Ili ujue ondoa mahaba kwa CCM weka mahaba yako kwa watanzania wote. Weka mahaba kwa taifa lako.
Usifurahie kuona watanzania wanateseka kwa sababu tu sio CCM au wazazi wao sio makada wa CCM au marafiki zao sio makada wa CCM.
Wengi wanaokula mema ya nchi hii katika madaraka ,ajira nzuri zenye mishahara minono,ama sehemu zenye maisha bora ni ama makada au marafiki zao au wanatokana na mizizi ya wazazi waliokua makada wa CCM.
Hawa akili zao zimegota mana hawajawahi kufikiri sawasawa kuhusu umaskini wa watanzania zaidi ya 80 % kwa kuwa marafiki zao pia ni hao wa kundi hilo. Hawa kamwe hawawezi kujua tatizo la sera , bunge na serikali ya CCM kupata ufaulu wa 20 % tu na kufeli kwa 80%.
Nikirejea kwenye mada :
Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji mambo MANNE:-
1. Watu
2. Ardhi
3. Siasa safi
4. Uongozi bora.
Hapo namba Tatu ndipo tulipo kosa sana na kupoteza uelekeo tangu CCM ilipofanya mapinduzi na kuua azimio la Arusha.Na pia kuzuia juhudi za kulirejesha kwa kupinga Katiba ya Warioba.
Namba nne haijawahi kuwa na shida sana mana kila mmoja anafuata udhaifu wa CCM( chama na bunge lake lenye 78% makada na wakuu wa taasisi zote ambao ni makada.)
Kuna sera nyingi tunazolazimishwa na CCM kuzifuata za kutuletea umaskini na kamwe hatutaweza kutoka kama tutaziendekeza.
Mara nyingine hata marais wetu wanakuja naawazo bora na dhamira ya kujenga nchi lakini sera na misimamo ya CCM ina waangusha chini na kuwagalagaza.
Mfano ni nia nzuri ya kishujaa aliyokuwa nayo Rais wa awamu ya nne ya kutuletea katiba ya wananchi.
Wazo lake na nia yake ilizimwa na CCM na wabunge wake. Chama kilisimama kidete kulinda sera zake na kuangamiza taifa kwa kutuachia katiba ya mkoloni. Katiba inayowafanya wafrika wenzetu kututawala kikatili kinyume na walivyokusudia babu zetu walipinga utawala wa kikatili wa mkoloni.
Yani mtanzania na mtanzania hawawezi kuvumiliana na kukosoana kwa hoja. Watu wanazungumza kwa pingu,risasi na virungu .
Bunge limekuwa ni sehemu ya vyama kuadhibiana na kuwajibishana badala ya kuiwajibisha serikali na kuiadhibu pale inapokuja hoja ya wazi ya serikali kukosea.
Chama kimetoka mbali kabisa na malengo ya waasisi wa taifa hili waliokusudia kujenga,uhuru, umoja, mshikamano na amani ya kweli kwa waafrika wa nchi hii kwa kujenga ustawi wa watu kama makazi bora na kilimo chenye tija na kuwainua wakulima na wafanyakazi.
Chama kimekua ni mali ya wanasiasa na watawala badala ya wakulima na wafanyakazi. Mfanyakazi haruhusiwi tena kukosoa chama chake(CCM).
Nyundo imekua ni kwa ajili ya kuwaponda watanzania na kuwaua na Jembe limekua kwa ajili ya kuwachimbia kaburi.
Mleta mada nadhani umepata jibu kama utaruhusu akili yako isimame kwenye ukweli.
Sent using
Jamii Forums mobile app