FaizaFoxy;3269000]Hapo sio sahihi, Mjerumani aliwekeza reli inayopita sehemu zote muhimu, kulikuwa kuna central, south na north Routes. Mwingereza aliirithi reli na akahakikisha inafanya kazi vizuri kabisa, na wakati tunachukuwa Uhuru, kulikuwa kuna reli kila siku ya kwenda Mwanza, ya kwenda Tanga, Ya kwenda Arusha na ya kwenda mpaka Kenya. Ambapo hakuna reli kulikuwa kuna mabasi ya Railway na magari ya mizigo ya railway. Barabara ingawa zilikuwa si za lami lakini wakati tunachukuwa Uhuru barabara zote kubwa zilikuwa zikipitika misimu yote, si mvua si jua. Kulikuwa kuna PWD (Public Works Department) ikifanya kazi inavyotakiwa na mabarabara yote makuu yalikuwa na vituo vya TRM (Tanganyika Road Maintenance) hawa walikuwa wanahakikisha barabara zinapitika wakati wote
Sina nia ya kubadili au kutafuta mbinu za kuua mjadala makini wa Mkandara kwa kuendekeza chuki.
Ninajaribu kuweka kumbu kumbu sawa ili watu wasipotoshwe.
1. Tulipopata uhuru kulikuwa hakuna reli ya Dar es Salaam hadi Tanga nikimaanisha Kutoka Mnyuzi hadi Ruvu. Reli hiyo imejengwa baada ya uhuru. Ni upotoshaji wa hali ya juu kusema mkoloni aliiacha.
Wasafiri wa kutoka Tanga walikuwa wanasafiri kwa trni hadi Korogwe halafu wanachukua mabasi kupitia Handeni, Morogoro hadi Dar.
2. Hakukuwepo na bara bara ya Chalinze Segera, imejengwa baada ya Uhuru.
3. Hakukuwepo na Bara bara ya mkomazi hadi Same, ilikuwepo inayopitia Same, kisiwani, Gonja hadi Mkomazi.
4. Shirika la reli lilijulikana kama East African Railway Cop. shirika hili lilikufa mwaka 1977 baada ya jumuiya kufa.
Ndipo shirika la reli Tanzania lilipoanzishwa kwa kutumia mabehewa ya abiria na mizigo yaliyokuwa nchini.
Kama kuna mtu aliwahi kulalaia mashuka meupe basi ilikuwa EAR
Hatua ya dharura kukabaliana na kifo cha EAR ilikuwa kuagiza injini kutoka Bombardier Cananda zilizokuwa maarufu kwa jina la Mcanada. Halafu zikaagizwa injini kutoka India zilizokuwa zinafungwa mbili. Hizi zilikuja na mabehewa ya abairia
5. Kama zamani ya mashuka na vikombe ni ya 1977 nakubaliana, na nakumbuka kulikuwa na madaraja yote na lile la second sitting.
6. Huduma za kila siku kati ya Dar/Moshi/Tanga zilikufa mwaka 1997( around 1997-1980) na si kweli ilikufa kabla ya mwaka 1985.
7. Reli ya Arusha ipo, ya Chekereni hadi Voi ipo. Reli ya kati imefanya kazi kawaida matatizo yameanza tulipotoa zawadi kwa wahindi chini ya Jakaya Mrisho Kikwete.
Tuitafakari mada ya Mkandara na tuachane na tararira zinazotutoa katika mada tukiendekeza chuki za mtu au watu.