Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Tatizo baadhi ya wanyama wakishakuwa kwa binadamu huwa wanajiona kama binadamu kweli, huwa wanawaletea dharau wanyama wenzao hata binadamu ambao mifukoni ni apeche alolo.
Sasa binadamu akishaona mnyama analia mbele yake, yeye anajistukia, anahisi mnyama anamn'gong'a kwa sababu hana hela. kinachofuata ni teke kubwa sana au jiwe.
[emoji23]
 
Hebu chukulia mfano yanayoendelea Ukraine, mtu unamkuta anaenda kutafuta hifadhi pamoja na mnyama wake, leo hii sitashangaa hapa kwetu mtu akihamia hata mtaa wa nne basi atamtelekeza mbwa wake.

kuwatesa wanyama ni kumtemea mate usoni Mwenyezi Mungu alieumba viumbe vyote,

kuna hizi tabia mbaya sana zimezoeleka na watanzania wengi kwa wanyama 👇👇

-unakuta tu mtaani mbwa anajipitia zake, mtu anaanza kumrushia mawe.

-nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!! aende wapi sasa wakati hapo ni kwao ?

-Mtu kavimbiwa nyama, zile zilizobaki ambazo hata hajazila anaenda kutupa badala ya kumpa hata mbwa au paka wanaeishi nae

-kuku yupo bize anatafuta chakula, mara mtu anaanza kumkimbiza tu bila sababu.

-Mbuzi ameletwa kwajili ya nyama ya sherehe, usiku umefika anaachwa ukutani, yani mtu hata hajali kama kuna baridi, mvua, mbuzi angalau apumzike vizuri siku yake ya mwisho, n.k.

-usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.

-Dume limempanda jike, mtu anaanza kuwarusha mawe.

-mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga.

-Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kutembea inakuwa shida lakini mtu wala hajali.

-Mbwa kila usiku anakulinda wewe, familia yako na mali ila kibanda chake hakijasafishwa mwaka mzima kimejaa viroboto, chakula chake ni makombo kila siku, yani mtu hajiongezi hata kumpa nyama mara moja kama shukrani ya ulinzi anaompa.


Hivi hawa wanyama wanakosa lipi?
sasa mtu hataki ngombe wale uroda anapiga mawe 😀
 
Hii haina tofauti na wale watanzania pale kivukoni wakishashuka kwenye ferry wanaanza kukimbia, bc ujue matatizo na shida ndiyo yanawafanya watu waheuke wafanye mambo kama hayo.
Kukimbia kwa pale kivukoni ni jambo la kihistoria na mazoea zaidi.

Kama ushafika Dar es salaam zamani na kufika kivukoni tambua zamani magari yalikua ya shida sana na daladala zilikua zinapaki right after lango la panton, basi watu walikua wakishuka tu ni mbio kuwahi daladala.

Ila kwa sasa kituo kipo mbali na bado utamaduni ukabaki ule ule....
 
Kukimbia kwa pale kivukoni ni jambo la kihistoria na mazoea zaidi.

Kama ushafika Dar es salaam zamani na kufika kivukoni tambua zamani magari yalikua ya shida sana na daladala zilikua zinapaki right after lango la panton, basi watu walikua wakishuka tu ni mbio kuwahi daladala.

Ila kwa sasa kituo kipo mbali na bado utamaduni ukabaki ule ule....
Ndo umaskini wenyewe huo na sio wote wanakimbilia usafiri.
 
Elimu unahitajika sana kwenye hili, kwa Tanzania wanyamq wanayimwa haki zao ni mwendo wa cheos Kila kona
 
Akili yako haipo sawa, yaan mtoto anafanana na mbwa?? Hao wazazi labda ni masikini sana ila ingekua mm show ungeipata vzur
Mbwa wangu ni muhimu kuliko mtoto wa watu anayetafuta matatizo ya kujitakia. Una shida na hili pia?
 
Sasa mbona wewe ndio mkatili kuliko hata hao wanaopiga wanyama?unamuingiza mtoto ndani ili ashambuliwe na mbwa?hio ni akili kweli?

Hao watoto ilikuwa ni kuwaelimisha tu,angalau kama ungekuwa na hasira basi Kofi moja lilitosha kutoa funzo ukaachana nae.
Ni kwa sababu nilishawachoka awa watoto. Nilishawakataza mara kibao na kuwalalamikia wazazi wao lakini hakuna walichpkifanya kwani bado watoto wao wanazidi kuongezeka na kuwapiga walinzi wangu. Dawa pekee ya kuondoa huu ujinga ni ukatili tu, wembe kwa wembe. Na toka nifanye vile kwa yule mtoto inakaribia mwezi sasa hajakuja mjinga yeyote hapa nyumbani zaidi ya kunguru kuwaudhi hawa mbwa.
 
Nikikumbuka mbwa wangu watatu niliowapoteza kwa kulishwa sumu dah ni zaidi ya maumivu tena wote walikufa siku moja..
 
Back
Top Bottom