Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Hiyo ni tabia ya magovi
 
Hapanaaaa sina urafiki na hao wanyama awe nyau au mbwa sitaki urafiki nao
 
Huko mambele unapewa kesi vizuuri kabisa. Yani umpige mnyama kimaanda maandazi tu[emoji2]

Wenzetu wapo mbele sana
Kweli wako mbele Sana,yaani wao mtu kuoa mke wa pili haikubaliki kabisa lkn dume akioa dume mwenzake inakubalika kabisa na hapo wanasema haki za binadamu zimezingatiwa.
 
Whaat!
ulimkamata Mtoto ukampeleka kwa Mbwa amng'ate!!

hii ya kwako imevuka mipaka aiseee na Mtoto ana Makovu ya kung'atwa na Mbwa!![emoji15]

dude! ni Mtoto kama Mtoto au alikua Mtu Mzima Kibaka!!??
 
Tatizo ni kule kusema 'Watanzania' wako hivi na vile. Wale uliowaona ni asilimia ngapi ya Watanzania wote? Na ulitembelea nchi ngapi zingine ukaona hawafanyi hivyo? Pale tu ukilinganisha asilimia ya wanaofanya hivyo Tanzania ukaona ni kubwa zaidi ya nchi nyingine ndipo unastahili kushutumu Watanzania kwa ujumla. La sivyo, ishia kusema binadamu tunakosea kufanya kadhaa. Siyo kuwabagua Watanzania kama vile una uhakika ni wao tu ndiyo wanaofanya hivyo wakati raia wa nchi nyingine hawafanyi.
 
Niliua paka mwenyewe tena kwa kutumia kwanja ndani tulikimbizana nikakata mguu alijikunyata mahala nilipiga kwanja kadhaa za kichwa mpk akafa nikazika.

Wanyama ni wazuri ila wakila mifugo yetu kama kuku ni hatari sana.
 
Good!
Lesson learnt the hard way!
 
Inatokana na malezi mabaya. ni kiashiria cha jamii yetu kulea kwa ukatili na unyanyapaa. Tabia hii mbaya haitofautiani na ile ya kurushia mawe na pingili za miti mwembe uliopamba maembe.
 
Ni kithibitisho kwamba waafrika wengi bado hawana utu na huruma pia hawajastaarabika.
 
Ukitaka kujua wabongo wengi ni sadists angalia wanavyoshangilia raia wa Ukraine kuuwawa wakati karibu dunia yote inasikitishwa na mauaji yanayoendelea huko.
Binafsi sifurahishwi kabisa na mauaji dhidi ya raia wasio na hatia huko Ukraine. Lakini siungi mkono unafiki na undumilakuwili unaooneshwa katika huu mgogoro. Halafu unapenda sana kuwasema vibaya wabongo, una tatizo nao gani? Ma Sadists wapo dunia nzima.
 
Binafsi napenda viumbe hai, nikimkuta nge porini ambapo hakuna watu nimuue ili iweje? ninafuga mbwa na nawapenda sana,mbwa wangu akizaa huwa simpatii mtu watoto hovyo, nikikuhisi utawatesa jua umewakosa sikupi hata kama utumie lugha gani .
Safi sana kiongozi. Hata mimi
 
kwetu Tanzania hakuna haki za wanyama wafugwao, pets
Zipo za Veterinary Animals welfare Act 2003, lakini hata Polisi hawazijui. Mtu ananing'iniza kuku kwenye baiskeli na kuendesha mjini kuwauza, mtu anamshindisha kuku njaa barabarani kwenye jua kali na anamnyanyua kila gari linapopita eti ni biashara. Ukatili, ukatili, UKATILIII.
 
Sasa na wewe ulifanya nini sasa? Unamuonea huruma Mbwa lakini unamfanyia ukatili Mtoto.
 
Hapanaaaa sina urafiki na hao wanyama awe nyau au mbwa sitaki urafiki nao
Basi bro. tafuta mahali ambapo hawapo uishi wewe. Kumbuka wewe binadamu u mavumbi na mavumbini utarudi. Dunia ni yetu wote- wanyama ,ndege na vyote viijazavyo nchi na ni mali ya Aliyetuumba. Acha roho mbaya ya ubaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…