Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mkandara,

Mkuu umetuuliza swali muhimu sana, na nilikua naifutalia hii mada hila hawa jamaa nao saa zingine mambo yao ya kuchanganya habari yanachosha that is (Mods) kidogo nisiielewe kwani kuna watu walikuja na maelezo mazuri sana especially member mwenye jina la sijui nini tena alafu mwishowe kuna 'dude', sasa tena wameenda kuchanganya maswali yako na nakala ya 2007 hawa nao sometimes mambo yao kha!!.

Hila bado sijaona watu kukuelewa vizuri kwani ni wachache so far waliokupata ya kwamba sisi ni maskini its a fact na si hadithi, the sooner we realize that the better. Na tuache hizi hisia za kwamba tuna sijui mariasili nyingi hivyo sisi si maskini, ni sawa na mtu ambae anasubiri urithi wa mamilioni lakini mlo wa siku unampa tabu hivyo kwa situation yake ni fukara mpaka apo atakapo shika hiyo hela mkononi ndio unaweza sema vinginevyo.

Hivyo licha ya maliasili sisi ni maskini, again labda sio wachangiaji wa humu ndani walioko tanzania na kwengineo hila proportion kubwa ya watanzania ni maskini wengi ni maskini.

Amini usiamini umaskini ni tabia rather than the belief 'ndivyo tulivyo' ni fikra kama hizi ndio tunakubali situation kama hizi za umaskini.

Tuna matatizo matatu makubwa yanayo tuletea umaskini tanzania watanzania wenyewe kujitakia (kwa kujua au kutojua matendo yao) na muongozo (tabia za washika madaraka sehemu zote) na sheria zisizo fanya kazi yake. Yaani hivi ni vyanzo ambavyo inabidi tuvitatue kabla hata atujachunguza uchumi kwani bila ya kutatua haya matatizo matatu ni kama tuna cheza mduara tu.

Watanzania, wengi hawajajua kuchukua personal responsibility na maisha yao hivyo kujitia kwenye mashimo makumbwa ya matatizo na choices ambazo wanazi-make on their daily lives. Mfano wa mtu ambae ana kipato kidogo lakini sijui watoto sita nyumbani na bado wengine wa nyumba ndogo hivyo ni kuongeza idadi ya watanzania watakao kuwa maskini mpaka hao vijana waanze kujitegemea ikiwa wata muiga baba sijui mimi ni mtoto wakiume warudie matendo yale yale picha umeipata.

Kitu kingine bado wengi wetu atujajua kwamba tuna majukumu na maisha yetu hivyo choice tunazochagua au maisha tunayo taka saa zingine ni kuleta matatizo, watu wanaishi kama vile amna kesho leo mi ni siku ya mshahara wacha nikajilushe katikati ya mwezi njaa upya, leo mi nimepika sufuria chafu wacha nimwage hiki kiporo kwenye mfereji, na taka zingine za nyumbani kesho kipindu pindu kwa watoto wao, leo mi sina kitu wacha nikope, kulipa shughuli kesho umepoteza mtu ambae alikua anakunyanyua unapo kwama. Hii inaonyesha ni jinsi gani hawa watu wanavyoishi in ignorance sasa watu wa dizaini hizi hata ukiwajengea cha maana uishia kuburunda kwa kuwa wanamaisha yao ni ya leo. Nii ignorance ya kutowajibika ndio maana ata hawaelewi ni nani ana responsibility ya kusaidia kuinua maisha yao hili waweze jisaidia. Ndio maana wakipelekewa pilau na mtu ambae ana responsibility ya kusimamia maslahi yao na ni fisadi tunaemsema hapa kila siku wao watampa kura kisa pilau na mengine hawaya jui tena. Sasa embu chunguza na mifano mingine ya leo hawa jamaa wanavyoishi utajua kuwa ni kazi kweli kweli kuwasaidia hawa watu na kuwaelezea msimpe kura mtu kama Lowassa.

