Kwanini watoto wa viongozi wa umma hawasomi shule za umma?

Kuna siku wabunge walichachamaa kweli lugha ya kiswahili iendelee kufundishwa primary, eti tutapoteza utamaduni wetu, nikacheka sana maana najua hakuna mtoto wa mbunge anayesoma huko, wanawachora wananchi tu
Gen Z mko wapi?
 
WANASOMA SHULE ZA VIJIKO VIKUBWA VYA KUPAKULIA MBOGA
 
kwa kodi zetu
 
WANASOMA SHULE ZA VIJIKO VIKUBWA VYA KUPAKULIA MBOGA
Halafu watoto wetu ndiyo wanasoma kwenye shule wanazolishwa kande/ugali maharage wakati wa mchana, baada ya sisi wazazi kuchangishwa debe mbili za mahindi, na debe moja la maharage pamoja na elfu 20-50 kwa mwaka.
 
Kwanza niulize,
Hivi watoto wa Hayati Mwl.J.K.Nyerere walisoma shule za umma?.
Mimi nikiwa rais watoto wangu watasoma shule za umma zikiwemo hizi za kata(kwa sekondari).
 
wanatufanya wajinga kwelikweli. Eti mbuga zetu, misitu yetu, madini yetu, gesi yetu, bandari zetu, biashara zetu na kodi zetu vyote hivi havitoshi kutoa elimu nzuri ambayo hata watoto wao wanaweza kusoma humo. Halafu wanatuomba kura sisi mabwege na sisi mabwege tunatoa kura. KAMA CHAKULA WANACHOTUPIKIA NI KIZURI NA SALAMA BASI TULE NAO SAHANI MOJA.
 
Ongezea na hii

Alafu haohao wakuu ni wanaotunga sera na ndio wafanyao mabadiliko ya mifumo ya elimu.

Mwisho wa siku changamoto za elimu yetu wanaokuja kuumia ni watoto wa maskini. Wakati huo wakwao wapo South.
 
Kwa sababu zina viwango duni ukilinganisha na zile binafsi
 
Kuna mzazi asietaka kumsomesha mtoto wake shule nzuri?
 
Ndio hao Kila siku wanalazimisha lugha ya kufundishia shule za umma iwe kiswahili alafu wao watoto wao wanawapeleka English Media
 
Kwanza niulize,
Hivi watoto wa Hayati Mwl.J.K.Nyerere walisoma shule za umma?.
Mimi nikiwa rais watoto wangu watasoma shule za umma zikiwemo hizi za kata(kwa sekondari).
Huna hela wewe tafuta hela utoe mentality ya kimasikini,
Yaani uwe Rais mwanao akasome shule ya msingi Mwembetogwa B au Kunduchi then umpeleke
Gerezani secondary school?
Aweeee aweeee wozaa!
😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…