Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
GS,

Kwa hivyo wewe unaona tatizo ni uongozi na CCM pekee? what about you and I, what have we done to jikomboaring from Ulalahoi? are we obligated to wait for Serikali or new ruler? si heri turudie Ukoloni then Nyani Ngabu atapata trademark rights and super benefits for his thesis kuwa Miafrika Ndivyo Ilivyo and No Black Africa can never progress on its own?

Rev
Im triying to play my part as a citizen ili nijikwamue na suala hili la ulalahoi thats why am not one of them.Afrika tunaweza kabisa kujikomboa wenyewe kama tu tutakuwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kulibadilisha taifa hili na sio kwa maslahi ya familia yake au kabila lake au dini yake au hata rafiki zake bali kwa watanzania wote kwa ujumla..Hili linawezekana..Hizo nchi zilizoendelea anazozidai Nyani Ngabu ndio zinazotuongezea umaskini kwa masharti yao yakipuuzi..Huwa namsapoti Mugabe sometimes kwa misimamo yake.
 
ukombozi wa kweli kutoka kwenye umasikini ni pale kila mwananchi atapojua thamani ya kura yake
 
Je Watanzania wanajijua kithamani na kuwa kila mmoja ana thamani gani?
 
Rev. Kishoka, kwa mtazamo wangu finyu, labda yafuatayo yanaweza kutusaidia. Kwanza kabisa:
We need to grow up and takecare of ourselves, that is it! Hakuna siri zaidi ya hiyo, haya mambo ya misaada kila siku kamwe hayatatusaidia. Wenzetu kule Asia walikuwa kama sisi four decades ago, lakini leo hatuwezi hata kujilinganisha nao. Nadhani yafuatayo yanaweza kubadilisha mustakbali wa nchi yetu:

-Fight corruption: this is a reasonable indicator of quality of government and rule of Law
-Elect capable and honest leaders i.e Baba wa Taifa J.K. Nyerere
-Sound economic policies
-Well structured institutions i.e executive , legislative, and Judiciary branches of government
-Very disciplined and hard working citizens, tupunguze ubabaishaji wa Simba na Yanga kwani maendeleo hayaji kwa kupunga mkono, yanakuka kwa kufana kazi kwa bidii.
-Nationalism i.e who are we as people, and what we want
-Make sure the government work for its people, and not for the individuals.
-Accountability i.e stop kubebanabebana
-We have to learn how to live within our means, and stop this nonsense of "grab what I can while I can" Mobutu-like syndrome.
Kama nilivyosema hapo juu, nchi kama Indonesia, Singapore, na Malyasia walikuwa kama sisi. Lakini walipata viongozi wazuri na wenye uzalendo; ambao hawakuwa na Mobutu Syndrome ya kukimbiza mali ya nchi Switzerland kama baadhi ya viongozi wa Africa. Nina uhakika we can do that! Trust me, we can! At the end of the day, only Tanzanians can improve their situation. No one else could.


 
wow! swali zuri, naungana na mchangiaji aliyesema kuwa, siku CCM itakapoondoka madarakani ndipo dira mpya ya TZ itaanzia hapo. kwa sasa, tunafuga mafisadi tu, pachika fisadi, pakua fisadi. hata kama kikwete siyo fisadi, kwasababu at least anaonyesha trust, lakini system yake aliyoikuta, system yoote ya hawa wazee wa kizamani kwenye uongozi, imejaa dili dili tu za wizi na kulindana. hivyo, bila CCM hakika sidhani kama tutaweza kufika popote sisi watz.

mwenye akili awe mmoja wao wa wanaopiga kampeni against CCM kwa nguvu zote, kuanzia ndani kwake, mkewe, watoto wake, mahousegirl, dada zake, marafiki ndugu na jamaa, au hata mtu yeyote atakayemkuta njiani, hakuna kusubiri mikutano ya viongozi wa vyama , awahamasishe wakapige kura na wapigie chama kingine ambacho si CCM.
 