Pili viongozi wetu hii sii itaji kukwambia unajua ni watu wa dizaini zipi ndio wenye madaraka Tanzania na jinsi wanavyo yatumia hayo madaraka. Lakini hii ni reflection ya watanzania wenyewe tumia nafasi yako kujiboresha ni maisha ya leo na mwishoe kuishia kuua na hiyo miundombinu, sijui biashara au kuwa na secta mbovu ya uzalishaji again hii ni ile ile ignorance ya kuishi kwa leo na kutokua na mipango ya kesho.

Mwisho ni sheria zetu ambazo kwa kweli aziwahusu wakubwa wetu kwenye jamii na ni watu ambao wengi wako kwenye tatizo la pili. Sasa kama tunachagua watu, kutusaidia alafu awawajibiki na isitoshe mali zenyewe wanatia mfukoni utapata maendeleo gani hapo? isitoshe vyombo vyenyewe vyasheria vina utaratibu huo huo kutowajibika na inafika mpaka mkuu wa polisi kuwa jambazi tutaenda wapi. Hivyo hata kama upendi kinachoendelea kusema utaogopa kwani sheria inayo kulinda aiko side yako utaishia kuambiwa si mtanzania upelekwe rumande kuna namna hapo vinginevyo wote humu tungekuja na majina yetu ya kweli na kuomba ukombozi wetu na si kujiita sijui nani wala na nani.

Sasa bado atuja chambua sababu za uchumi wetu kwanini mmbovu, kwa nini madaktari wetu ni hovyo na sababu zingine nyingi ambazo tunazijua ni tatizo la taifa na itakuwa point less kwenda huko iwapo bado tunaishi kwenye disfunctional society first things first.

ps. pole na msiba wenu
 
Mkuu Zakumi Tanzania is very rich, it has never been poor. Perhaps, its people. Kuna propaganda kuwa Tanzania ni nchi masikini ili masikini (watawala wa Tanzania na mabwana/wake?? zao wa Ulaya na marekani) waweze kupora vizuri utajiri na kuwa matajiri ili mwisho wa siku Tanzania iwe masikini kweli. Na ndo safari imeanza kwa kuachiwa mashimo na sumu za kuchimbia madini
Mkuu hebu fikiria tukiahamishwa hapa wakaletwa Wachina au Wamalay kutatokea nini? Almasi kule, dhahabu hapa, uranium bwerere, maji usiseme, milima na mabonde ndio hayo ngedere kibao Serengeti jamani roho za kimasikini na uvivu wa kufikiri wa viongozi wa Tanzania jumlisha na ujinga wa Watanzania ndio tatizo. Hebu tuache ujinga kwanza

Mwalimu Zawadi:

Ukisoma posti ya Juma Contena, nadhani majibu utayapata. Lakini kwa kuongezea naona watanzania wengi tunashindwa kutofautisha kati ya potential na ability (au talent).

Kwa mfano, Kenya ina wakimbiaji wazuri na wengi wao wanatoka kwenye maeneo yanayofanana na sehemu Tanzania. Hivyo Tanzania nayo ina uwezo wa kutoa wakimbiaji kama Kenya.

Tofauti iliyopo hapa ni kuwa Kenya imeweza ku-transform potentials waliyo nayo kuwa kwenye talents au abilities za kukimbia kwenye mashindano. Kwa upande mwingine, Tanzania haijafanya transformation yoyote ya maana.

Maliasili zote ulizotaja hapo juu, zisikudanganye sana. Kwanza zilikuwepo kabla jamii nyingi hazijaamia maeneo yanayoitwa Tanzania. Hivyo hata Tembo wanaweza kudai kuwa ni mali yao.
 
Acheni longolongo...jengeni majengo kama ya New York, daraja kama la San Fran, maabara kama za Los Alamos, tengenezeni ndege zenu wenyewe, tengenezeni ma bullet train yenu wenyewe...achaneni na magari moshi ya mwaka 1919.

Acheni longolongo fanyeni kweli!!
 
Kimbo Slice?.....oh oh oh.....Kevin Ferguson?......oh oh.....Tea Party?.....oh oh...."YOU LIE"..........

kweli kabisa.......sisi ni maskini kwa sababu ni wavivu sana ktk kila kitu........duuh!!
 
