Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Ame make it kwa kuiba. Huyo ni mwizi. Mimi riziki yangu ni halali and I live a good life and if living it up was a crime I'd be in maximum security prison serving 25yrs to life...

Mbona huyo Mnyantuzu mwenzako hayuko maximum security prison?
 
Duh! lakini wewe sii mweusi kama mimi au Companero au?.. imekuwaje uwe tofauti na Miafrika yooote tupe siri yako mkuu.

Wewe uko T-Dot (kwa mizungu) na mimi niko (GA) kwa mizungu. Ninachosema ni kwamba, mimi siyo maskini wala fukara. Nina uhakika na mlo wangu, malazi yangu, na vijimambo vingine vidogo vidogo na kwa kweli nimeridhika na hali yangu.

Hata ningekuwa Tanzania nisingekufa njaa. Nisingekosa pa kulala. Walau ningejibanza kwenye kijumba changu cha udongo. Nina akili timamu na naiamini sana akili yangu kuniwezesha kupata angalau yale mahitaji muhimu.

Akili ya kujenga maroketi hiyo sina. Niko kama Miafrika mingine kama wewe na LiCompanero....ninaota tu na kupiga soga
 
Mbona huyo Mnyantuzu mwenzako hayuko maximum security prison?

Hiyo reference ya maximum security prison kuhusu mimi ni sarakasi ya lugha tu niliyokuwa nacheza nikimaanisha kama kuishi maisha mazuri ingekuwa kinyume na sheria basi mimi nigekuwa kwenye hilo gereza la ulinzi wa hali ya juu zamani tu kwa sababu siishi maisha mabaya. I love my life.

Sasa hilo Linyantuzu lenzangu haliko maximum security prison kwa sababu limevunja sheria kwenye jamii ya Miafrika. Lingekuwa huku majuu lingekuwa linanyea debe tu saa hizi. Umemsahau fisadi Maddoff au Ken Lay?
 
Julius,
Akili ya kujenga maroketi hiyo sina. Niko kama Miafrika mingine kama wewe na LiCompanero....ninaota tu na kupiga soga
Nakusoma mkuu wangu, sasa tunarudi ktk swali langu la awali, Kwa nini Tanzania ni nchi maskini ikiwa wewe (kati ya Miafrika) upo GA mambo mswano, unaendesha maisha yako vizuri tu na hesabu kubwa ya watu waishio Marekani. Hali hiyo haipo Tanzania hesabu kubwa ya wananchi wanaishi maisha duni kabisa ingawa wao wanaweza sema ndio standard yetu kuridhika na Umaskini. lakini haiondoi ukweli kwamba maisha mazuri hayana standard kwa mipaka, ati wabongo hawatakiwi kuwa na maisha mazuri kama ya Marekani.
Mimi nataka kujua ni sababu gani?.. Je Miafrika Ndivyo Tulivyo inatokana na kutokuwa na ujuzi wa kujenga maroketi?. Na iweje sisi tuwe nchi hizi tuweze kufanikiwa zaidi na kufanya kazi kwa juhudi kuliko tunapokuwa Bongo.. watu wale wale (Miafrika) ambao hawakusoma na wavivu..Je kuna ukweli kuhusu kujenga miroketi kuwa sababu?.. mbona North Korea, Pakistan waya ni ule ule kama Bongo.. Nini hasa sababu ya umaskini wetu tukiachana na hao wengine kwani binafsi naamini kwa kutambua WATU na MAZINGIRA jibu lazima liwe within..
 
Mimi nataka kujua ni sababu gani?.. Je Miafrika Ndivyo Tulivyo inatokana na kutokuwa na ujuzi wa kujenga maroketi?

Naam! Ni Ndivyo Tulivyo. Hata tukikataa hadi makaburini, kukataa kwetu hakubadilishi ukweli.

