Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mbona vidole vyote tunelekeza kwa wengine yaani sisi mmoja mmoja tumefanya nini kupambana na umasikini na kuwasaidia wengine kupambana na umasikini?

Soma post yangu hapo juu kama haikunijumuisha mimi na wewe. Umaskini wetu unaanzia kwenye akili zetu.
 
Kwa sababu Serikali ni corrupt, watendaji ni corrupt na wabinafsi, Mfano mdogo tu, Serikali imekuja na mpango wa kukopesha pembejeo W/Kilimo badala ya kununua trekta bora yakanunuliwa matrekta ya kichina limepakwa rangi vizuri kabisa, mtanzania for God sake hajui hili wala lile anachukua trector mwezi miwili tu trector is irreparable anaendelea kudaiwa 20mil badala ya kumsaidia unamsukuma zaidi kwenye umasikini!

Tumesikia habari ya pesa za kilimo kwanza zilivyotafunwa na wafanyabiashara wakishirikiana na watedaji kule Mpanda, zaidi ya 75% wamekula! What do you expect!

Mbaya zaidi wanaofanya madudu haya wanajulikana wanaendelea kudunda maisha tu and the Gvt is just watching! Yule mhasibu corrupt wa Bagamoyo licha ya kufukuzwa kazi amefanywa nini?

The answer is very obviouse! Watu wako kwenye nyadhifa kwa Masilahi yao Binafsi and with that a developed Tanzania will never never come!
 
Me ningependa kuuliza, sababu ya Tanzania kuwa nyuma kimaendeleo ni Viongozi wabovu, au watanzania wenyewe kwa ujumla? Unaposema viongozi unazungumzia tabaka fulani, ambalo ni sehemu ya watanzania (sisi wenyewe). Lakini kitu ambacho mimi nimekiona, na ambacho hata wewe ukifungua macho yako utakiona, ni kuwa tabia zinazoonyeshwa na hawa tunaowaita viongozi wabovu ndizo hizo hata sisi watanzania wengine (tusio viongozi) tunazionyesha - tofauti ni scope, na mahali haya madhambi yanapotendeka.

Kama kuna changamoto za msingi zinazoikabili Tanzania, moja wapo ni uaminifu. Watanzania sisi sio waaminifu (wengi wetu), hata kwenye vitu ambavyo hutarajii mtu atakwibia - mtanzania atakudhulumu hadi kwenye sh 100. Leo hii ukijiuliza ni nani ushirikiane nae kufanya biashara ni utata mtupu!

Tukirudi kwenye ajira, ndio kabisa. Kupata kazi ni mpaka kumjua mtu! Hauna network ya kutosha, basi utaozea na vyeti vyako - shauri yako hakuna anayejali!

Mtanzania huyo huyo utamsikia akisema - "we unahurumia mali ya serikali, cha umma hakina mwenyewe". Na mtu akipata nyadhifa akaastaafu bila kujilimbikizia basi huyo ni mjinga. Hivi ni wangapi watakusaidia kukupa huduma bila kudai ten percent?

Suala ni kwamba, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake. Kama wewe ni Nurse, unatoza wagonjwa chochote kitu kuwapa huduma, we unadhani waziri yeye anakula wapi? Akila rushwa waziri kosa, ila nurse hatusemi. Hivi huyu nurse akipewa ubunge itakuaje? Na ndio maana waswahili wakasema "kunya anye kuku, akinya bata kaharisha" - raia tunakunya, ila viongozi wanaharisha, na hii ndio maana yake!

Suala la rushwa, kukosa uzalendo na kutojali maslahi ya wenzako, ni suala la tabia, ambazo zimejengeka kwetu watanzania. Kama tunataka maendeleo ni lazima watanzania wote tubadilike. Kumbuka kuwa viongozi huchaguliwa kati yetu sisi watanzania. Hao ni wawakilishi wetu, na wanawakilisha zile tabia zetu kiujumla. Kama watanzania tutakuwa na tabia zinazochochea kubomoa maendeleo, we unadhani viongozi watakuwa na tabia gani?

Nakumbuka msemo wa Mbatia, alisema "kila mtanzania ni fisadi, tofauti ni kiwango". Na kuna ukweli ndani wa huu msemo. Ingawa sikubaliani nae kuwa ni kila mtanzania, ila tulio wengi kwa tabia zetu inatosha kabisa kuitwa mafisadi. Sisi wananchi ni mafisadi dagaa, na viongozi ni mafisadi papa.

