Fursakibao
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 6,813
- 11,540
Ndio maana nikamwambia huyo no limbukeni na hajatembea. Binafsi nilikuwa sisalimii watu lakini baada ya kukaa na wapoli Poli nimejifunza kusalimia watu.Kiufupi sijaona tatizo lolote kwenye salamu, ingawa mleta mada anaweza kuona yupo sahihi ila si vyema kwa kuwa ameingia kwa watu wenye utamaduni huo. Itikia salamu then endelea na mambo yako. Nyodo unazozionyesha kwa watu hazifai, vinginevyo ujihakikishie unajitosheleza kwa Kila kitu na hautowahitaji hao watu kwa lolote lile.. Inawezekana akipata changamoto akiwa kwa watu pori (kama alivyowaita) ataleta watu wake kutoka Dar waje wamsaidie
Kuna siku tulienda na jamaa yangu sehemu wakati wa kurudi tukapotea Giza likaingia alafu Piki Piki ikaisha mafuta. Ikabidi tutembee kufika sehemu tukasikia mbwa wanabweka ikabidi twende kwa kufuata sauti za mbwa maana giza lilikuwa tororo kufika kwenye mji jamaa akatumulika na tochi, sikumfahamu huyo jamaa Lakini yeye alikuwa ananifahamu;
Ilibidi nimuulize mbona ananifahamu alafu simfahamu. Akanikumbusha Kwa kuniuliza wewe si ndio ulipoteza ufungu wa gari nyeupe nikamwambia ndio Mimi; jamaa akatuuliza mnashida gani tukamweleza akachukua mafuta akatupa tukapewa na maziwa tukanywa.
Wakati tunaondoka akasema nimekupa mafuta kwa sababu hujisikii, unasalimia watu na lift unatoa. Akatuelekeza njia tukasepa
Imagine kama ningekuwa kama mleta mada siku hiyo ingekuwa je?