Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Bibi Ntilie; Umezungumzia umuhimu wa kilimo sema umetumia lugha ya tofauti tu,sasa ulitakiwa kuuendeleza mjadala mbele...Kwamba ni kwa vipi tumeshindwa kwenye kilimo?

Mushi,

Siamini ktk hii nadharia kwamba ili tuendelee tunahitaji asilimia 80 ya watz wajishughulishe na kilimo per se. Mi nadhani kungekuwa na mgawanyiko wa kazi / shughuli mzuri kulingana na suitability ya mahali, mfano, sehemu zenye maji ya kutosha zijishughulishe na kilimo cha mazao yanayohitaji maji ya kutosha, maeneo mengine kuna sources of fossil fuel, viekwe viwanda vyenye kuhitaji hiyo nishati, sehemu za maziwa na bahari ziekwe kwenye priority ya uvuvi, na shughuli za bandari, et etc. Nadhani awamu ya kwanza ambapo serikali ilikuwa inajitahidi kueka mgawanyo wa viwanda mathalan, vya nguo kwenye kilimo kikubwa cha pamba, katani kule Tanga etc, ilikuwa move nzuri, na at least tunaona kulikuwa na ka-vision ingawa hakakuwa realised in fully kwa sababu mbalimbali.
 
SASA mkuu duniani kuna nchi ambayo raia wake wanaendelea kuliko/pasipo serikali yake? Sijawai kuona may be ianzie Tanzania. Maana ya kiongozi ni KUONGOZA. Wao wakitangulia raia wanafuata tu. Kuwa kiongozi vile vile kuna-element ya kuwa umeelemika relatively compared to wanakijiji kwaiyo wanategemea kutenda unayotenda na kuwaamuru wewe.Africa tatizo moja tu nayo ni mtu wa KUONGOZA.

Zhule you are right.

Kama serikali haituongozi kwene muelekeo sahihi wa maendeleo aau ina ZERO inputs it is now, mie binafsi sioni kaa ina-legit reason ya kuepo.It is better kaa itaenda motoni PERIOD. Serikali inatarajiwa iwe 'mkono mrefu' ambao mtu mmojammoja hana ubavu au capacity ya kuazimia kutekeleza mambo fulanifulani. Ndio maana we need to be govern at national level by ONE ORGAN, nia ni kuwa na uniformity ktk njia ya kuyafikia maendeleo. Nilikuwa naangalia documentary moja mchina mmoja akasema hana haja ya kuipenda serikali yake bali anaiamni serikali yake. Ningependa siku moja na sisi watz tujivunie serikali yetu.
 
Swali hapa siyo "Ni Lini Tutaondoka kwenye Kundi ..." bali "Ni Vipi Tutaondoka kwenye Kundi ..."

Inavyoonekana hili la pili ni swali gumu zaidi kupata majibu, siyo?

Njabu the Dude,

Si kwamba hatujui vipi, bali tunajua sana ni vipi kuachana na Umasikini na ni jinsi gani ya kuondokana na Umasikini. Tatizo letu ni utashi kuamua kuanza kufanyia kazi, ndio maana nauliza ni LINI?

Kwa wengine,

Kwa nini tunaendelea kuwa kama fisi tukisubiri mkono uanguke ndipo tule? Kwa nini tudai ni mpaka CCM iondoke? Je isipoondoka?
 
Njabu the Dude,

Si kwamba hatujui vipi, bali tunajua sana ni vipi kuachana na Umasikini na ni jinsi gani ya kuondokana na Umasikini. Tatizo letu ni utashi kuamua kuanza kufanyia kazi, ndio maana nauliza ni LINI?

Kwa wengine,

Kwa nini tunaendelea kuwa kama fisi tukisubiri mkono uanguke ndipo tule? Kwa nini tudai ni mpaka CCM iondoke? Je isipoondoka?

Basi isipoondoka ndiyo tutakuwa hivi hivi! Hata kama una vision zako za kuachana na umaskini as an individual utawakuta CCM wamesimama wanakuzuia!!
 
