Mtani,
Nadhani la msingi ni elimu.
Elimu itakayomfanya Mtanzania aelewe:
- kuwa yeye ndiye aliyesababisha yeye mwenyewe na nchi yake kuwa maskini. Hata kama anaishi kwenye nyumba ya kiyoyozi, anafanyakazi kwenye ofisi ya kiyoyozi na anaendesha gari la kiyoyozi wakati ndugu zake wanaishi kwa mlo mmoja kwa pato la kulima banghi au mahindi ya msaada wa njaa.
- kuwa amekalia uchumi, yeye mwenewe kwa makusudi na hasa kwa ujinga wake ameacha nchi ifike hapa ilipo
- kuwa ni yeye ndiye anayetakiwa kusimama na kudai malipo sahihi ya madini yake, mazao yake, ardhi yake, rasilimali zake nk.
- kuwa ana haki ya kuuza mazao yake anayovuna kwa kilimo cha jembe la mkono popote pale bila kuwekewa vigezo. Kwani daktari aliyehamia Botswana amewekewa kigezo chochote? Mwanasiasaje, mbunge je, mbona anatanua bila hata kunawa?
- rasilimali za nchi ni za wananchi wenyewe.
- kura yake inahesabika na ni muhimu katika mstakabali wa nchi
- kuwa haitoshi kupiga kelele tu, inabidi watu wasimame na kuwatoa wanasiasa wakongwe ambao hawana jipya zaidi ya kuimalisha utawala na ugandamizaji wa koo zao.
- kuwa wakulima ndiyo wengi zaidi kwa hiyo mikakati yote ya maendeleo lazima iwalenge wao.
- kuwa mzazi mwenye uwezo anayejisifia kwa kumsomesha mtoto wake kwenye shule za kata ambazo kweli zina usajili wa serikali lakini hazina walimu, vitabu, maabara sembuse kuona, kunusa au kuwa karibu tu na hata gramu moja ya Potassium Permanganate, ni ujuha au upumbavu au dalili za utaahira. ... kwake mwenyewe na anayemwelezea kitu tofauti na hiki.
- kuwa elimu au uwezo wa kujitambua na kuelewa nafasi ya kila mtu ndiyo ufumbuzi wa matatizo yetu na siyo:
-- idadi ya mashangingi na helikopta kwenye kampeni za uchaguzi,
-- umahiri wa mwanasiasa kuongea na kutoa ahadi za uongo kuwa ndiye anafaa kuongoza milele
-- usomi wa kununua ili kuwakoga wakulima waliokosa elimu / pHD za uongo
-- idadi ya fulana na kofia za bure kwenye kampeni
-- idadi ya majengo marefu Dar, Mwanza, Arusha nk.
-- idadi kubwa ya wabunge bungeni
nk.
Mimi mtani naona elimu ndiyo inagomba. Hatuna elimu. Tena siyo hii elimu inayodaiwa na wengie ya ujuvi wa Kiingereza bali elimu yenyewe. Elimu ya dunia, siasa, jamii, utamaduni, miti shamba, kilimo cha kisasa, kilimo cha kijadi, utawala bora, haki, nk.