Rev
Im triying to play my part as a citizen ili nijikwamue na suala hili la ulalahoi thats why am not one of them.Afrika tunaweza kabisa kujikomboa wenyewe kama tu tutakuwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kulibadilisha taifa hili na sio kwa maslahi ya familia yake au kabila lake au dini yake au hata rafiki zake bali kwa watanzania wote kwa ujumla..Hili linawezekana..Hizo nchi zilizoendelea anazozidai Nyani Ngabu ndio zinazotuongezea umaskini kwa masharti yao yakipuuzi..Huwa namsapoti Mugabe sometimes kwa misimamo yake.

ndugu, kukiwa na accountablility na uelewa wa kutosha, something can happen. Kama wananchi watakuwa na uelewa wa kinachoendelea, kiongozi yeyote tuliyemkabidhi dhamana yetu akila rushwa wananchi wakaandamana na kushinikiza awekwe ndani pamoja na kutaifishwa kila alichonacho, kukiwa na viongozi waliojitolea kuhakiksha kuwa hakuna wahindi wanaokwepa kodi ya viwanda vyao hapa Dar es salaam, kukiwa na viongozi wanaosimamia kuwa kila mtu anatoa kodi kulingana na kiwango chake, mbona ni kitu rahisi tu. tutaendelea hata kesho.

Tatizo ni kwamba, uliyemweka TRA, anajaza watu wa kabila lake, anataka cha juu wakati wa kulipa kodi ili zingine ziende kwenye account yake badala ya kwenda kwenye account ya selikali, uliyemweka bandarini naye, kila uliyemweka popote, wameweka chain kuanzia mfagiaji hadi boss juu, kuanzia trafick police hadi mkuu wao, kukusanya kidogokidogo, na kula pamoja na boss wao. hii ni ktk kila sector. so, ofisi yoyote utakayowapa watu, wanafanya mradi wa familia, ukoo au kabila, wengine dini. ni ajabu sana. sijui ni lini tutapata viongozi wenye uwezo wa kufuatilia na kuyateketeza kabisa mambo ya ajabu kama haya.
 
Swali hapa siyo "Ni Lini Tutaondoka kwenye Kundi ..." bali "Ni Vipi Tutaondoka kwenye Kundi ..."

Inavyoonekana hili la pili ni swali gumu zaidi kupata majibu, siyo?
 
tutaondoka kenye umaskini pale ambapo;

tutaacha kuwa tegemezi kama nchi na individually, watawala wetu wamejijengea imani kwamba bila misaada/mikopo hawawezi kuendesha nchi. wanafikiri suluhu ya matatizo ni kuombaomba na kufanya kila linalowezekana kuwafurahisha wanatoa hiyo misaada. wananchi kwa upande wao wanaona bila serikali kuwajibika hawawezi kuendelea. hawajiungi na vikundi vya wajasiriamali, hawa chukui mikopo kupanua biashara zao wana poteza muda mwingi kulalamikia serikali

tutaacha kuwa tegemezi pale ambapo tutaelewa kwamba ili kujiendeleza kiuchumi nchi za africa hasa sub saharan africa lazima zisaidiane, tutafaidika sana kwa kuendeleza viwanda na kuuziana bidhaa zetu wenyewe kwa wenyewe

tutaondokana na umaskini pale ambapo viongozi watatambua kwamba kuendelea ni jukumu letu wenyewe, lazima wajiulize sisi kama watanzania/waafrica wa sub saharan africa - tunafanya nini kujiendeleza? kama kweli watoa misaada wana mipango genuine ya kutusaidia kwa nini hawaweki uzito kwenye kuendeleza viwanda na kusaidia wakulima wadogo wadogo na kufungua world market ili na sisi tuuze bidhaa zetu badala yake wameshupalia kutoa misaada a.k.a mikopo yenye masharti yasiyo tupa faida na kutokemea makampuni yao yanayo ongeza utajiri kwenye nchi zao tajiti kwa kuiba mali asili zetu?
 
Swali hapa siyo "Ni Lini Tutaondoka kwenye Kundi ..." bali "Ni Vipi Tutaondoka kwenye Kundi ..."

Inavyoonekana hili la pili ni swali gumu zaidi kupata majibu, siyo?

I couldn't agree more. Nadhani tungekuwa na jibu la how then ni rahisi kueka timelines ktk prospect ya projection...but this happens in theory..most of the time..lol
 
Ni Lini Tutaondoka kwenye Kundi la Nchi Masikini na kuwa katika Nchi Zinazoendelea

Tutakapotambua kuwa ustawi wa jamii sio wa mtu mmoja mmoja bali jamii nzima

Tatizo letu tumejawa na UBINAFSI aka U-MIMI na hili linatutafuna vibaya sana!

Kuanzia kwenye mitaa tunamoishi mpaka IKULU

1) Elimu: Kila "individual" anajitahidi kumpeleka mtoto wake "nje" kusoma badala ya kuchangia shule zetu za msingi, sekondari, na vyuo vikuu viwe kwenye kiwango stahili
2) Jamii: Mtu anajenga ghorofa halafu anatiririsha maji majafu barabarani
3) Watawala: Kila kiongozi anajitahidi kumiliki kiasi chochote cha mali bila kujali - eka 200 wakati hata kulima hajui wala hajawahi kufuga hata sungura!
4) e.t.c
 
TANZANIA NI MASIKINI KWA SABABU YA WANANCHI WAKE WENYEWE!

Hapo ndipo penyewe MwanaFalsafa1!

Kila siku napiga kelele na watanzania wenzangu, na napinga vikali wale wanaosema tatizo la umaskini Tanzania ni UONGOZI MBOVU!

Tunawasingizia viongozi, wachawi ni sisi wenyewe!
 
Ufisadi, uroho, ulafi, ubinafsi, kujilimbikizia mali na ubadhilifu unaoendelea miongoni mwa viongozi wa siasa ndio unaotufanya nchi yetu iwe masikini mpaka leo. Maadili yameporomoka mpaka viongozi wanageuza mali ya umma kuwa ya kwao binafsi. Nchi yetu imefika pabaya

Hapa benye bold ndio pa kurekebisha. Sio miongoni mwa viongozi wa siasa, ni miongoni mwa wananchi wenyewe.

Ukichukua mafuta kwenye gari la serikali ukaweka kwenye gari lako nyumbani na huu si ubadhilifu? Je, anayeiba mafuta ni nani, dereva au waziri?
 
Tutakapotambua kuwa ustawi wa jamii sio wa mtu mmoja mmoja bali jamii nzima

Tatizo letu tumejawa na UBINAFSI aka U-MIMI na hili linatutafuna vibaya sana!

Kuanzia kwenye mitaa tunamoishi mpaka IKULU

1) Elimu: Kila "individual" anajitahidi kumpeleka mtoto wake "nje" kusoma badala ya kuchangia shule zetu za msingi, sekondari, na vyuo vikuu viwe kwenye kiwango stahili
2) Jamii: Mtu anajenga ghorofa halafu anatiririsha maji majafu barabarani
3) Watawala: Kila kiongozi anajitahidi kumiliki kiasi chochote cha mali bila kujali - eka 200 wakati hata kulima hajui wala hajawahi kufuga hata sungura!
4) e.t.c

Barabara..

Kuelewa kwanza how to overcome poverty is PARAMOUNT. Lakini what do u expect ktk taifa ambalo Rais, the head of state, hajui kwanini sisi ni maskini? Kaa hajui kwanini sisi ni maskini ataeza vipi kujua atatupeleka vipi kwenye promise land, kwene nchi ya maziwa na asali?

Umeongea suala la umimi..Hii ni kansa kubwa ktk dunia...Capitalism and capitalist forces..Umimi unasimamiwa na kuhubiriwa na unalindwa kisheria!. Ni vigumu sana kuelewa watu tunaezaje kupiga mbio za sakafuni (ambazo huishia ukingoni) ktk mazingira yanayoeleweka wazi kuwa capitalism is not the way forward kwa sababu haiwezi kuhakikisha maisha bora ya watu wote bali baadhi tu? .

Unaeza vipi kupiga vita rushwa wakati capitalism inadai kuwe na winner mmoja tu na wengine wate wawe loosers...? Ndo maana rushwa ipo kila mahali, kuanzia wanaohitaji rushwa kukidhi mahitaji yao ya kibinaadamu mpaka wale wanaodai rushwa ya kujengea nyumba viamda!

Tunaezaje kukubali mfumo unaruhusu baadhi wa watu wajukusanyie utajiri bila kipimo wala ukomo wakti tukijua kuwa utajiri ule unahitajika pia na watu wengine, at least ili kukidhi mahitaji yao ya kibinadamu?

Unaezaje kusema uchaguzi uwe na mshindi mmoja tu bila ya watu kutumia mbinu chafu? Unaezaje kuwa na chama kipo madarakani kwa miongo minne lakini kinaomba kikamilishe miapngo yake ya maendeleo? Maendeleo ambayo hayaonekani? Unaezaje kuwa na maendeleo wakti vyama vya upinzani vinashindwa kuepa the most fundamental challenge ya kuelimisha wananchi na badala yake vinakimbilia kushiriki uchaguzi na kuendelea kuburuzwa left and right?

Unaezaje kuendelea huku rasilimali ukiwamilikisha wageni ili wachume na kujiendea zao, tena tunawapa na tax holiday kana kwamba sisi ni matajiri saana kaa masultan wa Brunei! Rasilimali zikiwa exhausted tutakuwa wageni wa nani? maana tangu exploitation iaenze hatuoni hata dalili ya maendeleo kwa watu wetu.
 
Kama budget yako 40% unategemea donors ,basi utabaki kundi hili.Viongozi wetu hawaoni aibu kwa hili!
Mtu hapa ametoa mfano wa Malaysia.angalieni safari za msanii wetu mkuu ,halafu mlinganishe na Dr Mahathir Mohamed kama aliruka ruka na Private Jet kwenda Ulaya.

Someni kitabu cha msichana wa Zambia anaitwa Dr DAMBISA MOYO,ameandika kitabu entiltled DEAD AID.Ni kizuri sana,maana AID ni biashara mbaya sana imetufanya sisi Waafrika tuwe nyuma.Bado tunamawazo ya kinyani,siku tukiacha hayo mawazo ,tutapiga hatua
 
Unnecessary excesses zinatufanya tuishi beyond our means. Hii simply maana yake ni kuwa siku zote tutaishi kwa kutegemea mikopo (wenyewe wanaita misaada). Na hakuna njia nyepesi zaidi ya kuendelea kuwa maskini kama kutegemea mikopo. Simply ni kuwa katika kuishi hata individual, ukitegemea sana mikopo, hatimaye kila ulicho nacho kitachukuliwa. Mikopo tunayochukua kama nchi haiingii kwenye productive sectors, zinaingia kwenye service na kwenye luxuries kama magari, majumba ya fahari kwa viongozi, shoping za nje kwa viongozi n.k.

Mpaka tutakapofikia hatua kama taifa ya kuona tatizo la kuishi beyond our means, tutaendelea kuwa maskini na itafikia hatua wanaotudai watachukua kila tulicho nacho. Watu wanalalamikia sera za madini n.k. Lakini sera hizi zinatungwa kwa malengo ya kuwafurahisha wale wanaotukopa ili waendelee kutupa mikopo. Tukikataa hawatatupa mikopo na utakuwa ndo mwisho wetu, hili ndo Tatizo kubwa.

Kuishi juu ya uwezo wetu ndo tatizo kubwa. Serikali yetu inatumia fedha nyingi sana kuwalipa posho na marupurupu maofisa wake. Ni fedha chache sana zinazoingia kwenye mfumo unaozalisha. Hizi fedha wakishalipwa hawa watu huzitumia kununua vitu vya anasa ambavyo hatimaye havitozwi kodi!! Matokeo yake ni kuzalisha tabaka la Mamwinyi ambao kusema kweli lazima wawe ni watu waliokwisha fanya kazi serikalini tena kwa nafasi za juu. Hawa hujijengea mfumo wa kujizungusha (recycling) kwa kuhakikisha wanao ndo wanachukua madaraka wao wanapotoka.