Na iweje sisi tuwe nchi hizi tuweze kufanikiwa zaidi na kufanya kazi kwa juhudi kuliko tunapokuwa Bongo

Jibu mbona rahisi sana Bob. Tayari umeshasema tuko huku kwa Mizungu which means idadi kubwa ya vitu vinamilikiwa na kuendeshwa na Mizungu. Hata hapo T-Dot sehemu nyingi za wazungu zina vitu ns mazingira bora kuliko kwa weusi. Marekani vivyo hivyo. School districts kwa mfano, zinazoendeshwa na weusi ndio hushika mkia katika kila kitu.

mbona North Korea, Pakistan waya ni ule ule kama Bongo.. Nini hasa sababu ya umaskini wetu tukiachana na hao wengine kwani binafsi naamini kwa kutambua WATU na MAZINGIRA jibu lazima liwe within..

North Korea na Pakistan hao si wenzetu bana. Rumba lao kali kiaina lakini sio kali kama la Afrika!!
 
Julius,
Jibu mbona rahisi sana Bob. Tayari umeshasema tuko huku kwa Mizungu which means idadi kubwa ya vitu vinamilikiwa na kuendeshwa na Mizungu. Hata hapo T-Dot sehemu nyingi za wazungu zina vitu ns mazingira bora kuliko kwa weusi. Marekani vivyo hivyo. School districts kwa mfano, zinazoendeshwa na weusi ndio hushika mkia katika kila kitu.
T.Dot hakuna sehemu wala mazingira ya weusi watupu. Hakuna vibanda wala kina Tyron kukaa nje vifua wazi mtaani!
Mkuu hapa kidogo nashindwa kukubaliana nawe.. Mtoto wangu kaingia nchini majuzi tu toka Bongo na kila siku anashika nafasi ya kwanza darasa zima wamejaa mizungu tena sii ya kuapiza...
Huko Bongo hakuwa wa kwanza kila mara na hakuonekana genius... Hii imekuwaje maanake karushwa darasa sasa..
 
Bob, siyo kwamba wazungu wote ni vipanga. Hapana ndugu. Sasa huyo bwana mdogo wako anaweza akawa wa kwanza darasani mwake lakini haina maana ukimpambanisha na madogo wengine vipanga atawatoa nishai.
 
Bob, siyo kwamba wazungu wote ni vipanga. Hapana ndugu. Sasa huyo bwana mdogo wako anaweza akawa wa kwanza darasani mwake lakini haina maana ukimpambanisha na madogo wengine vipanga atawatoa nishai.
Mkuu kisha weza tayari... Hii shule inasifika kwa elimu, iwaje tena mpaka akutane na vipanga hali kawakuta wanaosifiwa tayari. yaani kabla hajaingia kulikuwa na mtu wa kwanza wa pili na wakisifiwa kuwa ni vipanga iweje leo ibadilike kwa sababu kaingia Mbongo mbele yao.

Labda nishereheshe somo langu vizuri upate kunielewa. Mimi siamini sana matumizi ya ELIMU ya darasa ikiwa mtu hana ubunifu, vifanyia kazi, lengo la kutumia elimu hiyo ktk vipaji alivyonavyo, kuleta utajiri na mambo mengine muhimu ambayo yanaweza kumwendeeleza mtu. Tanzania na nchi nyingi masikini sii kweli hazina wasomi, au shule zetu ni mbovu ati kwa sababu tu sisi ni weusi au zinafundisha kiswahili ama ati wasomi wetu hawazungumzi kiingereza..

Ukweli ni kwamba wasomi wetu wengi sana wamesoma, kuna vijana wanafanya vizuri sana madarasani iwe tanzania na hata huku Ulaya isipokuwa kutokuwepo kwa ulazima wa Ubunifu, ulazima wa kuunda vitendea kazi, kutoweka vipaji vyetu mbele ya goals zetu za kimaisha ni moja ya sababu kubwa sana za kiujumla wa NDOVYO TULIVYO. Theory ya - Tunaishi ili tule, badala ya kula ili tuishi ndio hujenga strategies za maisha yetu kiujumla..

