Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Nimejibu nilichoulizwa.

Mtoa mada kasema Watanzania ni masikini.

Nikamjibu kwamba siyo wote masikini. Mimi siyo moja wapo ya hao masikini anaowasema.

Kwani utajiri ni kuwa na mabilioni tu?
Kwani wewe ndio unayeitwa watanzania?.Watanzania ni utambulisho wa jumla na Mo na bahresa wako umo ndani.sasa sijajua kwanini unataka mtoa mada amwongelee mtu mmoja mmoja wakati iko wazi kua nchi hii ni moja ya nchi maskini duniani.Wewe mtu mmoja kuweza kukidhi mahitaji yako hakuiondoi nchi kutoka kwenye umaskini.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naomba nikuletee vijana kumi maskikini wa kitanzania angalau uwape ajira waweze kujipatia angalao uhakika wa mlo[emoji848]
Unakuta hata kuajiri watano tu hana uwezo huo. Mara nyingi masikini wengi ndio hao wanaojitutumua kujiona tajiri.
 
Ttzo ni vyama pinzani vya siasa visivyo imara ndo vinasababisha yote haya yatokee
Leo ukiitoa CCm madalakani utampa nchi nan
Chadema chama kina zaidi ya miaka 20 hakina ofisi hakina katiba, chama cha ukanda
TLP ni yale yale
CUF kila sku wanagombea vyeo
ACT bado wapya
NCCR chama ya mbatia na akijui kinataka nn nchi au CCM b
Tupiganie kujenga mifumo thabit ya nchi ili yoyote awe na uwezo wakuongoza.Hii kasumba yakuangalia watu na vyama kamwe haiwezi kutufikisha mahali.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kila binadamu amezaliwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake yaani hahitaji kufundishwa.

Fanyeni kazi tafuta hela acha kutegemea watu watakupa pesa
Sawa. Wanaendelea kutafuta hela,hilo halijaweza kumaliza tatizo la nchi yako na watu wake na wewe ukiwemo kuitwa masikini
 
Una rasilimali ila huna mtaji wana technolojia,1+1 sio mbili kila sehemu
 
Tatizo la nchi hii ni matumizi makubwa ya serikali, angalia kuanzia Rais mpaka wakuu wa idara, mishahara mikubwa, marupurupu, na mengine bado magari n.k
Hilo kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Imagine Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya nk. wote hao utakuta wanatumia zaidi ya gari moja kwa siku. Tena magari ya gharama kubwa ...... Wengine mpaka wanatumia magari ya serikali kupeleka watoto wao mashuleni. Tanzania nafikiri nchi inayoongoza kwa serikali kuwa na madereva wengi .....!!

Personally, huwa anangalia kampuni kama ya TANROAD au TRA hivi kweli hao Maofisa na Mainjinia hawawezi kujiendesha wenyewe. Yaani mtu kwenda lazima apelekwe na kurudishwa naa Driver .... Engineer mzima!!

Kuna watu wanaendeshwa na Madereva mpaka kwenye michepuko yao ..... Yaani ni kama vile serikali imebariki hayo ....Pathetic!!
 
Nchi nyingi za kiafrika ndivyo zilivyo, iangalia Kongo.
Tatizo ngozi nyeusi bado haijastaarabika. Yaani haijafikia katika hatua ya juu ya ubinadamu.

Hapo hata ichukue CHADEMA au CHAWATA hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
Ikichukuwa Chadema au cuf mabadiluko yanaweza kutokea endapo hakutakuwepo na vinyongo na malalamiko
Asikwambia mtu huku kukwama kwetu kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi nikutokana na baadhi ya Watanzania wenzetu kuweka vinyongo na chuki

Mf; suala la Elimu Bure limeleta mkanganyiko kwa walimu waliozoea kujipigia mapesa ya michango ya wananchi maskini, sasa Serikali iliposema Elimu Bure ikawaacha njia panda
Kwa hali kama hiyo usitegemee kama tutaondokana kwenye lindi la umaskini.
 