Lini tutaondoka?: ni ngumu kubashiri time frame ...ya kuondokana na umaskini...
Namna gani tutaondoka? tuanze na hilo katika mjadala huu!
My opinion!
Kuna umaskini katika level mbili ya kwanza katika level ya mtu moja moja (individual level)-kuondoa umaskini huu ni kubadili tabia za watu kuhusu mazingira na raslimali zinazowazunguka..mtu akibadilika akatambua nafasi zilizopo katika mazingira yake ya kujipatia mali na kuzitumia bila kukosa umaskini wake binafsi utakwisha..kabisa mfano. mmasai mwenye ng'ombe 200 anaishi kimaskini wakati yeye ana vitu vyenye thamani ya mamilioni kwanini? tabia, mtazamo kutukufahamu..mkulima mwenye kulima na kuvuna mahindi gunia 200 kwa mwaka anaishi kimaskini wakati ana thamani kubwa kupita mfanyakazi ofisini...so "BADILI TABIA na TAMBUA FURSA ZILIZOKUZUNGUKA period!

Umasikin katika level ya taifa yafanyike yafuatayo:-
a) punguza matumizi ya serikali....ondoa bunge lote bakiza madiwan wanatosha kutunga sheria za nchi.., badili katiba kuwe na wizara si zaidi ya kumi hivyo mawaziri kumi tu..etc
b) corruption zero tolerence...kill, jail ..prosecute severely ..ifanyike kwa miaka 30 mpaka kizazi chote kifahamu hatari na adhari ya rushwa...
c) Vocational and skill training to all people (citizens)

That sound good Tuma, naona watu wanavyopigana humu hata kutuletea habari za wabunge, hamna kitu kule, kupotezeana muda na kutuletea umaskini tu.

Yaani hata bunge likiondolewa leo hii hutajua kuwa halipo au lipo!
 
SASA mkuu duniani kuna nchi ambayo raia wake wanaendelea kuliko/pasipo serikali yake? Sijawai kuona may be ianzie Tanzania. Maana ya kiongozi ni KUONGOZA. Wao wakitangulia raia wanafuata tu. Kuwa kiongozi vile vile kuna-element ya kuwa umeelemika relatively compared to wanakijiji kwaiyo wanategemea kutenda unayotenda na kuwaamuru wewe.Africa tatizo moja tu nayo ni mtu wa KUONGOZA.

Why not be the first one? Si ndio maana kuna kitu kinaitwa mapinduzi? Yalianza mapinduzi ya kuvumbua moto, yakaja ya viwanda na hata kilimo na sasa kuna ya fikra na hata teknolojia.

Kwa nini Watanzania wasiwe wa kwanza kufanya mapinduzi ya kujituma na kujiendeleza na kuiacha Serikali solemba?
 
Bibi Ntilie; Umezungumzia umuhimu wa kilimo sema umetumia lugha ya tofauti tu,sasa ulitakiwa kuuendeleza mjadala mbele...Kwamba ni kwa vipi tumeshindwa kwenye kilimo?

Mushi,

Kwani vijijini ni lazima shughuli za uzalishaji mali ziwe ni Kilimo pekee? Je hauwezi kupeleka viwanda na shughuli nyingine na kutumia internal cheap labour?
 
There are a million ways Tanzania can develop and move forward. The problem is we are trying a little bet of everything and ending up failing miserably. I say we should prioritize. What are the things most important and most urgent to us as a nation? After we prioritize we find ways to achieve success in the priorities. Make clear short term and long term plans which are implementable and stick to it! Siyo tuna sema "Kilimo kwanza" then there is nothing done about kilimo. Pinpoint the problems, make goals, implement. Tatizo tunaangalia urefu wa pua, nobody wants to see 10, 20 or 30 years ahead.
 
Naomba niwanukuu hawa ndugu zangu fulani (jina kapuni) ili kupanua wigo wa mjadala huu (tahadhari, nimewanukuu bila idhini ndio maana sikuweka wasifu wao)

Wa kwanza
Reverend

Tunahitaji kubadilisha sio tu fikra zetu bali pia namna ya kufikiri kuhusu suala la maendeleo. Kwenye kitabu changu cha CHANGAMOTO nimeongelea zaidi suala hili.