Kimbo Slice?.....oh oh oh.....Kevin Ferguson?......oh oh.....Tea Party?.....oh oh...."YOU LIE"..........

kweli kabisa.......sisi ni maskini kwa sababu ni wavivu sana ktk kila kitu........duuh!!

Wewe unaangalia Spike Tv nini? Lol...

Kimbo is ma man...
 
Acheni longolongo...jengeni majengo kama ya New York, daraja kama la San Fran, maabara kama za Los Alamos, tengenezeni ndege zenu wenyewe, tengenezeni ma bullet train yenu wenyewe...achaneni na magari moshi ya mwaka 1919.

Acheni longolongo fanyeni kweli!!

Kwani wewe huhusiki?
 
Kwa hiyo ni Wazungu (weupe) Wamarekani wenye asili ya ulaya wanaoishi kwenye "nyumba za udongo" huko kusini mwa Miami, FL?

Sijaongelea nyumba za udongo wala wajipsi. Umaskini ndio nimeuona Ulaya na Marekani. Ila nadhani unataka nijibu kuwa wanaishi hawa ili ufurahi:

obama-witchdoctor-muck.jpg


Obama+Witchdoctor+1.jpg


Source: http://swahilitime.blogspot.com/2009/09/rais-obama-anavyotukanwa-hapa-marekani.html
 
Mkandara jibu la Samir Amin hili hapa - zingatia zaidi hapo kwenye wino mwekundu:

When we think of the historical limitations of nationalist populism and Soviet socialism we realise that in the two cases where we have a vision of capitalism without capitalists, the target is to reproduce a society which is very close to the reality of a capitalist society with a view to 'catching up' or reducing the historical gap which is a result of imperialism and unequal development till it is reduced to the point of the countries becoming equal partners; and a qualitative change in the power structure and the economic system to having normal capitalism with capitalists. And if it is normal capitalism, we in Africa are bound to be more mediocre, because for historical reasons, the West and particularly Europe has maintained us in the old role of the periphery. We are still producing raw materials, agricultural and mineral, and not moving into industrialisation at the very time when parts of Asia ,either through Communist leadership or through bourgeois leadership (India and South East Asia), and with different historical reasons Latin America, are moving into industrialisation more or less successfully - in terms of the capacity to be competitive."
 
Sijaongelea nyumba za udongo wala wajipsi. Umaskini ndio nimeuona Ulaya na Marekani. Ila nadhani unataka nijibu kuwa wanaishi hawa ili ufurahi:

obama-witchdoctor-muck.jpg


Obama+Witchdoctor+1.jpg


Source: http://swahilitime.blogspot.com/2009/09/rais-obama-anavyotukanwa-hapa-marekani.html

Angalau maskini wa wenzetu wana afya!! Kuna welfare, social security disability, kuna ma food bank, kuna ma homeless shelters..yaani majuu kama ukilosti basi tatizo kubwa ni wewe mwenyewe. Kama mimi Julius, msukuma kutoka Ntuzu nime make it sielewi kwa nini wazawa wa hapa wasi make it na wao!!!
 
Kwa sababu watu wake wana roho za kimaskini
hamna roho ya kimasikini
ila sababu ni kwasababu kuna viongozi wanaotaka kujitosheleza kwanza ndio wageukie maslahi ya nchi kitu ambacho ni kigumu kwa sababu binadamu huwa hardhiki akipata 100,000 atatamani 1,000,000 akipata hiyo atatamani zaidi na zaidi. Tatizo ni uongozi huo mbovu na kutumia mamlaka ya nchi katika kuwakandamiza wananchi wa kawaid kwa mfano uko Loliondo na kwingineko kwingi
 
