kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watoto na wajukuu wa viongozi wakuu wa umma (Rais, Marais wastaafu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge, wakurugenzi wa wilaya, wakuu wa mashirika ya umma, wakuu wa chama tawala, nk) hawako kwenye shule za umma wanazozijenga na kuziongoza kwanini? Ni watoto na wajukuu wa wakulima, wafugaji na watumishi wadogo wa umma wanaosoma kwenye shule za umma. Kuna nini kwenye shule za umma? hakuna nini kwenye shule za umma kulinganisha na shule wanakopeleka watoto wao? Ni sawa?
Hali hii iendelee hivihivi au kuna kitu kifanyike?
Hali hii iendelee hivihivi au kuna kitu kifanyike?