Kwanini watoto wa viongozi wa umma hawasomi shule za umma?

Kwasababu ni viongozi wa umma
 
Huna hela wewe tafuta hela utoe mentality ya kimasikini,
Yaani uwe Rais mwanao akasome shule ya msingi Mwembetogwa B au Kunduchi then umpeleke
Gerezani secondary school?
Aweeee aweeee wozaa!
😁😁
Atafute Hela ampeleke mtoto shule kwasababu niyeye aliyesababisha awepo duniani Hilo swali wengi wameliuliza hakuna jibu kwasasa jibu Zuri litakuwa la uchochezi
 
Lakini pia Tanzania viongozi wengi ni wazee

Walishamaliza kusomesha
 
Ili shule za umma zirudi kwenye ubora iwepo sharia kuwa watoto wa viongozi kuanzia rais, waziri, RC, DC na DED wasome shule za serikali.

Vv
 
Nani amlete mwanae shule ya umma ya Tanzania?
Ili
1. Achapwe hovyo na kuonewa na walimu.
2. Afundishwe na walimu vilaza. (Baadhi)
3. Atukanwe, adhalilishwe na kusemewa maneno mabaya anapokosea ili akose confidence.
4. Abanane kwenye samani chache zilizopo.
5. Akutane na watoto wa wazibua vyoo, mama ntilie na hohe have kama hao badala ya kukuza network ya marafiki waliozaliwa na vijiko vya shaba midomoni wenye wazazi wanaomiliki uchumi.

Shule za umma zina hali mbaya.

Mtu yeyote mwenye uwezo lazima amuepushe mwanaye na hiyo dhahama.
 
Kila mtu ana haki ya kusoma shule anayotaka,
Kisa baba angu waziri ndio nisome shule ta Umma, hata kama nataka Feza ?
 
Wanasomea walikowekeza wazee🫠
 
Hata hao ma teacher wenyewe,wanawapeleka watoto wao private schools.
Vya dezo vinatesa
 
Hizo shule wanapelekwa kwa ajili ya usalama wa watoto wa Viongozi wetu wazalendo
Mara nyingi viongozi wanaokuwa na maadui wengi
huwezi kuwaweka na watoto wa maskini wasiovaa hata viatu hakuna chakula Wenye chuki na hasira kwa ajili ya ugumu wa maisha
Ni rahisi kuwadhuru watoto wa Viongozi

Alisikika kiongozi mmoja akitetea hoja πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Ukishangaa ya Musa,Mbowe na Lissu watoto wao Wana Uraia wa Marekani,halafu wanataka sisi watoto wa Masikini tufe kwaajili ya Nchi yetu,ila ndio Africa unafiki Jadi yetu...

George Weah wakati anatawala Liberia,mtoto wake alikua ana uraia wa Marekani,and anachezea timu ya taifa ya ya football Marekani,

Mjukuu wa Nyerere(Chief rocker) wakati anasoma,alikua na Hela kuliko mapedeshee,..
 
Mbona sisi tulisoma nao Azania na Tambaza na haikuwa shida? Kama kuna hofu basi watawala wawajibike maana wao ndio chanzo.

Vv
 
Kwanza niulize,
Hivi watoto wa Hayati Mwl.J.K.Nyerere walisoma shule za umma?.
Mimi nikiwa rais watoto wangu watasoma shule za umma zikiwemo hizi za kata(kwa sekondari).
WAMESOMA SHULE ZA UMMA. MIMI NILISOMA SHULE MOJA NA KUKAA DAWATI MOJA NA MTOTO WA WAZIRI WA ELIMU MUNGAI, MTOTO WA MKUU WA WILAYA BW. KILIVATA. LEO HII HATA MTOTO WA DIWANI HASOMI SHULE HIZO, LAKINI WAKATI WA KAMPENI
Huwa nina mashaka makubwa sana na uzalendo wa viongozi wetu wengi.
Mfano waziri wa fedha.
Kuna dhambi nyingine wanaofanya hawa watunga sera na watunga Sheria wetu kwenye elimu. Watoto wao hawasomi shule za msingi na sekondari za umma lakini wanasoma kwenye vyuo vikuu vya umma vyenye unafuu wa ada. Hivyo watoto na wajukuu wanakwenda shule za private ili kupata ufaulu mkubwa ambao watautumia dhidi ya watoto wa walalahoi kupata nafasi ya kuingia vyuo vikuu vya umma vyenye ada ndogo na walimu wengi na scholarships mbalimbali zinazolenga watoto wenye ufaulu mkubwa. Hivyo wanatangeneza tabaka la walalahoi wa milele na walalahoi.
 
Wao
Ongezea na hii

Alafu haohao wakuu ni wanaotunga sera na ndio wafanyao mabadiliko ya mifumo ya elimu.

Mwisho wa siku changamoto za elimu yetu wanaokuja kuumia ni watoto wa maskini. Wakati huo wakwao wapo South.
Watoto wao wanasoma mifumo ya Cambridge
 
Siku hizi shule za uma sio shule ni viwanda vya kuzalisha wajinga
 
Jibu ni rahisi, "shule zetu ni kayumba, hawataki kuyumbisha watoto wao ".
amkeeni amkeni amkeni bwaanaa!! kitanda wasichokilalia hawezi kuwajua kunguni wake. Lazima viongozi na watumishi wa umma wasome na kutibiwa shule na hospitali za umma ili wajue wapi panapovuja ikinyesha.
 
Lazima zitungwe sheria kali watoto wa viongozi wote lazima wasome shule za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…