Hizo zisizo za umma nani atasoma sasa kama wote wakienda huko?!Watoto na wajukuu wa viongozi wakuu wa umma (Rais, Marais wastaafu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge, wakurugenzi wa wilaya, wakuu wa mashirika ya umma, wakuu wa chama tawala, nk) hawako kwenye shule za umma wanazoziongoza kwanini? Ni watoto na wajukuu wa wakulima, wafugaji na watumishi wadogo wa umma wanaosoma kwenye shule za umma.
Hali hii iendelee hivihivi au kuna kitu kifanyike?
siku moja nyuma nilikwenda ofisini kwa mo, nikakuta maji ya kunywa ya chupa ya brand nyingine badala ya maji yake ya masafi. Tangu siku hiyo na mimi niliyakataa maji ya masafi maana sikujuwa yalikuwa yana nini hadi mwenye nayo hayanywi.Hizo zisizo za umma nani atasoma sasa kama wote wakienda huko?!
Mkuu kiswahili ndio lugha ya taifa kufundishwa shuleni ni wajibu,lakini kujifunza lugha ya kiingereza kama tunavyojifunza katika masomo mengine kama hesabu,chemia na mengine kwa kuwa kiswahili ni changa hahijitosherezi kwenye nyanja nyingine.Kuna siku wabunge walichachamaa kweli lugha ya kisawahili iendelee kufundishwa primary, eti tutapoteza utamaduni wetu, nikacheka sana maana najua hakuna mtoto wa mbunge anayesoma huko, wanawachora wananchi tu
Dawa sio hiyo, bali dawa ni watoto na wajukuu wa Rais na mawaziri lazima wasome shule zao hizihizi wanazozijenga na kuzisimamia. Wakati wa Nyerere tulisoma na watoto na wajukuu zake.Dawa yake kila mzazi asomeshe shule za private za umma zitakufa zenyewe kifo cha mende
Mkuu namaanisha masomo mengine kama sayansi kufundishwa kwa mtaala wa kiswahili, afu wakifika form 1 wanabadilishiwa GIA anganiMkuu kiswahili ndio lugha ya taifa kufundishwa shuleni ni wajibu,lakini kujifunza lugha ya kiingereza kama tunavyojifunza katika masomo mengine kama hesabu,chemia na mengine kwa kuwa kiswahili ni changa hahijitosherezi kwenye nyanja nyingine.
Matokeo yake hata kazi ya udereva vijana wetu kupata kazi Saudia,Iraq,Bahrain,Kuwait, Qatar, UAE,hawapati kwa kuwa communication skills wanataka English tena basic.Lakini Kenya na Uganda wako madereva kwa maelfu.