mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Hii yote inatokana na "socialism hangover" kwa kuwa wawapo madarakani wanajifanya wao ni maskini na pia ni watetezi wa wanyonge. Kwa hiyo basi watokapo madarakani, licha ya kuwa na ukwasi mkubwa, inawapasa waishi kinafiki ili wadanganyika wasiweze kuwatambua.
Viongozi waliohudumu wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere ndiyo waliishi na kujijenga kwa vipato vyao halali. Awamu zote zilizofuata, viongozi wake ni wapigaji wakubwa wa dili na majizi ya kutupwa ya mali za taifa letu.
Nchi za kibepari suala la kuwa na mali si la kificho, cha msingi tu, uwe na uthibitisho kuwa unazimiliki kihalali. Ubepari unaishi katika kanuni kuu moja tu, "somebody can be better off at the expense of the other"
Kwa hiyo basi mtu kujinufaisha na kutajirika kutokana na fursa aliyokuwa nayo wala siyo "big deal" Ni jinsi mtu mwenyewe anavyochachalika kujilimbikizia mali zake, huku akiwadhulumu kwa akili maskini wengi wasiojitambua.
Jaribu kufuatilia kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Rais wa Kenya, huwezi kusikia mgombea akijinasibu kwa maneno kama "kuwakomboa wanyonge" ama "kutetea wanyonge". Wanatambua kuwa na kundi kubwa la hao wanyonge ndiyo fursa pekee na nzuri kwao kuweza kuendelea kulimbikiza mali.
Mnyonge mkope fedha kidogo kidogo akishindwa kukulipa chukua mali zake ambazo ameziweka kama dhamana, mnyonge mtumikishe kazi nyingi kwa "low pay", hizi zote ni fursa za kuweza kupata kongole kutoka kwao hata pale unapoanikwa hadharani utajiri wako.