Mwanangu pamoja na watoto kibao wanaotoka Afrika huja Ulaya wakafanya vizuri sana.. na walimu hushangaa kuona uwezo huo wa watoto wetu kwani mara nyingi huku shule za msingi hata hesabati bado hutumia calculator madarasani.. Mbongo zinapigwa hesabu kichwani. tu.. Maswali yote huwa ni multiple choice yaani unapewa tip ya jibu ambalo hata kama ulisahau utalikumbuka..

Hivyo darasani wazungu wanaweza kutokuwa wazuri sana lakini wenzetu hawakariri..Kwao ELIMU ni kiunganisho cha makubwa yote yanayokuja mbeleni wanakuwa na dira tofauti ya kimaisha. Mtu anasoma hadi chuo kikuu ili kupata mwanga zaidi wa shughuli anayokusudia kuifanya.. Wakati sisi tunasoma ili tupate kuajiriwa. Tunakariri na Kuhifadhi volumes za masomo utadhani sifa ya elimu ni kuhifadhi masomo kichwani ukafa na shahada zako ukutani..

Msomi kamaliza chuo kikuu na Phd yake mwambie akueleze kitu kwa kiswahili - utachoka!.. Sasa wewe ulienda kusoma hadi havard na unarudi TZ kufanya kazi ukitegemea ku serve watu wanaozungumza kiingereza? inakuwaje vigumu kwa wasomi wetu kurejesha elimu waliyosoma kuielezea kwa kiswahili?..
Amini maneno yangu mkuu kama umewahi kufuatilia kwa makini hoja nyingi hata hapa JF zinapokuwa na utaalam fulani mwandishi hutumia lugha ya kiingereza kwa sababu (wanavyodai wao) ni rahiusi kwao na lugha inajitosheleza.. kumbe ni elimu waliyokariri kichwani, haiwezi kuwekwa wazi kwa lugha nyingine isipokuwa kiingereza!..Asilimia 80 kama sii 90 ya watanzania hawazungumzi kiingereza sasa hapa inakuwaje! hivyo elimu yote ile inapotea kichwani kwa mtu mmoja kwa sababu hawezi kui apply nyumbani vijijini.

Kichekesho, zaidi ni kwamba sisi wote tunapinga matumizi ya kiiswahili mashuleni huko nyumbani lakini ajabu ni kwamba inamchukua mtoto miezi sita sana sana tuseme mwaka kuongea kiingereza fluent akija huku, nimeona na sii swala la kusimuliwa na mtoto huyu anapofuzu masomo ana uwezo wa kuitumia lugha hiyo kirahisi ktk society ambayo kiingereza ni lugha ya mawasiliano..Tanzania kila kitu ni kinyume!
Mkuu wewe na mimi tumeweza kujiingiza huku kirahisi sii kwa sababu kuna wazungu, ila nadhani kwa sababu tunafuata mfumo wa kimaendeleo uliokuwa architected kurahisisha ujenzi wake.. hivyo hata miye mbeba zege (box) nafuata sheria za ujenzi wa nchi hizi..
Kifupi Uchumi wa nchi za kiafrika ni sawa kabisa na zile nyumba za kuezeka ulozitolea mfano... wakati wenyetu wanajenga kwa ramani, sisi tunaezeka kwa kutegemea vifaa vilivyopo.
 
Last edited:
.....it's perfectly simple!!!!!!!!!!!!!!!!! sisi Wa-Tanzania tulio wengi ni MASIKINI WA AKILI!!!....na hakuna umaskini mbaya kama huo ktk dunia ya leo....na taabu kubwa ni kwamba hata YULE asiye jua anajua kwamba hatujui!!!
 