Zakumi,
Mkuu nimeipokea point yako kuhusu wakimbiaji wa Kenya, nakubaliana nawe sana tu na hakika ni tofauti kama hizi ktk nyanja mbali mbali ndio zinaweza kuchagia tofauti ya hizi. Nachukulia kama huu ni mfano mmoja tu na bila shaka ipo mingi sana ambayo kama sii Kenya basi kuna nchi nyingine wanafanya tofauti nasi..mfano mwingine, Botswana miaka yote wana safirisha nyama ya ng'ombe kuliko sisi Tanzania, wakati Tanzania tuna ng'ombe na wanyama wanaoliwa kuliko Botswana. Somalia inasafirisha ndizi na nyama ya mbuzi kuliko Tanzania hali sisi tuna ardhi yenye rutuba ya ndizi kuliko Somalia.. Hii ni mifano ya karibu tu na ipo nyingi sana ukienda nje ya bara letu..
Utajiri wetu ni wa kuchora, ni utajiri uioweza kumnufaisha Mtanzania kama dhahabu tunazovaa. Wamasai ni matajiri wa mifugo lakini kama Kabila sidhani kama utajiri huo una tofauti na huu tunaozungumzia hapa.. Utajiri usokuwa na manufaa, tena afadhali wao Masai wanapenda kuendelea culture yao ya utajiri ni ng'ombe si fedha..lakini sisi Bongo tunataka kuwa kama Ulaya tuishi kama wazungu lakini picha haziendi tukiwa na mali chabwa ardhini..
Na pengine kwa kumjibu Julius bila shaka nchi zote maskini (Third world) zinashindwa kutumia vipaji kama hivi ktk kujiendeleza wao wenyewe. Hao Kenya pamoija na kwamba wanao wakimbiaji wazuri lakini pia inashindwa katika mambo mengine.


Campanero,
Mkuu nakusikia sana na hilo la nchi tajiri na huu mfumo wa ukoloni mamboleo.... lakini iweje ukoloni mamboleo umeweza kuzifaidisha baadhi ya nchi nyingine kama vile Maleysia, Vietnam, Botswana, Dubai, na nchi zote za Kiarabu ambazo up to 1970s walikuwa maskini.. Tena basi nasikia hata Ghana inatutoka taratibu...na kibaya zaidi leo hii nchi kama Ethiopia na hata Rwanda wamesimama juu yetu..yaani sisi maskini kuliko hata Rwanda (per capita)..wakati wao pia wanalia na ukoloni mamboleo.
Hivi kweli unaamini tukiingia ktk dunia ya utengenezaji (industrialize) tutaweza kushindana ikiwa hali ya maisha ni kubwa kiasi kwamba hatuwezi kuwa na cheap labor ktk soko la ajira duniani! Je, does it worth kutengeneza malia mabao gharama yake ni kubwa kuitengeneza nchini kuliko kuisafirisha ikatengenezewe India na China! - Nani Tanzania anaweza kuishi kwa senti 30 hadi 50 kwa saa ya kazi?

Juma Contana,
Watanzania, wengi hawajajua kuchukua personal responsibility na maisha yao hivyo kujitia kwenye mashimo makumbwa ya matatizo na choices ambazo wanazi-make on their daily lives. Mfano wa mtu ambae ana kipato kidogo lakini sijui watoto sita nyumbani na bado wengine wa nyumba ndogo hivyo ni kuongeza idadi ya watanzania watakao kuwa maskini mpaka hao vijana waanze kujitegemea ikiwa wata muiga baba sijui mimi ni mtoto wakiume warudie matendo yale yale picha umeipata.

Mkuu shukran sana kwa kunisoma kwani sii kazi ndogo kupata jibu la hili swali ambalo binafsi mwanzoi nilifikiria kuwa rahisi sana. Lakini baada ya kukaa na kujiuliza kwa muda nimekuta majibu mengi sana yanayonichukua kufikira mahala ninataka kukubali kwamba pengine kweli sisi tumepigwa laana. Hivyo kunipa picha ya kutojali hata uchaguzi ndani ya nchi wala mapendekezo ya kiongozi yeyote.. Hivyo hata hao waliotoka nje ya hoja yangu nadhani bado wanawakilisha ujumbe usiokuwa popular masikioni mwetu.. but still kuna uwezekano ndani ya maelezo yao..Tusipokubali laana na imani hii ya Kibaniani, haina maana kwamba hakuna uwezekano huo pia..

