kila mahali kwa kuleta revolution ideas za kimaendeleo. Lakini wapi, hata kiwanja tu cha kujenga ofisi ya makao makuu ya chama hawana!
Kama tunataka kupata solution halisi ya umaskini wetu, ni lazima tuliangalie tatizo ndani yaidi ya ccm peke yake.
Btw, huko kenya, Uganda, DRC, nk hakuna ccm, lakini nao ni maskini!
 
Jibu ni uwepo wa CCM madarakani.
 
Tanzania sio maskini!

Bali Kuna matumizi mabaya ya fedha za wananchi!!

Fedha nyingi zinateketea Kwa kulipa mishahara na posho Kwa wanasiasa kuliko kuhudumia wananchi kwenye kilimo,Afya na elimu!

Ajira bado zipo.nyingi sana na fedha za kuajiri zipo tatizo hayo.mapesa wanasiasa wanajilipa maposho na kupiga dili!!!

Nikiingia huo mchezo hautokuwepo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…