Mkandara,

Inabidi watu wajue kuchukua majukumu yao kama bwana cha ubishi alivyoelezea, ni jinsi gani inakuonesha mtu asivyokua na mikakati ya maisha yake na kuweza kujilinda yeye mwenyewe kwanza kwa kujipunguzia majukumu ambayo awezi mudu. Sasa wewe unawatoto wa kumwaga je utaweza walisha wote au hatma yake nini? si kuwalaza njaa tu hao watoto au ndio kuwanyima utoto wao na kuanza kuwapa majembe wakalime wakati muda wa shule, au sijui wakasimame barabarani kuuza bajia ili uongeze kipato cha kusaidia lisha hiyo familia.

Ni nini hasa atma ya asilimia kubwa ya hawa wototo ukubwani ambao shule una wanyima una hela sijui ya kununua uniform, au wakienda shule kama ni mjini kunyanyasika na wenzao kwa mavazi yao yaani hawa watoto ni maskini kwa sababu mzazi awezi kuwa-angalia sasa mtu ana sababu gani ya kuongeza wengine. Iwapo ni kuleta shida tu kwa hawa binadamu hivyo hawa jamaa nao inabidi wapewe somo la responsibility.

Sasa embu angalia na shida zingine nyingi ambazo zinatokana na watanzania kujiletea utagundua ni kwamba hawa watu wana reason ability ndogo mno kwenye matendo yao.

Ntakupa mfano wa karibu mimi na dada yangu wa tumbo moja ambae yupo tz. sisi tumepoteza wazazi ambao walikua kwenye harakati za kutujengea sisi wamwisho mwisho kabakia yeye uko bongo peke yake ulaya ilimchosha (ajulikani huku) kwa hivyo hati za viwanja kazi kamata yeye huko bongo. Mimi huku nilivyokamata papers jamaa passport yangu waliipoteza hivyo ikawa mbide nikienda ubalozini hadithi nyingi yaani vikorosho tuu na usumbufu wa kutuita wakimbizi nyie sijui na nakadhalika. Kwa kuwa yeye yupo bongo na ni mtoto wa mjini nikasema wacha nimpe chenji afanye kazi. Hela yote kaenda kuila na ikawa simu apokei.

Nikaja dokezewa anakuogopa ukienda kiwanja kaweka pawn na hela ya kulipa ana. Haya nikamwambia potelea mbali basi hata kama umeuza wewe leta huo mkoba mi nishasamehe nianza upya. Nikapeleka na chenji nyingine nyingi wapi hela kala tena sasa wakati huo mimi huku ndio natakiwa kuanza chuo na chuo uingii ata kama umeshapata barua ya malipo bila ya mkoba sasa tena unakuwa unaenda kuongeza matatizo juu ya matatizo kwa fikra zake za kipumbavu. Kazi za maana nakosa, maisha unaninyima kwani hamna lolote la maana linalofanyika bila ya mkoba, kisa yeye anaogopa, wakati nilishampa kauli yangu forget it naelewa ulizidiwa na una mtoto peke yako huko.

Haya mimi leo nikienda bongo namuona anavyo angaika na nimegundua kitu especially kwenye maduka na vitu jamaa wanavyowabana. Sasa mimi leo nina uwezo wa kwenda kumchukulia genuine high street names kwa paundi mbili mpaka saba tu na vitu ambavyo vina cost 20 to 50 on the shops. Na wabongo sikuizi high street ya mamtoni wanaijua na market wanaijua. Nikienda bongo huwa na nunua simu za £20 na nauza mpaka laki mbili kisa ina camera sijui, simu babu kubwa wako watu wananunua mpaka millioni. Huku mimi nina rafiki ana duka la simu na hununua kwa retail price ana uwezo wa kuniodea ninazotaka. Haya nikimfungulia duka la simu huyu na nguo za high street hali. Si nina mpunguzia gunia la matatizo lakini unajiuliza je wewe utaikuta faida yako. Kwani wengine bado tuna mambo mengi ya kufanya huku? kwa hivyo umeshajua ni mtu gani unaeeenda kudili nae.

