Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Masikini labda ni wewe.

Usitujumlishe wote.

Mimi ni Mtanzania na ni tajiri.

Tafadhali; usiniite masikini.
Unaelewa maana ha nchi maskini? Wanaposema nchi maskini haimaanishi kila mtu ni maskini, Bali walio wengi ni maskini.
Ni Kama wanavyosema nchi tajiri, haimaanishi kila mtu ni tajiri.
 
Wewe umefanya jitihada gani kujikwamua?

Bila kuwa na akili hata uwe unalala kwenye dhahabu utaishia kuwa maskini.
Kuna mbegu fake na madawa fake yamejaa, wakulima wamelalamika serikali kimya.
Mbolea, madawa bei juu, unalima serikali inakupangia bei na wakumuuzia.
Sheria za kulinda ajira zipo, lakini ona waajiriwa binafsi wanavyo nyanyaswa na kulipwa ujira mdogo.
Hio ni mfano michache ya jinsi watu wanavyo hangaika lakini siasa zetu hazipo katika kuboresha uchumi, zinalenga uchaguzi tu.
 
Wewe umeyaona mangapi? Vitu fake vimejaa China huko wanakonyonga sembuse Tzn?

Chanjo fake imekamatwa huko Uingereza na watu walichanja sembuse Tzn?

Hizo fake hazijaanza leo,tafuta hoja nyingine.
 
Wewe umeyaona mangapi? Vitu fake vimejaa China huko wanakonyonga sembuse Tzn?

Chanjo fake imekamatwa huko Uingereza na watu walichanja sembuse Tzn?

Hizo fake hazijaanza leo,tafuta hoja nyingine.
Hujajibu hoja, jibu hoha kwa mazingira ya Kitanzania, basi nasisi tukubali Ushoga maana UK upo.
 
Hujajibu hoja, jibu hoha kwa mazingira ya Kitanzania, basi nasisi tukubali Ushoga maana UK upo.
Kwani ushoga haupo? Serikali ijibu nini zaidi ya kufuatilia na kufanya majukumu yake ya kila siku?

Kwani kuna siku uhalifu umewahi kuisha? Na huo ni sehemu ya uhalifu.
 
Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?

Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.

Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.

Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.

Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Ukweli ni kwamba Nchi hii ina watu wengi wasiokuwa na Elimu.

Either hata kama Elimu iko kidogo lakini mfumo wetu hautusaidii.

Nadhani pia na IDEOLOGY yetu siyo sahihi.

WATU wanadhani ya kwamba RASILIMALI ni Madini tu.

Hapana.

Ardhi ni RASILIMALI.

Mifugo ni RASILIMALI.

Sasa Tizama aina ya kilimo tulicho nacho.

Duni.

Mifugo tuliyonayo-Duni

Yaani mfano MDOGO tu wa miezi miwili iliyopita tulikuwa na Vifo vya Mifugo kutokana na Ukame.

Lakini miaka zaidi ya 5 kulikuwa na Mvua iliyosababisha Malisho mengi sana.

Hakuna Mfugaji aliyejiwekea akiba ya Majani.

Hii yote inatokana na Ujinga.

Elimu ndogo.

Watu waliojiajiri kwenye Kilimo na Ufugaji ni wale wa kimila.

Hata Rais awe mzuri kiasi gani-Bila kuwa na watu wenye uwezo wa kutafsiri fursa bado ni tatizo.

Lakini pia Serikali nayo inalo la kufanya.

Kupeleka pesa nyingi kwenye kilimo cha kisasa na Ufugaji wa Kisasa.

Food Banking.

Intergrated SILOS.

Post Harvest losses control.

Grain deposit...Banking system/Model...Stakabadhi Ghalani...

Marketing ya bidhaa za kilimo hapa kwetu ni sawa na kuuza ndege walio juu ya mti...

Proper way ni kwanza kuanzisha intergrated SILOS...Grain Deposit in SILOS...then Serikali inatafuta masoko...ya bidhaa zilizoko Ghalani.

Mifugo-Iko wapi.
Nani anamiliki .
Iko mingapi.

Sasa tunapanga kwa takwimu.

Kwa hivo shida ni kwanza Elimu na au Mfumo wa Elimu.

RASILIMALI ya kwanza kabisa kukabiliana nayo ni RASILIMALI WATU.

WATU WAEREVUKE.

Tufundishwe mambo ya zamani mfano -Ardhi ni Mali...

Halafu tumaanishe.

Halafu iko wizara moja nadhani ingeundwa-

Wizara ya Afya ya Udongo.

Hii iko kwa nchi zikizoko serious katika FARMING...

UDONGO NDO MAMA YETU...

HAKUNA MTU ANAJALI AFYA YA UDONGO....

ELIMU
ELIMU
ELIMU.
 