The bottom line is, maendeleo yatakuja pale watanzania tutakapo badilika kitabia na ki fikra, na si kwa kubadilisha vingozi.
 
Jibu wanalo Viongozi na wanasiasa wa CCM sababu hakuna aliye masikini sasa badala ya kukaa na kuanza kupotezeana muda wa kutafakari hao wenzetu watuambie walivyoupiga teke umasikini pamoja na familia zao ili nasisi walalahoi tuwe kama wao
 
Sisi ni maskini kwa sababu watanzania tumeamua kuwa na kubaki maskini milele. Siku akili zetu zikipevuka tutakuwa kati ya matajiri wa dunia hii.
Lini? itategemea na sisi wenyewe na ohhhhhhhh Mungu wangu kama utajiri wenyewe utakuwa bado upo!

Hilo ndilo jibu sahihi kabisa, sijui tumemkosea nii mungu, hatutumii kabisa akili ninaposema akili ni kuanzia mimi ninayechagua kiongozi asiyetumia akili, mimi nisiejiandikisha kupiga kura wakati haki ninayo, mimi niliyejiandikisha kupiga kura lakini siendi kupiga kura ni mimi ninayeona kiongozi ambaye simkuchagua analeta madudu nakenua tu meno bila kufanya chochote.
 
Hilo ndilo jibu sahihi kabisa, sijui tumemkosea nii mungu, hatutumii kabisa akili ninaposema akili ni kuanzia mimi ninayechagua kiongozi asiyetumia akili, mimi nisiejiandikisha kupiga kura wakati haki ninayo, mimi niliyejiandikisha kupiga kura lakini siendi kupiga kura ni mimi ninayeona kiongozi ambaye simkuchagua analeta madudu nakenua tu meno bila kufanya chochote.

Kweli kabisa,tatizo ni mimi,kwa nini sina kitambulisho cha kupigia kura na umri unaruhusu,kwa nini nimeuza shahada ya kupigia kura, kwa nini namsifia mwizi wa ushirika wetu wa wakulima wa Pamba,kwa nini nimechukua spear ya gari ya ofisi na kuifunga ktk gari yangu,kwa nini nimeuza mtihani wa kidato cha nne mwaka jana,Kwa nini nakaa kwa shemeji ktk umri huu wa kujitegemea,kwa nini nimeingiza condom fake sokoni,kweli nimeuza kiwanja kwa watu wawili,juzi nimechukua watu wa kabila langu tu kuingia jeshini, etc etc

Kwa hiyo usione kosa lako dogo,kwa nafasi yako hiyo hiyo ndogo umeporomosha uchumi wa mwenzio hatimaye taifa.
 
1. Ujinga
2. Ubinafsi
3. Anasa na starehe
4. Uvivu
5. Kutojali hali uliyomo....
6.
 
Sababu kubwa ya umasikini Tanzania ni wananchi wenyewe na fikra potofu za kutaka kufanyiwa kila kitu. na kuta kwenye ukoo mtu mmojs akiwa na maendeleo basi ndugu wote wengine wana taka kumyonya yeye na kuona kwamba mali za ndugu ni mali zake. Hii ina sababisha wengi kuwa wavivu wakidhani kwamba hata iweje kuna mtu wa kumnyonya.

Tanzania ni masikini kwa sababu watu hawaja jua thamani ya elimu. Sawa nakubali shule ni chache na siyo kila mtu mwenye nafasi ya kwenda. Lakini ni mara ngapi tunaona mzazi haweki elimu ya mtoto kama kipaumbele?

Tanzania ni maskini kwa sababu tuna tegemea serikali itufanyie kila kitu. Watanzania wana tegemea maendeleo yana anzia ngazi za juu kumbe maendeleo yana anzia ngazi za chini. Mtu mmoj mmoja, familia moja moja, jamii moja moja mpaka juu.

Tanzania ni maskini kwa sababu tuna population ya waongeaji siyo watendaji na hii siyo kwa wanasiasa tu. Tuna taka mabadiliko lakini wakati huo huo tuna tegemea maendeleo hayo aanzishe na kufanye mtu mwingine. Hatuna initiative kwenye chochote.