Leo mimi na yeye atuongei watu wanamfuata wewe sema hizo hati ziko wapi sisi tutatoa hela anakua mkali viwanja vipo nendeni mkaone kama kuna mtu kajenga. sawa avijajengwa lakini wape basi wenyewe au kama ni hela inahitajika sema basi tutoe bure we uwape haki zao. sasa mtu kama huyu we kweli unamuona mzima na nikikwambia dar-es-salaam nzima alwatan na anaonekana mjuaji. ndio ujue wapuuzi walio jaa nchi yetu yaani wana ignorance kubwa na reason ability ndogo mno wao questions never enter their heads before decisions kwa kweli hili ni moja ya tatizo kubwa sana kulii-ignore tanzanians are very ignorant people. This sort of thinking as to be sorted.
 
Kutokana na mfano huo naona picha kamili ya sisi kuitwa NDIVYO TULIVYO...ni pamoja na maajabu kama haya ndio yameijenga community hii.. Je, unafikiri vitu kama hivi ndio sababu kubwa ya umaskini wetu?..Kwa maana kwamba kama wewe ungekuwa nafasi ya mh. rais wetu Kikwete siku ile ya mahojiano ungesema nini sababu ya Tanzania kuwa nchi maskini?..
 
Mkuu nakubaliana nawe ktk hili saaana tu.... lakini huu Utaifa na Patroitsm waliokuwa nao wenzetu umekuja vipi?

Umekuja kwa propaganda kama hizo za huko kwa Lijulius zilizofanya wabandike vibendera vya 'America the Beautiful' na 'Land of the Brave' kwenye hivyo vita vya 'ki-patriotism' vya 'War on Terror'-cum-'War for Oil' - Yaani washikaji mpaka wakaweka na 'Patriotism Act' kuwadhibiti wakuja!

Hata siku moja hutawasikia wakiongelea 'Nationalism' ila utawasikia wanaimba 'Patriotism' hasa kama ishu inagusa maslahi yao. Sasa sisi tunadai ni 'nationalist' ila tunashindwa kuwa 'patriotic' kwenye ishu zinazogusa maisha yetu kama Rasilimali Nishati (Richmond), Rasilimali Madini (Barrick), Rasilimali Watu (Ortelo) n.k.!

Nationalism without Patriotism is Rhetoric!
 
Hiyo reference ya maximum security prison kuhusu mimi ni sarakasi ya lugha tu niliyokuwa nacheza nikimaanisha kama kuishi maisha mazuri ingekuwa kinyume na sheria basi mimi nigekuwa kwenye hilo gereza la ulinzi wa hali ya juu zamani tu kwa sababu siishi maisha mabaya. I love my life.

Sasa hilo Linyantuzu lenzangu haliko maximum security prison kwa sababu limevunja sheria kwenye jamii ya Miafrika. Lingekuwa huku majuu lingekuwa linanyea debe tu saa hizi. Umemsahau fisadi Maddoff au Ken Lay?

Mbona mamafioso na mafisadi wa Farenheit 9/11 are walking scot-free?
 
Oh! The reason behind our poverty is not the Government nor is it the ruling party. Tanzania has the best of policies, laws and highly trained professionals. Let us face it; it is our work attitude and ethics which is behind our object poverty! We are a nation of We are a nation of complainants40 million complainants and blame levellers! We complain and blame everyone else except ourselves. First, we blamed wakoloni. We blamed them for having under-developed us. We got our independence more than forty years ago, we have found many other matters to complain about and blame for our ills!

Evidence of our blaming and complaining is very visible even here in JF! Intellectuals of JF complain and blame. Ordinary mwananchi has been brought up to blame and complain. Politicians with power, law and policy to fix our problems complain and blame! Professionals we have trained to fix our problems complain and blame. Our students complain and blame. Our Lecturers and Professors at our universities complain and blame. There is no doubt that our loud complains and blames has made our country very unattractive to investors. This would be OK if we had internal means to invest and utilize our resources, we do not. We blame investors, yet we cannot work hard, save and invest on our own. We blame our laws and policies, but these we have been changing upside down, inside out for over forty years now.

