Kwanini watoto wengi wanaua mama zao?

Kwanini watoto wengi wanaua mama zao?

Acheni kupeleka watoto wenu boarding wakiwa wadogo..eti kitoto kina 2 yrs kinakaa shule..mpk kinafika chuo hakina hata bond wala mapenzi na mzaz wake....KAENI NAO WALEENI..KTK MAADILI sio mnawaachia walelewe na janii eti kisa mko busy....ona sasa..wanawaua hawana bt uchungu
Umenena point
 
hapo sababu ukiachana na masharti ya ushirikina ni tmaa zote ni juu ya kupta mali ila kwa wale walizaliwa katika jamii ambazo hazijastaarabika yaani hazina elimu za kijamii wantagemea za wazungu basi ni hatar sana kwao

elimu ya jamii ni malezi tosha kuweza kuwa kuishi na watu pia kuheshimiana nao kujitambua mali sio kitu ila utu ndo kila kitu

jamii zingine mali wameweka mbele hapas sijati mtu maana zipo nyingi kama hawatoau kwa nguvu basi hata kwa waganga kuna hii pia unakuta mtu yupo kachiikaaa
 
Vipi yupe dogo bonge wakichaga clip inasambaa amefungwa pingu alienda iba na kenta kabisa dukani kwa baba yake ILHALI BABA ALISHAMFUNGULIA BIASHARA YAKE ..ila akaona akaibe na kwa baba??

Kuna kitu nitakielezea kidogo kwenye hizi issues za vijana kuua mama zao unaeza kuona mauaji mengi yanatokea kwa kina mama zaidi ushajiuliza ni kwann zaidi ya kusema ni tamaa ya mali na roho mbaya? mm nimeishi na mama yangu sana nakumbuka kipind flan alikua ananiambia hapa sio kwako tukizeeka tutauza hii nyumba nikiwa yanki unadhan kweny nafsi ananitengenezea nini zaidi ya chuki?

Kuna baadhi ya wamama wana ubinafsi sana.

Mimi mama yangu alikuwa ana appartments kibao. Na akastaafu akapata mafao mazuri tu. Ila hatoi mtaji kwa yeyote. Yeye anapenda kutegemewa tu siku zote na sifa. Kanisani sadaka anatoa mamilioni ila wewe mwanae ama ndugu akikupa pesa ni kidogo ya kula tu sio mtaji na lazima iwe na matangazo kwa ndugu wengine wote.
 
Kumekua na ungezeko la watoto kuua mama zao wa kuwazaa hivi karibuni jambo linaloibua huzuni na hofu kwenye jamiii.

Asilimia kubwa imekuwa wahanga ni kina mama zaidi ya kina baba nimewaza jambo hili kwa kina ndani ya siku mbili hizi kuna mambo nayohisi yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi ya tamaa ya mali na kupenda starehe.

1-Maneno ya kina Mama kwa watoto.Wanawake wengi ni watu wa maneno wanapenda kuongea sana wanapokasirika na kutoa maneno mabaya kwa watoto wao kama kusema ndiyo maana huolewi,mbona mtu fulani kapata kazi wewe huna au mzazi wa kike anamwambia mtoto wake hapa nyumbani sio kwako hamna utakachokipata hapa hata tukifa/nikifa unategemea apo mtoto unamweka kwenye hali gani.

2-Kumnyima mtoto uhuru.Kina mama wengi wanapenda kuona watoto wao wanashinda nyumbani mtoto haruhusiwi kujichanganya na wengine.Mtoto saa kumi na mbili awe nyumbani mtoto anakosa furaha hamna kitu mtoto anapoanza kukua anakasirika kama kuona ananyimwa haki ya kua na watoto wengine au vijana wenzake tunajua dunia imeharibika ila sio sababu ya kuwanyima vijana kua na wenzake watoto wanachoka kukaa nyumbani na kuwachoka pia wazazi kutokana na masharti yao mengi yakiwa ni kuwanyima uhuru wao.

3-Wazazi kuwa wabinafsi.Kuna kina mama ukimwona anavyovaa na gari analoendesha na ukimwangalia na kijana wake tofauti iliyopo ni mbingu na ardhi hii inasababisha mtoto kuhisi mama hampendi na anajipenda yeye tu hiii huamsha hasira kali sana kwa mtoto na kuleta roho ya kisasi.

4-Chuki.Watoto wengi hua muda mwingi wanashinda na Mama zao kutokana na maisha ya kila siku kuna mambo hua yanatokea kati ya mama na mwanae mama anakua anamtishia mwanae akifanya kosa labda baba akija leo nitamwambia akuchape au leo hutakula hapa nyumbani hiii huleta chuki sana kwa watoto na kumchukia sana mzazi wake.

5-Msukumo kutoka kwa marafiki.Vijana hupenda kua na marafiki wa rika lao kuanzia mashuleni hadi mtaani hapa hukutana na mambo mengi na kulinganisha maisha yake na wengine mbona huyu mama yake anampa gari,mbona huyu anaruhusiwa kwenda kumbi za starehe hiii huleta chuki na ushauri kutoka kwa marafiki kwamba mama yako anakunyima gari, anakunyima kwenda club.

N:b haya ndio mambo niliyoyawaza mimi karibuni wengine kwa mengi au ushauri kuhusu mambo haya yanayoendelea kwenye jamiii hakika yanaleta huzuni kubwa
Hamna lolote ni njaa tu imezidi maisha magumu na watoto wanatamaa sana sikuhiZ
 
wazazi wamekua wabinafsi sana unakuta anajenga nyumba 7 na maduka kibao ila kukupa mtaji anaona nomaaa kila siku kiswahili hlf anapiga cmu kwa watu wampe mwananae kazi.

wakati roho yake ngumu kutoa mtaji sasa nani akupe kama tu weww huwezi kutoa cha kutosha mwisho wake ndo huo kwa watoto wasio na uvumilivu.
Yeye mzazi alipewa mtaji nani? Acha ujinga, komaa kijana tafuta zako.
 
Fanya hii research mleta mada,hawa watoto wanaoua wazazi wao ndio watoto ambao udogoni walipewa mapenzi mazuri na ya kiwango cha juu kuliko kawaida...
 
Umetoa sababu za kijinga Sanaa

Hakuna sababu yoyote ya KU justify mauaji..kuua tu kosa iwe ulikerekwa au iwe vipi mauaji ya kukusudia ni mbaya Sana tena hasa Hawa wanao ua wazazi wao kisa Mali (Kama inavyodaiwa)
🤙🤙🤙
 
Back
Top Bottom