Tanzania maskini kwa sababu watu siyo wachapa kazi na wanao chapa kazi wana chapa kazi kwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili.

Dah! Yani mkuu sidhani kama thread ina tosha kuelezea kwa nini Tanzania maskini. Inabidi mtu akae chini aandike kitabu au series za vitabu kuelezea hili swala. Sababu ni nyingi lakini it all boils down to TANZANIA NI MASIKINI KWA SABABU YA WANANCHI WAKE WENYEWE!
 
Hilo ndilo jibu sahihi kabisa, sijui tumemkosea nii mungu, hatutumii kabisa akili ninaposema akili ni kuanzia mimi ninayechagua kiongozi asiyetumia akili, mimi nisiejiandikisha kupiga kura wakati haki ninayo, mimi niliyejiandikisha kupiga kura lakini siendi kupiga kura ni mimi ninayeona kiongozi ambaye simkuchagua analeta madudu nakenua tu meno bila kufanya chochote.

Tusimsingizie Mungu umasikini wetu.
 
Kweli kabisa,tatizo ni mimi,kwa nini sina kitambulisho cha kupigia kura na umri unaruhusu,kwa nini nimeuza shahada ya kupigia kura, kwa nini namsifia mwizi wa ushirika wetu wa wakulima wa Pamba,kwa nini nimechukua spear ya gari ya ofisi na kuifunga ktk gari yangu,kwa nini nimeuza mtihani wa kidato cha nne mwaka jana,Kwa nini nakaa kwa shemeji ktk umri huu wa kujitegemea,kwa nini nimeingiza condom fake sokoni,kweli nimeuza kiwanja kwa watu wawili,juzi nimechukua watu wa kabila langu tu kuingia jeshini, etc etc

Kwa hiyo usione kosa lako dogo,kwa nafasi yako hiyo hiyo ndogo umeporomosha uchumi wa mwenzio hatimaye taifa.

Hapo ndo tunatatizo, nadhani kila mtu sasa unauona mchamgo wake ktk kuleta huu umasikini!
 
Wanadai wenyewe kuna Dunia Tatu. Nchi za dunia ya kwanza ni nchi ambazo zimeendelea, halafu kuna kundi la dunia ya pili ambalo ni nchi zinazoendelea na mwishoni ni nchi za dunia ya tatu, nchi masikini, nchi zenye maendeleo madogo na finyu.

Vipimo hivi hutokana na uwezo wa kirasilimali na kujitegemea kibajeti, kifedha na ubora wa maisha ya watu pamoja na mengineyo kama miundombinu, afya, elimu, ajira na hata mahusiano ya jamii.

Zaidi ni kufahamika kama nchi tajiri zenye kujitosheleza na nchi masikinin ambazo ni tegemezi kabisa na hazina uwezo wa kujitosheleza.

Sasa ni lini basi, Tanzania itakapoondoka kwenye kundi la nchi masikini zilizo na maendeleo kiduchu na hata kwenda daraja la kati la nchi zinazoendelea?

Kama vile katika watu kuna tabaka la juu, la kati na la chini kutokana na mapato na uwezo, je Tanzania kama nchi itaachana lini na Ulalahoi? Je ni jukumu la nani kuitoa Tanzania kutoka Ulalahoi na kuipandisha chati kufikia hata ile hatua ya kuwa Wa-Benzi?

Tanzania ni nchi ya tatu kwa wingi wa dhahabu duniani. Tanzania imerudia kwenye usukano wa nchi inayoongoza kwa kuzalisha katani. Tanzania iko katika nchi kumi zilizo na Uranium ya kutosha. Ongezea madini kama makaa ya mawe, gesi, rubi, almasi, chuma, shaba na hata Tanzanite ambayo ni sisi pekee tunaozalisha.

Tanzania tuna mbuga za wanyama kubwa sana na maarufu duniani. Tanzania kuna mlima mrefu Afrika na inazungukwa na Maziwa makubwa matatu ya dunia hii na ongezea Bahari ya Hindi. Tanzania ina visiwa maarufu vya Zanzibar na Mafia ambako si mazao tuu hata utalii unaweza shamiri.