So, the problem is not our laws or policies. I was bemused to hear employees of our Tanzania Railway Company volunteering to revive some of the engines to persuade the Government to terminate an existing investment agreement. Where were they when the former Tanzania Railway Corporation broke down to its knees? There are no perfect AGREEMENTS out there. An AGREEMENT will be perfect only if we inject huge investment into the Railway Company. We do not have that investment.

Over our life of independence we have blamed many things. Some are busy blaming our Constitution. It is as if we overhaul it, Tanzania will become a small paradise in the region! At this moment very few nation are bothered about their constitutions. Nations are bothered about the national, regional and world economy.

I can dare say, without fear that Tanzania is in the best hands under Kikwete. He has the best intentions for this nation. But, he needs all of us the professionals, intellectuals to change our work ethics. Tanzania has always had the best leaders since independence. But we should not forget that our own main problem is our work ethics and attitude. We like to spend what we do not produce, sweat and work for. We all imagine that the Government has pots and pots of money waiting for us to complain and agitate for. We forget that the perceived pot of money is paid for from our taxes (if we pay it). We can have huge pots if we work, save, invest and of course talk less and complain less! We like huge salaries without wanting to know who will bear taxes to fund increased salaries and life styles. Donors will not. Donor assistance comes with humiliations and intimidations.
Tero-buru
 
Mheshimiwa njoo JF upate sababu:

* Asema anajiuliza swali hilo kila siku bila jibu
* Apinga fikra za siasa za ujamaa kuwa tatizo
* Aeleza mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo
*Akiri kuna kipengele katika madini hakimfurahishi

Na Waandishi Wetu (Mwananchi)

RAIS Jakaya Kikwete amesema haelewi ni kwa nini Tanzania bado ni fukara ingawa imejaliwa rasilimali nyingi za asili kuliko nchi nyingi za bara la Afrika.

Rais Kikwete aliyasema hayo Oktoba 4, mwaka huu mjini Paris Ufaransa katika mahojiano na Mhariri wa masuala ya Afrika wa gazeti la Financial Times, William Wallis na Mwandishi wa gazeti hilo,Tom Burgis.

"Hata mimi sielewi. Hili ni swali ambalo hata mimi huwa najiuliza kila siku, ni nini ambacho hatujafanya? Nafikiri tunaongoza barani Afrika katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini."

Alisema hata yeye haelewi ni kipi ambacho bado hakijafanywa ili kuifanya Tanzania kuwa katika nchi zenye maendeleo mazuri katika bara la Afrika.

"Lakini bado tunaendelea kuvutia uwekezaji katika sekta nyingine. Labda ujumbe bado haujafika vilivyo," alijibu Rais Kikwete alipoulizwa kwanini Tanzania bado ni masikini.

Alipoulizwa iwapo tatizo pengine bado ni kutawaliwa na mawazo ya kijamaa, Rais Kikwete alisema:

"Sidhani hilo kama bado ni tatizo. Uwekezaji mara nyingi unatoka sehemu moja kwenda nyingine. Labda wakati wetu utafika katika muda mfupi ujao."

Alipoulizwa juu ya utata wa vivutio vinavyotolewa katika sekta ya madini katika miaka ya nyuma, Rais Kikwete alisema hajui kama kuna utata wowote katika sekta hiyo.

Hata hivyo alikiri kuwa kulikuwa na kipengele kilichowaruhusu wawekezaji katika sekta hiyo kuendelea kudai kuwa wanapata hasara hivyo kila wanachozalisha wawekezaji katika sekta hiyo walitumia kipengele hicho kufidia 'hasara' hiyo.

Alisema kutokana na kipengele hicho wawekezaji walikuwa wakichukua chote walichozalisha bila kulipa kodi kwa madai ya kupata hasara na kwamba wenye mali (wananchi) hawakulindwa, na suala hivi sasa linajadiliwa kwa lengo la kurekebisha.