Pamoja na majibu yako umezungumzia Watanzania wengi hawajajua kuchukua personal responsibility na maisha yao na ukatoa mfano wa mtu mwenye kipato kidogo lakini ana watoto kibao kuwa sababu mojawapo.. Hii kidogo imenikalia kinyume kidogo kwa sababu nchi tajiri zote zina population kubwa sana kuliko sisi..Ukitazama Ulaya yote karibu kila nchi inahesabu kubwa ya watu kuliko sisi, sasa uzazi wao ulianza vipi hadi wao wakafikia hesabu kubwa kiasi hicho na bado wakawa matajiri..Bila shaka hapa tutapata jibu la kwamba wao hawakuwa na mfanyakazi aliyeishi kwa pato dogo kuliko maisha..
Unajua kwamba nchi zote maskini ikiwa ni pamoja na sisi Tanzania wananchi wake wafanyakazi hulipwa mshahara chini ya kiwango cha maisha!. Inashangaza sana kuona mfanyakazi serikalini au kiwandani akilipwa mshahara wa Tsh, 100,000 wakati fedha hiyo haitoshi hata kwa kodi ya nyumba acha mbali chakula, usafiri na kadhalika. Leo hii Watanzania wanapokea mshahara mdogo kuliko wakati wa mkoloni yaani ndani ya Uhuru wanatumika kwa malipo ya UTUMWA..

Ni katika mtazamo huu narudi tena kwa Companero ambaye amehoji zaidi mfumo wetu wa kuendeleza biahsra ya utumwa ktk kuzalisha malighafi badala ya sisi kuingia ktk Utegenezaji (industrial) kwani kufanikiwa kwa nchi kama India, China Vietnam, Maleysia ktk mifumo tofauti ya kiuongozi wameweza kufanikiwa tu kwa sababu wameweza kuiweka hali ya maisha kuwa chini.. Cost of living katika nchi hizo imebakia chini kiasi kwamba hata mfanyakazi wa kiwanda cha nguo kwa senti 50 ameweza kuishi kwa fedha hiyo mwezi mzima na wengine hata kutuma fedha kwa wazazi wao huko vijijini. Kifupi ukienda nchi hizo iwe Indioa au China utaweza kuona tofauti ya masiha kati ya mfanyakazi na asiyekuwa na kazi.

Narudi palepale ktk hoja ya Kichuguu,, Je, hii inatokana na roho mbaya! roho mbaya ya viongozi wetu na pengine dhulma ya jasho la wananchi kwa kuwafanya watumwa ndani ya Uhuru wanaojivunia!.. Iweje sisi Watanzania tujivunie Uhuru wetu wakati wananchi wake zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wanalipwa mshahara chini ya kiwango cha maisha, halafu serikali hiyo hiyo inatuambia inflation ipo chini ya aslimia 10. Hata tukifanya hesabu za haraka haraka iwe mji ndogo Tanzania nina hakika kabisa gharama ya maisha ni zaidi ya 300,000 kwa mwezi. lakini ni wafanyakazi wangapi wanapokea kiwango hicho! ikiwa zaidi ya robo tatu ya wafanyakazi nchini wanaishio mijini!.
Je, tuna sababu gani ya kulaani mfumo wa ukoloni mamboleo ikiwa sisi wenyewe tuna practice UTUMWA right in our backyard,...kuwafanya wananchi Watumwa ndani ya Uhuru wao na inakubalika kikatiba!..
 
Last edited:
Mkandara wao wana nationalism (utaifa) na patriotism (uzalendo) ila sisi tuna utaifa bila uzalendo!

Nationalism without Patriotism is dead!
 
Angalau maskini wa wenzetu wana afya!! Kuna welfare, social security disability, kuna ma food bank, kuna ma homeless shelters..yaani majuu kama ukilosti basi tatizo kubwa ni wewe mwenyewe. Kama mimi Julius, msukuma kutoka Ntuzu nime make it sielewi kwa nini wazawa wa hapa wasi make it na wao!!!

Hata Nduguyo Mzee wa Vijisenti ni Msukuma kutoka Ntuzu na ame-make it na alipokuwa Harvard alishangaa kwa nini wazawa wa huko hawa-make it!
 
Hata Nduguyo Mzee wa Vijisenti ni Msukuma kutoka Ntuzu na ame-make it na alipokuwa Harvard alishangaa kwa nini wazawa wa huko hawa-make it!