Tanzania ina ardhi kubwa ya kutosha yenye kuweza kuzalisha mazao ya biashara na kutawala soko la dunia, mazao kama Chai, Kahawa, Tumbaku, Korosho, Pamba na hata mazao ya chakula kama Mahindi, Mpunga, Maharage, matunda, mboga za majani, Mtama, Mihogo, Ngano, Shayiri, Karafuu na mengineyo.

Tanzania tuna samaki wa aina nyingi sana, tuna mifugo mingi ambayo inatufanya tuwe katika nchi tano zenye mifugo mingi Afrika.

Tanzania ina watu takribani Milioni 40 na wanazidi kuongezeka.

Lakini haieleweki pamoja na hazina yote hii na nguvu kazi yote hii ya watu Milioni 40, ambao wamefunikwa na mshikamano na kufungamana kuliko leta Amani na Utulivu wa namna fulani, hadi leo hii tunaendelea kuwa Taifa la Kilalahoi, tukitegemea misaada na mikopo na hata watu kutoka nje waje kuzalisha na kutupa kipato.

Si suala la ni nani Rais au ni chama gani kiko madarakani au ni Siasa gani hata kwa wale wanaodai bado tu nchi changa au ni makosa ya sera, itikadi au mfumo wa kiuchumi ambalo ndi kizingiti cha kuleta maendeleo na kuliendeleza Taifa letu likanawiri na kuachana na umasikini na unyonge unaotufanya tuendelee kuwa Walalahoi.

Si suala la kudai ni mafisadi, wahujumu, wanasiasa, makaburu, wawekezaji, ukoloni, utumwa au lolote lile la kuhalalisha kuwa mpaka leo tunaendelea kuwa Taifa masikini.

matumizi yetu ni makubwa sana, tena ya anasa sana! Ripoti ya wikii hii inasema deni limeongezeka, matumizi yanaongezeka, lakini hatutumii hazina vizuri hata kuitumia katika kujenga msingi imara wa nyumba yetu ili tuweze kuishi hata vizazi 10 bila kuporomoka.

Je twahitaji mme, mke, mtawala hata mshenga wa kutuamsha na kujitambua kuwa Uchumi tumeukalia?

Naibu Waziri wa Fedha Omar Mzee katoa kauli majuzi bungeni akisema tena kwa ukweli mtupu bila kutia vikolombwezo kuwa ni wajibu wa kila mtu kutamani maendeleo na kujiendeleza na si kuisubiri Serikali.

Kauli kama hii iliwahi kutolewa na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya aliposema kila mtu atabeba Msalaba wake!

Je tumeridhika na Ulalahoi kiasi hicho na kufurahia kuwa Masikini?

Je ni kisingizio gani tulichonacho kwa nafsi zetu moja moja au kwa ujumla wetu kama Taifa kuhalalisha umasikini wetu huu uliokubuhu na kupita kiasi huku kuna wanaoneemeka kupita kiasi kutokana na hazina na rasilimali tulizonazo?

Je ni uzao gani tuusubiri uje kulivusha Taifa letu kutoka kundi hili la nchi masikini na tegemezi na kuwa ni nchi yenye kujitegemea na maendeleo yyake yakawa ni endelevu na kuiendeleza jamii kuelekea kuwa nchi iliyoendela?

Je ni miaka mingapi tunahitaji kuendelea kujifunza na kutamani kufikia tabaka la kati na kuachana na tabaka la kuwa masikini?

Je tunamsubiri Rais au chama gani kishike madaraka ndipo tukate shauri kuachana na unyonge wa mawazo na kujitutumua kila mmoja kibinafsi na kwa ujumla kuijenga nchi yetu na kuvuna na kufurahia rasilimali zetu na hivyo kuondokana na karaha na adha za kuwa masikini?

Ni lini tutaondoka kutoka kwenye kundi la Nchi za Dunia ya Tatu na Masikini na kwenda japo katika kundi la Nchi za Dunia ya Pili zinazoendelea na kupiga hatua mbele?
 
Ni lini tutaondoka kutoka kwenye kundi la Nchi za Dunia ya Tatu na Masikini na kwenda japo katika kundi la Nchi za Dunia ya Pili zinazoendelea na kupiga hatua mbele?

Never! Ni nchi gani ya Black Africa isiyo kwenye kundi la nchi za dunia ya tatu? Do you see a pattern here...?
 