Kama unampeleka kijana shule kutoka primary, secondary, advanced secondary yapata miaka 14, lakini kijana huyo hatokuwa na ujuzi wa aina yeyote unaohusiana na mazingira yake, kwamfano katoka kijijini kuna shamba, kuna mbuzi au ng'ombe lakini sisi hakuna tulicho mwelewesha juu ya kwenda kuyaendeleza mazingira yanayo mzunguka bali tumemfundisha logarithms na velocity formula ya ndege as if tunahitaji marubani tu, huku hata technologia ya kutengeneza ndege hatuna. ni kwa muujiza upi you expect kijana mwenye miaka ishilini hajapewa skill zozote ataweza kujikwamua kiuchumi?. Pili tumeruhusu aridhi kuhodhiwa na watu kiholela hata kama haiendelezwi lakini vijana wachache wenyebahati wakitaka aridhi waweze kufanya uthubutu imekuwa changamoto na hata wakifuata kwenyemaharimashauli rushwa imewekwa mbele na wakati vijana wetu wanamitaji labda hafifu. Ajira pekee sasa imekuwa bodaboda shughuli ambayo siyo ya uzalishaji. ni kwa namna gani taifa litaendelea?. Education reform and better land management that gives land access to our people its the only options we have for better tanzania
Mkuu umesahau Ajira nyingine ni Ulinzi na ndiyo kimbilio la vjana wengi ukiachilia Bodaboda na umachinga.
 
Sijajua, mleta mada anataka Serikali isikope - viongozi wajitolee kazini?

Dhana ya umaskini ametumia parameters zipi kuubaini?

(a). Mtanzania wa mwaka 1961 alipata huduma ya elimu kwa kutembea umbali mrefu, leo ipo?

(b). Mtanzania wa mwaka 1961 alitembea umbali mrefu kupata huduma za afya - leo ipo hivyo?

(c). Mtanzania wa mwaka 1961 alisafiri wiki mbili KM 1500 toka Kigoma - Dar, - leo ipo? Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa akina Prof Lipumba kwenye jukwaa walishutumu Serikali ya CCM kuhusu Miundombinu ya barabara kuwa ya vumbi - leo wanaweza?

Dhana ya umaskini ni pana na Serikali ya CCM imejitahidi kujenga Miundombinu ili ichoche juhudi za watu kujikwamua. Lkn pia kukopa si jambo baya labda kama kuna shida ktk matumizi ya mikopo hiyo.
Sawa Leo hii anatembea umbali mdogo ila Elimu anayoipata inamashiko au anapewa huduma Bora ya Afya wameongeza mashule na mahospitali lakini watendaji ktk secta hizo na zero.
 
Sawa Leo hii anatembea umbali mdogo ila Elimu anayoipata inamashiko au anapewa huduma Bora ya Afya wameongeza mashule na mahospitali lakini watendaji ktk secta hizo na zero.
Serikali imejenga mazingira mazuri ya kukua kwa sekta binafsi - haiwezi kutokea wahitimu wote wakapata kazi - himizeni vijina kuitumia kutumia fursa zilizopo kujiajiri "kamwe acheni kuwakatisha tamaa".
 
Masikini labda ni wewe.

Usitujumlishe wote.

Mimi ni Mtanzania na ni tajiri.

Tafadhali; usiniite masikini.
Una utajiri gani wakati asilimia 50 ya wananchi wakiwa na vipato chini ya dola 1 kwa siku?Tajiri usiye na msaada katika HAKI za wengi ni maskini kama wengine.
 
Una utajiri gani wakati asilimia 50 ya wananchi wakiwa na vipato chini ya dola 1 kwa siku?Tajiri usiye na msaada katika HAKI za wengi ni maskini kama wengine.
Dola moja inakisiwa kuwa = na Tshs 2,500..

Mimi kwa wastani kipato changu ni zaidi ya dola 1/ Tshs 2,500.

Kwa hiyo mimi siyo masikini.
 
Uongozi bora kwa maendeleo, ukipigwa katika uongozi umepigwa katika maendeleo. Fuatilia historia yetu, utaona kuna awamu fulani za uongozi zilileta mabadiliko makubwa sana katika maendeleo ya taifa hili tofauti na awamu zingine.
 
Dola moja inakisiwa kuwa = na Tshs 2,500..

Mimi kwa wastani kipato changu ni zaidi ya dola 1/ Tshs 2,500.

Kwa hiyo mimi siyo masikini.
Tunajivunia mali na ufahari badala ya UTU na tumeridhika.Raslimali asilia zilizopo nchini mwetu zingetumika ipasavyo kusingekuwa na mwananchi wa kuishi kwa kipato cha chini ya US$ 1.Tumeongozwa/kutawaliwa na watu wabinafsi kwa miaka zaidi ya 60 ya UHURU bila maendeleo ya watu.
Tuache kupotoshana kuwa Tanzania ni nchi ya kuombaomba misaada/mikopo huku tukichekelea kama mazuzu na kuwasifia/kuwatukuza watawala.
 
Tafuta ugali wako. Serikali ipo kazini
 
Tafuta ugali wako. Serikali ipo kazini
Ugali haujawahi kuwa miongoni mwa changamoto yangu.Ninapigania HAKI na UTU kwa binadamu wote.
Kuhusu serikali kufanya kazi ndicho tunachopigania.Tunataka Katiba mpya ili nchi isonge mbele kwa sababu katiba tuliyonayo imeshindwa kujisimamia na siyo shirikishi.
 
Back
Top Bottom