Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Hawaitwi kunguru
Kwa hiyo Kosa lao ni jina Kunguru? Kwa hiyo ww ukienda kule Songea ukamkuta jamaa anaitwa Kunguru (Majina hayo yapo kule) na ikatokea amepita mbele yako basi jiwe litamhusu? Tukubaliane hapo.
 
Naona mnaongea sana,hamjawahi kuishi geto...huna kitu na vidagaa vyako amekula Paka unakutana naye mlangoni anatoka........wengi mnaongelea Paka aliyefugwa Kwa kufundishwa......Sasa hawa wanyama wetu hawa mimbwa koko na mipaka inapambana na binadamu ,vita lazima iwe kali sana.....
 
Naona mnaongea sana,hamjawahi kuishi geto...huna kitu na vidagaa vyako amekula Paka unakutana naye mlangoni anatoka........wengi mnaongelea Paka aliyefugwa Kwa kufundishwa......Sasa hawa wanyama wetu hawa mimbwa koko na mipaka inapambana na binadamu ,vita lazima iwe kali sana.....
🤣 🤣 🤣 Nimecheka sana. Eti vidagaa vyako amekula paka unakutana naye mlangoni anatoka...🤣
 
viumbe hivi tumepewa mamlaka ya kuvitawala kwa haki na sio kuvinyanyasa ama kuvitesa, viumbe hivi kuvifanyia ubaya ni sawa na kumtemea mate usoni Muumba wetu alietuumba sisi na hivyo viumbe. Hata Biblia imeweka wazi sehemu nyingi juu ya kuwajali wanyama, Kwa upande wa uislam Mtume (pbh) alikuwa na paka wake aliemjali sana alimwita "Muezza"

kuna hizi tabia mbaya sana zimezoeleka na watanzania wengi kwa wanyama [emoji116][emoji116]

-unakuta tu mtaani mbwa anajipitia zake, mtu anaanza kumrushia mawe.

-nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!! aende wapi sasa wakati hapo ni kwao ?

-Mtu kashiba nyama, anaenda kuitupa badala ya kumpa paka mwenye njaa,

-kuku yupo bize anatafuta chakula, mara mtu anaanza kumkimbiza tu bila sababu.

-Mbuzi ameletwa kwajili ya sherehe, usiku umefika anaachwa ukutani badala ya kumweka hata stoo aweze kupumzika, kujikinga na baridi, mvua, n.k.

-usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.

-Dume limempanda jike, mtu anaanza kuwarusha mawe.

-mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga.

-Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kutembea inakuwa shida lakini mtu wala hajali.

-Mbwa kila usiku anakulinda wewe, familia yako na mali ila kibanda chake hakijasafishwa mwaka mzima kimejaa viroboto, chakula chake ni makombo kila siku, yani mtu hajiongezi hata kumpa nyama mara moja kama shukrani ya ulinzi anaompa.


Hivi hawa wanyama wanakosa lipi?
"-Dume limempanda jike, mtu anaanza kuwarusha mawe.,,"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wakiwa wamenatana matako [emoji240] wanakuwa ata kujitetea hawawezi

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Ametunga hii story sidhani kama ana roho chafu kiasi hicho ingawa binadamu anafanya mengi

Watoto hawajui kitu wanatakiwa kufundishwa maadili
Yaani umtupie mtoto mbwa je kama angemuua?
Halafu eti Polisi wakaiacha kesi iishe tu

Hakuna ukweli hapo
Labda kama ametunga sawa ila kuna watu humu wanaona eti ni sawa tu
 
Labda kama ametunga sawa ila kuna watu humu wanaona eti ni sawa tu

Hao wana malezi mabaya tangu mwanzo

Unajua humu kuna wazuri na wabaya pia kuna majambazi sugu, na kila aina ya watu kama tunaowaona live
Wala sishangai kwa ukatili huo na mtu anasapoti
 
Kwa hiyo Kosa lao ni jina Kunguru? Kwa hiyo ww ukienda kule Songea ukamkuta jamaa anaitwa Kunguru (Majina hayo yapo kule) na ikatokea amepita mbele yako basi jiwe litamhusu? Tukubaliane hapo.
Ndio apite tu mbele
 
umenikumbusha utotoni nilkua na hyo tabia ya kuwinda mijusi na kuifanyia operation kwa kiwembe, akifa naenda kuzika..nilitenga kabisa makaburi na mochwari ya mijusi.

Nilkua katili kwa wadudu yani walikua wakiniona wanaanza mbio...ila cha kushangaza kwenye ndege na wanyama hawa nilkua na huruma nao sana.Nilkua siwezi kuchinja kuku kabisa, walikua wakichinja kama kuku namjua nilkua nalia hatari [emoji23] , bora nifuge kuku mpaka afe mwenye kuliko kuchinja.

Siku hizi niko peace na viumbe hai sipendi kuvidhuru, nikiona watu wana piga wanyama najisikia vibaya niko radhi nikule hela uache kumpiga huyo mnyama.

Kuna siku nilkua natoka kwenye mishe zangu maeneo flani hivi nikakutana na mzee fulani alikua watoto wameshika mbwa wawili mmoja mkubwa kengine kadogo, cjui hata hao mbwa waliwakosea nini.

Walikua wanataka kuwaua kwa kuwa nyonga ( just imagine ) kwanza hao mbwa walikua wamesha chapika hatar...pona yao ilikua ni mimi kutokea.

Niliwaomba wasiwadhuru hao mbwa lakin wapi mpaka nikatoa buku ten nikampa huyo, uzur alkua ni choka mbaya alikubali akanipa hao mbwa.

Niliwahudumia hao mbwa asee jinsi nilivyo wakuta na walivyo kuwa ni vitu viwili tofauti.Na huyo mbwa mkubwa kumbe alkua na mimba siku alivyozaa cjui alifuata nini barabarani akapigwa tairi na gari la wagonjwa akafa.Aliacha vitoto 6 vidogo hatar hata havioni kasheshe ikawa ni kuvilea, sema nilipambana navyo mpaka vikakua vikubwa.

[emoji256][emoji256][emoji256]
 
Na wenzetu wanawapa mpaka Vitamins Mbwa na matangazo kila kona
IMG_6373.jpg
 
Lakini usisahau. Unaweza ukaenda na hasira zako kwa nia ya kutia vilema wote yeye na mbwa wake halafu kibao kikageuka na ukajikuta wewe ndo unatiwa kilema. Hilo pia linawezekana au vp. Hasira Hasara.
Kweli ndio maana ukajiita kirumberumbe Yani ulitaka nikafungue jarada la kesi au ulitaka nikaanze kumuomba msamaha,bullshit!!!
Yani na huo mtaa angehama kwa mudA Kwanza labda isiwe kijana wangu aliyefanyiwa hivyo
 
Kweli ndio maana ukajiita kirumberumbe Yani ulitaka nikafungue jarada la kesi au ulitaka nikaanze kumuomba msamaha,bullshit!!!
Yani na huo mtaa angehama kwa mudA Kwanza labda isiwe kijana wangu aliyefanyiwa hivyo
Hapana mkuu; Sikutaka lolote kati ya hayo mawili bali Nilitaka tu utumie busara na hekima kuli-handle hilo suala . Ni hayo tu.
 
Ila mapaka yanadharau sijapata kuona, linaweza kukukata jicho kwa dharau likakupandisha na kukushusha halafu likamalizia kwa kukusonya[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom