Tutakapotambua kuwa ustawi wa jamii sio wa mtu mmoja mmoja bali jamii nzima
Tatizo letu tumejawa na UBINAFSI aka U-MIMI na hili linatutafuna vibaya sana!
Kuanzia kwenye mitaa tunamoishi mpaka IKULU
1) Elimu: Kila "individual" anajitahidi kumpeleka mtoto wake "nje" kusoma badala ya kuchangia shule zetu za msingi, sekondari, na vyuo vikuu viwe kwenye kiwango stahili
2) Jamii: Mtu anajenga ghorofa halafu anatiririsha maji majafu barabarani
3) Watawala: Kila kiongozi anajitahidi kumiliki kiasi chochote cha mali bila kujali - eka 200 wakati hata kulima hajui wala hajawahi kufuga hata sungura!
4) e.t.c
Barabara..
Kuelewa kwanza how to overcome poverty is PARAMOUNT. Lakini what do u expect ktk taifa ambalo Rais, the head of state, hajui kwanini sisi ni maskini? Kaa hajui kwanini sisi ni maskini ataeza vipi kujua atatupeleka vipi kwenye promise land, kwene nchi ya maziwa na asali?
Umeongea suala la umimi..Hii ni kansa kubwa ktk dunia...Capitalism and capitalist forces..Umimi unasimamiwa na kuhubiriwa na unalindwa kisheria!. Ni vigumu sana kuelewa watu tunaezaje kupiga mbio za sakafuni (ambazo huishia ukingoni) ktk mazingira yanayoeleweka wazi kuwa capitalism is not the way forward kwa sababu haiwezi kuhakikisha maisha bora ya watu wote bali baadhi tu? .
Unaeza vipi kupiga vita
rushwa wakati capitalism inadai kuwe na winner mmoja tu na wengine wate wawe loosers...? Ndo maana rushwa ipo kila mahali, kuanzia wanaohitaji rushwa kukidhi mahitaji yao ya kibinaadamu mpaka wale wanaodai rushwa ya kujengea nyumba viamda!
Tunaezaje kukubali mfumo unaruhusu baadhi wa watu
wajukusanyie utajiri bila kipimo wala ukomo wakti tukijua kuwa utajiri ule unahitajika pia na watu wengine, at least ili kukidhi mahitaji yao ya kibinadamu?
Unaezaje kusema uchaguzi uwe na mshindi mmoja tu bila ya watu kutumia mbinu chafu? Unaezaje kuwa na chama kipo madarakani kwa miongo minne lakini kinaomba
kikamilishe miapngo yake ya maendeleo? Maendeleo ambayo hayaonekani? Unaezaje kuwa na maendeleo wakti vyama vya upinzani vinashindwa kuepa the most fundamental challenge ya kuelimisha wananchi na badala yake vinakimbilia kushiriki uchaguzi na kuendelea kuburuzwa left and right?
Unaezaje kuendelea huku rasilimali ukiwamilikisha wageni ili wachume na kujiendea zao, tena tunawapa na tax holiday kana kwamba sisi ni matajiri saana kaa masultan wa Brunei! Rasilimali zikiwa exhausted tutakuwa wageni wa nani? maana tangu exploitation iaenze hatuoni hata dalili ya maendeleo kwa watu wetu.