darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 9,101
- 18,055
Kumbe we jamaa ni Msukuma😂😂😂Umenikumbusha mbali sana.
Kuna kipindi nilienda likizo Mwanza, nikakuta kuna vitoto fulani barabarani nikavipita tu. Vitoto vidogo tu, hata siku vi register.
Basi wee, vile vitoto vilimind vibaya sana. Vikawa vinasema Kisukuma kwamba huyu mbona kapita tu kama hajatuona.
Nilishangaa sana, nikaja kugundua siko Dar. Halafu nilishanmgaa kwa sababu nilitegemea wao kwa sababu ni wadogo, kama wana mind kusalimiana sana wangeanza kunisalimia wao.
Nilikuja kugundua kuwa kum recognize mtu pale ni kitu cha muhimu sana.
Ila, unaweza kuvipita vitoto hivi, halafu ukakutana navyo ukaambiwa ni vitoto vya shangazi yako fulani, vinakujua ila wewe huvijui.
Sasa hapo muhimu kusalimiana tu.
Tatizo bora salamu zingekuwa fupi zile kama za Kiswahili "Za saa hizi?" unajibiwa "Salama" unapita.
Msukuma salamu anakusimamisha, ukimaliza kumtajia ukoo wako, anakuuliza na mkeo hajambo, na watoto? Na hapo hapo anaunga stories, kama una haraka unachelewa.
Nilifikiri Waukae Mwenzangu.