Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?
Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.
Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.
Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.
Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Ukweli ni kwamba Nchi hii ina watu wengi wasiokuwa na Elimu.
Either hata kama Elimu iko kidogo lakini mfumo wetu hautusaidii.
Nadhani pia na IDEOLOGY yetu siyo sahihi.
WATU wanadhani ya kwamba RASILIMALI ni Madini tu.
Hapana.
Ardhi ni RASILIMALI.
Mifugo ni RASILIMALI.
Sasa Tizama aina ya kilimo tulicho nacho.
Duni.
Mifugo tuliyonayo-Duni
Yaani mfano MDOGO tu wa miezi miwili iliyopita tulikuwa na Vifo vya Mifugo kutokana na Ukame.
Lakini miaka zaidi ya 5 kulikuwa na Mvua iliyosababisha Malisho mengi sana.
Hakuna Mfugaji aliyejiwekea akiba ya Majani.
Hii yote inatokana na Ujinga.
Elimu ndogo.
Watu waliojiajiri kwenye Kilimo na Ufugaji ni wale wa kimila.
Hata Rais awe mzuri kiasi gani-Bila kuwa na watu wenye uwezo wa kutafsiri fursa bado ni tatizo.
Lakini pia Serikali nayo inalo la kufanya.
Kupeleka pesa nyingi kwenye kilimo cha kisasa na Ufugaji wa Kisasa.
Food Banking.
Intergrated SILOS.
Post Harvest losses control.
Grain deposit...Banking system/Model...Stakabadhi Ghalani...
Marketing ya bidhaa za kilimo hapa kwetu ni sawa na kuuza ndege walio juu ya mti...
Proper way ni kwanza kuanzisha intergrated SILOS...Grain Deposit in SILOS...then Serikali inatafuta masoko...ya bidhaa zilizoko Ghalani.
Mifugo-Iko wapi.
Nani anamiliki .
Iko mingapi.
Sasa tunapanga kwa takwimu.
Kwa hivo shida ni kwanza Elimu na au Mfumo wa Elimu.
RASILIMALI ya kwanza kabisa kukabiliana nayo ni RASILIMALI WATU.
WATU WAEREVUKE.
Tufundishwe mambo ya zamani mfano -Ardhi ni Mali...
Halafu tumaanishe.
Halafu iko wizara moja nadhani ingeundwa-
Wizara ya Afya ya Udongo.
Hii iko kwa nchi zikizoko serious katika FARMING...
UDONGO NDO MAMA YETU...
HAKUNA MTU ANAJALI AFYA YA UDONGO....
ELIMU
ELIMU
ELIMU.