Matumaini yetu yapo kwenye kuligundua hili tatilzo na kulifix. Ikiwa tutaendelea kuishi maisha ya juu kwa fedha za mikopo au misaada, hakuna matumaini asilani.
Mkuu kwenye hiyo blue nimekuelewa lakini kwenye nyekundu umenichanganya kidogo. kwa sababu tukikata ni kwamba hivyo ulivyotaja kwenye blue vitakosekana. je kukosekana kwa hivyo vya blue ndo kukwama kwa taifa kama ulivyobainisha kwenye nyekundu? fafanua kidogo.
 
GS,

Kwa hivyo wewe unaona tatizo ni uongozi na CCM pekee? what about you and I, what have we done to jikomboaring from Ulalahoi? are we obligated to wait for Serikali or new ruler? si heri turudie Ukoloni then Nyani Ngabu atapata trademark rights and super benefits for his thesis kuwa Miafrika Ndivyo Ilivyo and No Black Africa can never progress on its own?
SASA mkuu duniani kuna nchi ambayo raia wake wanaendelea kuliko/pasipo serikali yake? Sijawai kuona may be ianzie Tanzania. Maana ya kiongozi ni KUONGOZA. Wao wakitangulia raia wanafuata tu. Kuwa kiongozi vile vile kuna-element ya kuwa umeelemika relatively compared to wanakijiji kwaiyo wanategemea kutenda unayotenda na kuwaamuru wewe.Africa tatizo moja tu nayo ni mtu wa KUONGOZA.
 
Lini tutaondoka?: ni ngumu kubashiri time frame ...ya kuondokana na umaskini...
Namna gani tutaondoka? tuanze na hilo katika mjadala huu!
My opinion!
Kuna umaskini katika level mbili ya kwanza katika level ya mtu moja moja (individual level)-kuondoa umaskini huu ni kubadili tabia za watu kuhusu mazingira na raslimali zinazowazunguka..mtu akibadilika akatambua nafasi zilizopo katika mazingira yake ya kujipatia mali na kuzitumia bila kukosa umaskini wake binafsi utakwisha..kabisa mfano. mmasai mwenye ng'ombe 200 anaishi kimaskini wakati yeye ana vitu vyenye thamani ya mamilioni kwanini? tabia, mtazamo kutukufahamu..mkulima mwenye kulima na kuvuna mahindi gunia 200 kwa mwaka anaishi kimaskini wakati ana thamani kubwa kupita mfanyakazi ofisini...so "BADILI TABIA na TAMBUA FURSA ZILIZOKUZUNGUKA period!

Umasikin katika level ya taifa yafanyike yafuatayo:-
a) punguza matumizi ya serikali....ondoa bunge lote bakiza madiwan wanatosha kutunga sheria za nchi.., badili katiba kuwe na wizara si zaidi ya kumi hivyo mawaziri kumi tu..etc
b) corruption zero tolerence...kill, jail ..prosecute severely ..ifanyike kwa miaka 30 mpaka kizazi chote kifahamu hatari na adhari ya rushwa...
c) Vocational and skill training to all people (citizens)
 
Tupeleka macho yetu na akili kwa asilimia 80 ya wananchi wanaoishi vijijini kuona wanawezaje kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini. Nini kinatakiwa kifanyike ili hawa asilimia 80 watoke kwanza kwenye umaskini. Kwa maoni yangu, hao wakishatoka kwenye umaskini ndipo tunapoweza kuanza kuona mwanga wa kutoka kwenye kundi la nchi maskini duniani.
 
Tupeleka macho yetu na akili kwa asilimia 80 ya wananchi wanaoishi vijijini kuona wanawezaje kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini. Nini kinatakiwa kifanyike ili hawa asilimia 80 watoke kwanza kwenye umaskini. Kwa maoni yangu, hao wakishatoka kwenye umaskini ndipo tunapoweza kuanza kuona mwanga wa kutoka kwenye kundi la nchi maskini duniani.

Bibi Ntilie; Umezungumzia umuhimu wa kilimo sema umetumia lugha ya tofauti tu,sasa ulitakiwa kuuendeleza mjadala mbele...Kwamba ni kwa vipi tumeshindwa kwenye kilimo?
 
Back
Top Bottom