Alisema makampuni yote ya madini yamekubaliana na suala hilo kwa kuwa wameona kuna hoja ya msingi katika kumlinda mwenye mali inapotokea hasara.

Alipoulizwa iwapo anaridhika na malipo ya dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka kama kodi kwa halmashauri migodi ilipo, Rais Kikwete alisema anakubaliana ingawa angependa malipo hayo kuongezwa ili kuwanufaisha zaidi wananchi wa maeneo husika.

Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema pamoja na kukua kwa michango ya sekta ya madini na utalii katika uchumi, msisitizo wa serikali ni kuibadilisha sekta ya kilimo ili itoe mchango mkubwa zaidi.

Alisema katika mkakati huo mabadiliko makubwa yatafanyika katika sekta hiyo kwa kuongeza kilimo cha umwagiliaji, kuongeza matumizi ya mbegu bora na utumiaji zaidi wa mbolea.

"Matumizi ya kawaida ya mbolea katika kilimo chetu kwa sasa ni ya chini mno ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano, sisi tunatumia kilo nane za mbolea kwa ekari moja ukilinganisha na kilo 577 kwa ekari zinzotumiwa nchini Uholanzi," alisisitiza Rais Kikwete.

Alisema katika mpango wa miaka saba wa kuboresha kilimo, mkazo pia unatiliwa katika kuwatumia wataalam wa kilimo kuwafundisha wakulima mbinu za kisasa za ukulima.

Aidha alisema pia kuwa mpango huo unaangalia masoko kwa ajili ya mazao yatakayozalishwa na wakulima na uimarishwaji wa miundombinu hasa barabara vijijini ili iwe rahisi kwa wakulima kupeleka mazao yao sokoni.

Mbali ya mpango huo kwa wakulima wadogo, Rais Kikwete pia alisema wanaangalia mpango wa kuwavutia wakulima wakubwa katika kilimo cha mazao ya biashara kwa kuweka vivutio vya kifedha.

Alisisitiza kuwa sekta ya utalii bado inaweza kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni kwa kuendeleza ujenzi wa hoteli zaidi katika fukwe na mbuga za wanyama ili kuwavutia watalii zaidi.

Katika mahojiano aliyoyafanya akiwa njiani kurejea nyumbani kutoka katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete alizungumzia masuala mbalimbali ikiwamo rushwa ndani ya CCM, vyama vya siasa nchini na utegemezi wa wafadhili katika bajeti unavyopungua mwaka hadi mwaka.

Pia alizungumzia kwa kirefu matatizo ya Zimbabwe na uhusiano katika mataifa ya Afrika na China na kuonyesha jinsi nchi hiyo ilivyo rahisi katika utoaji wa misaada ambayo haina masharti magumu kama zilivyo nchi za Magharibi na uwekezaji wa nchi hiyo katika Afrika.

Wakati huo huo, Joyce Mmasi anaripoti kwamba Rais Kikwete amesema ifikapo mwaka 2010 migodi yote ya madini nchini itakuwa inalipa kodi kikamilifu.

Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya wiki mbili nchini Marekani ambapo alikiri kuwa mikataba ya madini iliyosainiwa zamani ina mapungufu makubwa kutokana na walipa kodi kutolipa kodi ya maana.

Rais Kikwete ambaye aliripotiwa akiyasema hayo kupitia kituo cha Televisheni cha ITV cha jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kuwa mikataba ya zamani ina mapungufu, serikali itahakikisha inabadilisha mikataba mipya ili kuondoa mapungufu ya zamani.

"Wawekezaji wapya hawawezi kupewa mikataba kama ile ya zamani...sasa kama wapya wamepewa asilimia 15, basi hapa hakuna haja ya kuhangaika, huyo atakuwa amekiuka maagizo yangu, huyo mniachie mimi, hiyo ni kazi yangu."

Hata hivyo Rais Kikwete alisema, mipango ya serikali ni kupata asilimia 33 ya faida inayopatikana na akasema, "kama mgodi unapata dola 100, serikali itapata dola 33, hizi ni pesa nyingi na zitasaidia sana" alisema.