Kuhusu suala la maendeleo, tatizo letu ni kuwa hatujaweza kujitegemea kifikra na kimtazamo, bali tunatumia fikra za wakoloni mamboleo:

[URL="http://www.theurbanfly.com/Newz/what-is-development-colonialism-deconstructed"]http://www.theurbanfly.com/Newz/what-is-development-colonialism-deconstructed[/URL]

Wa pili
Mtani,

Nadhani la msingi ni elimu.

Elimu itakayomfanya Mtanzania aelewe:

- kuwa yeye ndiye aliyesababisha yeye mwenyewe na nchi yake kuwa maskini. Hata kama anaishi kwenye nyumba ya kiyoyozi, anafanyakazi kwenye ofisi ya kiyoyozi na anaendesha gari la kiyoyozi wakati ndugu zake wanaishi kwa mlo mmoja kwa pato la kulima banghi au mahindi ya msaada wa njaa.

- kuwa amekalia uchumi, yeye mwenewe kwa makusudi na hasa kwa ujinga wake ameacha nchi ifike hapa ilipo

- kuwa ni yeye ndiye anayetakiwa kusimama na kudai malipo sahihi ya madini yake, mazao yake, ardhi yake, rasilimali zake nk.

- kuwa ana haki ya kuuza mazao yake anayovuna kwa kilimo cha jembe la mkono popote pale bila kuwekewa vigezo. Kwani daktari aliyehamia Botswana amewekewa kigezo chochote? Mwanasiasaje, mbunge je, mbona anatanua bila hata kunawa?

- rasilimali za nchi ni za wananchi wenyewe.

- kura yake inahesabika na ni muhimu katika mstakabali wa nchi

- kuwa haitoshi kupiga kelele tu, inabidi watu wasimame na kuwatoa wanasiasa wakongwe ambao hawana jipya zaidi ya kuimalisha utawala na ugandamizaji wa koo zao.

- kuwa wakulima ndiyo wengi zaidi kwa hiyo mikakati yote ya maendeleo lazima iwalenge wao.

- kuwa mzazi mwenye uwezo anayejisifia kwa kumsomesha mtoto wake kwenye shule za kata ambazo kweli zina usajili wa serikali lakini hazina walimu, vitabu, maabara sembuse kuona, kunusa au kuwa karibu tu na hata gramu moja ya Potassium Permanganate, ni ujuha au upumbavu au dalili za utaahira. ... kwake mwenyewe na anayemwelezea kitu tofauti na hiki.

- kuwa elimu au uwezo wa kujitambua na kuelewa nafasi ya kila mtu ndiyo ufumbuzi wa matatizo yetu na siyo:

-- idadi ya mashangingi na helikopta kwenye kampeni za uchaguzi,
-- umahiri wa mwanasiasa kuongea na kutoa ahadi za uongo kuwa ndiye anafaa kuongoza milele
-- usomi wa kununua ili kuwakoga wakulima waliokosa elimu / pHD za uongo
-- idadi ya fulana na kofia za bure kwenye kampeni
-- idadi ya majengo marefu Dar, Mwanza, Arusha nk.
-- idadi kubwa ya wabunge bungeni
nk.

Mimi mtani naona elimu ndiyo inagomba. Hatuna elimu. Tena siyo hii elimu inayodaiwa na wengie ya ujuvi wa Kiingereza bali elimu yenyewe. Elimu ya dunia, siasa, jamii, utamaduni, miti shamba, kilimo cha kisasa, kilimo cha kijadi, utawala bora, haki, nk.

Wa tatu
Mtani,

Tanzania we have a generation problem. Hii haiishi leo wala kesho it is a combination of attitude and culture problem that is so deep in our minds and it is so difficult to see it.

Tunatakiwa mimi na wewe tubadilishe kabisa mawazo yetu na style ya maisha tunayoishi kama tunataka kufanya mabadiliko ya kiuchumi. Tuanze sasa hivi kuwaelemisha watoto wetu wanaozaliwa leo kuipenda nchi yao, tuwasomeshe ili wakikuwa accomplishment zao ziwe katika kuijenga nchi na wawe proud kufanya hivyo.