Nyani,

We can be the first one....if there is a will and desire to become a progressive and developing country, yes we can!
 
mipango na utekelezaji ndio tatizo kubwa kwetu, maneno mengi lakini vitendo hakuna
nadhani wananchi ndio wenye ufunguo wa kutaka na kuleta maendeleo
 
uwezo wa kirasilimali na kujitegemea kibajeti, kifedha na ubora wa maisha ya watu pamoja na mengineyo kama miundombinu, afya, elimu, ajira na hata mahusiano ya jamii.
tutakapoweza kuacha kulalamika na kuchukua hatua,kuweka nia ya kuhakikisha tunanyanyua maisha ndipo tutakapoondoka kwenye kundi la nchi maskini kwa kufanya kazi kilimo nk,wengi wetu walalamishi,tumejaa ujinga wa serikali wafanye kila kitu,kama raslimal tunazo tunahaja gani ya kuwa maskini???mfano mdogo vijijini watu wanashinndwa kujiorganize kulima hata barabara zinazoelekea sehemu za huduma kungojea serikali ije iwalimie........kubwa tuhakikikishe serikali inatuletea sera zinazotekelezeka na sio sera hewa halafu na sisi tunakaa na kuwachekea bila kufanya kitu.kufanikisha haya tutaweza kuondoka hapo na wala hakuna uchawi mwingine
 
Unnecessary excesses zinatufanya tuishi beyond our means. Hii simply maana yake ni kuwa siku zote tutaishi kwa kutegemea mikopo (wenyewe wanaita misaada). Na hakuna njia nyepesi zaidi ya kuendelea kuwa maskini kama kutegemea mikopo. Simply ni kuwa katika kuishi hata individual, ukitegemea sana mikopo, hatimaye kila ulicho nacho kitachukuliwa. Mikopo tunayochukua kama nchi haiingii kwenye productive sectors, zinaingia kwenye service na kwenye luxuries kama magari, majumba ya fahari kwa viongozi, shoping za nje kwa viongozi n.k.

Mpaka tutakapofikia hatua kama taifa ya kuona tatizo la kuishi beyond our means, tutaendelea kuwa maskini na itafikia hatua wanaotudai watachukua kila tulicho nacho. Watu wanalalamikia sera za madini n.k. Lakini sera hizi zinatungwa kwa malengo ya kuwafurahisha wale wanaotukopa ili waendelee kutupa mikopo. Tukikataa hawatatupa mikopo na utakuwa ndo mwisho wetu, hili ndo Tatizo kubwa.

Kuishi juu ya uwezo wetu ndo tatizo kubwa. Serikali yetu inatumia fedha nyingi sana kuwalipa posho na marupurupu maofisa wake. Ni fedha chache sana zinazoingia kwenye mfumo unaozalisha. Hizi fedha wakishalipwa hawa watu huzitumia kununua vitu vya anasa ambavyo hatimaye havitozwi kodi!! Matokeo yake ni kuzalisha tabaka la Mamwinyi ambao kusema kweli lazima wawe ni watu waliokwisha fanya kazi serikalini tena kwa nafasi za juu. Hawa hujijengea mfumo wa kujizungusha (recycling) kwa kuhakikisha wanao ndo wanachukua madaraka wao wanapotoka.

Matumaini yetu yapo kwenye kuligundua hili tatilzo na kulifix. Ikiwa tutaendelea kuishi maisha ya juu kwa fedha za mikopo au misaada, hakuna matumaini asilani.
 
Tutaondoka kwenye lindi hili la umaskini kama tutawachagua viongozi serious na kuwawajibisha wale wanaoshindwa kupafomu inavyotakiwa..and CCM lazimaitoke madarakani.
 
GS,

Kwa hivyo wewe unaona tatizo ni uongozi na CCM pekee? what about you and I, what have we done to jikomboaring from Ulalahoi? are we obligated to wait for Serikali or new ruler? si heri turudie Ukoloni then Nyani Ngabu atapata trademark rights and super benefits for his thesis kuwa Miafrika Ndivyo Ilivyo and No Black Africa can never progress on its own?
 
SIKU SISIEMU(CCM) ITAKAPOONDOKA MADARAKANI KWA AIBU, NDO TUANZE KULIJADILI HILI, ila kwa sasa, hii ndi ndoto, tena ndoto ya mchana kweupeeee.
 
Back
Top Bottom