Alisema tayari wameanza katika baadhi ya migodi, na kuwa ifikapo 2010, migodi yote tangu ule mdogo mpaka ule mkubwa wa Bulyankulu utakuwa unalipa kodi kikamilifu.

"Tusingebadilisha hiyo mikataba, wenye migodi hiyo wasingelipa kodi mpaka mwisho wa uhai wa migodi hiyo, lakini serikali imeona na kuamua kuipitia upya," alisema.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema lazima tukubali kuwa Watanzania ni wachanga sana katika sekta ya madini na akasema ndio maana serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa haiporwi madini yake.

Mimi narudi kwenye mzizi wa topic, kama kweli mkuu raisi alisema maneno haya miaka mitatu iliyopita hii thread ilipo bandikwa basi hiyo 2010 ndio hii inawadia, hizo asilimia 33 zipo wapi???? [/B

bila viongozi na watu kubadilika tutaendelea kuzika masikini kwenye ardhi iliyojaa utajiri
 
Oh! The reason behind our poverty is not the Government nor is it the ruling party. Tanzania has the best of policies, laws and highly trained professionals. Let us face it; it is our work attitude and ethics which is behind our object poverty! We are a nation of We are a nation of complainants40 million complainants and blame levellers! We complain and blame everyone else except ourselves. First, we blamed wakoloni. We blamed them for having under-developed us. We got our independence more than forty years ago, we have found many other matters to complain about and blame for our ills!

Evidence of our blaming and complaining is very visible even here in JF! Intellectuals of JF complain and blame. Ordinary mwananchi has been brought up to blame and complain. Politicians with power, law and policy to fix our problems complain and blame! Professionals we have trained to fix our problems complain and blame. Our students complain and blame. Our Lecturers and Professors at our universities complain and blame. There is no doubt that our loud complains and blames has made our country very unattractive to investors. This would be OK if we had internal means to invest and utilize our resources, we do not. We blame investors, yet we cannot work hard, save and invest on our own. We blame our laws and policies, but these we have been changing upside down, inside out for over forty years now.

So, the problem is not our laws or policies. I was bemused to hear employees of our Tanzania Railway Company volunteering to revive some of the engines to persuade the Government to terminate an existing investment agreement. Where were they when the former Tanzania Railway Corporation broke down to its knees? There are no perfect AGREEMENTS out there. An AGREEMENT will be perfect only if we inject huge investment into the Railway Company. We do not have that investment.

Over our life of independence we have blamed many things. Some are busy blaming our Constitution. It is as if we overhaul it, Tanzania will become a small paradise in the region! At this moment very few nation are bothered about their constitutions. Nations are bothered about the national, regional and world economy.

I can dare say, without fear that Tanzania is in the best hands under Kikwete. He has the best intentions for this nation. But, he needs all of us the professionals, intellectuals to change our work ethics. Tanzania has always had the best leaders since independence. But we should not forget that our own main problem is our work ethics and attitude. We like to spend what we do not produce, sweat and work for. We all imagine that the Government has pots and pots of money waiting for us to complain and agitate for. We forget that the perceived pot of money is paid for from our taxes (if we pay it). We can have huge pots if we work, save, invest and of course talk less and complain less! We like huge salaries without wanting to know who will bear taxes to fund increased salaries and life styles. Donors will not. Donor assistance comes with humiliations and intimidations.
Tero-buru
All this crap, doesn't answer my question!
 
View attachment 674

hapa tuseme mheshimiwa akilia kuonesha uchungu wa kuwa maskini au vipi?

Dhamiri yake inamsuta kwanini anawaachia mafisadi wanaendelea kuitafuna nchi, huku pia akiachilia waporaji wa mali zetu kama kwenye mbuga za wanyama, mikataba mibovu e.g makampuni ya madini, TITCS, makampuni ya umeme n.k
 
Back
Top Bottom