Asilimia 99.9 ya watanzania tumefundishwa toka tukiwa wadogo kuwa accomplishment katika life ni kuwa na gari zuri, nyumba nzuri, harusi kubwa na za gharama etc etc. Hizo ni baadhi ya problems za kizazi chetu, ni wachache mno wanaofikiri tofauti na mambo niliyataja, regardless of what, hata kama kuna umasikini as long wewe uko vizuri it is non of your business. Viongozi wetu wanafanyia watoto wao harusi za mamilio ya dollars wakati vijijini wanakotoka mjomba, shangazi hawana pesa hata ya mlo wa siku.

Tumeshuhudia watu safi kabisa na wapenda nchi lakini mara tu wanapopewa madaraka mambo ni yale yale. Hapa si suala la kuwa na resources au la, ni attitude kama hatutabadilika tutabaki kuwa pale pale. Hata huku tuliko ughaibuni watanzani utawajua tu we are very good kwenye harusi za gharama hata kama hatuzimudu, viji- functions vya kula na kujionyesha na kutaka kuonekana una gari zuri nyumba nzuri etc. Ndiyo sisi watanzania we need to change and stop complaining.
 
That sound good Tuma, naona watu wanavyopigana humu hata kutuletea habari za wabunge, hamna kitu kule, kupotezeana muda na kutuletea umaskini tu.

Yaani hata bunge likiondolewa leo hii hutajua kuwa halipo au lipo!

Yes mkulu Wabe, ze bunge is a useless distraction.

Kwanza lipo toothless, pili linatawaliwa na UCHAMA badala ya FACTS. Tatu lina watu wanaotaka kuhoji vitu wasivo na ujuvi navyo.

Ukiangalia kwa makini mamilioni ya fwedha za wavuja jasho yangeweza kuokolewa kwa kuscrape maigizo ya pale Dodoma, na kamati za kuchukua posho mara mbilimbili BILA OUTPUT.

Naamini kungekuwa na nia njema, watendaji ktk wilaya wangekuwa wawakilishi tosha kabisa wa wananchi kwa sababu kwanza wana ilmu kuhusu fani zao, pia wana madiwani huko ambao huwa-bombard maswali ya msingi kabisa kuhusu maeneo yao.

Labda ktk national level kungekuwa na system ingine ya check and balance kwa mikakati ya kiserikali ambayo ipo ktk national level. Lakini tulivo sasa hakuna nia njema na kila mtu anataka a-capitalize kwa kupitia siasa..
 
Never! Ni nchi gani ya Black Africa isiyo kwenye kundi la nchi za dunia ya tatu? Do you see a pattern here...?

Kinachotuweka na kuendelea kutushikilia kwenye kundi hilo pamoja na mambo mengine ni mawazo ya aina kama yako.
Watu wote wakiondokana na mawazo kama yako, tukajipanga vizuri kwa kuweka viongozi wenye fikra za kimaendeleo, wasiojali maslahi binafsi kama waliopo sasa, watz tuondoe fikra za kusaidiwa hata mambo tunayoweza, then twaweza kupiga hatua kutoka huko.
 
Tutaondoka kwenye lindi hili la umaskini kama tutawachagua viongozi serious na kuwawajibisha wale wanaoshindwa kupafomu inavyotakiwa..and CCM lazimaitoke madarakani.

Je wanachi tumejitayarisha vipi kutoka steji moja kwenda nyingine? Kwa mfano ukienda ofisi za serikali katika watu 10 wanaofanya kazi 2 wengine ni semina , warsha kongamano, maonyesho ya sabasaba, nanenane, utumishi wa umma , siku ya sheria, watoto , wastage of time left right and centre. Attitude ya wafadhili, wawekezaji toka nje bado tunayo. Ukija kwenye utekelezaji utasikia tunahitaji fedha wakati fedha tunazo nyingi tu ila hatujui jinsi ya kuzipata kutokana na resources zilizopo, na hizo chache tunazozipata hatuna priority na matumizi yake.