Ame make it kwa kuiba. Huyo ni mwizi. Mimi riziki yangu ni halali and I live a good life and if living it up was a crime I'd be in maximum security prison serving 25yrs to life...
 
Huyo Membe hajui chochote kuhusu mambo ya madini,ndo maana anongea ujinga huo.
Watanzania wenye ujuzi na mambo ya madini tupo kibao na ukitaka kuelewa hilo nenda GGM,Buzwagi,Tulawaka,Bulyanhulu,Mwadui,Nyamongo na Kiwira.Sehemu zote hizo wamejaa wabongo na ndo wanaendesha shughuli zote,hao wazungu mnaowaona hamna wanachofanya zaidi ya kukaa mtandaoni kuangalia ngono afu mwisho wa mwezi analipwa milioni 20!
 
Acheni kusingizia watu tatizo ni sisi wenyewe hatujakubali kutokana na umasikini.
Wewe nenda ktk karibu vijiji vyote uwe Tajiri wa nguvu, watakusema hao tena balaa na mwisho watakuja kama majambazi wakutwange risasi.

Cha maajabu hawa majambazi hawatachukua kitu baada ya kukutwanga risasi.
Mtamsingizia bure mzee wa vijisenti
 
Mkandara wao wana nationalism (utaifa) na patriotism (uzalendo) ila sisi tuna utaifa bila uzalendo!

Nationalism without Patriotism is dead!
Mkuu nakubaliana nawe ktk hili saaana tu.... lakini huu Utaifa na Patroitsm waliokuwa nao wenzetu umekuja vipi?
Ni elimu au kitu gani kinatakiwa maanake binafsi naona roho mbaya ya Wadanganyika kuchukua nafasi kubwa sana..Mathlan, sidhani kama mimi naweza kuwa na Utaifa na Uzalendo na Tanzania ikiwa nchi yangu yenyewe inapinga uraia wangu, Leo hii mimi sijui kama ni Mtanzania au laa. Nchi tumegawanyika ktk mafungu ya Wabara, Wazanzibar, Wazanzibara, Wabarazainji..na sisi wengine tunaitwa Wakimbizi...Kisha kuna kundi jingine linakuja la Waislaam na wakristu...imefikia mahala kila mmoja wetu ana kundi fulani ambalo Utaifa na Uzalendo wake unahitajika zaidi ya jina la nchi..
Kuna vitu kama Ufisadi, sisi soote tuna LAANI Ufisadi lakini tunashindwa kuwawajibisha Mafisadi...Tena tunawasifia na kuwatunza kiasi kwamba kuwa nao ndio Utaifa na Uzalendo..Accountability ni zero! na Excuse za viongozi wetu hasa wanatumia maneno ya Yesu, kwamba mwenye kuona makosa awe wa kwanza kurusha jiwe pasipo kuelewa maana na hekima ya aya ile ya Yesu. I mean hivi kweli unaweza kuamini JK anamfagilia Lowassa tena mwezi wa Ramadhan, haogopi hata Mungu wake kuongopa mwezi huu mtukufu kwa sababu ya kumbeba mshikaji akitumia ati kama unao ushahidi tuletee!.. ushahidi gani hali kapewa lakini hataki kuamini, kapewa ushahidi mwingine na marehemu Chifupa kautupa kapuni.

Hivi kweli usipokuwa pamoja na utawala wa kifisadi tuseme leo hii CCM ilivyo, ukakataa kuwaunga mkono Jk, Lowassa, Rostam utachukuliwa kweli wewe ni unasukumwa na Utaifa na Uzalendo au Utaifa na Uzalendo ni kuwakubali na kuwatumikia viongozi walipo madarakani!.
 
Ame make it kwa kuiba. Huyo ni mwizi. Mimi riziki yangu ni halali and I live a good life and if living it up was a crime I'd be in maximum security prison serving 25yrs to life...
Duh! lakini wewe sii mweusi kama mimi au Companero au?.. imekuwaje uwe tofauti na Miafrika yooote tupe siri yako mkuu.
 
Back
Top Bottom