Hilo kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Imagine Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya nk. wote hao utakuta wanatumia zaidi ya gari moja kwa siku. Tena magari ya gharama kubwa ...... Wengine mpaka wanatumia magari ya serikali kupeleka watoto wao mashuleni. Tanzania nafikiri nchi inayoongoza kwa serikali kuwa na madereva wengi .....!!

Personally, huwa anangalia kampuni kama ya TANROAD au TRA hivi kweli hao Maofisa na Mainjinia hawawezi kujiendesha wenyewe. Yaani mtu kwenda lazima apelekwe na kurudishwa naa Driver .... Engineer mzima!!

Kuna watu wanaendeshwa na Madereva mpaka kwenye michepuko yao ..... Yaani ni kama vile serikali imebariki hayo ....Pathetic!!
Mkuu huko nikuharibu Ajira za watu
Sasa wakisema wajiendeshe wenyewe hao madereva watakula wapi
Huoni kama utaingeza umaskini?
Acha watanzania wenzako wajipatie kipato kupitia fani yao.
 
Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?

Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.

Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.

Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.

Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Waafrika kwa ujumla wetu tunahangaishwa na:-
1 - Ushirikina
2 - Wizi
3 - Uongo
4 - Uvivu
5 - Kutojiamini
6 - Uthubutu
 
Hilo kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Imagine Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya nk. wote hao utakuta wanatumia zaidi ya gari moja kwa siku. Tena magari ya gharama kubwa ...... Wengine mpaka wanatumia magari ya serikali kupeleka watoto wao mashuleni. Tanzania nafikiri nchi inayoongoza kwa serikali kuwa na madereva wengi .....!!

Personally, huwa anangalia kampuni kama ya TANROAD au TRA hivi kweli hao Maofisa na Mainjinia hawawezi kujiendesha wenyewe. Yaani mtu kwenda lazima apelekwe na kurudishwa naa Driver .... Engineer mzima!!

Kuna watu wanaendeshwa na Madereva mpaka kwenye michepuko yao ..... Yaani ni kama vile serikali imebariki hayo ....Pathetic!!
Shida ipo hapo na utitiri wa taasisi, angalia kuna TANROAD lakini hapo hapo kuna TARURA, kuna RUWASA lakini hapo hapo kuna mamlaka za maji yaani ni mambo ya hovyo sn
 
Mkuu huko nikuharibu Ajira za watu
Sasa wakisema wajiendeshe wenyewe hao madereva watakula wapi
Huoni kama utaingeza umaskini?
Acha watanzania wenzako wajipatie kipato kupitia fani yao.
Hakuna fani ya udereva ni matumizi mabaya ya fedha za umma, kwanini wasipewe kazi zingine hata kuwa Forman kwenye miradi ya serikali?
 
Kwani wewe ndio unayeitwa watanzania?.Watanzania ni utambulisho wa jumla na Mo na bahresa wako umo ndani.sasa sijajua kwanini unataka mtoa mada amwongelee mtu mmoja mmoja wakati iko wazi kua nchi hii ni moja ya nchi maskini duniani.Wewe mtu mmoja kuweza kukidhi mahitaji yako hakuiondoi nchi kutoka kwenye umaskini.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sawa
 
Kwa mtazamo wako wew ni masikani na Kama ni mbunge Basi nyie ndio chanzo Cha huu umasikini na ufukara uliopo. Elewa kwamba umasikini ni neno ambalo ni husianishi na vitu vingine. Usifikirie kuhusu hivyo vyakula, mavazi na malazi.

Fikiria mbali kuhusu Uhuru wa kifedha, kuigusa jamii inayokuzunguka, Uhuru wa kufikiri, kupatwa fursa za kuchangamana na jamii nyingine, kupatwa vitu vinavyokuondolea sonono, ushiriki wako kwenye kujenga taifa, nkz
Hatari
 
Back
Top Bottom