Nenda wizara ya ardhi uone madudu nenda Brela ( Msajili wa makampuni) kitu cha dakika kumi kitachukua mwezi hata wangekuja democrats au republicans with that kind of attitude sidhani kama tunaweza kusogea hata sentimita moja. mawazo ya wananchi lazima yawe propgressive kwanza halafu mengine yatafuata.
 
Mkuu wa kaya mwenyewe alisema anashangaa?, ila mafanikio ya nchi yanatokana na mafanikio ya mtu mmoja moja, namaanisha kila mtu akifanya bidii kujiinua kimaisha,kisha tukawa na wananchi waliojiinua kimaisha inamaanisha itakua nchi yenye mafanikio
 
Kishoka,Abdulhalim et al;
Ni vipi tena wakuu?Asilimia kubwa ya raw materials si zinatoka shambani?Pia si lazima viwanda vifunguliwe huko vijijini,tunaweza kufungua processing plants,pia bidhaa za vyakula si lazima ziwe proccessed?Bi lazima investment ziwe mahali watu wapo otherwise mtaanza kuhamisha hamisha watu kaa vijiji vya ujamaa ama kuinvsest "Mijini" mifukoni mwa mafisadi?Ama mkisikia kilimo nyie ni mahindi na maharagwe pekee?
Kwa kifupi bidhaa ambazo raw materials zake hazitoki shamba ni chache sana!na hayo mambo ya kilimo persee ndugu Abdulhalim yametoka wapi ?
Pointi yangu ya msingi ni kwamba ni lazima tu invest vijijini.ni lazima tuanzie huko,hizo bidhaa mnazosema viwanda vianzishwe huko mnakotaka nyie ni nani atanunua kama asilimia 80 ni masikini?Ama ni uchumi wa mafisadi kwa mafisadi mnataka muuendeleze?
 
Tatizo la umaskini tz sio Jk bali ni misingi mibovu:baada ya uhuru tunaambiwa na tunaambiwa kwa upande waisla, kwa kuano education hawakupata nafasi ya kutumikia ja,ii: kanisa likachukua nafasi ya uongozi; umaskini ukaanza; rushwa ikaanza na ikapea na ikashinda; sasa maaskofu wanalia na kulaumu wanasiasa wa sasa na kusahau kua chanwo cha rushwa ni wao educqted kuzuia: kama kanisa kupitia waumini wake ambao tunaambiwa vipanga shuleni wangalikuwa waadilfu na kuwz na maadili basi rushwa isingefikia hapa:

sasa mkuu si utulie kidogo ili tukuelewe.
 
Akili zako zinaonekana ni za kushikiwa ndiyo maana unaandika vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Kama nchi yetu ni maskini inakuwaje basi Kikwete analipwa mshahara mkubwa kama wa nchi tajiri pamoja na Wabunge na mawaziri na marupurupu chungu nzima? Hebu acha kuandika upumbavu wako hapa!
 
Tatizo la umaskini tz sio Jk bali ni misingi mibovu:baada ya uhuru tunaambiwa na tunaambiwa kwa upande waisla, kwa kuano education hawakupata nafasi ya kutumikia ja,ii: kanisa likachukua nafasi ya uongozi; umaskini ukaanza; rushwa ikaanza na ikapea na ikashinda; sasa maaskofu wanalia na kulaumu wanasiasa wa sasa na kusahau kua chanwo cha rushwa ni wao educqted kuzuia: kama kanisa kupitia waumini wake ambao tunaambiwa vipanga shuleni wangalikuwa waadilfu na kuwz na maadili basi rushwa isingefikia hapa:

Haya sasa...

Malaria Sugu si kitu ya mzaha jamani!...Ogopa sana!

We juzi si ulisema kwa udi na uvumba kura yako ni kwa kikwete?...Sa shida yako nini?
Kaa utulie bana!
 
I think someone here would need brain surgery sooner than later!
 
walisema ccm ni ya waislamu na kwamba wao ndo wengi kwenye uongozi kwa sababu ndo waanzilishi. zamani hizo anazoongelea ilikua chama kushika hatamu ya uongozi yaani ndo ilikuwa dola. sasa yake hayo mbona ni kinyume.
 
Back
Top Bottom